google-site-verification: googleabbfd1327a3af7a3.html

Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Kujifunza zaidi juu ya maisha na mafanikio, nakualika kwenye kundi la whats app kujifunza kwa kina. Tututumie ujumbe kwa njia ya whats app kwenda 0687449428 kupata utaratibu wa kujiunga.

Feb 2, 2016

Pale Ulipo Una Hali Gani Ya Maisha?

No comments :
Na Noel Ngowi, Moshi.
Yawezekana wakati huu wa sasa pale mahali ulipo una wakati mgumu na umekata tamaa kwa vitu au sehemu fulani ya maisha yako. Pale unapoangalia mambo yalivyo magumu sana na kila jambo kwako haliendi na unadhani huwezi kutoka pale ulipo kwenda sehemu ya maisha bora, mafanikio na furaha.
Je, mpaka sasa umechukua hatua gani? Je, una wazo ya kwamba utapata mafanikio lini? Amka, acha kujidanganya usiruhusu mawazo ya umaskini kukutawala. Tambua ya kwamba hukuumbwa uwe maskini. Kwa hali yoyote uliyonayo, usijishushe wala kujiona wewe ni wa chini hivyo, hukuumbwa uwe hivyo kama unavyofikiri.
Japokuwa hali ya umaskini inakuwepo kwenye maisha, lakini unapaswa kutambua ya kwamba una uwezo wa kuushinda umaskini huo. Inawezekana umezaliwa kweli maskini, lakini sio kuja kuwa maskini. Kama ambavyo Bill Gates aliwahi kusema wakati fulani ‘kuzaliwa maskini sio kosa lako, bali kufa maskini ndiyo kosa lako’. Tumia uwezo na nguvu za ajabu ambazo Mungu amekupa kuwa na mafanikio.
Tambua wewe una thamani kubwa sana ya kuleta mafanikio makubwa yoyote unayoyataka katika maisha yako kuliko unavyofikiri. Kila kitu unacho mkononi mwako ukiamua iwe hivyo. Kama unaona huna kitu kwa sasa sawa, usilalamike sana jipange. Unayo nafasi kubwa ya kubadilisha kesho yako kwa kuitumia leo vizuri.

KIZUIZI CHOCHOTE UNAWEZA KUVUKA HADI KUFANIKIWA.
Kumbuka kuwa na mafanikio sio kitu cha siku moja, bali inakuhitaji wewe kuchukua muda na kuamua kupanga na kujitamkia namna utakavyopata mafanikio. Fahamu namna unavyojitazama sivyo Mungu anavyokutazama. Inawezekana unajiona mnyonge sana, maskini wa kutupwa lakini je, Mungu ndivyo unavyokuona?  
Una uwezo mkubwa sana ndani yako, fungua akili na macho, tafuta unachoweza kufanya na kifanye kwa utofauti zaidi ili ufanikiwe. Hebu jaribu kujiuliza utabaki kuomba omba na kuona wengine wakifanikiwa mpaka lini? Acha kukata tamaa mambo yote yanawezekana kama unafikiri yanawezekana.
Hujachelewa hata kidogo, kuchukua uamuzi wa kubadilisha maisha yako. Tambua kila siku ni mpya na wewe ni vyema ukaanza siku mpya leo na mawazo mapya ya kubadilisha maisha yako. Acha kulalamika na kuwalalamikia wengine ndiyo eti waliokukwamisha. Chukua hatua juu ya maisha yako mwenyewe. Wajibika juu ya maisha yako.
Jifunze kukataa kujiona hufai na anza kutafuta mafanikio siku zote bila kuchoka. Usingoje dakika nyingine kupita, inuka, tafakari na ishi maisha mapya ya furaha.  Hapo ulipo sio sehemu yako. Ni nini kinachokufanya ukae na kuendelea kuridhika bila sababu. Anza kuishi maisha ya mafanikio sasa.
Ukiamua unaweza kufikia mafanikio yako makubwa bila ubishi na hakuna mtu wa kukuzuia katika hilo. Wewe ndiye unayetakiwa sasa kuamua maisha yako unataka yawe vipi?
Tunakutakia  siku njema na mafanikio mema yawe kwako. Kumbuka endelea kutembelea DIRA YA MAFANIKIO kila wakati, kwa ajili ya kujifunza na kuhamasika.
Kama makala hii imekusaidia kwa namna moja au nyingine, fanya tendo la upendo kwa kumshirikisha na mwingine aweze kujifunza kupitia mtandao huu.
Diraya mafanikio inatoa pongezi na shukrani  za pekee zimwendee Noel Ngowi kwa kuweza kutushirikisha makala hii nzuri na bora kabisa.
Kama na wewe una makala nzuri ambayo unaona inaweza ikawa msaada kwa watu wengine, unaweza ukatutumia kwenye e-mail yetu ya dirayamafanikio@gmail.com

Karibu sana na tupo pamoja siku zote.

No comments :

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.