google-site-verification: googleabbfd1327a3af7a3.html

Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Kujifunza zaidi juu ya maisha na mafanikio, nakualika kwenye kundi la whats app kujifunza kwa kina. Tututumie ujumbe kwa njia ya whats app kwenda 0687449428 kupata utaratibu wa kujiunga.

Apr 1, 2016

Umuhimu Wa Kujenga Mahusiano Bora Na Watu Wengine.

No comments :
Binadamu ni viumbe ambao wana mizunguko mingi katika siku zao za kuishi hapa duniani. Binadamu hao hao hukutana na jamii za watu tofauti tofauti katika shughuli mbalimbali za kusaka Mafanikio kama vile mashuleni, kwenye semina mbalimbali na sehemu nyingine mbalimbali.

Binadamu hawa pamoja na kukutana kwako, ni watu wachache hutambua thamani ya kukutana kwako. Hebu tujiulize swali dogo tu, rafiki zako ulikuwa unasoma nao hata kucheza nao leo wapo wapi? Unajua wanafanya nini? Je ni wazima bado au walishafariki siku nyingi na wewe huna taarifa?

Nakumbuka sana enzi za utoto hasa katika mahafali yangu ya darasa la saba moja ya nyimbo ambazo tulizimba, nakumba tuliimba ya kuwa milima hakikutani ila binadamu hukutana, niliamini sana kwa kwa miaka ya mbeleni kuwa siku moja nitakuja kukutana na watu niliosoma nao lakini mawazo yangu hadi leo sijaona yakiitimia.

JENGA MAHUSIANO MAZURI NA WENGINE

Maana yangu ni kuwa huenda niengejua wale nilikuwa nasoma nao, ningejua walipo na wanafanya nini, ningesonga mbele kimafanikio au lah!

Tuachane na hayo maana kila nikiwaza sina majibu, lakini jambo la kuzingatia mimi naamini kila binadamu wakikutana sehemu yoyote ile kuna sababu, ila wengi wetu bado hatujalitambua hilo. Kwa mfano leo hii umekutana na mtu maarafu popote pale, jambo la kwanza utakaloliwaza katika akili yako ni kupiga picha na mtu huyo ili uje uweke mitaandaoni huku ukiandika maneno mbalimbali, kama vile katika ubora wangu.

Ndugu msomaji wa makala hii kila mtu unayekutana naye, kuna sababu huenda akakusaidia katika safari yako ya mafanikio na sio kupiga picha na kuzidi kuwa na maisha yale yale kila siku.

Kila mtu unayekutana naye kuna sababu. Cha msingi ni kujenga mahusiano bora na mtu huyo. Inawezekana ndiye atayekuwa msaada mkubwa katika kubadilisha maisha yako.

Kama wewe ni miongoni mwa watu ambao unajiona maisha yako yamebadilika kwa sababu ya mtu fulani ndiye alichangia kuwa hapo ulipo chukua dakika chache kumshukuru huyo aliyekusaidia. Japo wengi wetu hatuna tabia hiyo ya kuwashukuru watu waliotusaidia kufika hapa tulipo, basi ni muda muafaka wa kutoa shukrani.

Jambo la msingi la  kumbukumbuka kila unayekutana naye  kuna sababu hivyo jenga mahusiano na anayekutana naye.

Imeandikwa na Benson chonya

Simu:0757-909942
E-mail ; 
bensonchonya23@gmail.com
www.dirayamanikio.blogspot.com

No comments :

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.