Dec 31, 2017
HEKIMA ZA MAISHA NA MAFANIKIO; Usijitupe Kwenye Moto Kwa Sababu Ya Kuogopa Moshi.
Ni wakati na siku njema tena
, na kukaribisha katika siku ya leo katika jukwaaa letu la hekima za maisha na
mafanikio. Kama siku zote ambavyo nimekuwa nikikukumbusha, hekima za maisha na
mafanikio ni sehemu ya kujifunza busara na hekima za maisha.
Hilo linakujaje au kivipi?
Ni rahisi tu, ni kupitia misemo au maneno ambayo yaliweza kuzungumzwa na babu
zetu enzi za kale. Kwa kujifunza huko nasi tunatoka na vitu ambavyo ni adimu lakini,
vinatukomaza na kutufanya tupige hatua.
Naomba nikukaribishe
jamvini, vua viatu vyako hapo ulipo, karibu kwenye mkeka wangu hapa nilipo, ili
nikukaribishe kwa moyo mkunjufu na tuweze kujiunga pamoja tufunzane juu ya
hekima za maisha na mafanikio za siku hii ya leo.
Hekima
ya 1; Anaye elewa vibaya ni yule anayesikiliza vibaya.
Kuna watu ambao unaweza
ukasema jambo na ukarudia tena na tena huku wao kazi yao ikiwa ni kuitika tu
mara mbilimbili. Katika hekima yetu hii, inatuonyesha kwamba anayelewa vibaya
ni yule ambaye anasikiliza vibaya pia.
Hii ikiwa na maana kama wewe
ni msikilizaji mzuri, ni lazima na kwako utaweza kulewa vizuri kile ambacho
kimesemwa. Ikiwa lakini utaenda kinyume, basi ni lazima kwako utakuwa unaelewa
vibaya kila wakati.
Hekima yetu inatukumbusha
umuhimu wa kutega masikio vizuri pale jambo linaposemwa na mtu mwingine. Ni vyema
kuachana karibu na kila kitu na kujenga usikivu mkuu ili kusikiliza vizuri ili
kuepuka kulewa vibaya.
Hekima
ya 2; Usijitupe kwenye
moto kwa sababu ya kuogopa moshi.
Hii pia ni moja ya hekima ya
maisha na mafanikio iliyotolewa na wahenga wa kale ambayo inakutaka sana na
kukusihi usije ukajitupa kwenye moto kisa na sababu kubwa ni kwa wewe kuogopa
moshi.
Hekima hii ukiiangalia ina
chekesha kidogo, lakini ujiulize ina maana gani kwetu? au inafunzo gani kwetu
ambalo ni kubwa? Hapa ukichunguza tunaonywa kwamba usije ukajiingiza kwenye
matatizo makubwa sana kwa sababu ya kitu kidogo tu.
Hekima hii inawaonya watu
wale ambao wakipata tatizo wanakimbilia kujidhuru, ambapo madhara yake yanakuwa
makubwa kuliko hata ya tatizo lenyewe, hivyo inakuwa ni sawa na kujirusha
kwenye moto kwa sababu ya kukwepa moshi.
3.
Imara ya jembe kaingoje shamba.
Siku zote inaeleweka hivi,
iwapo jembe ni imara hujulikana pale linapolima shambani. Hiyo ikiwa na maana,
udhaifu wa mtu au kitu, huthibitika sana pale mtu au kitu hicho kinapokuwa
kazini na si vinginevyo.
Hapa tahadhari kubwa
tunayopewa na maneno haya ya hekima ni kwamba, tusikithamini sana kitu kwa sababu
ya maneno au kujidai kwake, thamamini kitu au mtu kwa sababu ya kazi, au uwezo
wake.
Kuna watu kwa sababu ya
tabia au huluka zao, hujikuta ni watu wa kujidai sana na kutoa kila tambo za
maneno kwamba wanaweza kitu fulani, lakini kumbe kiutendaji hakuna kitu. Hapa unatakiwa kuwa makini na kuangalia
uimara wao kwenye kazi na si maneno peke yake.
4.
Heri kupata mkate nusu kuliko kutokupata kabisa.
Funzo kubwa tunalolipata
kupitia hekima hii ya maisha ya mafanikio ni kwamba, kile kidogo ulichonacho ni
bora na ni nafuu sana kuliko kukosa kabisa. Huhitaji kukiona ni duni sana
wakati unacho, unatakiwa kushukuru hata kwa hicho kwani kitakusaidia.
Wapo watu ambao wao ni
kunung’unika tu, wakati ukiwaangalia kuna kitu ambacho wamekipata. Hapa maneno
ya busara kutokana na hekima za maisha na mafanikio yanatuonya tuachane mara
moja na tabia hii, inatuaangamiza.
Kama kuna kitu kidogo umepata
basi kaa chini shukuru na kisha ongeza juhudi itakayokusaidia kuweza kupata
kitu kingine zaidi na zaidi. Elewa nusu ya mkate uliyoipata ni bora zaidi
kuliko kuikosa kabisa.
Nikutakie siku njema na kila
la kheri katika kujifunza hekima hizi, kwa leo tunaishia hapa, naomba uwe na
wakati mwema zaidi.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO
YAIMARIKE,
Ni
wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na
mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713
048 035,
Email; dirayamafanikio@gmail.com
Dec 29, 2017
Vitu Vitano (5) Vya Muhimu Kuweka Kwenye Chakula Cha Kuku.
Kuna vitu vitano muhimu vinavyotaijika kwa
kuku ili awe na afya bora. Navyo ni kama vifuatavyo,
1. Protini.
2. Mafuta.
3. Wanga.
4. Madini.
5. Vitamini.
2. Mafuta.
3. Wanga.
4. Madini.
5. Vitamini.
1. PROTINI
Ni aina ya vyakula ambavyo kazi yake kubwa ni kukuza mwili navyo ni kama
ifuatavyo, Mtama, Dagaa, Alizeti na Soya. Hivi vyote inategemeana na
maeneo uliko, nini kinapatikana kwa urahisi.
2. WANGA.
Ni aina ya vyakula ambavyo kazi yake ni kuupa mwili nguvu. Navyo ni kama ifuatavyo; mahindi yaliyo balazwa, pumba ya mahindi na pumba ya mpunga.
Ni aina ya vyakula ambavyo kazi yake ni kuupa mwili nguvu. Navyo ni kama ifuatavyo; mahindi yaliyo balazwa, pumba ya mahindi na pumba ya mpunga.
3. MAFUTA.
Ni aina ya vyakula ambavyo kazi yake kubwa ni kuupa mwili joto pamoja na kulainisha mmeng'enyo wa chakula mwilini. Kundi hili kuna vitu vifuatavyo; mashudu ya alizeti na mashudu ya pamba.
Ni aina ya vyakula ambavyo kazi yake kubwa ni kuupa mwili joto pamoja na kulainisha mmeng'enyo wa chakula mwilini. Kundi hili kuna vitu vifuatavyo; mashudu ya alizeti na mashudu ya pamba.
4. MADINI
Hapa kuna madini ya aina mbalimbali ambayo kazi yake kubwa ni kuimarisha mifupa na ganda la juu la yai pia. Na haya madini ni muhimu sana, kwa sababu yanakazi kubwa katika mwili wa kuku. Yanamwezesha kuku kutembea vizuri na kwa ukakamavu.
Hapa kuna madini ya aina mbalimbali ambayo kazi yake kubwa ni kuimarisha mifupa na ganda la juu la yai pia. Na haya madini ni muhimu sana, kwa sababu yanakazi kubwa katika mwili wa kuku. Yanamwezesha kuku kutembea vizuri na kwa ukakamavu.
Pia yai la kuku ili
liwe imara lenye ganda gumu lazima apate madini ya kutosha. Bila kusahau madini
yanasaidia kuku kutonyonyoka manyoya yake. Madini hayo ni kama ifuatavyo, mifupa,
Chokaa ya kuku, D.C.P
hizuia kudonoana, kula mayai, maganda malaini. Pia uimarisha maganda ya mayai,
husaidia kuongeza mayai.
5. VITAMINI.
Ni aina ya vyakula ambavyo vinapatikana sana kwenye mbogamboga, lakini kazi
yake kubwa ni kuimarisha
mwili uwe vizuri kama vile kuona, kuwa na manyoya imara na afya bora. Kundi
hili linavyakula kama vifuatavyo, mchicha, chainizi, spinachi
na majani ya mpapai.
KUMBUKA:
Pia katika maduka ya mifugo kuna vitamini zinauzwa ambazo hutumika pia kama mbadala wa mazingira yetu yalivyo kuna baadhi ya maeneo kupata mbogamboga ni changamoto. Kuna "vitalyte" ni nzuri kwa kuku na hata nyingine pia.
Pia katika maduka ya mifugo kuna vitamini zinauzwa ambazo hutumika pia kama mbadala wa mazingira yetu yalivyo kuna baadhi ya maeneo kupata mbogamboga ni changamoto. Kuna "vitalyte" ni nzuri kwa kuku na hata nyingine pia.
Dec 25, 2017
KHERI YA CHRISTMAS NA MWAKA MPYA, MSOMAJI WA DIRA YA MAFANIKIO.
Habari za muda huu mpenzi msomaji
wetu wa mtandao huu wa DIRA YA MAFANIKIO,
bila shaka u mzima wa afya tele, na unaendelea vyema na majukumu yako ya kila
siku.
Kwa upande wetu sisi ni
wazima wa afya tele, tunamshukuru Mungu kwa ajili ya hilo.
Ikiwa na leo na tarehe 25 mwezi wa 12
uongozi wa mtandao huu, unapenda kuchukua nafasi hii kukushukuru sana wewe kwa
mchango wako wa hali na mali katika kuhakikisha mtandao huu unaendelea kufanya
kazi zake kila siku.
Kwani bila wewe, yale ambayo yanaandikwa
katika mtandao huu yatakuwa hayana maana tena, lakini kwa sababu umekuwa
unatenga muda wako ili uweze kujifunza mambo mbalimbali katika mtandao huu
hivyo tunarudia kusema asante sana.
Hata hivyo kwa kuwa nasi ni binadamu,
na hakuna binadamu ambaye huwa hakosei basi hivyo tunaomba tutumie wasaa huu
kuomba msahama hasa pale tulipokukwaza na kukosea.
Lakini upo usemi usemao yule
anayekosea naye zipo nyakati huwa unakosewa hivyo nasi pale ulipotukosea
tumekusamehe na kuacha jua liendelee kuangaza na mambo mengine yaendelee pia.
Tunachokuhasa ili uweze kuwa bora
katika maisha yako kwa mwaka ujao ni lazima uhakisha unawekeza muda
mwingi katika kujifunza vitu ambavyo vitakusaidia kuwa bora zaidi katika mambo
mbalimbali ambayo unayafanya.
Kwa kila siku mpya jifunze na
uhakikishe unakuwa bora zaidi katatika kutenda na kufikiri zaidi ya siku
iliyopita, yaani jifunze kuwa bora zaidi ya jana.
Kwani endapo utaaamua kufanya hivyo
nakuhakiishia ya kwamba yapo matokea makubwa sana ambayo utayaoona katika
maisha yako na jamii kwa ujumla.
Mpaka kufikia hapo hatuna la ziada
tukutakie sikukuu njema na maandalizi mema ya kupokea mwaka mpya wenye
mafanikio mengi kwa upande wako.
Muhimu : Uongozi mzima wa uongozi wa Dira Ya Mafanikio umekuandalia
mambo mengi mazuri ambayo yatakuapa hamasa kubwa ziaidi ya kuweza kufanikiwa
katika mambo mbalimbali ambayo unayafanya.
Dec 23, 2017
MAMBO MUHIMU YAKUYAJUA KABLA YA KUINGIA KWENYE UFUGAJI.
Habari za leo rafiki, karibu sana katika kujifunza mambo
mbalimbali yanayohusu ufugaji bora wa kuku, lengo kuu la makala haya kukupa elimu
iliyosahihi kuhusu ufugaji , Na mambo yote ninayoyaandika yanatoka kwenye
uzoefu wangu mwenyewe katika ufugaji karibu sana katika somo letu la leo.
Moja ya changamoto kubwa kwa watu wengi tunajiwekea malengo
makubwa kila mwaka kwamba nataka kufanya kile na kile ndani ya mwaka huu lakini
kila siku bado unashindwa kuanza hii inatokana na changamoto mbalimbali za hapa
na pale.
Pia wengi hushindwa kuanza kwa sababu kubwa ya kokosa hamasa ya ndani
juu ya kile walichokiwejiwekea malengo na hii inapelekea kila mwaka kuwa na
malengo yaleyale bila kupiga hatua na kwenye upande wa ufugaji mambo ni hayo
hayo kila siku.
Utakuta tunajisemea natamani kufuga huku tukiendea kuimba wimbo
usiokuwa na vitendo, nini ninachotaka kukwambia rafiki siku hii ya leo
unahitaji kuchukua hatua chukua hatua sasa nasiyo kusubili subili utachelewa
sana kufanikisha ndoto yako.
Unapochelewa kuchukua hatua ukumbuke siku zinaenda na majukumu
yanazidi kuongezeka huku umri nao unakimbia, ila rafiki yako nina jambo zuri ninalotaka
kukwambia na unatakiwa uchukue mara moja.
Jambo hili ambalo nakwambie uchukue hatua sasa ni juu ya wazo la
ufugaji. Unajua kwanini nakwambia ni sasa,
kwa sababu hakuna wakati mwingine mzuri wa kuanza zaidi ya sasa, anza kufanya na
kuweka mipango yako mapema juu ya ufugaji wako.
Hapa hapa nimekuandikia
mambo ambayo unatakiwa kuyajuwa kwanza na kuyafanyia kazi unapotaka kufanya
shughuli ya ufugaji za ufugaji ili uweze kufanikiwa katika ndoto yako ya
ufugaji, najua unafahamu kuwa ufugaji kwasasa ni moja ya kazi yenye faida.
1. ELIMU NA MAARIFA
SAHIHI KUHUSU UFUGAJI.
Hii imekuwa kama sehemu ya kujifichia kwa watu wengi
wanaposhindwa kuanza jambo lllote hasa la ufugaji unakuta wanaibuka na sababu
kuwa nashindwa kuanza kwasababu sina elimu sahihi juu ya ufugaji sasa sijui una
subiri nini kuitafuta hiyo elimu na maarifa sahihi unajichelewesha rafiki,
chukua hatua.
2. TAMBUA UNATAKA
KUFUGA KUKU KWA MALENGO GANI.
Nimuhimu kujua kwa nini unataka kufuga kuku kwa sababu ukijua
kwanini unataka kufuga kuku itakupa picha halisi juu ya kuku unaotaka kufuga
ili uweze kutafuta taarifa sahihi juu ya ufugaji wako kwasababu kuna aina
nyingi za kuku na kila kuku ana sifa zake na mahitaji yake hivyo ukijua malengo
yako kuhusu ufugaji wako itakusaidia sana katika kufanya maamuzi na kutafuta
taarifa sahihi kuhusu ufugaji wako.
3. ENEO UNALOTAKA KUFUGIA.
Unapojua tayari malengo uliyonayo katika ufugaji na kujua aina
ya kuku unaotaka kuwafuga sasa utakuwa na picha nzuri juu ya ufugaji wako,
baada ya hapo unahitaji kujuwa ENEO GANI UNALOTAKA KUFANYIA UFUGAJI hii
itakusaidia kujuwa mali ghafi ambayo itatumia katika banda lako, ni muhimu sana
kuandaa eneo la kufugia mapema mara tu ya kuweka malengo yako ya ufugaji, jua
eneo la kufugia mifugo yako.
4. GHARAMA ZINAZOHITAJIKA KATIKA KUFANYA UFUGAJI WAKO.
Baada yakujuwa malengo eneo unalotaka kufanyia shughuli zako za
ufugaji ni muhimu sana kuchanganua gharama zitakozotumika katika kuanza ufugaji
gharama hizo ni pamoja na banda, chakula, chanjo na tiba, hii itakusaidia
kuweka mipango yako sasa ili uweze kufanya ufugaji wako kwa ufanisi mzuri
5. ANZA NA ULICHONACHO.
Hii ni jambo la muhumu sana katika kutimiza malengo ya aina
yeyote, ni muhimu kuanza na kile ulichonacho usisubiri hadi uweze kujipanga
vizuri sana kwasababu unapoanza inakupa hamasa ya kuendelea kuchukua hatua
mbalimbali kuhusu ufugaji. Anza na kuku idadi yoyote, kama ni kumi, hamsini au
hata mia mbili kulingana na uwezo ulionao, kikubwa anza na ulichonacho.
Naomba niishie hapa kwa leo,
Endelea kunifatitia nina mengi mazuri yakukwambia kuhusu ufugaji
naamini yatakusaidia sana.
Pia
kama wewe ni mfugaji wa kuku na unahitaji vifaranga bora, waone DM POULTRY FARM PROJECT kwa huduma ya
uhakika. Hawa ni wauzaji wa vifaranga wa kuku aina ya KUROILER, SASSO, PURE KIENYEJI na KUCHI. Kwa mahitaji ya vifaranga
wasiliana nao kwa 0767 048 035 au 0686
141097 na wote mnakaribishwa.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO
YAIMARIKE,
Ni Mimi rafiki yako katika ufugaji,
Frank Mapunda,
0758918243/0656918243
Karibu sana,
*
Dec 19, 2017
Changomoto Kubwa Zinazojitokeza Katika Ufugaji Wa Kuku.
Habari rafiki, karibu
katika makala ya siku hii ya leo, makala ambayo itakuwa inakufikia mara kwa mara
kwa lengo la kukupa elimu bora ya ufugaji wa kuku kutoka hatua y akwanza hadi
ya mwisho karibu sana
Kwanini ufugaji wa kuku?
Ufugaji wa kuku ni sekta
ambayo inakuwa kwa kasi sana hapa nchini na sasa imekuwa ni sehemu ya ajira kwa
watu wengi, ufugaji kwa sasa umekuwa ukifanya vizuri sana kwa kuwa na soko zuri
kwa ndani ya nchi yetu na hata nje ya nchi.
Ufugaji umekuwa sehemu nzuri ya ajira kwa watu
wengi na imekuwa kazi rasmi kwa watu wengi, ufugaji umekuwa ni sehemu nzuri ya
uwekezaji unaompatia mtu kipato na kumtimizia malengo yake katika maisha.
Pia ufugaji umekuwa ni
rahisi kufanya na unafanyika katika maeneo yeyote mjini au vijijini, licha ya
kuwa ufugaji wa kuku kuwa na faida nyingi pia ufugaji wa kuku umekuwa na
changamoto zake ambazo zinawafanya wafugaji wengi kukata tamaa katika Ufugaji
huu wa kuku.
Jambo lililokuwa zuri
ni kwamba changamoto nyingi zilizopo kwenye ufugaji ni aina changamoto ambazo
inawezekana kabisa kuzipunguza ilimradi
tu tukiwa makini na kupata elimu bora na sahihi katika sekta hii ya
ufugaji wa kuku.
Changamoto hizi
zinatokana na wafugaji wengi wanaingia kwenye Ufugaji bila kuwa na elimu
sahihi ambayo itawapa mwongozo bora katika kufikia malengo waliyojiwekea katika
ufugaji wa kuku kulingana na eneo husika.
Kwa kukosa huko kujua
mambo muhimu yanayohusu ufugaji inawapelekea kupata hasara kubwa na kushindwa
kutimiza malengo ambayo walikuwa wamejiwekea katika maisha yao ya kila siku.
Mimi kwa kuliona hili
nimeona bora nikuletee elimu hii ili uweze kuwa na elimu sahihi katika
uwekezaji wako katika sekta hii ya ufugaji. Mara baada ya utangulizi huo, naomba
kwa leo tuanze somo letu moja kwa moja, linalohusu changomoto zinazojitokeza katika ufugaji wa kuku.
MAGONJWA.
Magonjwa yamekuwa ni changamoto
kubwa kwa wafugaji wengi hasa wanaoanza kuingia katika ufugaji na hii
inasababisha wafugaji wengi wakate tamaa ya kufuga na kuona kufuga hakuna faida
yeyote kwasababu inawapa hasara kubwa sana.
Jambo lakuvutia nikuwa
katika mfululizo huu wa makala zangu nitaeleza mbinu ambazo kama utatumia
utaweza kupunguza kwa kiasi kikubwa cha magonjwa ya kuku kwa kifupi nimekuja na
majibu juu ya changamoto hii.
GHARAMA KUWA KUBWA ZA CHAKULA.
Hii ni moja ya changamoto
kubwa kwa wafugaji wengi wa sasa kwa sababu wanapenda kufuga lakini wanajikuta
wanashindwa kwasababu ya kukosa mitaji ambayo itaweza kuwa saidia katika kuwapa
chakula mifugo yao.
Kutokana na changamoto
kuwa kubwa kwa upande wa chakula watu wengi wameshindwa kuendelea na ufugaji wa
kuku kwa wingi na wamekuwa wakifuga kwa idadi ndogo sana au kuacha kabisa kwa sababu
yakushindwa kupata chakula.
WIZI.
Hii ni moja ya
changamoto ambayo zinawakuta wafugaji wengi wa kuku hasa maaneo ya mijini, wezi
wamekuwa wakibomoa mabanda na kuingia kuiba kuku wengi nakupelekea hasara kubwa
kwa wafugaji.
Jibu la changamoto hii
kama unafuga kuku wengi ni bora ukaweka mlinzi anaweza akawa mbwa au mlinzi kwa
maana ya binadamu. Ukiweka mlinzi hapo itakuwa imekusaidia kwa kiasi kikubwa
kutatua chagamoto hii.
Kwa leo naomba niishie
hapa tutaendelea siku nyingine kwa llimu bora ya ufugaji wakuku. Endelea
kutufatilia......
Kwa mahitaji ya
vifaranga bora kabisa kwa ajiri ya ufugaji karibu sana vinapatikana,
pia kwa mahitaji ya
MASHINE bora za kutotoleshea vifaranga zinapatika na
bila kusahau mayai kwa
ajiri ya kutotoresha, kula yanapatika kwa bei nafuu sana yanasafirishwa popote
pale. Mayai na vifaranga vinavyopatikana ni yakuku chotara aina ya kuroiler.
Karibu sana na wote
mnakaribishwa.
Kwa mawasiliano zaidi,
0758918243/0656918243.
Ni mimi rafiki yako,
FRANK MAPUNDA .
KARIBU KATIKA UFUGAJI
BORA WAKUKU TUKUZE UCHUMI WA NCHI YETU.
Dec 18, 2017
Bila Kujali Kitu Gani Kinatokea, Taka Matokeo.
Ugunduzi
mkubwa duniani, ulianza au ulitokana na watu ambao walikuwa wana matatizo sana.
Kwa mfano, kuna eneo fulani duniani ambapo watu walikuwa wakitembea kwa miguu,
kutokana na kuchoka huko kutembea kwa miguu ndio utakaja ugunduzi wa magari na
hata ndege ili kurahisha.
Ubunifu
mkubwa duniani pia ulitokana na watu ambao walikuwa hawajaridhishwa na huduma
zinazotolewa. Kwa mfano, watu baada ya kuchoshwa na mabasi yenye ‘keria’ juu hapo ndipo yakaja mabasi yenye
‘buti’ ili kuepusha hata upotevu wa
mizigo na inakuwa salama wakati wote.
Mafanikio
makubwa duniani pia yanazaliwa na watu ambao walikutana na changamoto nyingi
sana. Kuna watu baada ya kuchoshwa na umaskini, basi waliamua kupigana usiku na
mchana mpaka kuhakikisha wanaupa umaskini mkono wa kwaheri, hakuna umaskini uliotolewa
kwa njia ya lelemama.
Hii
yote inadhihirisha kuwa, mafanikio makubwa hayaendi kwa watu ambao wanasema
siku nikipata muda au siku nikipata pesa za kutosha basi nitawekeza kwenye
mradi wa aina fulani, bali mafanikio makubwa yanaenda kwa watu wote ambao wako
tayari kuchukua hatua hata kama rasilimali zao kwa akili na macho zinaonekana
ni kidogo sana.
Hebu
jiulize aliyegundua ndege au aliyegundua meli ni pesa au rasilimali gani za
kutosha alikuwa nazo? Ukiangalia elimu, hawakuwa nazo za kutosha, ukiangalia ni
pesa hawakunazo za kutosha, kila kitu kilikuwa hakitoshi kwao, lakini
kilichowasukuma ni kutaka matokeo wanayoyataka bila kujali wana rasililmali
chache kiasi gani.
Lakini
tunaona mwisho wa siku, kutokana na ung’ang’anizi wao huo wakaja na kitu
kikubwa, endapo kama wangekaa na kuanza kulia lia kama wewe unavyolia kwamba ‘ooh sina mtaji na siwezi kufanya biashara,’
basi inawezekana kabisa leo hii tungekuwa labda tunatembea kwa miguu.
Maisha
ya mafanikio yanataka utayari. Upo tayari kutoa nini? Kwa chochote kile ulichonacho
mkononi mwako hata kiwe kidogo sana kina uwezo wa kukufanikisha ikiwa kitu
hicho utakilea na kukitunza vizuri. Haijalishi iwe ni kazi ya mshahara kidogo
au una biashara ndogo lakini unaweza kupiga hatua na kufika mbali sana
kimafanikio.
Kwa
nini uendelee kuteseka na kuamini kwamba huwezi kufanikiwa, wakati uwezo huo
unao. Kipi kinachokurudisha nyuma, je umeamua kukwama kwa sababu unaamini
kwamba wewe si kitu na hutaweza kipiga hatua kwa sababu ya rasilimali ulizonazo
ni chache sana, hiyo tu ni kwambie si kweli hata kidogo.
Kuanzia
leo, acha kabisa kusubiri kuwa kamili, fanya kila ufanyalo kuhakikisha unapata
matokeo unayoyataka. Kama unataka kwekeza kwenye mradi wa aina fulani, wekeza
pasipo kutafuta sababu yoyote ile. Sababu hazina nafasi kwenye mafanikio yako,
unatakiwa kufanikiwa tu.
Vizuizi
au vikwazo vipo tu katika maisha yako. ukitafuta sababu kwamba ipo siku
utavikimbia vizuizi hivyo hapo utakuwa unajidanganya sana. Tafuta njia ya
kuweza kuondokana na vizuizi hivo ili uweze kuwa mshindi wa maisha yako. Kwa namna yoyote ile, bila kujali nini
kitatokea, taka matokeo ya mafanikio yako.
Tunakutakia kila la kheri na
endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku kujifunza maisha na
mafanikio.
Pia
rafiki, kama unapenda kujifunza zaidi kuhusu mafanikio, fursa za mafanikio
zinapopatikana, ajira pamoja na uwekezaji, karibu kwenye kundi la WHATS APP LA MAFANIKIO, kujiunga tuma
neno THE UNIVERSITY OF WINNER’S
kwenda 0713 048 035, hapo utapata
utaratibu mzima wa kujiunga.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO
YAIMARIKE,
Ni
wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na
mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713
048 035,
Email; dirayamafanikio@gmail.com
Dec 17, 2017
HEKIMA ZA MAISHA NA MAFANIKIO; Hakuna Mkate, Pasipo Kazi.
Naamini
leo yako iko poa na unaendelea kuimalizia wikiendi yako kabla ya kesho hujatua
kazini kuanza kukamilisha majukumu ya Juma zima. Kama iko hivyo, shukrani za
pekee zimwendee Mola wetu.
Ni wakati
na jumapili njema kabisa nami na kualika katika jamvi letu la Hekima za maisha
na mafanikio. Kumbuka hizi ni hekima ambazo zilitolewa kitambo na babu zetu au
wahenga, sasa pia nasi ni muhimu tujifunze.
Na
kwa nini tunajifunza misemo au maneno ya wahenga wetu ni kwa sababu, wengi wetu
enzi hizo kwanza hatukuwepo, kwa hiyo kwa kujifunza hapa kupitia ukurasa huu, vipo
vitu vizuri vya maisha na kimafanikio ambavyo vitatusaidia sote kutujenga kifikra
na kimaisha.
Kwa
kuwa na mimi si mchoyo, na sipendi kukunyima kitu, naomba nikukaribishe moja
kwa moja na twende tujifunze hekima na mafanikio ambazo nimekuandalia siku ya
leo. Kikubwa kaa mkao wa darasa na karibu sana.
Hekima ya 1; Hakuna mkate, pasipo kazi.
Hekima
hii inajipambanua na iko wazi ikiwa na maana kwamba pasipo kazi, usitegemee
mafanikio. Kama utakuwa umekaa tu na huweki juhudi za makusudi za kukusaidia
kuweza kupata mafanikio yako, sahau kuhusu mafanikio. Mafanikio yanakuja kwa
kazi, na kazi ndio inatupatia mkate au ridhiki ya kila siku.
Hata
vitabu vya dini vimeweza kuandika hili ‘asiyefanya
kazi na asile’ na hicho ndicho kitu unachopaswa kuzingatia. Kama unataka
mavuno ya aina fulani, jiulize ni kazi ipi ambayo umeifanya. Kumbuka wahenga wetu
kutokana na hekima zao wanasema wazi,
hakuna mkate, pasipo kazi na hio ndio kweli halisi huwezi kupinga.
Hekima ya 2; Unapokwenda kununua kitu,
tumia macho na usitumie masikio tu.
Ni mara
nyingi sana wengi wetu tunapokwenda kununua vitu iwe dukani au sokoni, huwa
tuna tabia ya kuwasikiliza sana wale wanaotuuzia na kusahau kabisa kuangalia
ubora wa kitu. Matokeo yake sasa, tunajikuta ni watu wa kuingia hasara kwa
kuchukua vitu vibovu. Utakuta mtu anasikiliza sana maelezo bila hata na yeye kuangalia
ukweli uko wapi.
Tabia
hii wanayo wengi sana, miongoni mwao inaweza ikawa ni hata wewe, lakini hapa
leo hekima hii inatukumbusha hivi, unapokwenda kununua kitu, tumia macho pia na
usitumie masikio peke yake. Hiyo ikiwa inaonyesha kwamba ni vyema kujiridhisha
kwa macho yako na si kusikiliza peke yako. Kusikiliza peke yake ni sawa na
kuamua kuingia hasara.
Hekima ya 3; Ushauri mzuri, ni bora kuliko dhahabu.
Hii ni
hekima ambayo msingi wake umejikita
katika kuonyesha kwamba ushauri mzuri siku zote ni bora kuliko dhahabu. Unaweza
ukapata dhahabu leo au mafanikio makubwa leo, lakini kama huna ushauri mzuri hiyo
ni sawa na bure, kwani ni rahisi hata kuweza kuipoteza hiyo dhahabu au kitu cha
thamani ulichokipata kama huna ushauri wa maana.
Kwa hiyo
hapa tunaonywa kuwa ni bora kupata ushauri mzuri kwanza, na kisha ushauri huo
mzuri utakusaidia kuweza kutumika katika kupata mafanikio makubwa ambayo
yanafananishwa na dhahabu. Mifano hai tunayo, waangalie watu wote ambao
walipata ushauri mbovu na maisha yao pia yapo hovyo pia.
Hekima ya 4; Usijilinde sana kwa kutumia
fensi, jilinde kwa kutumia marafiki.
Wapo
watu ambao katika maisha wanaamua kujilinda sana kwa kutumia kuta za nyumba,
wanajilinda sana kwa kutumia fensi na vitu vingine kama hivyo, na kusahau kuwa
kujilinda huko kunaweza kukawa kwa bure kama usipojua kwamba hata marafiki
ulionao pia nao ni walinzi wazuri tu.
Katika
hekima hii inatuonyesha kwamba ulinzi mzuri na wa maana upo kwa marafiki zetu
pia. Marafiki zetu ndio watakaotuambia kipi kizuri na kipi kibaya. Pia marafiki
zetu ni rahisi wao kutuonyesha marafiki wengine
wabaya na wepi ni wazuri. Kupitia hekima hii ya maisha na mafanikio ni wajibu
wetu kutafuta marafiki bora ili wawe walinzi kwetu.
Naamini
mpaka hapo kutokana na hekima ulizojifunza kuna kitu cha kipekee ambacho
umejifunza. Nikutakie wakati mwema na tukutane wiki ijayo kwa hekima zingine
kama hizi za maisha na mafanikio. Kila la kheri.
Tunakutakia
kila la kheri na endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku
kujifunza maisha na mafanikio.
Pia
rafiki, kama unapenda kujifunza zaidi kuhusu mafanikio, fursa za mafanikio
zinapopatikana, ajira pamoja na uwekezaji, karibu kwenye kundi la WHATS APP LA MAFANIKIO, kujiunga tuma
neno THE UNIVERSITY OF WINNER’S
kwenda 0713 048 035, hapo utapata
utaratibu mzima wa kujiunga.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO
YAIMARIKE,
Ni
wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na
mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 713 048 035,
Email; dirayamafanikio@gmail.com
Dec 16, 2017
Kataa Sana Kujibebesha Mzigo Huu Unapotafuta Mafanikio Yako.
Visingizio
ni moja ya njia kubwa ambayo inakufanya ushindwe moja kwa moja kwa kile kitu
ambacho unakifanya. Haijalishi visingizo hivyo unavitafuta wewe mwenyewe ama
unavikubali tu kutokana na hali unayokutana nayo kimaisha.
Lakini
unachopaswa kujua ni kwamba visingizio ni kama bendera ya ishara inayokuonyesha
sasa kushindwa kwako wewe kunakujia wakati wowote. Ndio maana unatakiwa uwe
makini sana hasa pale unapoanza kutoa visingizio ujue kushindwa kunakujia.
Ili kutokana
na visingizio unatakiwa kuchukua hatua. Ikumbukwe pia kuchukua hatua kila wakati
ni njia ya kuondokana na visingizo, lakini pale unapochelewa kuchukua hatua kwa
jambo lolote lile au kutokuchukua kabisa hapo ujue ndio chanzo kinakuja cha
kukalibisha visingio ambayo haviwezi kukusaidia.
Katika
maisha yako ya mafanikio kwa namna yoyote ile visingizo havina maana na
havikubaliki hata iweje. Unapokubali visingizio hata viwe vizuri namna gani
kwako huko ndiko kushindwa kwako kunakuja pia.
Najua
kila kushindwa kwenye maisha yako kuna sababu au kisingizio. Na kila kukosea
kwa kile unachokifanya pia kuna sababu zake, lakini usikubali sababu au
visingizo hivyo ukavitumia. Kama kuna jambo umeshindwa kubali umeshindwa,
hakuna haja ya kutoa sababu au visingizio vyovyote vile.
Kila
kisingizio unachotoa ujue kabisa kinatoa mwanya wa wewe kushindwa kwa kile
unachokifanya kwa sehemu fulani. Kwa hiyo unachotakiwa kufanya ni kukataa kutoa
visingizo kwa nguvu zote.
Wewe
kama ni kazi, chapa kazi yako kwa uhakika mkubwa sana, lakini inapotokea
umeshindwa usitumie visingizio kama silaha ya kujihami na kueleza jinsi wewe ulivyoshidwa
huko, hapo utakuwa unajiangusha wewe mwenyewe.
Wapo
watu ambao katika maisha yao ni kama wameathirika na visingizo. Kikitokea kitu kidogo
watu hawa wanakuwa na sababu nzuri sana ambazo wanatumia kama ngao ya kuhalalisha
kushindwa kwao.
Ukiwaangalia
watu ambao mara nyingi maisha yao yamejaa visingizio kwa asilimia kubwa, mara
nyingi watu hawa hawafanikiwi sana katika maisha. Na huo ndio ukweli huwezi
kufanikiwa kama wewe ni mtu wa visingizio.
Ndio
maana kati ya jambo ambalo unatakiwa kulikataa sana katika maisha yako unapotafuta
mafanikio ni kujibebesha mzigo wa visingizio. Ukiona unajibebesha mzigo huo
ujue kushindwa kunakuhusu.
Kama
ulikuwa hujui au ulikuwa hujaanza, hebu leo chukua hatua kwa kuanza kuishi
maisha yako bila visingizio. Kama ulikuwa mtu wa visingizio sana, jaribu leo tu
peke yake kuishi bila visingizo vyovyote tuone nini kitatokea kwako.
Ukiona
leo umeshinda kuishi bila visingizio, kesho ishi hivyo, utashangaa wiki nzima
umemaliza mara mwezi na yanakuwa ndio maisha yako ambayo sasa unakuwa unayaishi
pasipo kuwa na visingizo vyovyote vile.
Naamini
utaanza kujenga maisha bora sana ukiamua kuishi bila visingzio. Kumbuka unawajibika
kwenye maisha yako kwa asilimia zote. Ukileta visingizo kwa namna yoyote ile ni
sawa na kuchagua kuamua kujiangusha wewe mwenyewe.
Kwa nini
ukubali kujiangusha kwa sababu ya visingizio? Ni wakati wa kukataa kujibebesha
mzigo huu wa visingizio, ukiendelea kujibebebsha utashindwa vibaya katika
maisha yako bila kutarajia.
Fanyia kazi haya na chukua
hatua kuhakikisha ndoto zako zinatumia.
Tunakutakia kila la kheri na
endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku kujifunza maisha na
mafanikio.
Pia
rafiki, kama unapenda kujifunza zaidi kuhusu mafanikio, fursa za mafanikio
zinapopatikana, ajira pamoja na uwekezaji, karibu kwenye kundi la WHATS APP LA MAFANIKIO, kujiunga tuma
neno THE UNIVERSITY OF WINNER’S
kwenda 0713 048 035, hapo utapata
utaratibu mzima wa kujiunga.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO
YAIMARIKE,
Ni
wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na
mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 713 048 035,
Email; dirayamafanikio@gmail.com
Dec 15, 2017
Tabia Hii Haifai Kwenye Biashara Na Uwekezaji Wowote.
Kuonekana umefanya makosa mbele za watu ni kitu kinachotishia
utambulisho wa mtu, ndiyo maana watu wengi wanachukulia kufanya makosa kama
jambo la kurudi nyuma. Mtazamo wa waliowengi ni kwamba kwenda mbele ni pale tu
wenzako wanapokuona uko sahihi kwa mtazamo wao binafsi. Kutaka kuonekana sahihi
mbele ya macho ya wenzako ndiyo usababisha hali ya kupenda
kila mara kujihami, kujilinda, kulaumu watu wengine au kusingizia kitu kingine,
hasa pale inapotokea mambo yemekwenda ndivyo sivyo.
Watu walio na shauku ya kuonekana sahihi, mara nyingi ukazana sana kufanya kazi au shughuli zile zinazowathibitisha kwa watu wengine kuwa wao wana uwezo. Ukiwa mtu mwenye shauku ya kuonekana sahihi kila wakati, mara nyingi utapendelea kufanya kazi zako kwa kufuata maoni ya watu wengine.
Matokeo yake na bila kujua unajikuta unakuwa mtumwa wa watu
wengine—wanageuka kuwa mabosi wako. Hii ni kutokana na ukweli
kwamba kila jambo inabidi uwasikilize wao wanasemaje—unapata ruhusa kutoka
kwao.
Endapo ukifanya jambo la lenye manufaa kwako na kwa watu wengine
lakini wale watu wako wa karibu wakasema siyo sahihi, basi wewe utaliacha “eti
kwasababu watu wanasema siyo zuri”.
Unapokuwa mtu wa kuongozwa na maoni kutoka kwa watu wengine, ujue kuwa muda si mrefu utaanza kupoteza ubunifu wako. Kwa sababu, kila wakati unafanya kazi zako kwa tahadhari sana, ukilenga kutoonekana mbaya. Hofu ya kufanya kazi kwa kuogopa kuonekana mbaya ikizidi, kinachofuata ni kuziba kwa mfereji wa ubunifu kutoka kwenye akili yako.
Kuziba kwa mfereji maana yake ni kwamba, juhudi na akili zako
hazijikiti tena kwenye kutafuta suluhisho kwa changamoto na matatizo yaliyopo,
bali kwa kiwango kikubwa utatumia akili nyingi katika kufanya vitu ambavyo
unadhani watu wako wa karibu watakupongeza au kukusifu.
Mtu anayependa kuonekana sahihi pia ni mtu asiyeamini kama kuna mtu mwingine anaweza kufanya vizuri zaidi ya yeye. Huyu ni mtu asiyeamini vipaji vya watu wengine. Siku zote anaamini asipofanya yeye hakutakuwepo na matokeo mazuri. Kila mara anakuwa ni mtu wa kujisemea rohoni ya kwamba“bila mimi kuwepo mambo hayawezi kwenda".
Mtu anayependa kuonekana sahihi pia ni mtu asiyeamini kama kuna mtu mwingine anaweza kufanya vizuri zaidi ya yeye. Huyu ni mtu asiyeamini vipaji vya watu wengine. Siku zote anaamini asipofanya yeye hakutakuwepo na matokeo mazuri. Kila mara anakuwa ni mtu wa kujisemea rohoni ya kwamba“bila mimi kuwepo mambo hayawezi kwenda".
Ukweli ni kwamba bidhaa au huduma yoyote ile tunayoiona sokoni
haiwezi kamwe kutolewa na mtu mmoja, kwa sababu hakuna binadamu anayeweza kuwa
na vipaji vyote.
Tabia ya kupenda kuonekana sahihi kwa watu, kwenye biashara na uwekezaji haifai. Hii ni kwa sababu, kwenye biashara na uwekezaji tunaamini sana katika kuunganisha vipaji vya watu mbalimbali (timu) kwa lengo la kuzalisha suluhisho kwa changamoto na matatizo yaliyopo kwenye jamii. Tunafanya hivyo kwasababu, bidhaa na huduma unazotumia leo hii, ni matokeo ya vipaji mbalimbali vilivyounganishwa pamoja na mfanyabiashara au mwekezaji.
Katika nyanja nyingine za maisha, kuongezeka kwa watu ambao wanakupongeza na kukusifu hakuleti faida ya moja kwa moja kwako, kama ipo. Na mara nyingi ukifanikiwa kupata faida, inakuwa siyo ya kudumu. Wakati huohuo, hali ya nyanja za maisha ya biashara na uwekezaji ni tofauti kidogo na uko kwingine. Kwenye biashara, mpango mzima ni kuelekeza juhudi na akili kwenye kuzalisha, kuongeza, na kutoa thamani kubwa kwa watu wengine.
Tabia ya kupenda kuonekana sahihi kwa watu, kwenye biashara na uwekezaji haifai. Hii ni kwa sababu, kwenye biashara na uwekezaji tunaamini sana katika kuunganisha vipaji vya watu mbalimbali (timu) kwa lengo la kuzalisha suluhisho kwa changamoto na matatizo yaliyopo kwenye jamii. Tunafanya hivyo kwasababu, bidhaa na huduma unazotumia leo hii, ni matokeo ya vipaji mbalimbali vilivyounganishwa pamoja na mfanyabiashara au mwekezaji.
Katika nyanja nyingine za maisha, kuongezeka kwa watu ambao wanakupongeza na kukusifu hakuleti faida ya moja kwa moja kwako, kama ipo. Na mara nyingi ukifanikiwa kupata faida, inakuwa siyo ya kudumu. Wakati huohuo, hali ya nyanja za maisha ya biashara na uwekezaji ni tofauti kidogo na uko kwingine. Kwenye biashara, mpango mzima ni kuelekeza juhudi na akili kwenye kuzalisha, kuongeza, na kutoa thamani kubwa kwa watu wengine.
Kwenye biashara hasa kubwa, wateja ndio rafiki zetu wa karibu na
ndio kipimo cha usahihi wa kile tukifanyacho. Jukumu kubwa ni pamoja na
kuendelea kujituma na kufanya kazi kwa juhudi na maarifa mpaka pale wateja
wanaporidhika. Uzuri wa kufanya kazi kwa lengo la kuridhisha wateja wako ni
kwamba, wale wateja wanaoridhika na kazi unayoifanya wanavyozidi kuongezeka,
ndivyo kipato chako kinavyozidi kuongezeka pia.
Kama unataka kuwa mfanyabiashara na mjasiriamali mkubwa, anza leo kujiwekea mazingira ya kufuta tabia hii ya kupenda kila wakati kuwafurahisha watu. Kamwe usitake kuwa sahihi kwa ajili ya watu wengine, bali kuwa sahihi kwa ajili ya wewe mwenyewe binafsi, pia kufanya yale unayotakiwa kufanya. Usipoacha tabia hii ya kila wakati kutaka kufanya vitu vinavyokuthibitisha kwao kuwa wewe una uwezo mkubwa, nakuhakikishia kuwa haitatokea hata siku moja ukafanikiwa kwenye biashara.
Kama unataka kuwa mfanyabiashara na mjasiriamali mkubwa, anza leo kujiwekea mazingira ya kufuta tabia hii ya kupenda kila wakati kuwafurahisha watu. Kamwe usitake kuwa sahihi kwa ajili ya watu wengine, bali kuwa sahihi kwa ajili ya wewe mwenyewe binafsi, pia kufanya yale unayotakiwa kufanya. Usipoacha tabia hii ya kila wakati kutaka kufanya vitu vinavyokuthibitisha kwao kuwa wewe una uwezo mkubwa, nakuhakikishia kuwa haitatokea hata siku moja ukafanikiwa kwenye biashara.
MAKALA HII IMEANDIKWA
NA Cypridion Mushongi WA MAARIFA SHOP BLOG.
Subscribe to:
Posts
(
Atom
)