Jun 3, 2015
Kilimo Bora Cha Pilipili Hoho Na Faida Zake.
Pilipili hoho
ni moja ya
mazao ya viungo
ambalo hulimwa kwa
wingi Mikoa ya
Arusha, Kilimanjaro, Tanga,
Morogoro, Mbeya na Iringa.
Zao hili
hutumika kama kiungo
kwenye vyakula mbalimbali
kama vile vyama,
viazi na ndizi.
Vilevile hutumika katika
kutengeneza kachumbari na
kuweza kukaushwa na
kusagwa ili kupata
unga.
Viini lishe
vinavyopatikana katika pilipili
tamu au hoho ni Vitamini
A,B,C na madini
aina ya chokaa
na chuma.
MAZINGIRA:
Zao hili
hukua vizuri kwenye
hali ya hewa
yenye joto la
wastani (nyuzi joto
18 hadi 20)
za Sentigredi, joto
likizidi vichomozo, maua
na matunda huanguka.
Huhitaji mwinuko
wa kuanzia usawa
wa bahari hadi
mita 1,500 na
mvua za wastani
kiasi cha milimita
600 hadi 1500.
Udongo unaofaa
kwa zao hili
ni ule wenye
rutuba, mboji nyingi,
kina kirefu na
usiotuamisha maji.
AINA:
Kuna aina
nyingi za pilipili
hoho. Baadhi ya aina
zinazostawishwa nchini ni
California, Wonder, Emerald
Giant, Sweet Neapotitan,
Yolo Wonder, Pimiento
na Keystone Resistant
Giant. Aina zingine
ni kama vile
Ruby King, Ruby
Giant, Libert Bell
na Yolo Wonder
B.
KUPANDA MBEGU:
Mbegu zinaweza
kupandwa moja kwa
moja shambani au
kuoteshwa kwanza kwenye
kitalu na baadaye
kuhamishiwa shambani.
Kuotesha mbegu
Kitaluni.
Kabla ya
kusia mbegu tengeneza
tuta lenye upana
wa mita moja.
Urefu wa tuta
utategemea eneo la
shamba linalotarajiwa kupandwa.
Weka mbolea za
asili zilizooza vizuri
kiasi cha ndoo
mbili au zaidi
katika eneo la
mita mraba moja.
Changanya mbolea na
udongo vizuri, kisha
tengeneza vifereji vyenye
nafasi ya sentimeta
10 hadi 15
kutoka kifereji hadi
kingine. Kina cha kifereji kiwe
sentimeta moja hadi
tatu katika eneo
hilo, kiasi hiki
kitatoa miche ambayo
itatosha kupandikiza katika
eneo la mita
mraba 100.
Baada ya
kusia fukia kwa kutumia
udongo laini au
mbolea za asili
zilizooza vizuri. Weka
matandazo na kisha
mwagilia maji. Endelea
kumwagilia kitalu kila
siku asubuhi na
jioni hadi mbegu
zitakapoota. Mbegu huota
baada ya siku
sita hadi 10.
Mara zitakapoota ondoa
matandazo. Endelea kumwagilia
maji hadi wakati
miche inakuwa tayari
kwa kupandikizwa.
KUTAYARISHA SHAMBA
Tayarisha shamba
vizuri mwezi mmoja kabla
ya kupandikiza miche,
katua ardhi katika
kina cha kutosha
sentimeta 30 kwenda chini,
weka mbolea za
asili kiasi cha
tani 10 hadi
15 kwa hekta.
Kiasi hiki ni sawa
na debe moja
kwa eneo la
mita mraba moja
changanya mbolea na
udongo vizuri.
Ikiwa eneo
hilo lina upungufu
wa madini aina
ya fosiforasi kama
itakavyothibitishwa na wataalam,
weka mbolea ya
chokaa aina ya
TSP. Kiasi kinachotakiwa ni
kilo 200 kwa
hekta. Lainisha udongo
siku tatu au
tano kabla ya
kupandikiza miche.
KUPANDIKIZA MICHE:
Miche huwa
tayari kwa kupandikizwa
shambani baada ya
wiki nne hadi
10. Wakati huu
huwa na majani
sita hadi manane
na urefu wa
sentimeta 10 hadi
15.
Pandikiza miche
katika nafasi ya
sentimeta 40 hadi
50 kutoka shimo
hadi shimo na
sentimeta 60 hadi 75
kati ya mstari
na mstari. Ikiwa
mbolea za asili
hazikuwekwa wakati wa
kutayarisha shamba, weka
kiasi cha nusu
kilo hadi moja
katika kila shimo
la kupandia.
Siku moja
kabla ya kung’oa
miche, mwagilia tuta
ili kulainisha udongo.
Ng’oa miche pamoja
na udongo wake
kisha pandikiza katika
kina cha sentimita
mbili zaidi kuliko
ilivyokuwa kwenye kitalu.
Pandikiza miche wakati
wa asubuhi au
jioni. Mara baada
ya kupandikiza mwagilia
maji ya kutosha.
KUTUNZA SHAMBA
·
Kuweka
matandazo.
Tandaza nyasi
kavu ili kuhifadhi
unyevu ardhini, kuongeza
rutuba ya udongo,
kuzuia uotaji wa
magugu, na mmmomonyoko
wa ardhi.
·
Palizi.
Palilia shamba
kila magugu yanapoota.
Wakati wa kupalilia
pandishia udongo kuzunguka
shina ili kuifunika
mizizi, na kuzuia
mmea usiangushwe na
upepo mkali.
·
Kumwagilia Maji.
Pilipili hoho
hustawi vizuri iwapo
zimepata maji ya
kutosha. Hivyo umwagiliaji
wa mara kwa
mara hasa wakati
wa kiangazi ni
wa muhimu.
·
Kuweka Mbolea.
Zao hili
huhitaji mbolea za
kukuzia. Hizi ni
kama mbolea ya
S/A, CAN, Urea
na mbolea ya
mchanganyiko aina ya
N.P.K Mbolea ya
mchanganyiko (N.P.K) huwekwa
wakati maua yanapoanza
kutoka. Kiasi kinachowekwa
ni gramu tisa
hadi 10 (kijiko
kimoja kikubwa) kwa
kila mmea. Majuma
manne baadaye weka
CAN, S/A au
Urea. Weka gramu
sita (kijiko kidogo
cha chai) kwa
kila mche, kama
utatumia CAN au
S/A. ikiwa utatumia
Urea, weka gramu
tatu ( nusu
kijiko cha chai)
kwa kila mche).
Wadudu waharibifu
na Magonjwa.
Wadudu.
·
Vidukari
au wadudu Mafuta
( Aphids).
Hivi ni
vijidudu vidogo vyenye
rangi nyeusi, kijani
au kahawia. Hushambuliwa majani
kwa kufyonza utomvu
wake na kusababisha
mmea kudumaa.
Vidukari huzuiwa
kwa kunyunyizia dawa
kama vile Dimothoate
au Selecron.
·
Mbawakau.
Ni wadudu
wenye rangi nyeusi
iliyochanganyika na kahawia.
Mabawa yao kwa
nje ni magumu.
Hushambulia shina karibu
na usawa wa
ardhi na kulifanya
liwe na nundu.
Zuia wadudu
hawa kwa kutumia
mojawapo ya dawa
zifuatazo; Carbaryl, au
Dimecron.
·
Fukusi wa
Pilipili (Pepper Weevil)
Mdudu huyu
ni hatari sana
kwa zao hili
na mashambulizi kufanywa
na funza wake
wenye rangi nyeupe.
Funza hawa hula
sehemu ya ndani
ya vichomozo na
matunda machanga nan
kusababisha kuanguka. Angamiza
wadudu hawa kwa
kutumia moja ya
dawa zifuatazo; Actellic,
Sumithion au Carbaryl.
·
Vithiripi (Thrips)
Hivi ni
vijidudu vidogo vyenye
rangi ya njano.
Hushambulia majani na
husababisha mmea kuwa
na rangi nyeupe
yenye kung’aa. Mmea
pia kunyauka kuanzia
kwenye ncha ya
jani. Vijidudu hivi
pia kueneza magonjwa
yatokanayo na virusi.
Zuia vijidudu
hivi kwa kutumia
dawa kama vile;-
Cyrmethrin, Sumicidin au
Dimercon.
·
Sota (Cutworms)
Hawa hukata
miche michanga karibu
na usawa wa
ardhi. Ili kuwazuia
wadudu hawa, tumia
dawa kama vile
Carbaryl, Sumicidin au
Ekalux. Nyunyizia mara
baada ya kupandikiza.
·
Inzi
Weupe (White flies).
Ni vidudu
vidogo vyenye rangi
nyeupe, na huonekana
kama vumbi la
unga vikiwa kwenye
majani. Mmea ukitikiswa
huruka.
Hushambulia mmea
kwa kufyoza utomvu
wake, na hueneza
ugonjwa wa virusi
unaosababisha kujikunja kwa
majani.
Inzi weupe
wanaweza kuzuiwa kwa
kutumia Sumicidin, Sapa
Diazinon au Diclorvos.
·
Utiriri Mwekundu
(Red Spidermites)
Hawa ni
wadudu wadogo wenye
rangi nyekundu au
rangi ya machungwa
yaliyoiva. Huonekana upande
wa chini wa
majani na hushambulia mmea
kwa kufyonza utomvu
wake.
Zuia utitiri
kwa kutumia dawa
kama vile Kelthane,
Dimethoate na Diazinon.
Magonjwa
·
Magonjwa ya
Virusi
Magonjwa haya
hutokana na virusi.
Husababisha majani kudumaa,
kukunjamana, na kuwa
na rangi ya
njano. Ili kuzuia
magonjwa haya, zingatia
yafuatazo;-
-
Panda
aina ya pilipili
zinazostahimili mashambulizi j
ya magonjwa haya.
-
Ng’oa
miche inayoonyesha dalili
za magonjwa haya.
-
Zuia
wadudu wanaoeneza magonjwa
ya virusi kwa
kutumia dawa ya
Kelthane 30 E,
C, Dimethoate, Diazinon
na Ekalux.
-
Badilisha
mazao. Baada ya
kuvuna pilipili tamu,
zao linalofuata lisiwe
la jamii la
zao hili kwa
mfano nyanya na
bilinganya.
Chule (Anthracnose)
Ugonjwa huu
husababishwa na ukungu.
Hushambulia matunda na
kuyasababisha kuwa na
makovu j ya mviringo yenye rangi
nyeusi iliyochanganyika na
kahawia.
Zuia ugonjwa
huu kwa kunyunyizia
mojawapo ya dawa zifuatazo:
Dithane - M 45,
Topsini - M,
Ridomol au Kocide,
·
Madoa
Bakteria (Bacterial Leaf
spot)
Ugonjwa huu
husababishwa na viini
vya vya bacteria.
Hushambulia majani machanga j na
baadaye matunda. Dalili j zake ni
kuonekana kwa madoa
ya njano kwenye majani na
matunda.
Zuia ugonjwa
huu hkwa kupanda mbegu
zilizothibitishwa na wataalam.
·
Kuoza
Mizizi (Root Rot)
Huu ni
ugonjwa wa ukungu
unaoshambulia mizizi na
kusababisha kuoza. Mmea
hunyauka na hatimaye
hufa. Ugonjwa huu
hupendelea sana hali
ya unyevunyevu na
joto jingi, hivyo
zuia hali hii
kwa kuepuka kupanda
pilipili kwenye sehemu h inayotuamisha maji.
Hali ikiwa
mbaya, tumia dawa
za ukungu h kama vile
Dithane M 45,
Tpsin - M
70 au Ridomil.
·
Mnyauko
Verticilium (Verticilim Wilt)
Huu pia
ni ugonjwa unaoletwa
na ukungu ambao
hupatikana kwenye udongo.
Hushambulia shina na
kulisababisha libadilike rangi
na kuwa ya
kahawia. Baadaye mmea
hunyauka na kufa.
Unaweza kuzuia ugonjwa
huu kwa kubadilisha
mazao.
KUVUNA
Pilipili hoho
huwa tayari kwa kuvunwa
baada ya wiki 10
hadi 14 tangu
kupandikiza miche. Uvunaji
huendelea kwa muda wa
wiki nane hadi
10. Muda wa
kuvuna hutegemea aina
na matumizi. Pilipili
kwa ajili ya
matumizi ya nyumbani
huvunwa zingali na
rangi yake ya
kijani kibichi inayong’aa . zile
za kisindika kiwandani
huvunwa zikiwa zimekomaa
na zenye rangi
nyekundu. Matunda yakivunwa
tangali machanga hunyauka
kwa urahisi, kusinyaa
na hupunguza wingi
wa mazao. Wastani
wa mavuno huwa
kwa hekta ni
tani 30 hadi
45.
Tunakutakia kila la kheri katika kilimo bora, endelea kutembelea DIRA YA MAFANIKIO kujifunza zaidi.
MAKALA
HII IMEADALIWA NA SAID MALOGO, MTAALAMU WAMASUALA YA KILIMO.
MAWASILIANO
0782 396 729
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
Nimependa sana shule hii. Lakini ninhependa update itolewe
ReplyDeleteNashukuru kwa maelezo mazuri. Ila nilitaman
ReplyDeletepia kufaham gram ngapi za mbegu zinatosha ekari moja, pia ekari moja inachukua kiasi gani cha miche. Na Je kwa wastani mche mmoja waweza kutoa kiasi gani cha mavuno?
Gram 100 hadi 150 kwa ekari moja kwa pv
ReplyDeleteVizur
ReplyDeleteThanks
ReplyDeleteGram ngapi naweza kupanda nusu heka?????
ReplyDeleteNzuri sana
ReplyDeleteAsante kwa elimu hii bora kabisa
ReplyDeleteAsante kwa elimu.
ReplyDeleteGram 50
ReplyDeleteElimu nzuri Sana hasa wakati huu ambapo vijana tunashauliwa kujiajili. Zaidi ningependa kujua mtaji kiasi gani kinatosha kwa ekari moja?
ReplyDelete