Jan 14, 2015
Mbinu 5 Muhimu Za kukupa Maisha Ya Mafanikio.
Unaweza ukawa upo
kwenye hali ya kulalamika maisha yako ni magumu na unashangaa kwa nini
hufanikiwi katika maisha yako kama jinsi unavyotaka wewe. Hali hii inaweza ikawa
inakuumiza pengine kila ukiangalia rafiki zako ama maisha ya wengine yanavyozidi
kuwa mazuri, wakati wewe upo katika hali ngumu. Na pengine umekuwa ukijiuliza
nini siri kubwa ya mafanikio yao ambayo
wanaitumia ambayo wewe huna. Kutokana na hali hiyo umekuwa ukijilaumu kujilaumu
na kujiuliza kwanini nyingi ambazo
hazina majibu. Kitu usichokijua watu hawa huwa wanatumia mbinu Fulani
kufanikiwa.
Kawaida, katika maisha
kama ulivyomchezo wa miguu, au michezo mingine mara nyingi huwa zipo mbinu za
kufanikisha kile tunachokifanya. Mbinu hizi huweza kutambulika kama sheria,
kanuni, au siri lakini zote hulenga kukufanikisha kama unataka mafanikio ya kweli.
Mbinu hizi zinapotumiwa kwa bahati mbaya au nzuri huwa hazifanyi ubaguzi
zinamwendea yoyote na kuleta matunda unayoyataka. Hata kama ikitokea umezitumia
mbinu hizi kwa bahati mbaya bila kujijua ni lazima utafanikiwa katika maisha
yako.
Mbinu hizi ndizo
wanazozitumia wengi wenye mafanikio na kuwafanikisha, ingawa huwa sio kwao kuwa
rahisi kukwambia mbinu hizo. Haijalishi unaishi kwa sasa maisha gani au upo
kwenye matatizo mengi vipi, ukizitumia mbinu hizi, zitakufanikisha na kukupa
maisha ya mafanikio unayoyataka. Acha kulalamika tena na kuishi bila amani.
Sasa unaweza ukawa na mafanikio makubwa kama hao unaowaona wamefanikiwa, ikiwa
utatumia mbinu hizi kukufanikisha. Unajua mbinu hizi ni mbinu zipi?
Hizo
Ndizo Mbinu 5 Za Kukupa Maisha Ya Mafanikio:-
1. Kuwa
na nidhamu binafsi.
Ili kupata mafanikio
makubwa unayoyahitaji sio suala la kufanya kazi kwa bidii tu, zaidi
unachohitaji nikuwa na nidhamu binafsi ambayo itakuongoza kwenye malengo yako.
Watu wengi hawana nidhamu binafsi kitu ambacho kinapelekea wengi ndoto zao
zinaishia kati. Ni muhimu kuelewa kuwa ni lazima kufanya mambo yale
yanayoendana na ndoto zako, hata kama kuna wakati unajihisi umechoka unalazimika
kujikaza kufanya jambo hata dogo ambalo litakufikisha kwenye malengo yako.
Ukishindwa kuwa na nidhamu binasi katk maisha yako elewa kuwa utashindwa
kufikia mipango na malengo iliyo jiwekea.
2. Jifunze
kila mara kwa watu waliofanikiwa.
Hii itakusaidia kujua
vitu vingi usivovijua kuliko kukaa na kung’anga’nia mbinu zilezile ambazo
hazikusaidii. Yapo mambo mengi sana usiyoyajua ambayo yanakufanya ushindwe
kufanikiwa. Ikiwa utakuwa na uwezo wa kujifunza kwa wale waliofnikiwa utakuwa
upo kwenye nafasi kubwa ya kufanikiwa na kusonga mbele. Maisha yako yanazidi
kuwa magumu siku hadi siku, kutokana na kukosa kujifunza kwa wengine kwa kujua
hilo badili mwelekeo wako na kuwa mtu wa kujifinza mwisho wa siku mafanikio
yatakuwa makubwa kwako.
3. Jifunze
kutokana na makosa uliyofanya.
Inawezekana kuna mahali
utakuwa umekosea kwa namna moja au nyingine,badala ya kulaumu na kuumia moyo
sana jifunze kutokana na hayo makosa liyoafanya ili isije ikawa kwako rahisi
kufanya makosa yaleyale kwa mara nyingine. Ikiwa utajifunza kutokana na makosa
na kufanyia kazi kile ulichojifunza hapo utakuwa umechukua hatua moja muhimu ya
kuweza kukusaidia kusonga mbele kuyafata mafanikio unayoyataka. Unataka
mabadiliko makubwa katika maisha jifunze kutokana na makosa yako na acha sana
kulaumu.
4. Jenga
tabia ya kujisomea kila siku.
Hili ni jambo ambalo
nimekuwa nikiliongelea sana kuhusu huu umuhimu wa kujisomea. Unapojisomea
unapata vitu vingi sana tena ndani ya muda mfupi. Kupitia huko utaweza
kujifunza mambo mazuri yatakayoweza kubadili maisha yako kwa sehemu kubwa na
kuwa mtu, tofauti kabisa. Acha uvivu jifunze vitu vipya kila siku. Unaweza
ukajifunza kupitia vitabu, ama mitandao mizuri inayoelimisha kama huu wa DIRA
YA MAFANIKIO kwa kupata maarifa bora na sahihi kabisa. Unapojifunza inakusaidia
kukabiliana na changamoto nyingi, ambapo kwako ingekuwa ngumu kuzikabili.
5.
Kuwa na mahusiano sahihi na watu waliofanikiwa.
Katika kutafuta
mafanikio ni vizuri ukawa na mahusiano ama mtandao na watu sahihi ambao
watakusaidia kukufikisha kwenye lengo ulilojiwekea. Haina haja kuwa na watu
ambao hawakusaidii kutimiza malengo yako. Watu hawa watakukwamisha na
kukurudisha nyuma katika maisha yako tu siku zote. Jenga tabia ya kuwa na watu
sahihi ambao utajifunza kitu kwao, utashirikiana nao na kujifunza mambo mengi
huko ya mafanikio na hatimaye utamudu kusonga mbele.
Unaweza kubadili maisha
yako, kama utafanyia kazi mbinu hizi. Nakutakia kila la kheri katika safari
yako ya mafanikio, karibu katika mtandao huu wa DIRA YAMAFANIKIO uendelee kupata maarifa bora yatakayoweza kuboresha yako, kwa pamoja
tunaweza.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA
MAISHA YAKO YAIMARIKE,
0713
048 035/dirayamafanikio@gmail.com
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
nimependa sana elimu yenu
ReplyDelete