Jul 31, 2021
Jambo Hili Huwezi Kulikosa Kwenye Safari Ya Mafanikio Yako.
Kama ilivyo vizuizi au changamoto katika safari ya mafanikio ni lazima, halikadharika pia, kukatishwa tamaa ni lazima au ni kituo kimojawapo katika safari yako hiyo ya mafanikio uliyonayo.
Ni lazima katika safari yako ya mafanikio ifike mahali kwa namna moja au nyingine ukutane na kukatishwa tamaa. Hili unatakiwa ulijue na ikitokea kwako umekatishwa tamaa usishangae na kuumizwa sana.
Jambo la kuzingatia unapokatishwa tamaa, wewe endelea kusonga mbele. Hata siku moja usijaribu, kuacha hicho unachofanya kisa umekatishwa tamaa. Utaweza kufanikiwa pia, kama ukiamua kwenda mbele.
Tambua, kukatishwa tamaa, nacho ni kituo kimojawapo katika safari ya mafanikio kama ilivyo tu changamoto zako. Acha kushangaa unapokatishwa tamaa, wewe amua kwenda mbele hadi kuweza kufanikiwa.
Kila la kheri katika kufikia
mafanikio yako.
Kama unapenda kujiunga na kundi la mafanikio
ili uweze kujifunza zaidi mambo mengi ya kimafanikio. Tuma neno THE
UNIVERSITY OF WINNER'S kwenda 0687449428 na utapewa utaratibu wa
kuunganishwa.
Hakimiliki©2021 Imani Ngwangwalu.
Haki Zote Zimehifadhiwa. Makala hizi hutolewa kwa ajili ya kuboresha maisha
yako. Ruksa 'kushare' na usibadili kitu chochote bila ya ruhusa ya mwandishi.
Jul 30, 2021
Kama Utachukua Hatua Hizi, Tayari Umeshindwa.
Kitu chochote kile ambacho utakifanya kwa kuchukua hatua za kusitasita, yaani unachukua hatua kama unaogopa hivi, basi tambua na matokeo yake utayapa kwa namna hiyo hiyo.
Huwezi kupata matokeo makubwa kabisa kama hatua zako ni za kusita sita kila wakati, ni lazima utapata matokeo yanayoendana na kusita kwako na haitakuwa kinyume cha hapo.
Hata kama umejiwekea malengo mazuri sana, kama hautaweza kujitoa kikamilifu kufikia hayo malengo na ukaishia kusitasita basi elewa, hutapata matokeo makubwa yanayotakiwa.
Acha kusita, chukua hatua huku ukiwa na moyo wote, nenda mazima mazima kuelekea kwenye ndoto zako. Fanya kila linawezekana kufanikisha ndoto yako na acha kusita sita.
Jambo la kuzingatia hapa, ni kwa wewe kuchukua hatua na acha kusita, jiamini, usiogope, chukua hatua zako mara moja. Nenda kwenye kuchukua hatua zako. Kama utaendelea kusitasita, kufanikiwa kwako itakuwa ni ngumu sana.
Kila la kheri katika kufikia mafanikio yako.
Kama unapenda kujiunga na kundi la mafanikio
ili uweze kujifunza zaidi mambo mengi ya kimafanikio. Tuma neno THE
UNIVERSITY OF WINNER'S kwenda 0687449428 na utapewa utaratibu wa
kuunganishwa.
Hakimiliki©2021 Imani Ngwangwalu.
Haki Zote Zimehifadhiwa. Makala hizi hutolewa kwa ajili ya kuboresha maisha
yako. Ruksa 'kushare' na usibadili kitu chochote bila ya ruhusa ya mwandishi.
Jul 29, 2021
Kama Unaogopa Kusubiria Kitu Hiki, Huwezi Kufanikiwa.
Kuna wakati unaweza ukajiwekea malengo yako, na ukaona malengo yako, yanatumia pengine miaka mitatu, mitano, kumi au zaidi na ukaona kazi sana, na ukajiambia hii ni miaka mingi sana, ngumu kuyafikia na ukaanza kuyafikiria kuyaacha.
Sasa nikwambie, miaka ya kusubiria yaani hiyo iwe mitatu, mitano, au kumi kabisa na ukaona ni mingi lakini sio kitu, ni michache sana. Unaweza usichukue hatua na kutofanya chochote lakini ukashangaa hiyo miaka unayosubiria imefika na huna kitu chochote.
Unatakiwa ujue siku na maisha vinaenda kama upepo. Hakuna miaka mingi katika kusubiri ndoto zako, miaka hiyo hata uone mingi vipi itafika, hivyo wajibu wako ni kuchukua hatua za kuelekea kwenye ndoto yako.
Acha kujidanganya kwamba, aah hii ni miaka mingi sana, siwezi kuvumilia, hapana, miaka hiyo kama nilivyosema itafika na hutaamini. Kila siku weka mipango yako na usiogope wingi wa miaka ya kusubiria.
Kila la kheri katika kufikia
mafanikio yako.
Kama unapenda kujiunga na kundi la mafanikio
ili uweze kujifunza zaidi mambo mengi ya kimafanikio. Tuma neno THE
UNIVERSITY OF WINNER'S kwenda 0687449428 na utapewa utaratibu wa
kuunganishwa.
Hakimiliki©2021 Imani Ngwangwalu.
Haki Zote Zimehifadhiwa. Makala hizi hutolewa kwa ajili ya kuboresha maisha
yako. Ruksa 'kushare' na usibadili kitu chochote bila ya ruhusa ya mwandishi.
Jul 28, 2021
Vurugu Nyingi Za Kimaisha Zipo Hapa.
Maisha ya chini, maisha ya kawaida ya kimafanikio ambayo kila mtu anaweza kuishi yana fujo na vurugu nyingi sana. Ndani ya maisha hayo ndio utasikia habari za kurogana, kuoneana wivu na kufanyiana kila aina ya fitina na hila mbaya.
Ili uweze kutoka hapo kwenye maisha ya watu wa chini ambayo yana kila chuki na ubaya, unatakiwa ufanye kazi sana na uwe na maisha ya juu. Ukiwa na maisha ya juu na umefanikiwa sana, hata wapige kelele, nakwambia kelele hizo zitaishia chini hutazisikia na wala hakuna wa kukuloga wala kukufanya kitu.
Kama hizo fitina za kulogana zingekuwepo kwenye mafanikio, kwa nini watu wenye mafanikio makubwa sana kama akina Bill Gates wao hawarogeki? hapo ndipo utajua uchawi hauendi kwa kila mtu, upo huku chini tu kwa walalahoi walio wengi.
Kama unataka kuishi maisha ya raha na mstarehe, ishi maisha ya watu wa juu, yaani maisha ya viwango vya juu, watu wa huku chini hata wapige kelele sana, nakwambia hutaweza kuwasikia tena, kaa ukijua hilo kabisa na lifanyie kazi na utaniambia.
Ninachotaka kukusisitizia hapa ni kwamba, tafuta mafanikio makubwa rafiki yangu. Ukiwa na mafanikio makubwa, hizi kelele za huku chini za fitina, kijicho au kurogana hutaweza kuzisikia kabisa maishani mwako na utaishi kwa amani ukisaka mafanikio yako tu.
Kila la kheri katika kufikia
mafanikio yako.
Kama unapenda kujiunga na kundi la mafanikio
ili uweze kujifunza zaidi mambo mengi ya kimafanikio. Tuma neno THE
UNIVERSITY OF WINNER'S kwenda 0687449428 na utapewa utaratibu wa
kuunganishwa.
Hakimiliki©2021 Imani Ngwangwalu.
Haki Zote Zimehifadhiwa. Makala hizi hutolewa kwa ajili ya kuboresha maisha
yako. Ruksa 'kushare' na usibadili kitu chochote bila ya ruhusa ya mwandishi.
Jul 27, 2021
Jiwekee Utaratibu Huu, Utafanikiwa.
Kila mtu ana mawazo mazuri ya mafanikio. Kila mtu mawazo hayo huwa anayo na hakuna ambae hana mawazo mazuri ya kumsaidia kufanikiwa. Mawazo hayo huwa yapo na ukiwa mwangalifu utayaona na kuyagundua mara moja.
Pamoja na kwamba mawazo hayo mazuri yapo kwa kila mtu, tatizo linakuja kwamba, mawazo hayo, wengi hawayatumii, na wanayapoteza kwa sababu hawayaandiki sehemu. Hawa wanakuwa wanafikiri kwamba watakumbuka mawazo hayo.
Kihalisia haiko hivyo, kila wazo unatakiwa uliandike ambalo unaona ni wazo bora na lina msaada kwako hata kesho ili lisipotee. Wewe unafikiria wazungu ni 'malofa' hadi walipoamua kuweka kila kitu kwenye maandishi?
Kuandika mawazo yako mazuri kila yanapokuja ni utaratibu mzuri wa kutunza mawazo yako ili yasipotee kwa urahisi. Ushauri wangu kwako, andaa kijitabu cha kuandika mawazo mazuri yanavyokuja kwako, yaandike, yafanyie kazi, utafanikiwa.
Kila la kheri katika kufikia
mafanikio yako.
Kama unapenda kujiunga na kundi la mafanikio
ili uweze kujifunza zaidi mambo mengi ya kimafanikio. Tuma neno THE
UNIVERSITY OF WINNER'S kwenda 0687449428 na utapewa utaratibu wa
kuunganishwa.
Hakimiliki©2021 Imani Ngwangwalu.
Haki Zote Zimehifadhiwa. Makala hizi hutolewa kwa ajili ya kuboresha maisha
yako. Ruksa 'kushare' na usibadili kitu chochote bila ya ruhusa ya mwandishi.
Jul 26, 2021
Kama Unataka Mafanikio Ishinde Sauti Hii.
Inawezakana umesema unaweza kuishinda changamoto hii iliyo mbele yako, lakini ndani yako bado kuna sauti inayokwambia kwamba hiyo changamoto huwezi kuishinda.
Inawezekana umefanikiwa kuushawishi ulimwengu wa nje kwa hicho unachokifanya, lakini umeshindwa kuishawishi sauti ya ndani mwako na inazidi kukwambia kwamba huwezi.
Ili kuwa mshindi wa kweli, unatakiwa kuishinda sauti ya ndani yako, sauti inayosema huwezi na kujiambia kwamba sasa unaweza,..unaweza kufanikiwa na kufika mbali kimafanikio.
Kila mtu ndani yake ana sauti hii ya mashaka. Sauti hii haitakiwi kukushinda unatakiwa uishinde na ujiambie unaweza, unaweza. Kila siku sema naweza, naweza na utashangaa utaweza kweli.
Kila la kheri katika kufikia mafanikio yako.
Kama unapenda kujiunga na kundi la mafanikio ili uweze kujifunza zaidi mambo mengi ya kimafanikio. Tuma neno THE UNIVERSITY OF WINNER'S kwenda 0687449428 na utapewa utaratibu wa kuunganishwa.
Hakimiliki©2021 Imani Ngwangwalu.
Haki Zote Zimehifadhiwa. Makala hizi hutolewa kwa ajili ya kuboresha maisha
yako. Ruksa 'kushare' na usibadili kitu chochote bila ya ruhusa ya mwandishi.
Jul 25, 2021
Ukijiambia Hivi, Kila Kitu Utaweza.
Inawezekana umejiambia huwezi kufanya biashara, huwezi kuongea mbele za watu, huwezi kuchora au hata umejiambia huwezi kutoka hapo ulipo kimafanikio na umeamua kubaki katika eneo ulilo zoea kimaisha.
Kama umejiambia hivyo mara nyingi, nataka nikwambie hiyo sio sababu ya wewe kubaki hapo. Unaweza ukaweza hicho unachojiambia kila wakati huwezi, na ukapiga hatua kubwa za mafanikio yako uyatakayo.
Nini unachojiambia huwezi leo, kitu hicho unaweza ukakiweza ikiwa utaamua. Hamna haja ya kubaki pale pale ulipo na kujiambia ooh huwezi huwezi, unaweza kufanikiwa na kuweza hicho unachosema huwezi.
Amua kutoka kwenye hali ya mazoea yako ya kila siku, na utaweza
hicho unachosema kila wakati kwamba huwezi. Kwa nini usiweze, inawezekana
ukaweza, jambo la kuzingatia jiambie "naweza" na utaweza kweli.
Kila la kheri katika kufikia mafanikio yako.
Kama unapenda kujiunga na kundi la mafanikio ili uweze kujifunza zaidi mambo mengi ya kimafanikio. Tuma neno THE UNIVERSITY OF WINNER'S kwenda 0687449428 na utapewa utaratibu wa kuunganishwa.
Hakimiliki©2021 Imani Ngwangwalu.
Haki Zote Zimehifadhiwa. Makala hizi hutolewa kwa ajili ya kuboresha maisha
yako. Ruksa 'kushare' na usibadili kitu chochote bila ya ruhusa ya mwandishi.
Jul 24, 2021
Vitu Hivi Havifatiliwi Katika Maisha.
Mara nyingi sana, hakuna mtu ambaye anapenda kufatilia vitu vilivyokufa au vitu vilivyokosa matumaini. Kila mtu anapenda kufatilia vitu vilivyo hai, vitu ambavyo vinaweza vikamsaidia leo na kesho pia.
Kwa mfano, kama umelima shamba, na shambani kwako kuna mimea imekufa, mimea hiyo iliyokufa utakuwa huna muda wa kuifatilia kabisa, utachokuwa ukifatilia ni mimea hai na yenye faida kwako.
Na kwenye maisha iko hivyo hivyo. Hakuna mtu ambae yuko tayari kufatilia vitu vilivyokufa. Ukiona watu hawakufatilii sana, basi elewa mambo yako mengi yamekufa na hakuna wa kutaka tena kuyajua.
Kama mambo yako mengi yamekufa, hakuna wa kukufatilia hiyo iko
wazi. Kama unataka mambo yako yaanze kufatiliwa hakikisha kila kitu unakifanya
kiwe hai. Kila kitu kifufue, utafatiliwa sana na hutaamini.
Kila la kheri katika kufikia
mafanikio yako.
Kama unapenda kujiunga na kundi la mafanikio ili uweze kujifunza zaidi mambo mengi ya kimafanikio. Tuma neno THE UNIVERSITY OF WINNER'S kwenda 0687449428 na utapewa utaratibu wa kuunganishwa.
Hakimiliki©2021 Imani Ngwangwalu.
Haki Zote Zimehifadhiwa. Makala hizi hutolewa kwa ajili ya kuboresha maisha
yako. Ruksa 'kushare' na usibadili kitu chochote bila ya ruhusa ya mwandishi.
Jul 23, 2021
Umechagua Kuwa Mshindi Au Mshindwaji Katika Maisha Yako?
Washindwaji katika maisha husema, "niko bize sana sina muda". Washindi katika maisha wao wanasema " nitatafuta muda na nitaweza kufanya".
Washindwaji kila wakati wao wanatafuta visingizio vya kufanya jambo. Washindi katika mafanikio wao hutafuta njia ya kufikia mafanikio yao makubwa.
Washindwaji katika maisha hulalamika sana juu ya maisha yao jinsi yalivyo, washindi katika maisha wao huchukua hatua na kuamua kuwajibika.
Washindwaji katika maisha hulaani kwa ajili mambo au matukio waliyokutana nayo jana, washindi wao huandaa kesho yao kwa ubora zaidi.
Washindwaji hutafuta majibu mepesi sana ya maisha yao, wakati washindi wao hutumia muda wa kutosha kutafuta majibu na suluhu ya maisha yao.
Washindwaji katika maisha hawataki kubeba jukumu lote la maisha yao, wakati washindi wao wanaamua kubeba jukumu lote la maisha yao, upo?
Kwa kila siku unayoipata, una nafasi ya kukaa upande wa washindi au washindwaji. Uamuzi unabaki ni kwako, unataka uwe upande upi wewe, basi.
Kila la kheri katika kufikia mafanikio yako.
Kama unapenda kujiunga na kundi la mafanikio
ili uweze kujifunza zaidi mambo mengi ya kimafanikio. Tuma neno THE
UNIVERSITY OF WINNER'S kwenda 0687449428 na utapewa utaratibu wa
kuunganishwa.
Hakimiliki © 2021 Imani Ngwangwalu.
Haki Zote Zimehifadhiwa. Makala hizi hutolewa kwa ajili ya kuboresha maisha
yako. Ruksa 'kushare' na usibadili kitu chochote bila ya ruhusa ya mwandishi.
Jul 22, 2021
Ndoto Yako Ni Ipi?
Gari unayoendesha ilibuniwa na kutengenezwa na mtu ambae alikuwa na ndoto ya kubuni gari na mtu huyo akabuni gari.
Barabara unayotumia kusafiria ipo hapo kwa sababu ilibuniwa na mtu ambae alikuwa na ndoto za kutengeza barabara.
Simu unayotumia ilibuniwa na mtu ambae alikuwa na ndoto ya kubuni simu ili kuweza kurahisha mawasiliano duniani kote.
Chochote kile unachokitumia, kimebuniwa na watu ambao walikuwa na ndoto kubwa ya vitu hivyo.
Mafanikio yote duniani huanza na ndoto. Hakuna mafanikio yasiyoanza na ndoto hata kidogo, ndoto ni lazima.
Kwa bahati mbaya, zipo ndoto nyingi ambazo hazijatimizwa au zimekufa hata kabla hazijatokea kwa nje na hazipo tena.
Unachotakiwa ni kutimiza ndoto zako na sio kuziacha mpaka ndoto hizo zife, timiza ndoto zako zile ulizonazo.
Ndoto yako ni ipi uliyonayo na unataka kuitimiza? basi itimize ndoto hiyo. Ifanyie kazi ndoto yako hadi itimie.
Vitu unavyotumia, viko hivyo kwa sababu kuna mtu alikuwa na ndoto juuya vitu hivyo unavyovitumia leo.
Je, wewe uko tayari kutumia ndoto za wenzako tu, hapana, isiwe
hivyo kwako, hakikisha na wewe uwe na ndoto yako.
Kila la kheri katika kufikia mafanikio yako.
Kama unapenda kujiunga na kundi la mafanikio
ili uweze kujifunza zaidi mambo mengi ya kimafanikio. Tuma neno THE
UNIVERSITY OF WINNER'S kwenda 0687449428 na utapewa utaratibu wa
kuunganishwa.
Hakimiliki©2021 Imani Ngwangwalu. Haki Zote Zimehifadhiwa. Makala hizi hutolewa kwa ajili ya kuboresha maisha
yako. Ruksa 'kushare' na usibadili kitu chochote bila ya ruhusa ya mwandishi.
Jul 21, 2021
Ukielewa Mafanikio Yanataka Kitu Hiki, Tayari Umefanikiwa.
Benki zinatabia ya kuazima watu pesa ambao tayari wameonyesha uwezo wa kutengeneza pesa. Waajiri pia wanatabia ya kuajiri watu ambao wanaamini wana uwezo mkubwa wa kuisaidia kampuni.
Hata watu ambao ambao tayari wamefanikiwa, ni watu ambao tunasema wana nafasi kubwa ya kuweza kufanikiwa hata baadae pia. Kwa nini iko hivyo, wala si kwa sababu wana bahati au wanajua siri na mbinu zilizofichika au fursa nyingi, HAPANA.
Chukua Hatua Chanya, Utafanikiwa |
Watu hao wanafanikiwa kwa sababu, wanajua namna ya kuchukua hatua chanya hata pale kwenye changamoto nzito zinazowakabili na kuweza hadi kufanikiwa kwa viwango vikubwa.
Pasipo kujali ni nini kinakuwakuta kwenye njia ya mafaniko yao, watu hao wana uwezo wa kukabiliana na chochote na kufika mbali kimafanikio. Hata wewe ukijua namna ya kuchukua hatua chanya katika hali yoyote hata kama ni ya kukatisha tamaa, utafanikiwa pia.
Kila la kheri katika kufikia mafanikio yako.
Kama unapenda kujiunga na kundi la mafanikio ili uweze kujifunza zaidi mambo mengi ya kimafanikio. Tuma neno THE UNIVERSITY OF WINNER'S kwenda 0687449428 na utapewa utaratibu wa kuunganishwa.
Hakimiliki © 2021 Imani
Ngwangwalu. Haki Zote Zimehifadhiwa. Makala hizi hutolewa kwa ajili ya
kuboresha maisha yako. Ruksa 'kushare' na usibadili kitu chochote bila ya
ruhusa ya mwandishi.
Jul 20, 2021
Chukua Hatua Hizi, Utafanikiwa.
Kwa kadri unavyochukua hatua chanya kuelekea kwenye ndoto zako, hapo unakuwa unapiga HATUA. Hata kama kuna kuna wakati unaonekana unarudi nyuma, unakata tamaa au una msongo wa mawazo na unaona mambo hayaendi, lakini kwa kuwa unachukua hatua chanya, weka akilini unapiga HATUA.
Kadri unavyochukua hatua chanya, utajua mafanikio unayoyataka ni mchakato wala si tukio la mara moja. Kuna mambo mengi ya kujifunza kabla hujafikia mafanikio yako, kama vile kujua kipi kinafanya kazi na kipi hakifanyi kazi. Unatakiwa kujua vizuizi si kitu ni muhimu kukupa fundisho la mafanikio.
Chukua Hatua Za Kuelekea Ndoto Yako |
Kitu cha kuzingatia, endelea kuchukua hatua za kuelekea ndoto yako. Endelea tu kuweka juhudi na kupiga kazi, utakaribia mafanikio yako. Hata kama unapata matokeo hovyo kwa sasa, lakini kwa kila juhudi unayoiweka inakusaidia kupiga HATUA. Ni nini au kipi unasubiria, chukua hatua, UTAFANIKIWA.