google-site-verification: googleabbfd1327a3af7a3.html

Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Kujifunza zaidi juu ya maisha na mafanikio, nakualika kwenye kundi la whats app kujifunza kwa kina. Tututumie ujumbe kwa njia ya whats app kwenda 0687449428 kupata utaratibu wa kujiunga.

Nov 1, 2016

Njia Zinazotumiwa Na Wengi Kufikia Mafanikio Makubwa.

No comments :
Mara nyingi linapokuja swala la kufikia mafanikio makubwa, nguvu ya uzingativu, uwezo wa kufanya kazi kwa bidii na ung’ang’anizi, ni mambo yanayotajwa sana kwamba yana mchango mkubwa wa kusaidia kufikia kwenye mafanikio makubwa.
Hata hivyo,pamoja na mambo hayo kuwa yana umuhimu na msingi mkubwa katika kufikia mafanikio makubwa, pia zipo njia nyingine ambazo zinatumiwa na watu wengi wenye mafanikio kufanikiwa kwa viwango vya juu.
Njia hizo ambazo zimethibitishwa na kutajwa na wataalamu mbalimbali wa mafanikio hasa baada ya kuzitumia na kuona matokeo chanya ndizo hizo tunakwenda kuziangalia kupitia makala haya.
Hebu twende pamoja tuangazie nukta kadhaa za kutusaidia kujua njia zinazotumiwa na wengi kufikia mafanikio makubwa.
 1. Maandalizi.
Kila wakati unahitaji kujiandaa ili kufanikiwa. Hakuna mafanikio ambayo unaweza kuyapata bila kuwa na maandalizi mazuri. Ni lazima ujiandae kiakili na kimwili, ili ikusaidie kukabiliana na kila changamoto unayokutana nayo.
Kwa mfano, wanamichezo wote duniani kabla ya siku ya mashindano husika wanakuwa wana maandalizi kwanza. Hakuna anayekwenda kushindana bila kujiandaa, kwa sababu wanajua maandalizi hayo huwaandaa kushinda.
Hata kwenye maisha yako ili uwe mshindi na kufikia kilele cha mafaniko ni lazima kujiandaa. Ni lazima ujiandae kwa kuandika mpango wako nini ufanye na nini usifanye, changamoto za kile unachataka kufanya ni zipi?

Njia Zinazotumiwa Na Wengi Kufikia Mafanikio Makubwa.
Tafuta njia sahihi ya mafanikio yako.
Tambua ni lazima ujiandae kufanya kazi kwa bidii na katika mazingira hata yale yaliyo magumu. Kile ambacho umeamua kukifanya kifanye kwa nguvu mpaka kikupe mafanikio. Acha kupoteza nguvu zako kwa kuishia katikati.
Unapokuwa na maandalizi ya namna hii, hakuna kitakachokushtua sana hata ukipata matokeo usiyoyategemea. Hivyo unaona kabisa kwamba, maandalizi ni njia mojawapo muhimu ya kukufikisha kwenye mafanikio makubwa.
2. Kufanya kila siku.
Najua kuna kitu ambacho umechagua kukifanya na unaamini kitu hicho kitakupa mafanikio, sasa kitu hicho kifanye kila siku. Kitengenezee kitu hicho ratiba ya kukifanya kila siku yaani ‘daily routine’.
Haijalishi siku hiyo umeamka unajisikia kukifanya au hujisikii kufanya kitu hicho, wewe fanya. Usisikilize sauti ya mwili wako. Mafanikio hayawezi kuja kwa kufanya mambo kwa kujisikia, yanakuja kwa kuchukua hatua za utendaji kila siku bila kujali hali uliyonayo.
3. Kufanya kwa uhodari.
Ili kufanikiwa unahitaji kutambua ni mambo yapi uliyobora na mambo yapi una udhaifu mkubwa ili kurekebisha na kusonga mbele zaidi. Mafanikio yoyote yanatengenezwa kwa kufanya mambo kwa uhodari na si kizembe.
Watu wengi wenye mafanikio wanatumia njia hii ya kujiimarisha kila siku na hadi kuweza kufanikiwa. Pale wanapokosea hujirekebisha, na kuzidi kufanya kwa ufanisi mkubwa unaoleta mafanikio.
4. Maarifa.
Kati ya kitu ambacho kinakubaliwa karibu na wataalamu wote wa mafanikio ni jinsi ya kuwa na maarifa bora. Maarifa bora ni nguzo kubwa sana ya mafanikio yoyote duniani.
Ili uweze kufanikiwa ni lazima uwe na maarifa bora. Utayapata maarifa haya kwa kujisomea na kujifunza kwa wengine pia. Hii ni njia muhimu sana ambayo ukiitumia itakufikisha kwenye kilele cha mafanikio.
Kabla sijafika mwisho wa makala haya, inabidi uelewe kwamba maandalizi bora, kufanya kile unachokifanya kila siku, kufanya kwa uhodari na maarifa ni njia mojawapo ambazo zinatumiwa na wengi kufikiwa mafanikio makubwa.
Tunakutakia kila la kheri katika kufikia mafanikio makubwa.
Endelea kujifunza kupitia dirayamafikio.blogspot.com kila siku.
Napenda pia kukaribisha wewe rafiki yangu kwenye kundi la Whats App ili tuweze kujifunza pamoja. Kujiunga tuma neno MAFANIKIO YANGU, kisha ikifutia na jina lako kwenda 0713 048035 ili uanganishwe. Hakuna gharama na karibu sana.
 Ni wako rafiki,
IMANI NGWANGWALU,




No comments :

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.