google-site-verification: googleabbfd1327a3af7a3.html

Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Kujifunza zaidi juu ya maisha na mafanikio, nakualika kwenye kundi la whats app kujifunza kwa kina. Tututumie ujumbe kwa njia ya whats app kwenda 0687449428 kupata utaratibu wa kujiunga.

Feb 16, 2016

Mambo Muhimu Ya Kukusaidia Kukuza Biashara Yako Wakati Wote.

No comments :
Kila mfanyabishara mwenye nia ya kufikia mafanikio makubwa, lengo lake kubwa la kwanza huwa ni kutaka kukuza biashara yake na kufikia mafanikio makubwa. Hakuna mfanyabiashara ambaye anakua hana nia hii, kila mmoja hutamani kuona biashara yake ipo sehemu fulani kimafanikio siku hadi siku.
Lakini pamoja na juhudi nyingi ambazo zimekuwa zikifanywa za kujitahidi kukuza biashara, wengi hujikuta wakishindwa kufikia lengo hilo. Hapo ndipo huanza kujiuliza tatizo ni nini? Leo katika makala yetu, nakushirikisha mambo muhimu ya kukusaidia kukuza biashara yako wakati wote.
Karibu sana na twende pamoja kujifunza mambo hayo ili yawe msingi mkubwa katika kukuza biashara yako;-
1. Toa huduma bora.
Kama hamu yako kubwa ni kuona biashara yako ikikukua kwa kasi, jifunze kutoa huduma bora kabisa na sio bora huduma. Kama hutabadilika na ukaendelea kutoa huduma mbovu, sahau kabisa biashara yako kukua. Utaendelea kubaki hapohapo. Siri kubwa ya kukuza biashara yako, hakikisha unatoa huduma bora siku zote bila kuacha.

TENGENEZA VYANZO VINGI VYA FEDHA.
2. Toa bidhaa zenye ubora mkubwa.
Njia bora kabisa itakayokusaidia kukabiliana na ushindani na kukuza biashara yako, ni kutoa bidhaa zenye ubora wa hali ya juu. Kama utakuwa unatoa bidhaa zina ubora wa hali ya juu popote pale utakapokuwepo ni lazima wateja wako wakufuate. Tumia muda wako mchache, kutafiti namna ambavyo unaweza ukatoa bidhaa bora kabisa itakayomridhisha mteja wako.
3. Jifunze kuwa na lugha nzuri.
Unaweza ukawa una huduma iliyobora na unatoa bidhaa bora, lakini kama huna lugha nzuri kwa wateja hiyo itakuwa ni sumu kubwa sana kwenye biashara. Kwa vyovyote vile iwavyo lugha nzuri, ni kitu muhimu sana kwenye biashara ambacho kinauwezo wakukusaidia kukuza biashara yako nyakati zote.
4. Jali muda wa wateja wako.
Muda siku zote ni mali. Ukipotea umepotea. Kama ni hivyo ili kijipa uhakika wa kukuza biashara yako, jifunze sana kujali muda wa wateja wako. Fanya chochote kile ufanyacho kulinda muda wa mteja usipotee hovyo. Usimpotezee mteja muda wake bila sababu.  Hii ni njia mojawapo bora sana itakayokusaidia kukuza biashara yako. Bila kufanya hivyo utapoteza wateja wengi sana.
5. Kuwa na punguzo maalum la bei.
Katika biashara yako acha kuacha bei ikawa juu kila wakati. Kuna wakati unatakiwa kuonyesha kwa wateja wako kuwajali zaidi kwa kuwawekea punguzo maalumu la bei. Hiki ni kipindi kinaweza kikawa cha sikuu au wakati maalumu ambao wewe utaamua. Hiyo itawapa hamasa kubwa sana wateja wako kuvutika na biashara yako.
6. Weka matangazo.
Matangazo ni  kitu cha muhimu sana katika ukuaji wa biashara yoyote. Itangaze biashara yako kupitia wateja wako hao hao ulionao. Hiyo haitoshi, unaweza ukatengeneza vipeperushi vidogo vidogo vinavyoonyesha biashara yako. Lakini kama mtaji unaruhusu unaweza  ukaitangaza biashara yako kupia redio au televisheni. Hiyo itakusaidia sana kukuza biashara yako eneo kubwa na kwa muda mfupi.
7. Boresha biashara yako mara kwa mara.
Kwa kawaida tunapofanya biashara huwa kuna mapungufu yale ambayo yanajitokeza. Mapunguf haya unaweza ukayapata kutoka kwa wateja kwa njia ya malalamiko au kutoa maoni yao moja kwa moja kwako. Inapotokea hivyo, fanya marekebisho ya haraka mno bila kuchelewa. Ikiwezekana wawekee kisanduku cha maoni. Hiyo itakusaidia kuza sana biashara yako na kuwa kubwa kuliko unavyofikiri.
Kwa kifupi, hayo ndiyo mambo muhimu yanayoweza kukusaidia kuikuza biashara yako wakati wote. Yafanyie kazi mambo hayo yatakusaidia sana kukuletea mabadiliko makubwa katika bishara yako leo na kesho.
Nikutakie siku njema na mafanikio makubwa katika biashara yako na endelea kuwashirikisha wengine kujifunza kupitia mtandao wa DIRA YA MAFANIKIO kila wakati.

Ni wako rafiki katika kusaka mafanikio ya kweli,
Imani Ngwangwalu,
Simu; 0713048035,

No comments :

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.