Oct 2, 2021
Jinsi Ya Kupika Tambi Za Mayai.
Najua kila wakati tumekuwa
tukikuletea makala mbalimbali ambazo kimsingi zimekuwa zikikusaidia kwa namna
moja ama nyingine katika kuulisha ubongo chakula ya akili. Au kwa maneno
mengine elimu ambayo umekuwa ukiipata hapa imekuwa ikikusaidia kuzaliwa upya kifikra
hatimaye kutimiza kusudio lako hapa duniani.
Lakini katika makala ya leo nataka
tujikite katika masuala mazima ya mapishi. Najua utakuwa unashangaa vipi leo
afisa mipango kuleta somo hili. Wala usishangae kila kitu ambacho unakiona
katika dunia hii ni fursa. Inawezekana kabisa ukawa hauna lengo la kupika
aina hii cha chakula.
Ila kutokana na ulichojifunza hapa
kukusaidia kutoa elimu kwa watu wengine na wao wakalipa pesa au chakula hiki
unaweza ukakipika katika sehemu mbalimbali kama katika sherehe mbalimbali na
wageni waalikwa na wasio waalikwa wakafurahia aina hii cha chakula.
Au unaweza ukapika aina hii ya
chakula kwa ajili ya biashara kama vile kwenye mahoteli, migahawa na sehemu nyinginezo.
Hebu tuangalie mahitaji kwa ajili ya
kupika aina hii cha chakula.
1. Tambi 1/2 paket
2. Vitunguu maji 2 vikubwa
Karoti 1
3. Vitunguu swaumu kijiko 1 cha
chakula
4. Carry powder kijiko 1 cha chai
pilipili hoho 1
5. Njegere zilizo chemshwa 1/2
kikombe
6. Mafuta ya kupikia kiasi
7. Chumvi kwa ladha upendayo
MAANDALIZI YA CHAKULA HIKI
a) Chemsha maji yachemke haswaa, tia
chumvi na mafuta kiasi, weka tambi katika maji yaliyo chemka ziache ziive
kiasi; kisha chuja maji na uziache kavu.
b) Chukua bakuli pasua mayai kisha
weka pembeni.
c) Chukua kikaango kilicho safi weka jikoni
tia mafuta kiasi na utaendelelea kuweka vitunguu maji,vitunguu swaumu,hoho
,karoti na carry powder,kaanga kwa pamoja katika moto mdogo mdogo na havitakiwi
kuiva sana.
d) Kisha tia tambi na njegere katika
mchanganyiko wako na uendelee kukaanga kwa dakika kadhaa.
e) Chukua mayai tia katika tambi
ongeza moto kiasi, ili tambi zako zichambuke ,moto hautakiwi kuwa mdogo sana
ikiwa moto ni mdogo tambi zako zitashikana na kutia mabonge , mayai ya kiiva
hapo chakula chako kitakuwa tayari kwa kuliwa.
Mpaka kufikia hapa chakula chako
kitakuwa tayari kwa ajili ya kuliwa, chakula hiki wakati wa kula unaweza ukawa
unashushia na juisi ambayo unayopendelea kunywa.
"Mwili hujengwi kwa mawe bali hujengwa kwa kula"
Ndimi Afisa Mipango Benson
Chonya.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.