Jul 11, 2020
Je, Unahitaji Kufanya Biashara Na Hujui Ni Biashara Ipi Ya Kufanya? Soma Hapa Kujua Ni Biashara Ipi Ya Kuifanya Sasa?
Wapo
watu ambao mara nyingi hujiuliza ni biashara gani wafanye katika maisha yao
ambayo itaweza kuwaingizia pesa nyingi ya kutosha. Ni wazo ambalo hutokea
kutokana na pengine kuona kila biashara wanayoitazama kwa wakati huo kama hailipi. Hali hiyo
husababisha mkanganyiko mkubwa wa mawazo ambao husababisha wabaki njia panda.
Kama
imeshawahi kukutokea hali kama hii kwa namna moja au nyingine makala hi ni
muhimu sana kwako kuisoma. Kwa kusoma makala hii inakuonyesha kwa uwazi orodha
za biashara ambazo unatakiwa uzifanye ukiwa katika mazingira uliyopo. Karibu
kila biashara ipo hapo, kazi ni kwako kuchagua mojawapo unayoipenda na
kuifanya, acha kulalamika tena kuwa huelewi nini cha kufanya.
Twende
kwa pamoja kuzijua biashara hizo ambazo unauwezo wa kuzifanya na kukufikisha
kwenye mafanikio makubwa:-
1. Kutengeneza na kuuza chaki.
Hii
ni moja ya biashara nzuri unayoweza kuifanya na soko lake liko juu. Unaweza
ukanunua mashine yako za kutengeneza chaki na kisha ukaanza kuzisambaza kwenye
stationary au mashuleni. Uzuri wake
mashine hizi za kutengenezea chaki gharama yake pia sio kubwa sana ni ya
kawaida tu ambayo hata wewe unaweza kuimudu. Hii inaweza ikawa ni sehemu
mojawapo ya kuingizia kipato chako.
2. Kufungua duka la kuuza asali.
Uzuri
wa bidhaa hii muda mwingi soko lake lipo juu. Ni biashara ambayo unaweza
ukaifanya kwa kuagizia asali kutoka kwa wakulima kama nilivyo mimi na kisha
kuanza kuiuza moja kwa moja katika vipimo vinavyotakiwa.
Kama
huwezi kufungua duka hili unaweza ukafanya mbadala wake ukaenda kutengeneza
mizinga wewe mwenyewe na kuwafuga. Pia hii ni biashara ambayo ni nzuri kwako
kukuingizia kipato kikubwa kwa urahisi.
3. Kuanzisha biashara ya kuuza
vyakula katika matamasha mbalimbali.
Hapa
siyo lazima uwe na Hotel au Mgahawa ndiyo uanzishe biashara ya namna hii.
Kikubwa unahakikisha unakuwa makini na sherehe katika eneo ulilopo. Kama ni
kuweka mawakala watakao kusaidia kukujulisha kuwa eneo fulani kuna sherehe ya
aina fulani na siku fulani itakuwa nzuri zaidi kwako kuchangamkia tenda hizo
mapema.
4. Kujenga nyumba za kulala wageni.
Kama
mtaji wako unaruhusu hii ni moja kati ya biashara nzuri kuifanya. Ni biashara
ambayo hahitaji kukimbizana sana ukishamaliza kujenga, zaidi unatakiwa kuweka
mfumo sahihi wa kusimamia na kuanza kuingiza pesa. Na kwa bahati nzuri kwa
Tanzania yapo maeneo mengi ambayo yanauhitaji mkubwa wa huduma hii. Ni Biashara
nzuri kuifanya hata kama umri umeenda, kwa sababu haihitaji mkimbizano mkubwa.
5. Kutengeneza matoroli/mikokoteni na
kuikodisha.
Katika
hili hapa unatakiwa kutengeneza kwa
idadi unayoitaka na unamwachia kijana ambaye anaikodisha huku ukiendelea na
majukumu mengine. Unaweza ukaiona ni biashara ndogo lakini fuatilia kwa
waliowekeza nguvu na mawazo yao hapo wakwambie kile wanachokipata utashangaa.
6. Kuazisha huduma ya AIRTEL MONEY,
MPESA, TIGOPESA, EZYPESA.
Hakuna
ubishi hii ni moja ya huduma ambayo imezagaa kila eneo na watu wengi wanaihitaji.
Kikubwa ni juhudi yako na kuzingatia eneo uliloweka biashara yako liwe hasa la
mzunguko mkubwa zaidi kukuwezesha kufanya biashara hii vizuri.
7. Kupamba maharusi na kumbi za harusi/sherehe.
Pia
unaweza ukajiingiza hapa na kushughulika na kupamba tu maharusi. Kama hujui
sana ni kitu cha kujifunza pia, kisha unachangamkia sherehe zinazojitokeza
mjini.
8. Kuanzisha kilimo cha kisasa.
Wengi
wanaposikia kilimo kichwa kinakataa. Lakini ikiwa utawekeza kwenye kilimo cha
kisasa na cha kitaalamu ambacho unategemea kumwagilia zaidi, uwe na uhakika
unatoka. Yapo mazao mengi unaweza ukalima lakini mojawapo ni kitunguu. Inaweza
ikawa ni njia rahisi ya kufikia mafanikio yako
kuliko unavyofikiri.
9. Mashine za kusaga na kukoboa
nafaka.
Pia
unaweza ukajitengenezea kipato chako na kuwa kikubwa na cha uhakika kwa kufunga
mashine hizi. Kila siku watu wanahitaji kula hivyo ukifunga mashine hizi ni rahisi
sana kupata wateja wa kuwauzia unga na kupata
faida. Na uzuri mahindi ya kusaga yanapatikana maeneo mengi kwa wingi
kama kule Kibaigwa (Dodoma), Gairo(Morogoro), Kiteto(Manyara) na maeneo mengine
mengi kama Iringa na mbeya.
10. Yadi kwa ajili ya kupaki magari.
Kitu
unachotakiwa hapa ni kununua kiwanja na kukigeuza kuwa yadi ambapo magari
yanakuwa yanapaki iwe kwa kulala au kwa muda. Kila gari linalokuwa linapaki
linakuwa linatozwa kiasi fulani cha pesa ambacho kinakuwa ndiyo hiyo huduma
unayoitoa.
Zipo
aina nyingi sana za biashara ambazo unaweza ukazifanya na kukuingizia kipato. Katika
Orodha ya kipande cha makala hii kinachoendelea zimebaki biashara zaidi 110
ambazo sijaziweka hapa kutokana na ufinyu wa nafasi. Kuzijua zinazoendelea na
ufafanuzi wake unaweza ukaniandikia
email kwenda diramafanikio@gmail.com
nitakutumia mara moja.
ILA
KAMA YOTE HAYO UTASHINDWA KUPATA LA KUFANYA WEWE UTAKUWA UMESHAPOTEA, ENDELEA
NA UTARATIBU WAKO WA KUILAUMU SERIKALI.
Tunakutakia
ushindi katika safari yako ya mfanikio, ila kumbuka daima tupo pamoja mpako
maisha yako yaimarike.
Ni
wako rafiki katika mafanikio,
IMANI NGWANGWALU,
0713 048 035,
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
SAFI SANA NDUGU YANGU UMETUFUNGUA PAKUBWA,HIZ NI ELIMU MUHIMU SANA WAKATI MWINGINE BIASHARA KAMA HIZI WATU WENGI HUZIDHARAU KUMBE HUWA NA KIPATO KIZURI SANA.ASANTE
ReplyDeleteblog yako iko vizuri kaka...
ReplyDeleteok ni vzr,,kuhusu mpesa mtaji unaweza kuwa shillingi ngapi,,!!
ReplyDeletekuusu mpesa sio biashara ambayo mtaji wake unaitaji uwe mdogo yani ukiwa na sehem yenye mzunguko mzuri kibiashara unatakiwa usipngue chini ya 1mil cash and flot 1mil apo kidogo utakua na msingi ambao unaweza ukaendana na mazingira uliopo
DeleteMungu akubaliki hakika mitazamo mizuri yenye mashiko.....
ReplyDeleteThis comment has been removed by a blog administrator.
ReplyDeletekwakweli mtu ukizingatia kwenye hii blog asee mtu unaweza ukafanya mambo makubwa sana sema kinachotuponza watu wengi hatuna subra yan tunapenda kufanyaj mambo bila kuwaza malengo yetu ni yapi ndo tunapofel apo tu na umu 65% biashara zilizotajwa so za mtaji mdogo yani mtu umekosa kabisa unatakiwa uwe na ata 1mil apo utakua umesogea kwenye lengo sio mm ndo nasema ivo ila kutokana na maelezo ya blog ila tunashukur kwa kutufumbua manaake mtu unaweza ukawa na mtaji ila kila unachojalibu kutaka kufanya unajiona unaenda kufeli ko kusoma uku kunatusaidia sana nn tufanye🙏
ReplyDeleteAsante mkuu nimepata elimu moja makini Sana
ReplyDelete