Mar 10, 2019
Ikiwa Unaishi Hivi, Maisha Yako Ni Mafupi Sana.
Ni jambo ambalo watu
hulisema mara nyingi bila kujua maana
yake. Unaweza kukuta mtu akisema, ‘ndio
maana amekauka, ana roho mbaya sana’. Ukimuuliza ni kwa nini anahusisha
kukauka au afya mbaya na roho mbaya au kukosa upendo alikonako mtu, hataweza
kukupa jibu sahihi. Lakini, anajua kwamba, kukauka huwapata wenye roho mbaya. Kauli
hiyo ina ukweli mkubwa wa kutosha. Watu wengi ambao wanatengeneza nguvu nyingi
hasi, hatimaye nguvu hizo huwarudia na kuwadhuru.
Kwa sehemu kubwa,
madhara ya nguvu hizo huja kujitokeza
kwenye miili yao. Mtu ambaye anaumwa mara kwa mara, anaweza kuwa anaumwa tu kwa
sababu nyingine, lakini pia anaweza kuwa anaumwa kutokana na nguvu hasi
anazotengeneza. Nikisema nguvu hasi, nina maana ya kufikiri na matendo ambayo
yanamuumiza mwenye mawazo na matendo hayo, pia wale wanaomzunguka. Kwa mfano,
mtu asiyeweza kusamehe, mwenye visasi, mwenye kijicho, mpenda makuu, mshindani
na mengine ya aina hiyo.
Kuna watu ambao hutengeneza sana nguvu hasi
kwa kufikiri kwao na tabia zao. Kwa kawaida, nguvu hasi huwa zinadhuru hisia na
mwili wa mhusika. Kwa vipi? Hebu tutazame kushindwa kusamehe na kijicho. Mtu ambaye
hawezi kusamehe, anajiweka mahali ambapo muda wote anakuwa kwenye hasira, hisia
chungu na mikakati ya kulipa kisasi. Hii ni sawa na mtu ambaye ana kijicho, kwa
mfano. Huyu naye, muda mwingi wa maisha yake, atakuwa akiumia kwani, kila
wengine wakifanikiwa kwa chochote, atajihisi vibaya tu. kwa hiyo, hisia zake
zitakuwa zinachokozeka karibu muda wote.
Kwa kawaida, hisia zetu
zinapochokozeka, tunaiiingiza miili yetu kwenye kuzalisha kemikali au homoni
ambazo wakati huo hazihitajiwi. Kwa uzalishwaji huo wa kemikali zisizohitajika
mwilini, tunaiumiza miili yetu kwa njia mbalimbali. Kemikali hizo, hatimaye
huanza kutuumiza kwa kuteleta maradhi mvalimbali miilini mwetu. Hili ni jamba
ambalo limethibitishwa kitaalamu.
Kuna maradhi zaidi ya
kumi ambayo chanzo chake ni mihemko yetu, maradhi ambayo kitaalamu hufahamika
kama Emotionally Induced Diseases. Haya
ni pamoja na maumivu ya mwili, tumbo, kufunga choo na mengine. Ndiyo maana,
wale watu wote wanaokwenda hospitalini wakiwa wanaumwa, ambao wanaambiwa vipimo
havioneshi maradhi yoyote, ukiwachunguza, utagundua kwamba, wanakabiliwa na
hofu, mashaka, visasi na matatizo
mengine ya kihisia.
Sisemi kwamba, wote
wanaopimwa na kuonekana hawana maradhi ndivyo walivyo, hapana. Lakini wengi
kati yao ndivyo walivyo. Hata wale wanaodaiwa kuwa na mapepo pia, utakuta
baadhi ni wale wenye hisia chungu. Kwa sababu ya maumivu ya kimwili na yale ya
kiakili, unakuta watu hawa wakiwa dhaifu. Kama walivyo wagonjwa wengine, suala
la udhaifu wa kimwili hujitokeza sana kwa watu hawa, kwani pamoja na maradhi
yanayoletwa na hisia chafu, kinga ya mwili hushuka sana pale miili inapohemkwa
mara kwa mara.
Ni rahisi kwa hali
hiyo, watu wenye roho mbaya kukauka au kukosa afya imara. Ingawa siyo kweli
hata hivyo kuwa watu wote wenye afya mbovu, inatokana na roho mbaya, hapana. Lakini,
kwa wale walio na roho mbaya, yaani kufikiri na tabia zenye kuzalisha nguvu
hasi, ni rahisi zaidi kwao kukosa afya bora kama tulivyoona. Ndiyo maana
tunasema hivi, kama unaishi maisha haya kuwa na roho mbaya tu, maisha yako ni
mafupi kwa sababu utakuwa ni wa afya mbovu kitu ambacho ni hatari sana kwako.
Nakutakia kheri ya
mwaka mpya, endelea kutembelea DIRA YA MAFANIKIO kujifunza na kuhamasika kila
siku.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA
MAISHA YAKO YAIMARIKE,
IMANI
NGWANGWALU,
0713
048 0345/dirayamafanikio@gmail.com
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.