google-site-verification: googleabbfd1327a3af7a3.html

Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Kujifunza zaidi juu ya maisha na mafanikio, nakualika kwenye kundi la whats app kujifunza kwa kina. Tututumie ujumbe kwa njia ya whats app kwenda 0687449428 kupata utaratibu wa kujiunga.

Dec 16, 2017

Kataa Sana Kujibebesha Mzigo Huu Unapotafuta Mafanikio Yako.

No comments :
Visingizio ni moja ya njia kubwa ambayo inakufanya ushindwe moja kwa moja kwa kile kitu ambacho unakifanya. Haijalishi visingizo hivyo unavitafuta wewe mwenyewe ama unavikubali tu kutokana na hali unayokutana nayo kimaisha.
Lakini unachopaswa kujua ni kwamba visingizio ni kama bendera ya ishara inayokuonyesha sasa kushindwa kwako wewe kunakujia wakati wowote. Ndio maana unatakiwa uwe makini sana hasa pale unapoanza kutoa visingizio ujue kushindwa kunakujia.
Ili kutokana na visingizio unatakiwa kuchukua hatua. Ikumbukwe pia kuchukua hatua kila wakati ni njia ya kuondokana na visingizo, lakini pale unapochelewa kuchukua hatua kwa jambo lolote lile au kutokuchukua kabisa hapo ujue ndio chanzo kinakuja cha kukalibisha visingio ambayo haviwezi kukusaidia.
Katika maisha yako ya mafanikio kwa namna yoyote ile visingizo havina maana na havikubaliki hata iweje. Unapokubali visingizio hata viwe vizuri namna gani kwako huko ndiko kushindwa kwako kunakuja pia.

Najua kila kushindwa kwenye maisha yako kuna sababu au kisingizio. Na kila kukosea kwa kile unachokifanya pia kuna sababu zake, lakini usikubali sababu au visingizo hivyo ukavitumia. Kama kuna jambo umeshindwa kubali umeshindwa, hakuna haja ya kutoa sababu au visingizio vyovyote vile.
Kila kisingizio unachotoa ujue kabisa kinatoa mwanya wa wewe kushindwa kwa kile unachokifanya kwa sehemu fulani. Kwa hiyo unachotakiwa kufanya ni kukataa kutoa visingizo kwa nguvu zote.
Wewe kama ni kazi, chapa kazi yako kwa uhakika mkubwa sana, lakini inapotokea umeshindwa usitumie visingizio kama silaha ya kujihami na kueleza jinsi wewe ulivyoshidwa huko, hapo utakuwa unajiangusha wewe mwenyewe.
Wapo watu ambao katika maisha yao ni kama wameathirika na visingizo. Kikitokea kitu kidogo watu hawa wanakuwa na sababu nzuri sana ambazo wanatumia kama ngao ya kuhalalisha kushindwa kwao.
Ukiwaangalia watu ambao mara nyingi maisha yao yamejaa visingizio kwa asilimia kubwa, mara nyingi watu hawa hawafanikiwi sana katika maisha. Na huo ndio ukweli huwezi kufanikiwa kama wewe ni mtu wa visingizio.
Ndio maana kati ya jambo ambalo unatakiwa kulikataa sana katika maisha yako unapotafuta mafanikio ni kujibebesha mzigo wa visingizio. Ukiona unajibebesha mzigo huo ujue kushindwa kunakuhusu.
Kama ulikuwa hujui au ulikuwa hujaanza, hebu leo chukua hatua kwa kuanza kuishi maisha yako bila visingizio. Kama ulikuwa mtu wa visingizio sana, jaribu leo tu peke yake kuishi bila visingizo vyovyote tuone nini kitatokea kwako.
Ukiona leo umeshinda kuishi bila visingizio, kesho ishi hivyo, utashangaa wiki nzima umemaliza mara mwezi na yanakuwa ndio maisha yako ambayo sasa unakuwa unayaishi pasipo kuwa na visingizo vyovyote vile.
Naamini utaanza kujenga maisha bora sana ukiamua kuishi bila visingzio. Kumbuka unawajibika kwenye maisha yako kwa asilimia zote. Ukileta visingizo kwa namna yoyote ile ni sawa na kuchagua kuamua kujiangusha wewe mwenyewe.
Kwa nini ukubali kujiangusha kwa sababu ya visingizio? Ni wakati wa kukataa kujibebesha mzigo huu wa visingizio, ukiendelea kujibebebsha utashindwa vibaya katika maisha yako bila kutarajia.

Fanyia kazi haya na chukua hatua kuhakikisha ndoto zako zinatumia.
Tunakutakia kila la kheri na endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku kujifunza maisha na mafanikio.
Pia rafiki, kama unapenda kujifunza zaidi kuhusu mafanikio, fursa za mafanikio zinapopatikana, ajira pamoja na uwekezaji, karibu kwenye kundi la WHATS APP LA MAFANIKIO, kujiunga tuma neno THE UNIVERSITY OF WINNER’S kwenda 0713 048 035, hapo utapata utaratibu mzima wa kujiunga.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Ni wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 713 048 035,



No comments :

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.