Dec 20, 2014
Kama Unafanya Mambo Haya, Utajiri Kwako Ni Lazima.
Kuwa na mafanikio
makubwa na hatimaye kuwa tajiri ni kitu ambacho kinaonekana kuwa kigumu kwa
wengi ama hakiwezekani kabisa. Hii yote inatokana na wengi kutokujua njia au
mambo muhimu ya kufanya hadi kufikia mafanikio makubwa. Kutokana na hili wengi
wamekuwa wakijiuliza wafanye nini au kitu gani kitakachowafanikisha katika
maisha yao.
Kiuhalisia, katika
maisha kuna vitu ambavyo ukifanya iwe kwa kukusudia au bahati ni lazima uwe
tajiri na pia kuna vitu ambavyo ukifanya, sahau mafanikio katika maisha yako. Vitu
hivi vinaweza kuwa tabia zetu au mienendo tuliyonayo ambayo inakuwa inaathari
kubwa kwetu na hii ndiyo naweza sema ni siri kubwa iliyofichika kati ya watu wenye
mafanikio na ambao hawana.
Watu wenye mafanikio
wamemudu kwa kiasi kikubwa kufanya mambo yanayowafanya wawe matajiri, huku
maskini wakiwa hawajui hilo na kuendelea kufanya vitu vinavyowafanya kuwa
maskini. Kwa wewe kulijua hilo tu, tayari una nafasi kubwa ya kufanikiwa na
kufanya mambo makubwa katika maisha yako. Kama
kweli umechoshwa na umaskini, na umedhamiria kweli kuwa tajiri hakikisha
unafanya mambo haya:-
1. Hakikisha
unajiwekea mipango na malengo makubwa.
Kama kweli unataka
kufanikiwa na kuwa tajiri ni lazima ufanye hili. Huwezi kufanikiwa kwa kiasi
kikubwa kama una tabia ya kujiwekea malengo kidogo. Watu wote wenye mafanikio
huwa ni watu wa kujiwekea malengo makubwa na ambayo huanza kuyafatilia kila
siku na kuhakikisha mpaka yanatimia.
Acha kujidharau au
kujiona hufai eti kwa sababu huna pesa na ukashindwa kujiwekea mlengo yako.
Panga mipango yako vizuri, kama ni pesa zitakuja zenyewe wakati unaendelea kutekeleza mambo
mengine. Ukiwa na malengo makubwa hii itakusaidia kufanya kazi kwa bidii kubwa
na hautaweza kukata tamaa mapema. Chukua tabia hii muhimu ikusaidie
kukufanikisha.
2. Hakikisha
unatumia muda wako vizuri.
Muda ni kitu muhimu
sana katika maisha yetu. Kama wewe ni mtunzaji mzuri wa muda na haupotezi muda
hovyo, elewa kabisa kufanikiwa kwako ni lazima. Watu wengi kutokana na
kutokujua ama mazoea ambayo wanayo toka mwanzo, ni watu wa kupoteza muda sana.
Kama tabia hii ndiyo unayo, kufanikiwa na kupiga hatua mbele itakuwa ngumu
katika maisha yako. Jifunze kutunza muda utaona mafanikio makubwa sana ambayo
hukufikiri hapo mwanzo.
3. Hakikisha
unajifunza vitu vipya kila siku.
Tatizo kubwa walilonalo
watu wengi ni kutopenda kujifunza vitu vipya.. Wengi ni wavivu wa kusoma hali
ambayo hupelekea kukosa vitu vizuri
vyenye uwezo mkubwa wa kubadilisha maisha yao. Kama unataka mafanikio makubwa
katika maisha yako, ni lazima uwe msomaji mzuri pia. Hii itakusaidia wewe
kupambana na changamoto kwa kujua wengine waliweza kukabiliana nazo vipi. Ni
lazima ujenge utaratibu wa kujisomea vitu vitakavyobadili maisha yako.
4. Hakikisha
usiwe mtu wa kulaumu tu.
Wapo watu ambao siku
zote ni watu wa kulalamika tu na kulaumu wengine ndio waliopelekea wao kuwa
hivyo. Hawa ni watu ambao mara nyingi hufikiri kuwa wao wamekuwa maskini
pengine kutokana na wazazi hawa kuwasaidia au hawakusoma na visingizio vingi
tu. Hii ni tabia ambayo haiwezi kukufikisha popote, zaidi ya kukurudisha nyuma.
Kama nia yako kubwa ni mafanikio achana na visingizio, chukua hatua za kusonga
mbele. Vipo vitu vingi vya kufanya na ukaondokana na kulaumu kwako. (Unaweza
ukasoma pia Huu Ndio utajiri mkubwa utakaoupata kama utaamua kufanya biashara hii)
5. Hakikisha
unaye ‘mentor’ wa kukuongoza kwenye
mafanikio yako.
Asilimia kubwa ya
matajiri wote walioko duniani wanao watu waliowaongoza katika maisha yao hadi
kufanikiwa. Ni muhimu hata kwako wewe kuwa na ‘mentor’ au mtu ambaye atakuongoza kwenye mafanikio yako. Mara
nyingi huwa hatujui kila kitu katika maisha yetu. Kama katika kitu ulichochagua
kufanya yupo mtu ambaye tayari amefanikiwa katika hilo eneo ni vizuri ukamtumia
ili akakuongoza ili usije ukapotea kiurahisi na kufanya makosa ambayo pengine
hukustahili kuyafanya.
6. Hakikisha
unaepuka madeni yasiyo ya lazima.
Kama umekopa mkopo benki,
hakikisha huo mkopo unakusaidia kuongeza kipato chako. Acha kukopa mkopo halafu
unaamua kujengea nyumba au kununua gari, na matokeo yake pesa zote unazipoteza
unaanza kuhangaika namna ya kulilipa deni hilo. Kati ya vitu ambavyo
vimewafanya wengi kujuta na kujilaumu katika maisha yao ni mikopo. Kama umeamua
kukopa, uwe mwangalifu ili usije ukaumia baadae wakati unarudisha hilo deni.
Kikubwa jifunze kutumia mkopo vizuri.
7. Hakikisha
unaweka akiba ya kutosha .
Kila pesa unayopata
hakikisha unajiwekea akiba yako. Wataalamu wengi wa masuala ya mafanikio
wanashauri angalau asilimia kumi ya kile unachokipata iweke kama akiba yako.
Pesa hii inapokuwa nyingi itakusaidia wewe kuwekeza katika miradi yako
mbalimbali. Hakikisha pesa hii unaiwekeza na usiitumie katika matumizi mengine
yasiyo ya lazima. Kama ukifanya hivi kwa pesa hii utakuwa upo kwenye nafasi ya
kupata mafanikio makubwa katika maisha yako.
Kwa kufanya mambo hayo
unao uwezo mkubwa wa kubadilisha maisha
yako kwa jinsi unavyotaka na kuwa tajiri. Kumbuka hukuzaliwa maskini au
mlalahoi kama unavyodhani, kikubwa jifunze kuwa na fikra sahihi zitakazo badili
maisha yako na kisha chukua hatua sahihi kuelekea malengo yako uliyojiwekea.
Hakuna kinachoshindikana kila kitu kinawezekana endapo tu ukiamua.
Nakutakia kila la kheri
katika safari yako ya mafanikio na endelea kutembelea mtandao huu wa DIRA YA MAFANIKIO kwa kujifunza na kuhamasika zaidi.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA
MAISHA YAKO YAIMARIKE,
IMANI
NGWANGWALU,
0713
048 0345/dirayamafanikio@gmail.com
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.