google-site-verification: googleabbfd1327a3af7a3.html

DIRA YA MAFANIKIO

Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Kujifunza zaidi juu ya maisha na mafanikio, nakualika kwenye kundi la whats app kujifunza kwa kina. Tututumie ujumbe kwa njia ya whats app kwenda 0687449428 kupata utaratibu wa kujiunga.

Jun 30, 2017

Wekeza Kwa Shilingi Laki Moja, Upate Zaidi Ya Milioni Moja Na Nusu Ndani Ya Siku 90.

No comments :
Na Boniface L. Pwele, Songea.
Leo nataka tuangalie kilimo cha matikiti kibiashara kwa mtaji wa shilingi laki moja tu(100,000/=). Nimeona niandae hili somo kwa kuwa watu wengi hulalamika kuhusu mtaji lakini kwa asilimia kubwa watu humililiki zaidi ya hii pesa laki moja, lakini bado utamkuta analalamika kuhusu mtaji wa kuanzia.
Leo tutaangalia mchanganuo wa shilingi laki moja ili ikuletee milioni moja na nusu(1,500,000/=) kwa makadilio ya chini kabisa hayo ni baada ya siku 75-90 na unaweza pata zaidi ya hapo, ikiwa utaweka juhudi nyingi katika kilimo ambacho unaenda kufanya.
Hapa tutaangalia mchanganuo kwa kutumia mbegu bora ya matikiti aina ya PATO F1. Na eneo linalohitajika ni chini ya robo ekari (yaani nusu ya robo ekari ) ila katika laki moja sijaweka gharama ya shamba ambayo ni nusu ya robo ekari yaani mita 500 za mraba.
Maandalizi ya shamba.
Andaa shamba lenye ukubwa wa mita 500 za mraba( 50m×10m).
Baada ya kuliandaa shamba lako hakikisha una mbolea ya kuku ya kutosha mashimo 500 tu na uhakikishe hiyo mbolea imeoza vya kutosha.
Chimba hayo mashimo 500, chukua mbolea ya kuku ichanganye vizuri na udongo. Kisha  piga dawa aina ya Colt kwenye mashimo ikae walau siku 14.
Baada ya siku ya 14 unaweza panda mbegu zako.
Mbegu ya PATO F1 50g ambayo unaweza kuipata kwa sh 35,000/= tu inatosha kupanda hilo eneo la mita 500 za mraba.
Panda kwa nafasi nzuri, mstari hadi mstari iwe mita mbili na shimo hadi shimo iwe sentimita 50( yaani mita 2 kwa sm 50)
Panda mbegu mbili mbili lakini hakikisha huziweki sehemu moja humo shimoni.
Baada ya kuota mmea ukisha fikisha majani matatu punguza mche mmoja kwa kuukata na siyo kuung'oa.

Matunzo shambani.
Siku ya 0-15 (Planting and germinating) mbegu itakuwa tayari  isha ota na inakaribia kutambaa.
Mmea wa matikiti hupendwa sana na wadudu, hivyo mara baada ya kuota ukiwa na majani angalau matatu tumia dawa ya wadudu aina Prosper 720EC (Profenofos 600g/L + Cypermethrin 120,000/=), ikichanganywa na Agrigrow starter NPK 14:28:18, hii inafanya mmea kuwa na mizizi imara na kuufanya mmea kuweza kufyonza virutubisho vizuri kutoka kwenye udongo,ikichanganywa na Agrilax .
Na hapo uwe na mbolea ya Yara Mila Winner kilo tano ambayo utaweka gramu tano (kisoda kimoja) kwa kila mche
Siku ya 16-25( Vegetative/Trailing)  hapo tikiti litaanza kutambaa hakikisha una Agrigrow vegetative NPK 30:10:10, hii itakuza mmea kwa haraka na kuongeza matawi, dawa ya wadudu Avirmec.
Siku ya 25-40 (Flowering) hapo mmea utaanza kutoa maua,hakikisha una mbolea ya Yara Mila Nitrabor ambayo utaweka gram 10 kwa mmea mmoja, dawa ya wadudu Colt, Agrigrow flowering and Fruiting NPK 15:5:35 hii itazalisha maua kwa wingi na kufanya yasipukutike.
Kuwa makini kwenye upigaji wa dawa wakati wa kipindi hiki, inakubidi upulizie dawa asubuhi sana au jioni sana,kwa maana hii hatua ndipo kunakuwa na wadudu wa muhimu shambani kama nyuki,ambaye ni muhimu sana kwa zao hili la matikiti,ndiyo maana unashauriwa kama unalima zaidi hata kama ni ekari moja unaweza weka mzinga wa nyuki shambani kwako ili wasaidie katika uchavushaji.
Siku 41-60-90 (Fruiting) hapo hapo mmea utakuwa umeanza kubeba matunda.
Hatua hii mmea unatakiwa upate maji ya kutosha lakini inatakiwa upunguze kiasi cha maji siku kumi kabla ya kuvuna kulifanya tikiti liweze kutengeneza sukari ya kutosha.
Mavuno.
Kwa eneo la mita 500 mita za mraba (Yaani mita 50 kwa mita 10) utakuwa na miche 1000 kwenye eneo la mita za mraba 500. Kwa kuwa kila shimo itakuwa ni miche miwili. Kumbuka nilikuambia zikiota inabidi upunguze mche mmoja mmoja.
Hivyo katika eneo lako utakuwa na miche 500. Na kwa matunzo mazuri mche mmoja huweza kufikisha hadi matunda matatu. Ila mimi nakupigia kwa hesabu ya tunda moja kwa mche.
Na hilo tunda litakuwa ni kubwa sana kuanzia kilo kumi hadi 15. Kwa matunda 500 na tunda moja kwa kuwa ni kubwa unaliuza kwa bei ya jumla sh 3000/=Matunda 500×3000= 1,500,000/=(Milioni moja na nusu)
Kama utayauza mwenyewe reja reja utayauza kwa sh 5000 hadi 7000 hadi 10,000 kwa tunda moja. Hivyo ukiyauza kwa sh 5000 utaweza kupata 5000×500=2,500,000/=Kumbuka hiyo ni shilingi laki moja imezalisha pesa hiyo ndani ya miezi mitatu (siku 90).
Sasa amua kuendelea kutunza pesa benki ambako makato yanaendelea au uwekeze baada ya miezi mitatu uweze kupata hizo fedha.
Nimeandaa hili somo kukupa mwanga wewe ambaye unatamani kulima lakini unasema huna mtaji na wakati una pesa zaidi ya hii niliyo itaja hapo juu.
Lakini ikumbukwe hyo laki moja sijaweka gharama sijui ya Kukodi hako kakipande ka shamba,kulima unaweza lima mwenyewe kabisa.
Na usiseme sina pesa ya kununua mafuta kwa ajiri ya kumwagilia miche mia tano unaweza chota maji kabisa kwenye ndoo na ukaimwagilia miche yote.
Gharama ya vitu vyote nilivo vitaja hapo juu
Mbegu PATO F1 50g 35,000/=
Agrigrow starter NPK 14:28:18 500g 5000/=
Agrigrow Vegetative NPK 30:10:10 500g 5000/=
Agrigrow flowering and fruiting NPK 15:5:35 500g 5000/=
Yara mila Winner 5kg 10,000/=
Yara Mila Nitrabor 5kg 10000/=
©Dawa za wadudu
Prosper 250mls 9,000/=
Colt 250mls 8000/=
Avirmec 50mls 4000/=
Agrilax 500g 9000/=
Mbolea ya kuku (Omba kwa mtu anayefuga kuku)
Bei za mbolea hizo za Yara inategemeana na wapi ulipo maana unaweza pata chini ya hyo bei.
Endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kwa ajili ya kujifunza na kuhamasika kila siku.
Wako mtaalamu wa kilimo, Boniface L Pwele,  bwana shamba nipo kwenye kampuni ya Agrichem Africa Tz Ltd. Kwa msaada juu ya ushauri kuhusu kilimo tuwasialiane kwa 0762 567 628 au nitumie e-mail kwenda blugahno95@gmail.com.



Jun 29, 2017

Kile Unachokiweka Kwenye Akili Yako, Ndicho Hicho Kinachokufanya Ufanikiwe Au Ushindwe.

No comments :
Kile unachokiweka ndani yako, ndicho hicho unachokitoa nje. Kama unaweka au unajirisha furaha, basi maisha yako yakatakuwa ya furaha. Kama unaingiza ndani yako hasira, basi utatoa hasira, kama pia unaweka ndani yako mafanikio, utayapata.
Jiulize, kuna wakati unakuwa na siku mbaya, siku ambayo hujisikii kufanya kitu kabisa, lakini hata hivyo ukiangalia nyuma au siku moja kabla kuna mambo ambayo uliyoyaweka akili mwako ndio yaliyokufikisha hapo ulipo.
Hata unapoona wengine wanafuraha, wanafamafanikio ni lazima ujue kuna kitu ambacho walichowekeza ndani yao na kikawapa furaha au mafanikio hayo ambayo unayaona kwa sehemu kubwa kwa nje.
Kitu unachotakiwa kuelewa, mawazo yako kila wakati yanaongozwa na hisia zako. Na hisia zako pia zinaongoza hatua unazotakiwa kuchukua, hatua hizo zinapelekea kukupa matokeo na mwisho wa siku matokeo hayo yanakutengenezea mfumo wa maisha uliokamili.

Weka mambo sahihi kwenye akili yako, ili ufanikiwe.
Kitu unachotakiwa kukumbuka, mawazo yako hayo, hayaji kwa bahati mbaya, bali yanatokana na vitu ambavyo unaviingiza akilini mwako mara kwa mara. Kwa vitu hivyo unavyoingiza ndivyo vinavyokupa mawazo hayo.
Ukijichunguza vizuri, angalia uhusiano wa taarifa unazoziweka kwenye akili yako na mtazamo wako juu ya maisha. Hapa sina shaka, utaona ni vitu vinavyofanana. Mtazamo wako ni lazima utaendana tu na yale mawazo yako.
Huwezi ukawa unaweka kwenye akili yako umbea umbea au mambo ya hovyo, halafu ukategemea kuwa na ubunifu au ukatengeneza maisha ya kimafanikio sana, hapo uwe na uhakika sana utaishia hapo hapo.
Wewe ni matokeo ya unavyofikiri. Hupendi hali ya maisha uliyonayo, hupendi sana hapo ulipo, badili sana vitu unavyoingiza akili mwako. Ukibadili vitu hivyo,hata vile unavyovitoa navyo vitakuwa na utofauti.
Kuwa na furaha, mafanikio au kuwa mtu wa hasira hasira, ni vitu ambavyo unatengeza mwenyewe na sio suala la muujiza wowote. Chunga sana kile unachokiingiza ndani ya akili yako, kumbuka hicho ndicho utakachokitoa kwa baadae.
Kila la kheri katika kufikia mafanikio makubwa, endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku.
Ni wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na mjasiriamali,
Blog, dirayamafanikio.blogspot.com
Mawasiliano; , +255 713 048 035,
Email; dirayamafanikio@gmail.com


Jun 28, 2017

Sio Kila Mtu Anafaa Kupewa Kitu Hiki Cha Kimafanikio…

No comments :
Sio kila mfuko unafaa kuwekwa pesa, unaweza ukaweka pesa kila mfuko mwisho wa siku ukakuta katika mfuko huo hakuna kitu.  Hivyo jitahidi kuwa na mfuko sahihi kwa ajili ya kuwekwa fedha.
Mwenye utashi wa kawaida anaweza asielewe usemi huu unamaanisha nini, ila mfuko ambao ninauzungumzia ni mazingira yako yote ambayo yanakuzunguka kwa namna moja ama nyingine.
Mazingira haya ni mkusanyiko wa vitu vyote vilivyomo ndani yake ikiwemo na mwanadamu mwenyewe. Na mwanadamu huyu ndiye mwenye uwezo wa kufanya mazingira hayo yaweze kuwa bora au mazingira hayo kwa namna moja ama nyingine.
Sio kila mfuko unafaa kuwekwa pesa. Katika safari yako ya kuelekea mafanikio makubwa, si kila mtu anafaa kumwambia jambo ambalo unalitaka kulifanya. Nasema hivi kwa sababu wengi wetu tumekuwa hatuwashirikishi watu sahihi katika mambo ambayo tunatamani kufanya, mwisho wa siku tumekuwa watu ambao maisha hayo tunayona machungu kama alovera.

Sio kila mtu anafaa kuambiwa kila kitu.
Hivyo kwa kila jambo ambalo unalifanya ili uweze kuwa bora na kufanikiwa zaidi, unachotakiwa kufanya ni kutafuta watu sahihi kwa kile ambacho unakifanya au kwa kile ambacho unataka kukifanya. Ukiwa na upele hakikisha unamtafuta mtu mwenye kucha, kwani endapo utamtafuta mtu ambaye hana kucha ni sawa ni kutwanga maji katika kinu.
Kama unataka kufanya biashara ya kuuza mchicha usiende kuomba ushauri kwa muuza mkaa kwani hatakuwa na ushauri wa kutosha kuhusu biashara ya mchicha zaidi atakupa maoni binafsi kwa kile ambacho anakiona kwa wafanyabiashara wa mchicha. Na mwisho wa siku atakwambia biashara hii haifai. Hivyo kwa kila chochote unachotaka kufanya hakikisha unafuta mtu ambaye anakifahamu kitu hicho kwa undani zaidi.
Hata wewe ndugu yangu mwenye siri ndani ya moyo wako, epuka kumwambia kila mtu hiyo siri yako kwani wapo  wengine katika dunia hii, wapo kwa ajili ya kusambaza siri za wengine. Hivyo jitahidi sana wewe mwenye siri nzito ndani ya nafsi yako, epuka kuweka pesa kila mfuko kwani mifuko mingine ni mapambo.
Pia kama wewe ni kiongozi wa serikali au kampuni binafsi, nawe nakwambia sio kila mfuko unafaa kuwekwa pesa. Kama unataka kufanya uchaguzi wa mtu fulani ambaye anafaa kusimamia ofisi yako, hakikisha unafanya uchunguzi sahihi kabla kumchagua mtu fulani. Kufanya hivi kutakusaidia kwa namna moja ama nyingine kuja kujutia maamuzi yako.
Mwisho ninamini umenielewa vyama ya kwamba si kila mfuko unafaa kuwekwa pesa.
Ndimi Afisa mipango wa mafanikio, Benson chonya,
0757 90 99 42,                                  
bensonchonya23@gmail.com

Jun 27, 2017

MAFANIKIO TALK; Siri Sita Za Kuanzisha Biashara Yenye Mafanikio.

No comments :
U hali gani mpenzi msomaji wetu wa mtandao huu wa dira ya mafanikio,  tukualike kwa mara nyingine katika kipindi hiki cha mafanikio talk ambacho hukujia kila siku ya jumanne, ambapo siku ya leo tupo na ndugu yetu  SHABANI SAIDI kutokea pale Dodoma ambapo atukumbusha mambo ya muhimu ya kuzingatia  katika biashara.
Shabani saidi anasema ya kwamba neno biashara lina maana kuu mbili ambazo ni kitendo cha kubadilishana bidhaa kwa bidhaa au ni kitendo cha kubadilishana bidhaa na fedha. Lakini anakwenda mbali zaidi na kusema ya kwamba katika biashara yeyote ambayo unaifanya ni lazima uweze kuwa na lengo la biashara hii ndiyo siri ya kufika mbali zaidi.
Ambapo alieleza ya kwamba katika biashara lengo kubwa ni kupata wateja zaidi, na katika hili wengi wamekuwa hawafahamu, wamekuwa wakizani ya kwamba lengo la kufanikiwa katika biashara ni kupata fedha pekee, lakini ukweli ni kwamba ukiwa na lengo hilo pekee utakuwa unakosea sana.
Kwani katika biashara ni lazima uweze kuwa mbunifu kila wakati, na ukiwa mbunifu kutakuwa na ongezeko la wateja na ongezeko la wateja hilo ndilo litalokufanya uweze kupata fedha, na fedha hizo zitakufanya uweze kuwa bora katika kukuza biashara yako.
Zifuatazo Ndizo Siri Sita Za Kuanzisha  Biashara Yenye Mafanikio.
1.    Kuwa na wazo bora la biashara.
Kuwa na wazo bora la biashara unayotaka kuifanya ndiyo msingi mkubwa wa kuweza kufanikiwa katika biashara uifanyayo au ambayo unataka kuifanya. Kuchagua wazo bora la biashara huenda sambamba na kuangalia mahitaji ya watu katika eneo husika.
Kwa mfano kama  unataka kuanzisha biashara fulani  ni lazima uangalie watu hao wanahitaji nini. Mara baada ya kujua wanahitaji nini ndipo na wewe utapata wazo la kufanya biashara husika. Hivyo wazo bora la biashara hutokea kwa watu wanaokuzunguka.

Zijue siri muhimu za kibiashara ili ukuze biashara yako.
2.    Kufanya uchunguzi wa eneo kwa ajili ya kufanya biashara.
Saidi anasema kabla ya kuanzisha biashara yeyete ile ni lazima uweze kutafuta eneo kwa ajili ya kufanyia biashara, na si eneo tu bali ni eneo sahihi kwa ajili ya kufanya biashara husika.
Kuchagua eneo sahihi la kufanyia biashara ni sawa na kuchagua mke bora wa kuoa, kwani endapo utakosea utajilaumu maisha yako yote. Hivyo kila wakati unachotakiwa kufanya ni kuhakikisha unachagua eneo lenye uhakika katika kufanya biashara yenye mashiko kwako.
3.    Kutafuta mtaji.
Mara baada ya kupata wazo bora la biashara, na mara baada ya kupata eneo bora kwa jaili ya kufanyia biashara jambo la tatu, unatakiwa kuanza kutafuta mtaji kwa ajili ya kukamilisha wazo ulilonalo.
Majibu ya namna ya kupata mtaji yatapatikana mara baada ya kupata wazo bora  la biashara, kwani mahali hapo unatakiwa kufanya uchunguzi yakinifu. Uchunguzi huo utakusaidia kuona kubuni pia namna ya kupata mtaji.
4.    Kuwa mbunifu.
Kwa kuwa katika dunia hii kila kitu kinafanana, hivyo ili uweze kujitofautisha na wengine unachotakiwa kufanya ni kuhakikisha unakuwa mbunifu ili uweze kufanikiwa zaidi katika biashara ambayo unaifanya, au biashara ambayo unatarajia kuifanya.
Unapokuwa mbunifu inakusaidia sana kujenga biashara yako na kuifanya biashara hiyo ikaonekana ya mafanikio kwa kupata wateja wengi. Popote pale utakapofanya ubunifu kwenye biashara yako uwe na uhakika utafanikiwa.
5.    Kujifunza kwa waliofanikiwa.
Mara baada ya kutafuta mtaji unachotakiwa kufanya ni kujifunza kutoka kwa watu ambao tayari wamekwisha fanikiwa katika biashara husika. Pia Saidi anasema ya kwamba endapo utajifunza kwa watu ambao wameshafanikiwa unachotakiwa kufanya ni kuhakikisha ni kuwa mbunifu zaidi ya yule ambao umejifunza kutoka kwao.
Lakini anazidi kusisitiza ya kwamba kujifunza ni lazima uweze kusoma vitu mbalimbali ambavyo vitakujenga katika kukuongezea maaarifa katika biashara unayotaka kuifanya. Kwa mfano unaweza ukatembelea mtandao huu wa dira ya mafanikio kila wakati kuna vitu vingi ambavyo vitakujenga sana, endapo utaamua kutenga muda wako kwa ajili ya kujifunza.
6.    Unahitaji uvumilivu.
Mara baada ya kuyajua hayo yote, jambo la mwisho ambalo unatakiwa kulifanya ni kuwa mvumilivu. Uvumilivu ndiyo siraha thabiti ya wewe kusonga mbele zaidi. Hivyo ili uweze kufanikiwa zaidi ni lazima uukumbuke ule usemi usemao mvumilivu hula mbivu.
Mpaka kufika hapo sina la ziada niwatakie wasomaji wenzangu kazi njema na mafanikio mema.
Kwa niaba ya uongozi wa blog hii ya dirayamafaniko.blogspot.com  nipende kumshukuru ndugu yangu Saidi kwa hicho alichotushirikisha siku ya leo.
Je ungependa na wewe uweze kutushirikisha somo lolote la mafanikio siku ya jumanne ijayo? Kama jibu ni ndiyo tuma neno MAFANIKIO TALK kwenda 0757909942 au tuma neno hilo hilo kwenda barua pepe yetu ambayo dirayamafanikio@gmail.com nasi tutakutafuta kwa ajili ya kufanya mahojiano mubashara.
Ndimi; afisa mipango Benson Chonya,



Jun 26, 2017

Hiki Hapa Ndicho Kinaongoza Mafanikio Yako.

No comments :
Kitu kinachoongoza matendo yako au hatua za namna fulani unazochukua kwenye maisha yako ni zile picha unazoweka kichwani mwako jinsi unavyotaka maisha yako yawe. Huwezi kuchukua hatua kubwa kama picha ulizonazo ni kidogo.
Ndio maana, kila wakati tunasisitiza ni muhimu sana kuwa na picha sahihi, maana picha hizo zitakuongoza pia kuchukua hatua sahihi. Hebu jiulize hapo, picha ulizoweka kichwani mwako kila wakati ni zipi?

Je, unaona nini kwenye maisha yako? Unaona kufanikiwa au unaona kushindwa? Kama unaona kufanikiwa, uwe na uhakika ni lazima utachukua hatua kubwa sana za kukufikisha kule unakotaka kufika.
Kila wakati, jitahidi kuongozwa na picha sahihi za mafanikio unayoyataka, ili picha hizo zikusaidie pia kuchukua hatua kubwa. Hatua anazochukua mtu kwenye maisha yake, ni ushahidi tosha kwa mtu huyo ana picha gani kichwani mwake.
Huhitaji kupiga ramli, huhitaji muujiza wowote ule. Ukitaka kujua mtu huyo anawaza nini juu ya maisha yake au atafika wapi kimaisha, angalia hatua anazochukua, hizo zitakuonyesha mtazamo na picha alizoweka kuhusu maisha yake.

Jun 25, 2017

Jitoe Kikamilifu Na Boresha Maisha Yako Kila Siku Hivi…

No comments :
Hitaji lako la kwanza ambalo unatakiwa ulijue katika safari yako ya mafanikio ni kwamba, unahitaji sana kujifunza, kukua na kuendelea yaani learn, grow and develop. Hili ndio hitaji lako la kwanza.
Kila wakati utahitaji ujue ni nini ufanye ili kuboresha maisha yako au hicho unachokifanya ili kuleta matokeo makubwa na unayoyataka kwenye maisha yako leo na hata kesho ili kikupe mafanikio
Unaweza ukaanza kuboresha chochote kile hata kwa kidogo sana. Unaweza ukaanza kuboresha tabia, biashara au hata maarifa yako kwa kujisomea zaidi na zaidi. Unapoboresha kila eneo unajikuta ndio unazidi kufanikiwa.
Kuendelea kujitoa kikamilifu na kuboresha maisha yako, kila siku jiulize, ni kwa namna gani unaweza ukafanya siku yako ikawa bora, ni namna gani unaweza kuboresha maisha yako yakawa bora kuliko jana?

Jifunze kila wakati kufikia mafanikio yako.
Kufanya mabadiliko na kubadilisha maisha yako, ni jambo ambalo linachukua muda (Becoming a master takes time). Unatakiwa kujifunza na kuchukua mazoezi tena na tena ili kuwa mbobezi kwa hicho unachokifanya.
Hakuna mpaka wa kuboresha maisha yako. Kila iitwapo leo, endelea kuboresha maisha  yako kwa jinsi unavyoweza. Ukiendelea kufanya hivyo, uwe na uhakika utafanikiwa tena kwa viwango vya juu.
Lakini mafanikio hayo ninayaongelea hapa hayawezi kuja  kama upepo wa kipunga au hayawezi kutokea usiku eti umelala na ukiamka ukawa tajiri, kumbuka inachukua muda hadi mafanikio yako kujengeka.
Kuwa mvumilivu katika kipindi ambacho ndoto zako zinapitia kwenye mchakato wa kuelekea kufanikiwa, vinginevyo hautaweza kufanikiwa kwa kitu chochote zaidi utaendelea kuacha ndoto zako nyingi zikiwa hewani.
Kujitoa kikamilifu na kuboresha maisha, fanya iwe ndio kanuni kuu ya maisha yako. Kwa wenzetu wa Japan kanuni hii wanaiita KAIZEN. Hio ikiwa na maana wao hujifunza sana katika hili la kuboresha maisha  yao kila siku.
Wajapan wakiwa tokea vijana wadogo wanajifunza juu ya hili na kuchukua hatua za kuboresha maisha yao na limejenga na kuwa utamaduni mzuri ambao kila mtu anaufuata kwenye maisha yao.
Hata wewe huhitaji kulala, angalia kila eneo la maisha yako ambalo haliko  sawa, amua kuliboresha kwa guvu zote na kwa bidii kila siku. Hivi ndivyo mafanikio makubwa yanavyojengwa.
Chukua hatua kwa kufanyia kazi haya uliyojifunza leo yawe sehemu ya maisha yako.
 Ni wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na mjasiriamali,
Blog, dirayamafanikio.blogspot.com
Mawasiliano; +255 713 048 035,
Email; dirayamafanikio@gmail.com



Jun 21, 2017

Epuka Kufanya Mambo Haya Katika maisha Yako.

No comments :
Kwa kawaida, yapo mambo manne tu ambayo yanafanya watu wengi kushindwa kufanikiwa, lakini si hivyo tu hayo ndiyo ndiyo mambo ambayo karibu maskini wote duniani wanayafanya sana maishani mwao. Na kwa kuendelea kufanya mambo hayo iwe kwa kujua au kutokujua ni chanzo kikubwa sana cha kuvuta umaskini kila iitwapo leo. Ikiwa hata wewe utaendelea kufanya mambo hayo sahau kutoka kwenye umaskini, hata ufanyaje utaendelea kubakia hapo.

1. Kulalamika. 

Watu wengi tumekuwa ni wazuri sana katika kona hii, hata kwa vitu ambavyo tunavimudu. Ulamikaji huu huenda sambamba na visingizio ambavyo kwa upande chanya havina mashiko kabisa,  Hata hivyo inasadikika ya kwamba walalamikaji wengi huwa ni ngumu kufanikiwa katika maisha yao, chunguza hilo kisha uone ukweli juu ya  jambo hili.

Endapo utachukua jukumu la kuwauliza watu wengi ni kwa nini wanakuwa hivyo walivyo leo, majibu yao unaweza sema labda dunia haina usawa, kumbe ukweli ni kwamba hakuna aliyewahi kependelewa katika dunia hii, kwa sababu katika sayari hii vitu vilivyopo vipo sawa kwa ajili ya watu wote. Hebu tazama masaa wote tuna masaa sawa. Sasa utafauti wetu unakuja wapi?
Ukweli ni kwamnba utofauti wetu unakuja pale ambapo tunakuja kuyatumia masaa haya, hapo ndipo yanapatengenezwa yale makundi mawili ya waliyonacho na wasionacho. Hivyo ili tuweze kutengeneza makundi sawa ya walinacho pekee, tunachotakiwa kufanya na kuacha kulalamika hasa kwa mambo ambayo hayana msaada wowote katika maisha yetu.

2. Kulaumu wengine.

Kama wewe ni mtu wa kulaumu wengine kwa kila kitu na kujiona ni mtu wa kutokosea , sahau kutoka kwenye umaskini. Huu ni kweli ambao upo wazi, kwa sababu watu wengi tupo katika maisha ya kawaida kwa sababu ya kukaa na kulaamu watu wengine. Kufanya hivi ni kulisindikiza jua kutimiza wajibu wake. Kwa kila kitu ambacho unakifanya acha mara moja kunyooshea kidole watu wengine na badala yake unachotakiwa kufanya fanya kazi kama vile dunia hii unaishi pekee yako.

3. Kutokuwajibika katika maisha yako.

 Hutakiwi kulaumu serikali, ndugu, jamaa au wazazi wako ya kwamba wao ndio wamefanya maisha yako yawe hivyo. Wewe ndiye mtu wa kwanza wa kuwajibika na maisha yako. Hivyo unachotakiwa kufanya kila wakati ni kuhakikisha unatoa maaumuzi sahihi hasa katika maisha yako. Hata kama dunia nzima  haita tambua mchango wako, mathalani wewe unajua ni nini ambacho unakitaka basi nakusihi uendelee kupana mpaka tone la mwisho.

4. Kutokuwa na shukrani.

Hiki ni kipimo tosha kwamba unafanikiwa au hufanikiwi. Kama huna shukran hata kwa kidogo unachopata, mafanikio makubwa kwako itabaki hadithi. Hivyo kwa kila wakati jambo la kwanza unalopaswa kulipa kipaumbele ni ile hali ya kuwashukuru watu wote walifanikisha wewe kuwa hapo ulipo ukianza na mwenyezi Mungu, kisha  watu wengi ndiyo wafuate.

Tunakutakia Kila la kheri katika kufikia mafanikio yako makubwa..
Kujifunza zaidi kuhusu maisha na mafanikio tembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku.

Ni wako rafiki yako katika mafanikio, 

Imani Ngwangwalu,
dirayamafanikio@gmail.com
dirayamafanikio.blogspot.com

Jun 19, 2017

Namna Unavyoweza Kuishi Katika Ulimwengu Wa Wakatishaji Tamaa.

No comments :
Dunia ya leo imejaa maneno mengi kuliko watu waliopo katika dunia hiyo. Hebu fikiria ya kwamba tafiti za wanasaikolojia zinasema ya kwamba, mwanaume huzungumza maneno 16000 kwa siku, wakati wanaweke wote duniani kwa kila mmoja mmoja huzungumza maneno 25000 kwa siku, kwa tafiti hizi najaribu kuwaza  hivi tuna watu wangapi? Na kila mmoja akizungumza maneno yake tutakuwa na maneno mangapi?
Najaribu tu kuwaza kwa sauti ili ujue ni kwa jinsi gani maneno yalivyozidi idadi ya watu. Nasema hayo kwa sababu katika maisha yetu ya kila siku tumekuwa tukiishi  katika ulimwengu wa kusema na kusikia. Na katika kusema wapo wale ambao huzungumza mambo chanya na wapo wale ambao huzungumza mambo hasi. Na katika kusikia ipo hivyohivyo  sawa na kusema.
Hata hivyo maneno ya watu ambayo yapo katika dunia hii ni yale ambayo yanatengeneza ulimwengu mpya, ulimwengu huo huitwa ulimwengu wa taarifa, katika ulimwengu huo yapo mengi ambayo utayasema na mengine utayasikia, na katika ulimwengu huohuo taarifa hizo hizo ambazo utakuwa unazisikia, yapo yale yatakayokujenga, lakini yapo yale ambayo yatakufanya uvurugike kabisa.


Na ukweli ni kwamba maneno ya watu ni sumu, maneno ya watu yana nguvu sana kuliko nguvu za Samson hii ni kwa mujibu ya wahenga wapya. Uhalisia ulipo katika sayari hii ya kupeana taarifa zimejaa tarifa za kukatishana tamaa kuliko kupeana mbinu za kusonga mbele kimaisha.
Na mara kadhaa hali  hii hutokea  na unaweza ukajikuta unaumia sana kwenye maisha yako, hiyo yote kwa sababu ya maoni hasi ya watu wanayokutolea wewe. Sasa ili usiendelea kuumia kwa jambo hilo, kumbuka hivi, hicho ambacho kinaongelewa juu yako ni kwa mujibu wa maoni yao wao wenyewe ila uhalisia wa wewe jinsi ulivyo unaujua wewe.
Hivyo, tunachotaka kukwambia siku ya leo ni kwamba  acha kuchukua maoni ya watu na ukaamua kuyatumia kuendesha maisha yako, kwa sababu kama ukifanya hivyo utaumia sana na utaiona dunia chungu.  Hivyo ni vyema ukaamua kuishi wewe kama wewe kwa kufata kile ambacho moyo wako unakutuma kukufanya. Kufanya hivyo itakufanya uishi maisha ya ushindi na mafanikio makubwa.
Tumalizie kwa sema ya kwamba endapo utamua kufanya maamuzi sahihi pasipo kuwasiliza wakatishaji tamaa katika dunia hii, kutakufanya uishi maisha ya ushindi siku zote za maisha yako. Lakini pia faida nyingine ambazo utazipata pale ambapo utamua kuishi maisha ya kujitolea hukumu, utakuwa na uhuru mkubwa katika kutoa maamuzi yako.
Asante sana kwa kuwa nasi, tunakutakia siku njema na mafanikio mema.
Imeandikwa na uongozi wa mtandao huu wa dira ya mafanikio,
Imani Ngwangwalu & Benson Chonya,
0713 04 80 35, 0652 015 024,
dirayamafanikio.blogspot.com.

Jun 16, 2017

Faida Utazozipata Mara Baada Ya kuacha kufanya Mambo Ya Msingi Kimazoea.

No comments :
Wakati nikiwa mdogo niliwahi kusikia wakubwa wangu wakisema ya kwamba mazoea yana tabu, kwa kipindi kile sikujua walikuwa wanamaanisha nini, ila kadri siku zinavyozidi kwenda ndivyo ninavyozidi kuelewa walikuwa wanamaniisha nini.
Nilichokuja kukigundua juu ya msemo huu ni kwamba mawazo ya binadamu ni mawazo ya mgando, naweza nikasema hivyo kwa sababu akili zetu tumezielekeza katika kufanya mambo katika mazoea. Kama mtu amezoea kula ugali muda wa mchana basi mtu huyo ukimpa wali muda wa mchana basi utamsikia mtu huyo akisema kwa kweli mimi kula wali mchana zijazoea.
Kwa mfano huo, angalia watu ambao wanafanya  biashara fulani ambazo hazilipi, ukimwambia wafanyabiashara hao wafanye biashara nyingine watakwambia ya kwamba hawawezi kufanya biashra ambayo hawaijaizoea. Kwa majibu ya aina hiyo ndipo nianapokubaliana na usemi ule usemao ya kwamba mazoea yana tabu, hii ni kwa sababu watu wengi tunashindwa kufanya vitu vingine tofauti na tulivyovizoea.

Zijue faida za kutokufanya kazi kimazoea.
Lakini kama kweli unataka mafanikio ya kweli ni vyema kwa jambo lolote ambalo unalifanya acha mara moja tabia kufanya vitu kwa mazoea kwani mazoea ni dalili za uvivu, unashangaa huo ndio ukweli ambao upo wazi. Hivyo kwa kila jambo ambalo unalifanya hakikisha ya kwamba unatafuta mbinu nyingine za kuweza kuwa bora zaidi.
Lakini pia unashauriwa ya kwamba Ili kufikia mafanikio zaidi ya hapo ulipo, ipo haja na ulazima wa wewe kujituma na kufanya kazi kwa bidii sana nje ya yale mazoea uliyojiwekea. Kwa mfano, kama umezoea kufanya kazi kwa saa 8, ongeza masaa mengine manne ya ziada. Kama umezoea kuamka sa 12, anza kuamka saa 11 alfajiri. Fanya kitu ambacho kitakutoa nje ya mazoea yako yaani ‘comfort zone’. Kwa chochote kile unachokifanya, fanya nje ya mazoea yako.
Hivyo kila dakika na kila sekunde, kama kweli unataka kuondoka katika hali uliyopo kwa sasa unachotakiwa kukifanya kwa sasa ni kuachana mara moja ile tabia ya kuishi katika misingi ya kimazoea (comfort zone) ambayo umeyazoea, na kufanya hivi  itakusaidia sana kujenga misuri mikubwa ya kukuwezesha kufika mbali  zaidi kimafanikio.
Endapo utandokana na hali ya kufanya vitu kwa mazoea tegemea kupata mambo makubwa ya fuatayo;
1   1. Utapata mafanikio makubwa ndani ya muda mfupi, hii ni kwa sababu utaongeza uwezo  na muda wako wa kufanya kazi.
 2. Lakini pia kama utaondokana na ile tabia ya kufanya kazi kwa mazoea basi jiandae kuwa mtaalamu kwa jambo ulifanyalo.
Hivyo tumalize kwa kusema ya kwamba unatakiwa kuachana mara moja tabia yako ya kufanya vitu kwa mazoe.
Tukushuru sana kila wakati kwa kuwa sehemu ya mafundisho  haya  kila siku, endelea pia kuwashirikisha wengine.
Imeandikwa na uongozi wa mtandao huu wa dira ya mafanikio,
Imani Ngwangwalu & Benson Chonya,
0713 04 80 35, 0652 015 024,
bensonchonya23@gmail.com,
dirayamafanikio.blogspot.com.


Jun 15, 2017

Aina Kubwa Tatu Za Watu Na Nafasi Zao Katika Mafanikio.

No comments :
Wewe ni Mtu wa aina gani?
Hili ni swali ambalo kimsingi kila mmoja lazima ajihoji kwa wakati wake.
Ukisoma katika vitabu mbalimbali vya dini vinasema ya kwamba binadamu wote ni sawa, hii ikiwa na maana ya kwamba ukiangalia katika mfano wa vitu kijinsia, organi pamoja homoni.
Lakini ukija katika ulimwengu wa mafanikio binadamu hatufanani hata chembe na hii ndiyo maana kuna watu maskini na wengine ni matajiri, na nilichokigundua ni kwamba utofati wetu huanza rasmi katika fikra.
Fikra ndiyo inayotufanya tuweze kuwa tofauti.  Hivyo ili binadamu  tuweze kuwa sawa ni vyema kila mtu aweze kutafakari yeye ni mtu wa aina gani? Ukishapata majibu ndipo utapojua  wewe ni wa aina gani na unawezaje kusonga mbele kimasha.
Ili mkupata majibu ya swali hilo, siku ya leo nimekuletea makala ambayo itakusaidia kuweza kujua wewe ni mtu wa aina gani. Hivyo yafutayo ni makundi ya watu ambao wapo hapa duniani katika kuyasaka mafanikio.

Watazamaji.
Aina ya kwanza ya watu wanaopatikana katika duniani hii ni watazamaji. Tabia za watu hawa huwa kama ifuatavyo;
Wao ni waoga katika kujaribu kufanya kitu kipya.
Wao huamini zaidi katika kushindwa kuliko kufanikiwa.
Wao ni wazungumzaji wazuri kwa yale ambayo yanatokea katika jamii.  Watu hawa huzungumza zaidi masuala ambayo huwa hayawasaidii mfano wa mambo hayo ni mpira, siasa na matukio mbalimbali yanayoendelea katika mitandao ya kijamii na mambo ya nje ya mitandao ya kijamii.
Lakini kubwa kabisa watu hawa  huwa hawana ubunifu wowote, na huwa wanaishi katika misingi ya kuwaangalia watu wanaopenda (role model), kwa misingi hiyo utagundua ya kwamba aina hii ya watu huishi maishi ya ganda la ndizi, kwa sababu husubiri mtu afanye jambo fulani ili na wao waanze kufanya.
Wapotezaji.
Kundi hili lina watu lukuki sana. Na watu ambao wapo katika kundi hili huwa wana tabia zifuatazo;
Kazi yao kubwa huwa ni kuwangalia watu wengine wanafanya nini katika maisha yao. Hata hivyo katika kundi hili, watu wengi huwa wapo kwa ajili ya kuwakosa wengine kwa yale wayafanyao, na katika kukosoa huko huwa ni katika kukatisha tamaa zaidi kuliko kujenga.
Watu ambao wapo katika kundi hili ni wale ambao wameathiriwa kwa kiwango kikubwa ugonjwa wa wa kuahirisha mambo ya msingi.
Washindi.
Kundi la tatu la mwisho ni kundi la washindi, kundi hili ndilo lenye watu wachache na wenye mafanikio. Na kundi hili lina watu wachache kwa sababu watu wengi wameng’angana’ katika makundi mengine ambayo nimekwisha yaelezea hapo awali.
Watu ambao ambao wapo  katika kundi hili huwa wanasifa zifutazo;
Wao hujua ni nini wanachokitaka katika maisha yao.
Wao hupanga na kukamilisha yale waliyoyapanga kwa wakati.
Lakini kubwa zaidi watu ambao wapo katika kundi hili huwa si wabinafsi kama walivyo makundi wangine, wao huwa wapo tayari kuwasaidia wengine.
Pia ni  watu ambao wamewekeza muda mwingi sana katika kujifunza na kutafakari.
Hayo ni machache kati ya mengi yaliyopo katika kundi hili.
Hayo ndiyo makundi matatu yaliyopo katika ulimwengu huu, Mara baada ya kuona makundi matatu ya watu yanayotufautisha hapa duniani. swali linakuja wewe mwenzangu na mimi upo kundi gani? Kama unahisi upo kundi ambalo hustahili, unachotakiwa kufanya ni kuhama mara moja na kuhamia katika kundi lenye mafanufaa kwako.
Asante kwa kuwa pamoja nasi kila wakati nikutakie siku njema na mafanikio mema.
Imeandikwa na Afisa Mipango Benson Chonya.
0757909942,
dirayamafanikio.blogspot.com

Jun 14, 2017

Hapa Ndipo Chimbuko La Mafanikio Yako Linapoanzia.

No comments :
Mara zote tunakumbushwa ya kwamba ajianavyo mtu ndivyo alivyo. Miongoni mwetu tumekwisha kukataa tamaa ya maisha kabisa, wengi tumeshapoteza matumaini kwa kiwango kikubwa, hatuamini kama ipo siku ambayo tutatafanikiwa, wengi tumejiona hatuna mamlaka ya kupata kile tunachokitaka.
Na hali hii imejitokeza ndani yetu baada ya kuanza kuishi mawazo ya watu wengine, wengi tumekuwa tukiwatazama wengine hasa pale ambapo wameshindwa hivyo, kujiona ya kwamba na sisi hatuwezi. Ila ninachotaka kukwambia ya kwamba kushindwa kwa wengine liwe somo kwako ili uweza kufanikiwa zaidi.
Hii ni kwa kwa sababu hali yoyote ile ambayo inatoka nje ya wewe haina mchango mkubwa sana wa kuweza kukukwamisha au kukufanya ushindwe kufikia mafanikio yako. Kitu ambacho kitakufanya ushindwe kufanikiwa ni ile hali inayotokea ndani mwako tu.

Piga kazi mpaka kieleweke kuleta mafanikio yako.
Hali hiyo inayotokea ndani mwako, ndiyo ina nguvu kubwa sana ya kubadillisha maisha yako. Hebu jiulize kila unapowaza mafanikio, ndani mwako unajionaje? Unajiona ni kwamba utafanikiwa au utashindwa? Kipi unachokiona ndani mwako?
Ni vyema kutafakari hivyo kwa sababu haijalishi watu wanasemaje au watasema nini juu yako, hata watu dunia nzima waseme kwamba utafanikiwa, lakini kama ndani yako huoni hivyo ni wazi huwezi kufanikiwa, pia hata dunia nzima iseme kwamba wewe ni wa kushindwa, lakini ikiwa ndani yako unajiona wewe ni mtu wa mafanikio basi ni lazima utafanikiwa.
Kitu kikubwa hapa unachotakiwa kujifunze kutokulaumu hali yoyote ile, inayotokea nje katika maisha yako kwamba ndio imekukwamisha.  Hii ni kwa sababu wengi wetu ni wazuri sana katika kulaum watu wengine ya kwamba wao wamesababisha wewe kuwa hivyo ulivyo leo na  inawezekana sababu hiyo ukaiona ina mashiko sana kwa upande wako, ila ninachopaswa kukwambia ni nyanyuka upya kwa kuanza kufikiri upya na pia dawa ya wapuuzi ni kuwapuuza.
Nasema hivyo kwa sababu  anakuzuia kupata mafanikio yako ni wewe mwenyewe pamoja na mawazo hasi unayozidi kuyabeba kila wakati. Narudia kusema tena uduni wa maisha yako hausababishwi   na  mtu mwingine bali wewe mwenyewe. Hivyo ni jambo lenye busara sana ambalo ni vyema kuanzia leo, amua kujenga hali bora ndani mwako itakayokupa mafanikio makubwa.
Hivyo ni malize kwa kusema ya kwamba huwezi kutokea kwa jirani bila kuanzia kwako, hii nikiwa na maana acha kulamu watu wengi anza kuona maisha yako mkoseaji mkubwa ni wewe ni si mtu mwingine, hata kama ni kweli mtu mwingine ndiyo sababu ya wewe kuwa hivyo ulivyo ninachotaka kukusihi ni kwamba ni tafuta mbadala wa kutatua changamoto inayokukabili na si kuwa walaam watu wengine.
Asante kwa kuwa msomaji wetu wa mtandao huu wa dira ya mafanikio nakusihi uwashirikishe na wengine kadri uwezavyo.
Imeandikwa na uongozi wa mtandao huu wa dira ya mafanikio,
Imani Ngwangwalu & Benson Chonya,
0713 04 80 35, 0652 015 024,
bensonchonya23@gmail.com,

dirayamafanikio.blogspot.com

Jun 13, 2017

MREJESHO; Zijue Faida Za Kumheshimu Kila Mtu Katika Kazi Yeyote Uitendayo-03

No comments :
Habari za muda huu mpenzi msomaji wa mtandao huu wa dira ya mafanikio, ni matumaini yetu u mzima wa afya tele, kwa upande watu sisi hatujambo kabisa. Wiki iliyopita tulipata kusoma kisa kimoja mahala hapa ambacho kilimuhusu mfalme Mhavila pamoja na mama mjane. Kisa hiki kilikuwa ni cha kusisimua sana.
Ambapo tulikisimulia kwa siku mbili na watu wengi walitutumia ujumbe mzuri ya kwamba wamejifunza mengi sana kupitia kisa kile. Hivyo kwa kuwa tunatambua mchango wako kwetu , hivyo tukaamua kukupa nafasi wewe msomaji wetu uweze ulichojifunza kutokana na hadithi ile;
Watu wengi sana walitutumia maoni yako miongoni mwa maoni hayo ni;
Naitwa FURAHA  MWIKOMBO kutoka Uyole Mbeya.
Kwanza kabisa nipende kuwapongeza waheshimiwa kwa elimu mnayotupatia katika kundi la whatsapp, facebook na blog yenu ya DIRA YA MAFANIKIO.
Mimi nilichojifunza kwenye hadithi hii ni;
1.      Kudharau kazi ya mtu hakuna faida yeyote.
2.      Kushukuru kwa kile kidogo unachokipata na kuwasaidia wengine. Ni jambo la busara.
3.      Mungu anapotupima heshima na upendo wetu huwatumia wale walio chini yetu, mfano viwete, vilema, vichaa na wenye shida kama ambavyo alitumia njia hii mfalme mhavila.
4.      Mara nyingi bahati, riziki na mafanikiohuwa ni vitu vilivyojificha sana, tukivumilia na vitatokea baadae sana.

Karibu tuongee mafanikio kila JUMANNE hapa DIRA YA MAFANIKIO.
Naitwa SHABANI SAIDI kutoka Dodoma
Mambo makubwa matatu ambayo nimejifunza kutoka kwenye hadithi hii ni;
1.      Anayewashweshea wengine kwa ukarimu na yeye pia atanyweshwa kwa ukarimu.
2.      Usiwanyime watu mema watu wanayostaili ikiwa mkono wako una uwezo wa kufanya.
3.      Usimwambie mwenzako nenda kasha urudi na kesho nitakupa kumbe una kitu unachokihitaji.

Naitwa SIMONI MAPUNDA kutoka mbinga.
Mimi nilichojifunza kwenye hadithi hii ni;
Kwamba  kuwa mkarimu kwa watu wote ni siraha, hata kama huna kitu fanya kitu kwa msaada wa wengine, kupitia ulichonacho hajalishi wewe ni maskini, mjane, yatima, kilema au una madaraka amini una uwezo wa kufanya makubwa.
Naitwa ISRAEL NDANG, kutoka Mwanza –Tanzania
Kupitia hadithi ya mfalme mhavilia nimejifunza  mambo yafutayo;
1.      Nimejifunza kutoa pasipo kutegemea malipo, hivyo kila wakati toa mazuri kwa wengine kadri uwezavyo huku ukijua Mungu ndiye mlipaji wa fadhira zako.
2.      Fursa zinaweza kukujia kwenye hali ngumu na utata mwingi ama katika mazingira magumu, hivyo usiyatilie maanani mazingira hayo bali wewe pambana mpaka uweze kupata mafanikio.
3.      Tuwe wakarimu, wanyenyekevu na hata wasikivu pia ili kuelewa hisia za binadamu mwenzetu pia.
TANGAZO MUHIMU
Asante sana kwa wale wote ambao walituma maoni yao kwa namna moja ama nyingine, maoni yako tuliyapenda  na kuyapokea kwa mikono miwili. Tulichokigundua ya kwamba watu wengi wana mambo mengi sana ambayo yatausaidia sisi pamoja na wewe kuweza kufanikiwa na kufika mbali zaidi..
Hivyo kwa kulitambua hilo uongozi wa mtandao wa DM tumeamua kuanzisha kitu kinachoitwa Mafanikio Talk (M.T), hiki ni kipindi maalumu kabisa ambacho kitakuwa kinahusisha mahuzungumzo baina ya uongozi wa mtandao huu wa dira ya mafanikio  pamoja na wewe msomaji wetu.
Tutakochokifanya ni kwamba tutakupigia simu na kufanya mazungumzo na kile ulichokizungumza tutakwenda kukiweka hapa siku ya jumanne Ili watu wengine wajifunze kutoka kwako.
Je ungependa kuwa wa kwanza kufanya kipindi hicho cha Mafanikio Talk (M.T) siku ya jumanne ijayo? Kama jibu ni ndiyo tuma ujumbe mfupi wa maandishi ukianza na neno Mafanikio Talk kisha jina lako  na mahali ulipo kwenda-0757909942/ au email yetu dirayamafaniko@gmail.com nasi tutakutafuta kwa ajili ya kufanya mazungumzo hayo.
Imeandikwa na uongozi wa mtandao huu wa dira ya mafanikio,
Imani Ngwangwalu & Benson Chonya,
bensonchonya23@gmail.com,
dirayamafanikio.blogspot.com.