google-site-verification: googleabbfd1327a3af7a3.html

Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Kujifunza zaidi juu ya maisha na mafanikio, nakualika kwenye kundi la whats app kujifunza kwa kina. Tututumie ujumbe kwa njia ya whats app kwenda 0687449428 kupata utaratibu wa kujiunga.

Mar 15, 2017

Mambo Sita (6) Ya Lazima Kuyajua Ili Kufikia Mafanikio, Kama Umeanza Na Kidogo Ulichonacho.

No comments :
Yapo mambo ya lazima kuyajua na kuyafatilia kwa ukaribu sana kama unaanza na kidogo ulichonacho ili kuweza kufikia mafanikio. Bila kuzingatia mambo hayo uwezekano wa kufanikiwa utakuwa ni mgumu.
Kwa yeyote anayezingatia mambo haya haijalishi unaanza na kidogo kiasi gani, mafanikio yataanza kuonekana mara moja kama utachukua hatua. Mambo haya yanazingatiwa sana na kila anayeanza na kidogo hadi kufanikiwa.
Yafuatayo Ni Mambo Sita (6) Ya Lazima Kuyajua Ili Kufikia Mafanikio, Kama Unaanza Na Kidogo Ulichonacho.
1. Kuwa kwenye mwendo.
Siri kubwa ya kuanza na kidogo ulichonacho hadi kufanikiwa ipo kwenye kukaa kwenye mwendo au ‘momentum’. Namaanisha nini ninaposema kukaa kwenye mwendo, yaani kuendelea kuchukua hatua kwa jambo ulilolichagua hata kama ni kwa kidogo sana.
Ni bora ukawa unafanya kitu kidogo kidogo, lakini mwisho wa siku utajikuta unasogea kuliko kutulia. Ni bora kuanza biashara hata ndogo kuliko kusubiri ile biashara iliyo kubwa ambayo hunayo. Anza na kidogo ulichonacho ili kikusaidie kuweza kukaa kwenye mwendo.

Anza na kidogo, hadi ufikie mafanikio makubwa.
Kaa kwenye mwendo. Hata kanuni za kisayansi zinatuambia kila kitu kilichoko kwenye mwendo kitazidi au kitaendelea kuwa kwenye mwendo, pengine itokee nguvu nje ya kuzuia. Sasa kwa nini usichukue hatua na kuamua kukaa kwenye mwendo kuliko kusubiri subiri.
Ili kufanikiwa kukaa kwenye mwendo, chagua kitu unachokitaka, kisha kitu hicho kifanye kila siku. Hiyo itakuwa ni njia nzuri sana ya kuweza kukuweka kwenye mwendo wa mafanikio yako. ukifanya kitu hicho kila siku utake, usitake ni lazima utasogea.
2. Maliza kila kitu unachokianza.
Ili uweze kuwa kwenye mwendo vizuri wa kufikia mafanikio yako, jifunze kumaliza kile ambacho unaanza nacho. Kama kila kitu ambacho unakianza hukimalizi, tambua unatengeneza nguvu kubwa ya kukufanya ushindwe kwa baadae.
Kwa vyovyote vile, kila siku jitahidi kumaliza kitu ambacho umejiwekea kufanya. Najua sio rahisi kuweza kumaliza kila kitu ambacho unakianza, kwa sababu vipo vinavyokwama pia bila kutarajia, lakini hiyo isiwe sababu, maliza kile unachokianza.
Kama kuna jambo umelianza, hata kwa macho ya kawaida kama linaonekana ni mlima lianze jambo hilo na kuhakikisha unalimaliza. Weka jitihada zitakazokuwezesha kulimaliza. Mafanikio yanajengwa na wewe jinsi unavyomaliza vitu na sio kuachilia kati.
3. Jenga tabia za kukusaidia kufanikiwa kila siku.
Kinachowangusha wengi kwenye safari ya mafanikio ni tabia zao. Tunapozungumzia tabia ni yale ,mambo ambayo kuna wakati tunayafanya hata bila kufikiria, unafanya tu kwa sababu ya mazoea ya kila siku. Hebu angalia ni mazoea gani yanakuzuia kufanikiwa.
Kwa mfano kuamka asubuhi na mapema ni tabia na pia kuchelewa kuamka ni tabia. Kulalamika ni tabia na hata pia kuwajibika ni tabia. Hiyo haitoshi kutumia pesa hovyo ni tabia na kuweka akiba nayo ni tabia. Ukichunguza zipo tabia nyingi ambazo tunazo.
Unaona mpaka hapo zipo tabia zinazokuangusha na zingine zinakusaidia kufikia mafanikio yako. Hivyo hapa unatakiwa ujue kabisa kwamba kumbe tabia ni lazima kuzijua ili kubadilisha maisha yako na kuwa ya mafanikio. Unapojenga tabia chanya zaidi unajitengenezea mazingira ya kufanikiwa.
4. Tafakari maisha yako.
Badala ya kuwa ‘busy’ muda wote katika kutwa nzima, kuna wakati unatakiwa utenge muda wako kwa ajili ya kutafakari siku yako imekwenda vipi. Ni muhimu kujua ni kitu gani umekifanya. Hapa ni lazima uwe na siku inayokupa faida kila siku.
Ni rahisi kujikuta kutwa nzima ukiwa uko ‘busy’ sana na shughuli hii mara ile nakushindwa kutambua kama kweli unaenda mbele au unarudi nyuma. Lakini kama utajenga tabia ya kutafakari nini ulichokifanya kutwa nzima na kimekusaidiaje itakusaidia kuelewa ni kipi uboreshe.
Unapotafakari juu ya maisha yako itakusaidia kuweza kujua ni maeneo yapi ambayo unatakiwa kuyaboresha zaidi na zaidi na mwisho wa siku utajikuta unazidi kuchanja mbuga kuelekea kwenye mafanikio yako. Anza mara moja kutafakari juu ya maisha yako bila kuchelewa.
5. Tengeneza utamaduni wa kufurahia mafanikio yako.
Hatua ndogo ndogo unazozipiga kila siku inabidi uziweke wazi kwa kuziona na kisha baada ya hapo anza kusherekea hayo mafanikio ako. Jenga utamaduni wa kuweza kusherekea mafanikio yako. haina maana umefanikiwa halafu unashindwa kujipongeza hata wewe mwenyewe.
Unapokuwa unafurahia na kusherekea mafanikio yako inakusaidia kukupa nguvu na hamasa tena na tena ya kuweza kusonga mbele na kufanikiwa kwa hicho unachokifanya.   Watu wenye mafanikio wanafurahia mafanikio yao hata kama ni kidogo.
Tunakutakia siku njema na kila la kheri, endelea kutembelea DIRA YA MAFANIKIO kujifunza na kuhamasika.
Ni wako rafiki katika mafanikio,
IMANI NGWANGWALU,
0713 04 80 35,




No comments :

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.