google-site-verification: googleabbfd1327a3af7a3.html

Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Kujifunza zaidi juu ya maisha na mafanikio, nakualika kwenye kundi la whats app kujifunza kwa kina. Tututumie ujumbe kwa njia ya whats app kwenda 0687449428 kupata utaratibu wa kujiunga.

May 11, 2016

Siri 7 Za Kuwa Mfanyabiashara Mkubwa.

No comments :
Inawezekana kila wakati umekuwa ukijiuliza ni kwa jinsi gani utaweza kutoka katika hali ya kufanya biashara ndogondogo au biashara ya kati hadi kuwa mfanyabiashara mkubwa. Leo katika Makala haya nitakwenda kukueleza bayana siri ambazo kama utaamua kuzitumia utaweza kuwa mfanyabishara wa mkubwa.

Ni lazima ujue kuwa mfanyabiashara ni lazima kuwa na imani. Imani ambayo ninazungumzia hapa ni kuamini sasa kitu ambacho hakipo. Huenda ukawa hujanielewa, tulia ili nikueleweshe ukweli ni kwamba ukitaka kuwa mfanyabiashara mkubwa ni lazima uamini kwamba kitu hicho kitakuwa kweli, kwa hapo baadae. Kuna usemi unasema ya kwamba imani ni bora kuliko matendo, maana yake amini kwanza.

Kuwa na imani thabiti ambazo zitakufanya ujipe moyo wa ushindi na wenye mawazo chanya ya ushindi juu ya kuwa mfanyabiashara mkubwa. Endapo utakuwa na imani nusunusu ni lazima utashindwa kutimiza jambo lako. Kanuni ya biashara inasema ya kwamba kama unahitaji Mafanikio makubwa matokeo yake huwa hayaonekani mapema na madhara yake huwa hayaonekani mapema pia. Huo ndio ukweli lazima ujiulize nikifanya jambo hili na nisipofanya matokeo yake ni nini?
Ukijiuliza maswali haya lazima uyapatie majibu ya kina yenye kuleta majibu sahihi. Kama nilivyosema hapo awali ya kwamba kuwa mfanyabiahara mkubwa ni Kuwa na imani, hivyo ni vyema ikumbukwe ya  kwamba kuwa mfanyabiashara wa mkubwa usitegemee mwanzoni mwa biashara yako kutengeneza faida, ila jiandae kupokea hasara ambazo ndizo changamoto zenye kukuletea mafanikio makubwa mbeleni. Unawezaje sasa kuwa mfanyabiashara mkubwa?

Zifuatazo Ndizo Njia 7 Za Kuwa Mafanyabiashara Mkubwa.

1. Chagua wazo bora la kibiashara.

Wazo bora la kibiashara ndilo litakalo kufanya kuwa mfanyabiashara wa mkubwa. Mara nyingi nimekuwa nikikutana na watu wakisema wanataka kuwa wafanyabiashara na kuishia kusema tu. Ila ukweli ni kwamba katika kuchagua wazo bora la kibiashara ni lazima ujiulize je unataka kuwa mzalishaji wa bidhaa au huduma? Je unataka kuwa mnunuzi na muuzaji?au  je unataka kuwa msambazaji tu ? Hayo yanaweza kuwa miongoni mwa maswali ya msingi ya kujiuliza.

Fanya utafiti wa soko.
2. Fanya uchunguzi juu ya washindani wako.
Hapa ndipo jicho la tatu linaposhindwa kufanya kazi mara nyingi. Tumekuwa si wachunguzaji wazuri juu ya washindani wetu ila tumekuwa wasikilizaji tu kwa watu wengine juu ya washindani wetu. Ila ikumbukwe ya kwamba fanya uchunguzi wa kutosha ili kujua washindani wako wanatumia mbinu zipi kukuza biashara zao. Hii itakusadia pia kujua ni wapi wanapokosea ili uweze kulizipa pengo hilo. Kwa kufanya hivi kutakufanya ndoto zako za kuwa mfanyabiashara wa kimataifa zitimie.

3. Tafuta mtu wa kukuongoza. (Helpful mental).
Tafuta mtu sahihi wa kukuongoza  na si mtu wa kukukwamisha. Watu wengi tunashindwa kuwa wafanyabishara wakubwa hii ni kutokana tunatafu watu ambao sio sahihi katika kutushauri. Stuka mapema juu ya jambo hili. Na anza kukaa na watu ambao tayari wamefanikiwa kwenye biashara zao watakusaidia sana kufika kule unakotaka kufika kibiashara. Siku zote ukitaka kuruka kama tai, ni lazima ujifunze kama tai wanavyoruka. Kwa maana huyo ukitaka kuwa mfanyabiashara mkubwa kubali kuchukua mwongozo wa wafanyabiashara waliofanikiwa.

4. Tambua biashara inayokua.
 Ukilijua hili ni jambo jema zaidi. Moja ya tatizo kubwa ni kwamba tumekuwa tukishuhudia biashara hazikuwi miaka nenda miaka rudi. Hii ni sababu kubwa ambayo inachangia tusiweze kujua ni kwa jinsi gani tusiwe wafanyabiashara wakubwa. Natamani kuona malengo yako yanabadilishwa kila wakati. Kwa mfano leo unauza nguo kwa kutembeza, ili kuona biashara inakuwa tunataka kuona unapata chumba kwa ajili ya kufanyia biashara hiyo napo kweli tunasema biashara inakua. Kama unafanya biashara mkoa wako mzima tunatamani kuona unaongeza mkoa mwingine na mwingine katika kusambaza huduma au bidhaa.

5. Panga malengo na mipango ya biashara yako.
Hapa inahusiana na juu ya kuuza, kununua bidhaa au huduma. Lazima malengo ya biashara yako uyapange kila robo ya mwaka ili kugundua kama biashara yako inakuwa au haikui. Na lazima pia katika kupanga malengo yako, utambue baada ya muda fulani biashara yako itakuwa imefika wapi. Kwa mfano ni muhimu kujua biashara yako itakapokuwa baada ya miaka miwili au mitatu mbeleni.

6. Tangaza biashara yako.


Wateja wako ni lazima wajue bidhaa na huduma ambayo unazalisha. Si kujua tu, lengo jingine la kutangaza bidhaa au huduma inamfanya mtumiaji aweze kujua jinsi ya kutumia kitu hicho. Kwa kutangaza biashara wateja huongezeka kwa asilimia kubwa sana na kufanya huduma au bidhaa yako kuweza kupendwa na wengi pia. Matangazo ni njia mojawapo bora ya kukufanya kuwa mfanyabiashara wa kimataifa ikiwa utaitumia vizuri.
7. Jenga mahusiano mazuri na wateja wako.

Jitahidi kulizingatia hili ya kwamba Kauli katika biashara ni mali kuliko hata  pesa. Jali wateja wako na kuwafanya wajihisi kama wanapata bidhaa bure. Kwa kadri utakavyozidi kujenga mahusiano bora na wateja hiyo itapelekea wao kupenda bidhaa zako na hiyo itakusaidia kukuza wateja wengi siku hadi siku.
Ni matumaini yangu umenielewa vizuri hizo ni baadhi ya siri chache kati nyingi zitakazokufanya kuwa mfanyabiashara mkubwa. Asante sana na usisite kumshirikisha mwingine.

Mwandishi;  Benson Chonya.
Email; 
bensonchonya23@gmail.com
Simu; 0757-909942

No comments :

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.