Jan 6, 2018
Aina Za Kuku Na Faida Zake.
Kuna aina mbalimbali za kuku ambazo mfugaji anaweza kufuga na
kila aina inategemeana na malengo ya mtu husika anayetaka kufanya shughuli hii
ya ufugaji, hivyo leo nimekuletea makundi makuu manne ya kuku ambayo
tunayafuga hapa Tanzania.
KUKU WA NYAMA.
Hii ni moja ya kundi
la kuku ambalo linafugwa sana hapa nchini na kuku hawa wanafugwa kwa malengo ya
kuzalisha nyama tu. Uzalishaji wa kuku hawa wanachukuliwa kuku wazazi kutoka
nje ya nchi na kuhifadhiwa sehemu maalumu kwa ajiri ya kuzalisha mayai na mayai
yanatotoreshwa na kupata vifaranga kwa ajili ya nyama ,
Faida ya kuku hawa.
Faida ambayo utaipata
kama mfugaji ni kuwa kuku hawa hufugwa kwa mda mchache muda wa miezi miwili au
mitatu na kuuzwa kwa ajili ya matumizi ya nyama, hivyo ni sehemu nzuri yakujipatia
kipato na kunufaika na ufugaji wako kwa muda mfupi.
Zingatia.
Gharama za kuwalea
kuku hawa ni kubwa kidogo hivyo unapoamua kufanya ufugaji kwa ajili yakupata
tija katika kukuza kipato chako ni muhimu ukafuga kuku wengi kwa wakati mmoja
hii itakufanya upate faida nzuri kuliko kufuga kuku wachache na ukapata hasara
na kuona ufugaji haulipi kumbe wewe mwenyewe haukuwa na taarifa kamili kuhusu
ufugaji wako.
Muhimu.
Ni muhimu sana kutunza kumbukumbu za gharama za
matumizi katika mradi wako wa kuku ili pale utakapo uza uweze kujifanyia
tathmini na kujua umepata faida au hasara katika mradi wako.
KUKU WA MAYAI.
Hawa ni aina ya kuku
ambao hufugwa kwa malengo maalumu ili kuzalisha mayai, kuku hawa wanataga kwa
wingi sana mayai na wanataga bila jogoo, kuku hawa wamendaliwa vizuri kwa ajili
ya kutaga tu hivyo kama utaamua kuwawekea jogoo watataga na kuatamia lakini vifaranga wake watakuwa hawana ubora
ule unaotakiwa.
Faida ya kuku hawa.
Kwakuwa kuku hawa ni
watagaji wazuri wa mayai basi wanampatia mfugaji uhakika wa kipato kwa kila
siku hadi pale atakapofikia mwisho wa mradi wake, yaani miaka miwili.
Zingatia.
Ili kupata faida
iliyokusudiwa katika mradi wako huu wa kuku unatakiwa uwape chakula bora na cha
kutosha pia uzingatie chanjo na tiba kwa magonjwa pale unapoona dalili ya
magojwa.
Muhimu.
Ufugaji wakuku ni moja
ya aina ya miradi yenye faida nzuri iwapo tu mfugaji atazingatia kanuni bora za
ufugaji. Ufugaji huu ili ukuletee tija ni muhimu ukafuga kuku wengi angalau mia
tatu na kuendelea hapo utaiona faida yake nzuri.
KUKU CHOTARA.
Hawa ni aina ya kuku
ambao wamechanganya aina fulani ya kuku na aina nyingine ya kuku na kupata aina
moja ya kuku, mfano: amechukuliwa jogoo wa kienyeji akachanganywa na
tetea wa kisasa na vifaranga vitakavyotoka vitakuwa chotara kwa maana
watakuwa na sifa baadhi za kienyeji na sifa baadhi za kisasa.
Kuku hawa kwa hapa
nchini wapo wengi na kuna makundi mbalimbali ya kuku kulingana na asili na
mahali walipo tokea, mfano: MALAWI, KENBRO, SASO na KROILA na hawa
wanatofautiana sifa na asili.
Faida ya kuku chotara.
Hapa nitataja kwa
ujumla faida zote ila wakati mwingine nitachambua aina moja moja ya kuku
chotara.
Wanakuwa kwa haraka na
wanakuwa na maumbo makubwa tofauti na kuku wakienyeji hivyo ni wazuri sana kwa
nyama.
Ni watagaji wazuri
sana tofauti na kuku wakienyeji (kuku hawa ukuwahudumia vizuri wanataga mayai
kati ya 180-300 kwa mwaka hivyo ni wazuri sana kwa mayai.
Wanaishi kwenye
mazingira yeyote yale kwa maana wanaweza kuishi vizuri wakiachiwa kujitafutia
chakula.
Wanastahimili sana
magonjwa (chanjo ni Muhimu kuwapa) tofauti
na kuku wa nyama au wa mayai.
Nyama yao ni nzuri
sana haina tofauti na kuku wakienyeji.
Wanauzito mkubwa
kuku mmoja anafika hadi kilo sita.
Soko lake ni kubwa.
KUKU WAKIENYEJI.
Hawa ni kuku ambao asili
yake ni hapa hapa Tanzania na tunao katika maeneo mengi ya nchi yetu, kuku hawa
wanakuwa wana maumbo madogo kulinganisha na kuku chotara, pia kuku hawa
hawakui kwa haraka ukilinganisha na kuku chotara, aina hii ya kuku hutaga
mayai machache sana kwa mwaka na wanataga mayai kati ya 40-120.
Faida ya kuku hawa.
Kuku hawa wanafugika
katika mazingira yeyote yale kwa sababu ni wazuri kujitafutia chakula, ili
upate faida nzuri ya mradi wako wa kuku huo unashauriwa kuwapa chakula cha
ziada ili waweze kukua kwa haraka na kuwa na uzito mzuri.
Kuku hawa hawana
gharama hivyo nashauri kama una eneo zuri ni muhimu ukaanza ufugaji wa kuku
hawa kwa sababu hawana shida katika ufugaji wake.
Kuku hawa wanapendwa
sana hapa nchini kwa sababu ya nyama na mayai yake kuwa mazuri sana na ni kuku
wa asili hivyo tunaamini hawana kemikali na hii ni kweli kabisa,
Hizi ni aina
mbalimbali za kuku katika nchi yetu na jambo la muhimu kuangalia malengo yako
na uhitaji ya jamii husika jambo nzuri na lakuvutia ni kwamba aina hizi za kuku
zinafugika katika maeneo yetu yote ya nchini hivyo angalia mazingira yako na
anza kufanya ufugaji.
Pia kama wewe ni mfugaji wa
kuku na unahitaji vifaranga bora, waone DM
POULTRY FARM PROJECT kwa huduma ya uhakika. Hawa ni wauzaji wa vifaranga wa
kuku aina ya KUROILER, SASSO, PURE
KIENYEJI na KUCHI. Kwa mahitaji ya vifaranga wasiliana nao kwa 0767 048 035 au 0686 141097 na wote mnakaribishwa.
DAIMA
TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Ni mimi rafiki yako,
Frank Mapunda,
0758918243/0656918243.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
je hao kuku wa nyama unafuga katika mazingira gani?
ReplyDeletena chakula chao ni kipi na vipi kuhusu namana ya kukabiliana magonjwa ya milipuko yaani kideri nk naomba kufunguliwa akili
Kuku hao aina ya krioler wanaatmia na kutotoa vifarang?
ReplyDelete