Jul 28, 2021
Vurugu Nyingi Za Kimaisha Zipo Hapa.
Maisha ya chini, maisha ya kawaida ya kimafanikio ambayo kila mtu anaweza kuishi yana fujo na vurugu nyingi sana. Ndani ya maisha hayo ndio utasikia habari za kurogana, kuoneana wivu na kufanyiana kila aina ya fitina na hila mbaya.
Ili uweze kutoka hapo kwenye maisha ya watu wa chini ambayo yana kila chuki na ubaya, unatakiwa ufanye kazi sana na uwe na maisha ya juu. Ukiwa na maisha ya juu na umefanikiwa sana, hata wapige kelele, nakwambia kelele hizo zitaishia chini hutazisikia na wala hakuna wa kukuloga wala kukufanya kitu.
Kama hizo fitina za kulogana zingekuwepo kwenye mafanikio, kwa nini watu wenye mafanikio makubwa sana kama akina Bill Gates wao hawarogeki? hapo ndipo utajua uchawi hauendi kwa kila mtu, upo huku chini tu kwa walalahoi walio wengi.
Kama unataka kuishi maisha ya raha na mstarehe, ishi maisha ya watu wa juu, yaani maisha ya viwango vya juu, watu wa huku chini hata wapige kelele sana, nakwambia hutaweza kuwasikia tena, kaa ukijua hilo kabisa na lifanyie kazi na utaniambia.
Ninachotaka kukusisitizia hapa ni kwamba, tafuta mafanikio makubwa rafiki yangu. Ukiwa na mafanikio makubwa, hizi kelele za huku chini za fitina, kijicho au kurogana hutaweza kuzisikia kabisa maishani mwako na utaishi kwa amani ukisaka mafanikio yako tu.
Kila la kheri katika kufikia
mafanikio yako.
Kama unapenda kujiunga na kundi la mafanikio
ili uweze kujifunza zaidi mambo mengi ya kimafanikio. Tuma neno THE
UNIVERSITY OF WINNER'S kwenda 0687449428 na utapewa utaratibu wa
kuunganishwa.
Hakimiliki©2021 Imani Ngwangwalu.
Haki Zote Zimehifadhiwa. Makala hizi hutolewa kwa ajili ya kuboresha maisha
yako. Ruksa 'kushare' na usibadili kitu chochote bila ya ruhusa ya mwandishi.
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.