Sep 18, 2018
Faida Ya Kutoa Yale Mazuri Kwa wengine Ni haya.
Siku zote katika maisha yako kabla hujatenda kitu
chochote, kabla hujasema kitu chochote, jiulize kitu unachotaka kutenda au kitu
unachotaka kusema je, kitaleta matokeo chanya kwako au hata kwa wengine?
Sio kwa sababu unayo nafasi nzuri ya kutenda au kusema
hiyo ikawa na maana kwako ufanye au useme tu hata mambo yanayoumiza wengine.
Unatakiwa kuwa makini na kuzingatia ni nini matokea ya kile ambacho unakwenda
kutenda au kukizungumza. Kwani kila wakati tunakumbushwa ya kwamba ni heri
kufikiri kabla ya kutenda.
Nisisitiza
suala la kufikiri kabla ya kutenda kwa sababu wengi wetu hukurupuka katika
kutenda mambo fulani, na kufanya hivyo kumekuwa chanzo cha kutotimiza jambo
hilo. Hivyo kwa jambo lolote kabla ya kulitenda au kulisema ni heri kulitakari
mara dufu zaidi.
Pia kufikiri kabla ya kutenda ni muhimu kwa sababu ni
dhahiri wapo watu ambao moja kwa moja utawaumiza, kama utatenda au kusema
maneno hasi, hata kama hujui jinsi
unavyowaumiza. Pia uelewe wapo watu utakaowaponya kama utaamua kusema au
kutenda matendo chanya ambayo yana msaada mkubwa katika maisha yao kwa ujumla.
Kila wakati, unayo nafasi nzuri sana ya kutoa mazuri
katika dunia, ingawa uamuzi ni wako. Acha kutenda au kusema mara moja kile
kinachokujia kichwani mwako, Jipe muda wa kukifikiri kitu hicho na kujua ni
nini matokeo yake katika maisha yako na ya wengine.
Kuanzia leo jifunze kutoa yale mazuri katika hii dunia
jenga utamaduni wa kutoa yale matendo au maneno mazuri iwe sehemu ya utamaduni
wako. Ukifanya hivyo dunia itakupa mazuri pia na utafurahia maisha yako kutokana na mazuri unayoyatoa.
Simama imara katika kuhakikisha unalitenda hili vyema kila wakati. Simamia
katika ukweli, ili kutengeneza amani ya moyo wako na mioyo ya watu wengine.
Usiwe kichocheo katika kusababisha watu wengine wakose furaha, bali jitahidi
kuwa katika kusimamia ukweli na haki daima. Kumbuka sana TOA YALE MAZURI
KATIKA MAISHA YAKO, GIVE GOODNESS TO
LIFE, ukifanikisha hili furaha na mafanikio vitakuwa upande wako.
Mwisho
tuweke nukta kwa kusema ya kwamba wewe ni matokeo ya mafanikio ya watu wengine
kama utaamua kuwa mkweli kwa kutakari kabla ya kusema na kutenda utafanya
vichocheo vya mafanikio kwa watu wengine.
Imeandaliwa
na mtandao huu wa dira ya mafanikio,
Imani
Ngwangwalu & Benson Chonya,
Sep 12, 2018
Nguvu Kubwa Tatu Za Kukusaidia Kufanikiwa.
Sijui
sana kama unajua una nguvu kubwa sana za kuweza kukusaidia kufanikisha jambo
lolote unalo lihitaji katika maisha yako. Nguvu hizo unazo, bila kujali unajua
kivipi au hujui lakini nguvu hizo zipo ndani mwako.
Ushahidi
wa kutosha upo, unaonyesha nguvu hizo zipo, ndio maana, chochote unachokitaka
ukiamua na ukapanga kweli, unaweza kukipata au maisha yako yapo hivyo yalivyo
kutokana uwezo ama matumizi ya nguvu zako.
Mpaka
hapa naona unashangaa na unajiuliza sasa nguvu zangu nitazijuaje au zipo kwenye
nini? Sikiliza nguvu zako kubwa ulizonazo, zipo kwenye mambo makubwa matatu
mabao yapo ndani ya uwezo wako mwenyewe.
1. Mawazo uliyonayo.
Nguvu
zako nyingi ulizonazo na ambazo zinaweza kufanya kitu chochote ukitakacho,
zinaanza kwenye mawazo yako kwanza. Mawazo yako
yana nguvu na kuumba kitu chochote unachokitaka na kikaonekana kwa nje.
Hebu
jiulize ni kitu gani ambacho hakijianzia kwenye mawazo? Kila kitu unachokiaona
kipo duniani kwanza ni matokeo ya mawazo. Unapoana gari au majumba makubwa hayo ni mawazo ya watu. Ukizingatia
matumizi ya mawazo vizuri, utafanikiwa sana.
2. Maamuzi uliyonayo.
Nguvu
nyingine kubwa uliyonayo ndani mwako ambayo ukiitumia vizuri itakupa chochote
ukitakacho ni maamuzi uliyonayo. Maamuzi yako ni ya muhimu sana katika kufikia
mafanikio yako unayoyataka.
Angalia
ni kitu gani unachokipata bila kuwa na maamuzi, utaona karibu kila kitu baada
ya kuwa kwenye mawazo yako ni lazima kwanza ukifanyie maamuzi ambayo
yatakupelekea ufanye kitu kile. Hakuna mafanikio utakayapata bila kuamua.
3. Hatua ulizonazo.
Umeona
mawazo ulionayo na maamuzi uliyonayo ni mojawapo ya nguvu kubwa uzilizona ndani
mwako za kimafanikio. Lakini hata hivyo nguvu hizo haziwezi kufanikiwa bila
kuchukua hatua. Inabidi ifike mahali uamue kuchukua hatua ili kufanikiwa.
Hatua
unazozichukua ndizo zitakazokufanya uweze kufanikiwa. Hata uwe na mawazo mazuri
na maamuzi mazuri vipi lakini itakulazimu uweze kuchukua hatua ili hatua hizo
zikuletee uhalisia wa kile unachokitaka kwenye maisha yako.
Kumbuka,
mawazo uliyonayo, uamuzi unaouchukua na hatua unazozichukua ni moja kati ya
nguvu kubwa sana za kimafanikio ambazo unatakiwa uzitumie ili uweze kufanikiwa.
Kwa kumiliki kwako nguvu hizo utakuwa na nafasi kubwa sana ya kuweza
kufanikiwa.
Fanyia kazi haya na chukua
hatua kuhakikisha ndoto zako zinatumia.
Tunakutakia kila la kheri na
endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku kujifunza maisha na
mafanikio.
Pia
rafiki, kama unapenda kujifunza zaidi kuhusu mafanikio, fursa za mafanikio
zinapopatikana, ajira pamoja na uwekezaji, karibu kwenye kundi la WHATS APP LA MAFANIKIO, kujiunga tuma
neno THE UNIVERSITY OF WINNER’S
kwenda 0713 048 035, hapo utapata
utaratibu mzima wa kujiunga.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO
YAIMARIKE,
Ni
wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na
mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713
048 035,
Email; dirayamafanikio@gmail.com
.
Sep 11, 2018
Njia Nne (4) Za Kuboresha Maisha Yako Sasa.
Kwa
jinsi unavyobadili mtazamo wako, ndivyo unavyozidi kujikuta ukibadilisha na
maisha yako pia. Maisha yako ni lazima yabadilike kama una badili mtazamo wako
kila wakati, hilo halina ubishi.
Kuna
wakati katika maisha tunajirudisha nyuma sana kwa sababu ya kuwa na mitazamo
finyu, mitazamo hasi ambayo haitusaidii. Ili kufanya maisha yako kuwa bora na
ya mafanikio unalazimika kubadili mtazamo wako.
Katika
makala haya, tutakupa njia muhimu ambazo ukizitumia, kwanza zitakusaidia
kubadili mtazamo wako , na pia si hivyo tu zitakusaidia kubadili na kuboresha
maisha yako;-
1. Fanya mambo yako kwa utofauti.
Mbinu
bora ya kuboresha maisha yako sasa ni kufanya mambo yako kwa utofauti. Kama ni
kazi fulani ifanye kwa utofauti. Kama ni kutembelea eneo fulani ulilolizoea
hebu libadilishe na kwenda sehemu nyingine.
Hali
zote zile za mazoea ambazo umekuwa ukiziishi naomba uzibadilishe na kuzifanya
kwa utofauti. Ukifanya hivyo utashangaa kuona maisha yako yakibadilika na kuwa
ya tofauti na mafanikio.
Badili maisha yako kila siku. |
2. Jitoe kwa ajili ya wengine.
Unaweza
pia kuboresha maisha yako kwa kuamua kujitoa kwa ajili ya wengine. Unapojitoa kwa
wengine hapa unamaansha usitegemee kupata kitu chochote kutoka kwao. Wewe jitoe
kwa ajili yao.
Ni
njia au mbinu ambayo itakuimarisha na kukufanya hata kazi zako mwenyewe utakuwa
unazifanya kwa ukamilifu mkubwa sana. Ukikubali kujitoa basi utakuwa umeweza
kuboresha maisha yako kwa sehemu kubwa sana.
3. Fanya mazoezi.
Upe
mwili wako mazoezi. Unyumbue mwili wako huko na huko. Ni njia nzuri ya kuweza
kuipa akili yako afya ya mwili, hali ambayo itakupelekea wewe uweze kufika
mahali ukaboresha maisha yako kiafya pia.
Si
rahisi sana kwa mtu ambaye anafanya mazoezi karibu kila siku kuweza kushambuliwa
na vitu kama magonjwa ya hapa na pale. Unaweza ukaendelea kuboresha maisha yako
kwa njia hii kwa utofati.
4. Furahi na marafiki zako.
Maisha
mazuri na maisha yalioyoboreshwa ni pamoja na kuwa na rafiki zako, mkafurahi
pamoja. Kama kuna rafiki wa zamani ambaye hujawasiliana nae muda mrefu mtafute
na uongee nae.
Unapokuw
na marafiki watakusaidia kuweza kubadilisha maisha yako kwa sehemu kubwa
kutokana na mwazo yao ambayo wanakuwa wanakupa. Hivyo, marafiki pia wanawez
kuboresha maisha yako.
Ukumbuke
kuwa kufanya kazi kwa utofauti, kujitoa kwa wengine, kufanya mazoezi na
kufurahia maisha na marafiki ni moja ya mambo machache ambayo yanaweza kukufanya
ukaboresha maisha yako.
Fanyia
kazi hayo na endelea kujifunza kupitia dirayamafnikio.blogspot.com kila siku na
maisha yako yatabadilika.
Ni
wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na mjasiriamali,
Blog, dirayamafanikio.blogspot.com
Mawasiliano; +255 713 048 035,
Email; dirayamafanikio@gmail.com
Sep 4, 2018
Hiki Ndicho Kitu Kiinachoongeza Thamani Yako Sana.
Kwa kawaida ipo hivi, ili uweze kutengeneza mafanikio ni lazima uweze kutoa thamani kwa uhakika. Kila mtu atakapoangalia kazi yako au kile unachokifanya ni lazima aone ubora na utofauti mkubwa juu ya kitu hicho ukifanyacho.
Inawezekana
ukawa unajua thamani ni hali ya kuwa katika ubora, hadi kuwafanya wengine
wakutamani wewe au watamani huduma yako unayoitoa. Kitu cha kujiuliza je, unajua thamani ya kitu
chochote inatengenezwa na nini?
Hapa
kwenye swali hilo juu ndipo wengi wanaanza kushindwa, wanakuwa ni watu kweli ambao
wanataka thamani kubwa katika maisha yao, lakini kwa bahati mbaya hawajui hiyo
thamani ambayo itawapa mafanikio inapatikana vipi na wapi.
Thamani
yoyote unayoitafuta kwenye maisha yako uelewe, imejificha kwenye muda. Upo ulazima
wa wewe kutumia muda wa kutosha ili kutengeneza thamani yako. Kama unakimbilia
kutengeneza thamani ndani ya muda mfupi, huo ni uongo.
Waangalie
watu ambao wana thamani kubwa sana na kwa maana hiyo pia watu hao wana
mafanikio makubwa. Watu hao ukiwaangalia walitumia muda mwingi sana katika
kutengeneza thamani hiyo ambayo imewapa mafanikio hayo mafanikio makubwa.
Ukiona
mtu thamani yake inaonekana ni kubwa lakini imepatikana kwa muda mfupi,
nikwambie tu thamani hiyo ni ya muda mfupi na wakati utafika thamani hiyo
itatoka na yale mafanikio yataporomoka na ushindwe kuamini ni kitu gani
kilitokea.
Kwa hiyo
kama unaona maisha yako yameshuka au maisha yako hayasogei kama vile utakavyo
wewe, amua kupandisha thamani yako. Kwa bahati mbaya sana thamani yako hiyo
haiji kwa bahati mbaya bali ni kwa wewe kujituma na kujipa muda.
Kweli
ukidhamiria kuongeza thamani yako na kuwa mtu wa tofauti hilo linawezekana. Anza
leo kubadilisha thamani yako kwa kusoma vitabu sana vya mafanikio na hilo litaleta
mabadiliko makubwa sana ya maisha yako na kwa kiasi kikubwa.
Ukumbuke
thamani uliyonayo inabadili maisha yako sana. Hakuna ambaye anashindwa kwenye maisha au
atashindwa kupata pesa kama mtu huyo hana thamani kubwa ndani yake. Mafanikio ni
lazima kama ndani yako una thamani ya kutosha.
Usikubaki
kuishi kizembe, kila wakati jaribu kujiuliza ni kitu gani nifanye ili niongeze
thamani yangu na kuwa bora na bora. Kwa kukijua kitu hicho na kukifanya, basi
unakuwa upo kwenye wakati sahihi wa kufanikiwa kwako.
Kitu
kinachoongeza thamani yako zaidi ni matumizi ya muda. Weka hili akilini na
fanyia kazi kila wakati. Kwa kufanya hivyo hapo utafanikiwa na kutengeneza
mafanikio makubwa kwenye maisha yako kwa ujumla.
Kama
unataka mafanikio ya muda mrefu na wewe hakikisha unatengeneza au ndani mwako
una thamani ya muda mrefu sana. Thamani hiyo kama nilivyosema haipatikani hivi
hivi tu, ipo kwenye muda, ni lazima kujipa muda wa kutengeneza thamani hiyo.
Fanyia kazi haya na chukua
hatua kuhakikisha ndoto zako zinatimia.
Tunakutakia kila la kheri na
endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku kujifunza maisha na
mafanikio.
Pia
rafiki, kama unapenda kujifunza zaidi kuhusu mafanikio, karibu kwenye kundi la WHATS APP LA MAFANIKIO, kujiunga tuma
neno THE UNIVERSITY OF WINNER’S
kwenda 0713 048 035, hapo utapata
utaratibu mzima wa kujiunga.
Kama
wewe ni mfugaji wa kuku na unahitaji vifaranga bora, waone DM POULTRY FARM PROJECT kwa huduma ya uhakika. Hawa ni wauzaji wa
vifaranga wa kuku aina ya KUROILER,
SASSO, KIENYEJI ASILIA na KUCHI. Kwa mahitaji ya vifaranga wasiliana nao
kwa 0767 048 035 au 0686 141097 na
wote mnakaribishwa.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO
YAIMARIKE,
Ni
wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na
mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035,
Email; dirayamafanikio@gmail.com
Sep 3, 2018
Mbinu Muhimu Itayokufanya Uondokane Na Msongo Wa Mawazo.
Msongo wa mawazo ni
ile hali ambayo humpata mtu kisha kumpelekea mtu huyo kuwa na mawazo mengi
kupita kiasi. Mawazo haya yanaweza kuwa chanzo chake mahusiano, kazi,elimu,
magonjwa, biashara, fedha na mengineyo mengi.
Pamoja
na kuweko kwa vyanzo hivyo au visababishi hivyo vya msongo wa mawazo inaelezwa
kuwa msongo wa mawazo mara nyingi husababishwa na mahusiano, usigune huo ndio
ukweli, pia leo sipo kwa ajili ya kuzungumzia msongo wa mawazo utakanao na
mahusiano bali nipo hapa kuzungumzia namna ambavyo utaweza kuondokana na msongo
wa mawazo.
Nataka
kuzungumzia namna ya kuondokana na msongo wa mawazo kwani athari ya kuwa na
msongo wa mawazo ni kubwa mno. Tumekuwa tukiwaona watu wakishindwa kufanya kazi
wazifanyazo kwa ufanisi eti tu kwa sababu watu hao wana msongo wa mawazo.
Lakini
athari iliyo kubwa kupita zote wapo baadhi ya watu ambao huchukua hata maamuzi
ya kujaribu kujiua kwa sababu tu mawazo waliyonayo yamewazidi akilini
mwao. Lakini athari nyingine ya msongo wa mawazo ni kwamba ni chanzo cha
magonjwa mbalimbali.
Swali
ambao huwa najiuliza hivi ni kwa nini watu hao hufikia uamuzi huo wa kutaka
kujiua? Hivi ni kweli watu hao hawajui namna ya kuweza kuondokana na hali hiyo
ya msongo wa mawazo? . Kwa majibu yangu ya haraka haraka nikagundua yawezekana
ni kweli watu wengi hawajui namna ya kuondokana na msongo wa mawazo.
Kwa kuwa hawajui basi naomba niwape
mbinu hii maridhawa ambayo itawafanya watu hao waweze kujifunza hapa namna ya
kuondokana na msongo wa mawazo kama ifuatavyo:
· Unatakiwa kutafuta majibu ya changamoto iliyokufanya uwe
katika msongo wa mawazo.
Msongo
wa mawazo sababu yake kubwa hutokana na changamoto fulani iliyokukabili katika eneo lako fulani. Hivyo kila wakati
usiwe ni mtu wa kunung'unika, au kuamua kuchukua uamuzi fulani ambao ni mbaya
utakaokufanya kuyagharimu maisha yako kwa namna moja ama nyingine, bali jifunze
kutafuta majibu chanya yatakayokufanya uondokane katika hali hiyo ya msongo wa mawazo.
Kutafuta
majawabu ya changamoto zinazomkabili mtu, humsadia mtu huyo kwa namna moja ama
nyingine kutengeneza amani ya moyo, na mtu anapokuwa na amani ya moyo huwa ni
mtu chanya kwa kuwa mara nyingi hujiwekeza katika mawazo mazuri yatakayomsadia
kufanya mambo yenye tija na si vinginevyo.
Mwisho
naomba nitamatishe kwa kusema mara zote epuka msongo wa mawazo kwa kuzingatia
njia hii ambayo nimeieleza hapa kwani msongo wa mawazo huwa una athari kubwa
sana katika maisha ya kila siku kimwili na kifkra pia.
Kwa
leo naomba niishie hapa tukutane tena panapo majaliwa,
Ndimi: Benson Chonya.
Sep 2, 2018
Hivi Ndivyo Unavyoweza Kuondokana Na Majuto Uliyonayo Na Kuishi Maisha Ya Amani Na Furaha.
Wengi wetu huwa tunajuta sana. Mara nyingi tunapokumbana na kushindwa kwetu au mambo yetu kukataa kwenda kama tulivyotarajia, huwa tunajuta sana. Nini yaweza kuwa hasa sababu ya kujuta kwako sana na pengine huweza kupelekea wewe mwenyewe kuanza kujiona kama hufai vile.
Kujuta huweza kujitokeza pale ambapo hukutenda itakiwavyo kwa kile
ulichokuwa ukikifanya. Kujuta sio kubaya kama ni kwa ajili ya kurekebisha
makosa. Kuyajua makosa hayo ina faida kwa maana kwamba sasa unaweza kubadilika
na kuwa tayari kwa ajili ya maendeleo au kufanya vizuri zaidi.
Huku ni kujuta kwenye kujenga na kwa hali hiyo hatupaswi kuita hali hii
kujuta. Kama tutajilaumu kwa kushindwa, bila kujali kama ni kosa letu au
hapana, hapo ndipo tunapoita kujuta. Kujuta siyo kule kujua kwamba, tumekosea
na pengine ni uzembe, lakini tukawa tayari kujifunza.
Kihoro cha mawazo kina uhusiano na mambo yaliyopita. Ili mawazo hayo yaweze
kudumu hayana budi kubaki ndani ya moyo wako. Kila siku unayoishi, yaani leo,
ndiyo siku yako kubwa ya kujisahihisha. Ukiruhusu mawazo yako yakutawale, basi
utakuwa umejilimbikizia kikwazo kikubwa dhidi ya maendeleo yako.
Kwa kadiri utakavyoendelea kujuta sana bila kujifunza kitu, ndivyo
utakavyojikuta maisha yako unazidi kuyaharibu. Hii inatokea kwa sababu unakuwa
hufanyi kitu kipya, unakuwa umeganda kwenye kujuta tu. Unawezaje kupambana na
majuto haya unayokutana nayo mara kwa mara katika maisha yako na ili
yasikuumize tena?
1. Kuwa na muda wa maamuzi.
Kufikia sasa utakuwa umeshajielewa wewe ni nani na unataka kuzoea nini
badala ya kile ulichokuwa umekizoea. Ukishajua unachokitaka fanya kile ambacho
unapaswa kufanya kama vile, kubadilisha imani. Njia yenye nguvu ni kuvifanya vitu
ambavyo una uwezo wa kuvifanya. Unachokifanya leo kinaathiri maisha yako ya
baadae na kitakusaidia usijute baadae.
2. Jiulize sana maswali.
Kile ukifanyacho ni kupambana kwa ajili ya kubadili unavyojisikia. Unataka
kujisikia vizuri kwa nini uhisi majuto ndani yako na kufadhaika. Kama una
utashi wa kweli wa kutaka kuondokana na kujilaumu, lazima upitie zoezi zima la
kujiuliza maswali mazito.
Hii ni aina mojawapo ya kubadili mwelekeo wa ubongo wako. Kwa yale yote
unayoyajua unaweza kuwa unayaalewa mambo pengine kimakosa. Endelea kujiuliza
maswali ili kuweza kugundua mambo ambayo ulikuwa hujayaona na ambayo
yanakufanya uumie na kujuta.
3. Badilisha picha katika mawazo
yako.
Mawazo kuhusu mwenendo wako mbaya au upumbavu wako husababishwa na picha
ambazo uliziunda ndani ya akili yako.
Unaendelea kujiadhibu, kwa kila wakati kwa kuziona taswira na
kukurudisha nyuma ulikotoka. Unavyozidi kukumbuka ya kale, ndivyo unavyozidi
kuleta majuto.
Una udhibiti juu ya yale tu yanayojionyesha kwenye fikira zako. Unaweza kufanya
hivyo kwa kupandikiza mawazo mapya na mazito juu ya yale ya zamani, ambayo
umeyagandisha kwenye ubongo wako. Inahitaji nidhamu na kujitoa mhanga, tena ni
jambo la maana ili kujiondoa kutokana na uozo uliopita.
4. Geuka na fanya mabadiliko.
Kama ulichokuwa umekifanya kilikuwa kibaya achana nacho. Badilisha
mwelekeo. Jipe ahadi mwenyewe kwamba hutarudia tena. Jisamehe kwa ujinga wako.
Kama umewakosea wengine au umewaumiza waombe msamaha, kisha songa mbele.
Fanya kazi na fanya vitu ambavyo vitakufanya ujisikie vizuri na kurudisha
kujiamini kulikokuwa kumepotea. Hujacheleweshwa kuanza upya wala usijali kuhusu
umri wako. Daima kuna kitu ambacho unaweza kukifanya ili kuyaweka maisha yako
na ya wengine sawa.
Kumbuka, ni lazima wote tuathiriwe na aina mbili za maumivu, maumivu ya
nidhamu na maumivu ya kujuta. Tofauti ni kwamba nidhamu ina uzito kidogo na
majuto yana uzito mkubwa. Hivyo, ndivyo unavyoweza kuondokana na majuto
uliyonayo na kuishi maisha ya amani na furaha.
Nakutakia mafanikio mema katika maisha yako, karibu sana na endelea
kutembelea mtandao huu wa DIRA YA MAFANIKIO kwa kujifunza mambo mazuri yatakayokuwa
yanakujia.
TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE.
Sep 1, 2018
Rafiki Sahihi wa Kukupa Mafanikio Ya Kweli Ni Huyu.
Mara nyingi marafiki wanaokuzunguka wanao mchango mkubwa sana wa kujenga au kubomoa kwa kile unachokifanya, hii inategemea na aina gani ya marafiki ulionao.
Pia
marafiki hao ulionao wewe ndiye unayemua na
kuchagua ni yupi rafiki sahihi wa kushikirikiana, naye na yupi si wa
kushirikiana naye? Nimesema hivyo kwa sababu wapo marafiki ambao wao kazi yao
kukatisha tamaa wengine, lakini wapo wengine wao kazi kutoa ushauri maridhawa
wakufanikiwa kwao na hawa ndio wa
kuwang`ang`ania.
Hivyo
mara nyingi katika maisha yako jifunze kuchagua marafiki sahihi wenye mchango sahihi
katika mambo unayoyafanya. Na miongoni mwa rafiki muhimu unayepaswa
kumng`ang`ania katika safari yako yote ya mafanikio hapa duniani ni yule rafiki
ambaye mara nyingi anakueleza ukweli pasipo kukuonea aibu.
Rafiki
huyu ndiye muhimu sana na kama unaye usimuache aende zake kwa sababu miongoni
mwa tabia walionazo watu wa aina hii ni kwamba wao husema ukweli daima. Hata
pale utakapokuwa umefanya jambo fulani ambalo wewe utaliona ni zuri, kwa kuwa
yeye ni mkweli basi yeye hata ona haya kukosoa ili uweze kufanya vizuri zaidi
na kwa ubora zaidi.
Mara
nyingi wengi wetu tunakosa aina hii ya marafiki kwa sababu huwa tunahisi labda
wanatuonea wivu kuendelea kusonga mbele kwa vitu ambavyo tunavifanya kumbe
ukweli haupo hivyo, bali marafiki hawa kucheza sehemu kubwa ya maisha yetu kwa
kuwa wao hutueleza ukweli ni jinsi gani tunakiwa kuishi na kufanya mambo yale
ya msingi.
Lakini
pia tunashauriwa ya kwamba kukaa na marafiki ambao wao kazi yao ni kusifia tu
ya kile tukifacho, marafiki wa aina hii hawafai
kwa sababu hawana mchango wowote ule wa sisi kuendelea kusonga mbele
bali kuturudisha nyuma hivyo hutuna budi kuwaepuka.
Marafiki
wa aina hii huwa na maneno mafupi lakini yasiyoleta mabadiliko yeyote
yale kwa kile ukifanyacho. Utawasikia wakisema aaah hongera sana, wengine
utawasikia wakipaza sauti aaah ndugu yangu umepasua na maneno mengine kama
hayo.
Maneno
kama hayo siyo mabaya sana hasa pale yapenyezapo maskioni mwetu kwani hufariji
sana mioyo yetu na kujihisi tupo sahihi kabisa .
Lakini
mimi nafahamu hukuzaliwa kuja hapa duniani kufarijiwa moyo na maneno ya watu pekee bali ulikuja hapa
duniani kwa leo la kutimiza kusudio lako maaalum.
Hivyo
ili uweze kutimiza kusudio hilo maalumu hauhitaji watu wenye kuufariji moyo
wako tu pekee, bali unahitaji watu sahihi wenye kukufariji pamoja na kukupa
ushauri wa kiutendaji kwa kile unachokifanya ili uweze kukufanya kwa ubora
zaidi.
Lakini
kabla sijaweka nukta kwa siku ya leo
nikuombe kitu kimoja kikubwa chukua walau dakika kadhaa kisha tafakari
hivi katika maisha yako unazungukwa na marafiki wangapi wasemao ukweli juu ya maisha yako ?
Mara
baada ya kupata jawabu la swali hilo usiache kichwa chako kipoe bali zama tena
katika dimbwi la fikra zako jiulize tena hivi kama hauna aina hii ya marafiki
je, hatua gani utakazotumia kuwapata marafiki hawa?
Pia
swali la mwisho je, na wale marafiki wasiokuwa na mchango wowote katika maisha
yako je, utawachukulia hatua gani?
Endapo
Ukipata majawabu ya sahihi ya maswali hayo ni imani yangu kubwa utakuwa katika
eneo sahihi ya kutengeneza njia ikupasayo kuyafikia mafaniko unayoyahitaji
kwani utachagua ni mtu wa kuchagua marafiki sahihi kila nyakati.
Asante
sana kwa kusoma makala haya, sina cha kukulipa zaidi ya kusema asante sana na
nenda kayafanyie kazi yale yote niliyokueleza.
Ndimi: Benson Chonya
Subscribe to:
Posts
(
Atom
)