google-site-verification: googleabbfd1327a3af7a3.html

Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Kujifunza zaidi juu ya maisha na mafanikio, nakualika kwenye kundi la whats app kujifunza kwa kina. Tututumie ujumbe kwa njia ya whats app kwenda 0687449428 kupata utaratibu wa kujiunga.

Nov 14, 2016

Tabia Unazotakiwa Kuzijenga Pale Unapokuwa Na Fedha.

No comments :
Katika hali ya kawaida, ili uweze kupata pesa na zikadumu mikononi mwako, zipo tabia ambazo ni lazima uwe nazo. Ni ngumu sana kuendelea kuwa na pesa kama huna tabia hizo ambazo ni kama msingi wa kukupa pesa zaidi.
Watu wengi maisha yao yamekuwa hovyo, kwa sababu ya kukosa tabia hizi. Utakuta mtu anapata pesa leo, ukionana nae kesho, pesa hizo hana, haya yote hutokea kwa sababu ya kukosa tabia hizo za msingi.
Ikiwa nia yako unataka kutengeneza pesa za kutosha na hata zile pesa ulizonazo ziweze kudumu, ni muhimu na lazima kuendeleza tabia hizi ambazo tunakwenda kuzijadili katika makala haya.
Hebu twende nami pamoja kujifunza kupitia makala haya, nikuonyeshe tabia unazotakiwa kuzijenga hasa pale unapokuwa na pesa.
1. Tabia ya kuweka akiba.
Kuweka akiba ni jambo la muhimu sana katika mafanikio ya mjasirimali. Uwe unataka au hutaki ni lazima sana kwa mjasirimali anayetaka mafanikio, kujifunza kujiwekea akiba kila wakati.
Zipo faida nyingi zitokanazo na kujiwekea akiba, ikiwa pamoja na kusaidia katika suala zima la kuwekeza pesa hizo zinapokuwa nyingi. Pia kujiwekea akiba inakusaidia kujenga msingi imara wa kipato chako.
Ni lazima uweze kujiwekea akiba kwa kiasi chochote cha pesa unachopata. Kila unapopata pesa anza kwanza kuweka akiba, kisha inayobaki tumia. Hii ni siri kubwa inayotumiwa na watu wote wenye mafanikio ya kifedha duniani.

2. Tabia ya kuweka vipaumbele juu ya matumizi yako.
Ili uweze kujijengea kipato cha kudumu, unalazimika kuweka vipaumbele juu ya matumizi yako. Vipaumbele hivi unavyokuwa unaweka vinakusaidia kujua, kipi ununue na kipi usinunue na pesa zako.
Kitendo cha kuwa makini na pesa zako, hadi kujua kipi cha muhimu na kipi si cha muhimu kwa sasa, hiyo itakuwa ni ishara tosha kwamba sasa unaweza kuitawala pesa, na si pesa ikutawale wewe.
Kuweka vipaumbele kwenye matumizi yako, ni njia mojawapo bora ya kukufanya ukawa ni mjasiriamali mwenye mafanikio. Unapokuwa na pesa muda wote, hakikisha unakuwa mtu wa kuweka vipaumbele, acha kupuuza juu ya hilo na utafanikiwa sana.
3. Tabia ya kuandika matumizi yako ya pesa.
Hautaweza kujua sana pesa zako zinatumikaje, ikiwa hauziwekei kumbukumbu. Mbinu ya kukusadia kujua hili vizuri, ni kuandika kila aina ya matumizi unayofanya. Hutakiwi kudharau juu ya hili kila kitu ni lazima uandike.
Kuna msemo usemao, ‘mali bila daftari hupotea bila habari,’ hivyo kwa kujua hili, nunua kijitabu chako cha mtumizi na kuandika kila aina ya shilingi ambayo unaitumia kwa siku.
Utafika mbali kimafanikio ikiwa utaikumbatia tabia hii na kuwa yako. Hiyo inakuwa hivyo kwa sababu kila matumizi yanapokuwa juu, inakuwa sawa kama una alamu inayokwambia punguza matumizi. Ishi kimafanikio kwa kuandika kila aina ya matumizi yako.
4. Tabia ya kuwekeza.
Huwezi kuendelea ukawa una pesa, kama kila pesa unayoipata unatumia yote. Upo umuhimu mkubwa sana wa kuwekeza angalau sehemu kidogo ya pesa yako unayoipata ili ikusaidie kuzalisha.
Pengine unajiuliza, sasa kama pesa ninayopata ni kidogo ninaanzaje hapo kuwekeza? Jibu ni rahisi tu, anza kwa kuweka akiba kwanza. Akiba yako itakapokwa nyingi itaenda kwenye uwekezaji moja kwa moja unaoutaka.
Kimsingi, ili uweze kutengeza kipato cha kudumu, kipato ambacho kitakuwa endelevu leo na kesho, ni vyema ukajifunza kujenga tabia hizo na zikawa za kudumu kwako wakati unapokuwa na pesa.
Chukua hatua na endelea kubadili maisha yako kwa kuwa na fikra sahihi za mabadiliko, kwa kutembelea DIRA YA MAFANIKIO kila siku.
Nikutakie siku njema na mafanikio mema.
Ni wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
0713 04 80 35,

No comments :

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.