Mar 8, 2019
Kama Utaruhusu Kelele Hizi…Utashindwa Kufanikiwa.
Usisikilize kila kitu |
Zipo
kelele nyingi sana katika dunia hii ya habari. Utasikia hiki mara utasikia kile,
ilimradi kukicha tu zipo habari na taarifa nyingi ambazo zinatolewa ambazo
lengo lake wewe uzisikie na pengine kuzifanyia kazi.
Usipokuwa
makini utajikuta kila kitu unataka kufatilia. Sasa njia ya kuweza kujiokoa na
kelele hizo na kuweza kufanikisha malengo yako ni kwa wewe kuweka nguvu zako za
uzingativu kwa kile unachokifanya.
Angalia
kipi unakifanya, kisha kifatilie kitu hicho kila siku. Kelele za huku mara kule
acha kuzifatilia zitakupoteza. Kumbuka, mikwenzi mingi ilimpoteza mbwa
mawindoni, usiwe miongoni mwa watu watakao potea kwa sababu ya kelele.
Simamia
na fatilia mipango yako kwa kuweka nguvu za uzingativu kwa kile ukifanyacho na
utafanikiwa. Kuendelea kusikiliza kelele au kila linalosemwa utakuwa ni sawa na
mtu ambaye ameamua kujipoteza yeye mwenyewe.
Katika
dunia ya sasa, ni rahisi sana kusikia fursa hii au ile, lakini kwa ukweli
uliowazi wewe kama wewe huwezi kufanya kila kitu. Kama ni fursa ni lazima
utafanya chache na si kila fursa itakuwa yako.
Hivyo
unatakiwa kuwa makini na taarifa unazozipokea. Unatakiwa kuwa mtulivu na usiwe
mtu ambaye unaendeshwa na mihemiko isiyo ya maana. Kelele za dunia zisikuyumbishe
hata kidogo, fuata malengo yako.
Ikitokea
umekubali kuyumbishwa na dunia au na kelele za dunia, basi utaishi kama bendera
fuata upepo maana hutafika popote. Utagusa hiki mara kile na kila kitu utakuwa
unakianza na kukiacha kila ukisikia kuna kingine kizuri kinalipa.
Kuanzia
leo jifunze kuweka masikio yako pamba, jifunze kuweka nguvu zako za uzingativu
eneo moja, mahali ambapo utafanya kitu na kitaonekana cha thamani. Ukiziba masikio
usisikie kitu, utajenga uwezo mkubwa wa kufanikiwa.
Chukua
hatua kwa kufanyia kazi hicho ulichojifunza na endelea kutembelea
dirayamafanikio.blogspot.com kujifunza na kuhamasika zaidi kila siku.
Ni
wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na mjasiriamali,
Blog, dirayamafanikio.blogspot.com
Mawasiliano; +255 713
048 035,
Email; dirayamafanikio@gmail.com
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.