Dec 29, 2015
Muda Sahihi Wa Mafanikio Yako Ni Huu Hapa.
Bila
shaka umewahi kuliona hili kuwa wengi wetu tumekuwa tukitafuta sana muda sahihi
wa kuweza kufanikisha mipango au malengo yetu tuliyojiwekea. Muda huu ambao tumekuwa
tukiutafuta, mara nyingi hupelekea sisi
kufanya maandalizi mengi sana ya kusubiri mambo mengi yakamilike ndio tuanze
uwekezaji ule tunaouhitaji.
Lakini
kitu kisichoeleweka kwa wengi ni kwamba siku zote hakuna wakati sahihi wa wewe
kuanza jambo unalotaka kulifanya zaidi ya sasa. Kama kuna jambo unalotaka kulifanya
au kulitimiza ni bora ukaanza kulifanya hivyohivyo sasa bila kuweka maandalizi
mengi sana kama unavyofikiri. Tambua siku zote muda sio rafiki sana na
wewe hadi ukusubiri sana.
Kosa
kubwa wanalolifanya watu wengi bila kujua ni kule kufikiri kuwa kuna vitu fulani
hawana ambavyo ni lazima wavikamilishe kwanza ndipo waanze kufanya kile
wanachokitaka kukifanya hadi kufikia mafanikio. Kama haya ndiyo mawazo yako kwa
namna fulani utakuwa unachelewa.
Kwa
sasa huhitaji kusubiri taarifa zaidi, huhitaji kusubiri muda zaidi ya ulionao
wala huhitaji eti hadi uwe una mtaji wa kiasi fulani ndiyo uanze biashara.
Unachotakiwa kufanya sasa ni kuanza na kile ulichonacho. Mambo mengine
unayofikiria sana hayajakaa sawa, yatakaa sawa wakati umeanza kufanya.
Utakuwa
unajidanganya kama utakuwa unafikiri ukijiandaa sana hutakosea na utakuwa
kamili kila eneo, makosa na kujifunza ni lazima. Kwa hiyo lilokubwa kwako ni
kuwa tayari kufanya kile ambacho unaona kitakufanikisha tena kwa haraka kuliko
ukasubiri sana.
Ukweli
wa mambo ulivyo ni kwamba hakuna muda sahihi unaokusubiri wewe wa kuanza
kufanya jambo unalolitaka kama ulionao sasa. Huu ndiyo muda sahihi kwako wa
kufanya mambo yako. Jiulize kama hutafanya sasa utafanya lini? Je, hauoni
kwamba utazidi kujichelewesha kufikia malengo yako makubwa kama utakuwa ni mtu
wa kusubiri?
Kama
umekuwa mtu wa kusubiri sana, leo tambua kitu kimoja hiyo imetosha. Sasa ni
wakati wa kuchukua hatua kwa kutumia kile kidogo ulichonacho kukufanikisha.
Acha kudharau kile ulichonacho, hata kama ni kidogo vipi kinuwezo wa
kukufanikisha. Tumia ulichonacho hadi kikupe mafanikio.
Weka
mawazo pembeni ya kushindwa na anza kujiamini kwa kile unachokifanya kuwa ni
lazima kikupe ushindi. Anza utekelezaji kwa kuchukua hatua kwa hatua kila siku
hadi uyaone mafanikio. Hivi ndivyo mafanikio yako yatakavyokuja na hakuna muda
wa kusubiri.
Kama
utaendelea kusubiri elewa kabisa unajichelewesha kwenye mafanikio yako
mwenyewe. Fanya mafanikio yako yaonekane sasa. Muda sahihi wa mafanikio yako
ni sasa. Chukua hatua siku zote hata kama ni kidogo lakini mwisho wa siku
ushindi utakuwa ni wako.
Tunakutakia
ushindi katika safari yako ya mafanikio na endelea kutembelea DIRA YA MAFANIKIO
kwa kujifunza na kuelimika zaidi.
DAIMA
TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Ni
wako rafiki katika mafanikio,
Imani ngwangwalu,
Kama
una maoni, ushauri au changamoto yoyote inayokuzuia kufikia mafanikio yako
wasiliana nasi kwa:-
Simu;
0713 048 035,
Dec 16, 2015
Je, Umefanya Nini Mwaka 2015?
Mwaka 2015 unakaribia kuisha, kwani zimebaki wiki chache mwaka kuisha na
kuingia mwaka mpya wa 2016. Kwa mtu mwenye busara atajiuliza sana maswali
mbalimbali ya msingi kuhusiana na mwaka huu.
Maswali ya Msingi ya Kujiuliza:
·
Je nini/kipi ambacho
hutasahau mwaka 2015?
·
Je mwaka 2015
umeutumia vyema?
·
Je mwaka 2015
umeutumia kivipi katika kuboresha maisha yako na kupanga malengo yako?
·
Je ni vipi unavyopaswa
kubadili au kuboresha katika mwaka unaokuja?
Ni jambo la busara
sana kutafakari. Lakini msingi mkuu ni kuhakikisha kuwa; katika matendo yako,
maneno yako, na katika tafakari zako unapaswa kuzibadilisha kwa kuhakikisha
unazidi kuendeleza hali hizo tatu na kuziboresha. Ukiweza kuboresha mawazo
yako, matendo yako na maneno yako kiusahihi utaweza kubadili maisha yako vyema.
Hivyo kaa na tafakari, mwaka 2015 umeutumia kivipi. Ikiwezekana andika hata
katika kitabu chako au diary ya kumbukumbu itakusaidia kuhakikisha unapanga
malengo mazuri na unatambua maendeleo yako ya kimaisha.
Subscribe to:
Posts
(
Atom
)