May 29, 2020
KAMA UTAKOSA KITU HIKI,SAHAU KUISHI MAISHA YA FURAHA NA MAFANIKIO
Imani Ngwangwalu
May 29, 2020
BIASHARA
,
FEDHA
,
FURSA
,
HAMASIKA
,
SIMULIZI NA VITABU
No comments
:
kwenye maisha yako ukitaka kufika mbali kimafanikio kitu kimojawapo unachotakiwa kuwa nacho ni kujifunza kuwa na msamaha.
Unapokuwa na msamaha, inakusaidia kuondoa uchungu, hasira, visasi vyote unakuwa umeweka pembeni na matokeo yake unakuwa huru kufanya mambo mengine na kusonga mbele.
Sikiliza Yote kwa Urefu 👇👇👇👇
Usiache ku Subscribe na Kuwasha kikengere kwa makala zaidi.
IMANI NGWANGWALU.
GODMADE GEL SANITIZERS 3000 TSH
Unamjua mwanafunzi anayepaswa kurudi chuo wakati huu? mtakie heri ya masomo anakwenda kupambana katika mkusanyiko hatari kwa afya yake mkinge na corona kwa kumpa hizi taarifa muhimu kama zawadi yako kwake.
KWA MAWASILIANO ZAIDI WASILIANA NAO
INSTAGRAM: BOFYA HAPA
EMAIL; godmadeproduction@gmail.com
AU PIGA MASAA 24hrs
+255673433101
+255693086499
May 14, 2020
Utaacha Alama Gani Duniani Siku Ukifa?
JE UTAACHA ALAMA GANI SIKU UKIFA?
Utaacha Alama Gani Duniani Siku Ukifa?
Lazima ujiulize ya kwamba ni alama gani utaicha chini ya jua kabla hajafa? Kimsingi tunaambiwa na vitabu vya dini ya kwamba kila binadamu ni mavumbi na atarudi kuwa mavumbi, kauli hiyo inaashiria wazi hakuna atakayeishi milele katika ulimwengu wa mwili labda katika ulimwengu wa roho hii ina maana ya kwamba kila nafsi itaonja umaiti kwa wakati wake. Nisizungumze sana ila maana ibaki pale pale ya kwamba utaacha Alana gani siku ukifa?
SIKILIZA SIMULIZI HII KATIKA YOUTUBE CHANNEL YETU USISAHAU KU SUBSCRIBE
May 1, 2020
Mambo Manne Yanayohitajika Katika Mafanikio Ya Mjasiriamali.
Safari
ya mafanikio kwa mjasiliamali, mara nyingi ni safari ambayo inachangamoto
nyingi sana. Kupitia changamoto hizo ndizo huwaangusha wengi na matokeo yake
kushindwa kufanikiwa. Ili kufanikiwa kwenye ujasiriamali kuna mambo ya msingi
unayotakiwa kuyajua na kuyafatilia karibu kila siku.
Na
ni mambo hayo hayo, ndio yaliyonifanya mimi nishike peni na kalamu ili niweze
kukujuza. Nimeamua kufanya hivyo kwa sababu, kama hutayajua mambo hayo, utakuwa
ni mtu wa kuanguka anguka sana na kushindwa kufanikiwa. Je, mambo hayo ni yapi,
fuatana nami niweze kukujuza moja baada ya jingine.
1.
UNG’ANG’ANIZI.
Kuendelea
kung’ang’ania na kutaka matokeo unayataka yatokee kwenye maisha yako, naweza
kusema hili ni moja ya jambo la muhimu sana katika ujasiriamali. Iko wazi
utakutana na changamoto kwenye njia ya mafanikio, lakini huwezi kuchoka ni lazima
ung’ang’anie mpaka lile lengo lako liweze kutimia.
Unapokutana
na changamoto na ukaamua kuwa mbishi kwa kupambana nazo, hapo utakuwa upo
kwenye njia sahihi ya mafanikio yako. Wajasiramali walio wengi ni watu wa
kung’ang’ania na kwa sababu hiyo huwasaidia sana kuweza kufikia mafanikio yako.
Ukishindwa kuwa king’ang’anizi sahau mafanikio ya ujasiriamali.
2. MAENDELEO.
Lazima
uendelee kuwa king’ang’anizi, lakini itakuwa ni kazi bure kama utaendelea kuwa
king’ang’anizi na ukashindwa kuona
maendeleo kwa kile unachokifanya. Hapa ndipo wajasiariamali wengi ninapoona
wanakosea, wanafanya kazi kwa muda mrefu, wiki, miezi, miaka, lakini ukija
kuwatamazama wapo pale pale, hili linaumiza.
Lazima
uwe wazi kwenye malengo yako ya kijasiriamli. Hiyo ndiyo njia ya mwisho ya
kuthibitisha kuwa unafanya progress/maendeleo au unapiga makitaimu. Andika
malengo yako ya ujasiriamli na kisha anza kuyatekeleza kidogo kidogo. Kwa
kifupi, fanya ufanyavyo, lakini ni muhimu kuona maendeleo ya kile ukifanyacho.
3. MABADILIKO.
Mara
nyingi, mabadiliko yanakwenda sambamba na maendeleo. Kama kuna kitu unakifanya
na huoni maendeleo yake, ni lazima kufanya mabadiliko kwa kubadili mambo ambayo yanakwamisha usione maendeleo
hayo. Kama usipofanya mabadiliko na unaona mambo hayendi unajichelewesha wewe.
Katika
hatua hii ya mabadiliko ni kama vile unakuwa unafanya tathmini kwa kuangalia mambo
yanaenda au hayaendi. Ukiona mambo hayaendi sawa, kama nilivyokwambia ni ruksa
kuweza kufanya mabadiliko, ambayo yatakusaidia kuweza kupata matokeo ambayo
unayataka na ya faida kwako.
4. FAIDA.
Hakuna
mjasiriamali ambaye anaendesha mambo yake tu kiholela bila kuona faida. Faida ndio
lengo la kwanza la mjasiriamali yeyote yule. Unapoona mjasiriamali anang’ang’ania,
anafanya mabadiliko na kutaka kuona maendeleo, ujue hapo anachokilenga ni
kutafuta faida.
Naamini
ukiyapitia mambo hayo manne tena na tena, ni dhahiri utaelewa ni mambo ambayo
yatakusaidia sana kuendelea kufanikiwa ukiwa kama mjasiriamali. Huhitaji kukata
tama, unachohitaji ni kuendelea kujifunza na kufanyia kazi kila aina ya
mafundisho unayoyapata hapa kila siku.
Tunakutakia kila la kheri na endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila
siku kujifunza maisha na mafanikio.
Pia rafiki, kama unapenda kujifunza zaidi kuhusu mafanikio, karibu
kwenye kundi la WHATS APP LA
MAFANIKIO, kujiunga tuma neno THE UNIVERSITY OF
WINNER’S kwenda 0713 048 035, hapo
utapata utaratibu mzima wa kujiunga.
. DAIMA
TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Ni wako rafiki katika mafanikio,
Imani ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na mjasiriamali,
Whats app; +255 713 048
035,
Email; dirayamafanikio@gmail.com
Subscribe to:
Posts
(
Atom
)