Oct 4, 2021
Mawazo Kumi (10) Yatakayokupa Nguvu Kubwa Yakufikia Mafanikio Yako.
Mafanikio siku zote yanaanza na mawazo. Kama hakuna wazo sahihi ieleweke pia hakuna mafanikio sahihi ambayo yataweza kuchipua kwa nje, sana sana utakuwa ni mtu wa kushindwa kila wakati. Kupitia makala haya utajifunza mawazo muhimu yatakusaidia kuweza kufikia mafanikio yako. Karibu na twende tujifunze;-
1. Usifanye
maamuzi kwa muhemko kwani utaahirisha tu, ni wachache wanaofanikiwa na maamuzi
ya muhemko. Kwa mfano, utakuta mtu kasikia habari kwamba biashara ya aina
fulani inalipa, mtu huyo utakuta anakurupuka na kujikuta kwenye wakati mgumu
sana wa kuweza kushindwa. Kabla hujafanya maamuzi, tafakari kwanza.
2.
Usitake mafanikio kama unavyotaka wewe. Mafanikio yana njia yake na misingi
yake pia. Kama unataka mafanikio kwa jinsi unavyotaka wewe na unategemea
utayapata huo ni uongo hutaweza kuyapata. Futa njia, kanuni na miiko ya
mafanikio inasema nini utafanikiwa. Ulikilazimisha kufanikiwa kama unavyotaka
wewe, haitawezekana.
3. Usikae
tu na kusubiri mambo yatokee, utajichelewesha sana. Amua kupambana kufanya
mambo yaweze kutokea na hiyo itakusaidia sana kuweza kufanikiwa. Kuwa mtu wa
kulazimisha matokeo uyatakayo na uyapate. Kusubiri subiri tu mambo yajiendee,
utajikuta unasubiri sana na mambo hayawi kama utakavyo, komaa.
4.
Kama unaona maisha yako ni magumu sana, rudi kwenye mawazo yako, rudi na uende
ukaanze kufikiri upya tena, maana ugumu wa kila kitu unaanzia kwenye akili na
si kwingine tena. Inawezekana maisha yako ni magumu kwa sababu umeshindwa
kuifikirisha akili yako vya kutosha, fikiri hili na chukua hatua.
5.
Kuwa tayari kwa wakati ufaao na wakati usiofaa kwenye maisha. Kuna wakati
maisha yanakutaka uwe tayari hata wakati wewe unajiona hauko tayari iwe hivyo.
Unatakiwqa uwe kama mwanajeshi kwa kuamua kufanya chochote kile na wakayi
wowote ule ilimradi tu kuyafanya maisha yako yasogee mbele na kuleta mafanikio yatakiwayo.
6. Fanya
ufanyalo kwenye maisha yako, lakini hakikisha uwe una kitu cha watu kujifunza
kwako. Usiishie kujifunza kwa wengine ila hakikisha watu nao wajifunze kwako
kupitia wewe kama wewe. Fanya vitu ambavyo watu watakuiga na wakuone kwamba
wewe ni mfano wa kuigwa na wakufate nakufanya maisha yao kuwa bora.
7. Ukiwa
unafanya kazi, hakikisha uwe una kitu cha kuuza yaani una bidhaa ambayo unaweza
ukawauzia watu na wakanunua kwako. Fanya ufanyalo lakini hakikisha uwe na pesa
ya ziada, pesa hiyo ya ziada au akiba itakusaidia. Anza kuuza kitu ambacho
kitakusaidia sana kuweza kukuza uchumi wako nje ya kazi uifanyao.
8. Kila
mtu anaweza akawa na wasiwasi na wewe, lakini ukijitoa na kuamua basi kila kitu
kinawezekana kwako na utafanya maajabu makubwa kwako. Jiamini kwamba unaweza
ukafanya mambo makubwa maishani mwako hata kama hakuna mtu anayekuamini. Jiamini
wewe kama wewe na utatoboa na kufikia mafanikio makubwa.
9. Weka
juhudi sana kwa kila unachokifanya pasipo kuyumbishwa na wakati unaweka juhudi
ili uweze kwenda mbele zaidi kubali kujifunza kwa kukosolewa. Bila ya juhudi, kukubali kukosolewa au kuelekezwa kwa
usivyojua, hauwezi kwenda. Kukosolewa si dhambi, wewe kosolewa na kubali kujifunza
na utafanikiwa pa kubwa.
10. Kila jambo lifanye kwa wakati wake. Kama kwako upo kwenye
muda wa kuwekeza, nikwambie tu wekeza sana na mtu asikutanie katika hilo. Usipoteze
muda mwingi sana kwa kuwaza kwamba muda upo pale pale au unakusubiri, utapotea.
Utumie muda wako kufanya yale yaliyo ya msingi na yale ambayo yatakusaidia
kufanikiwa.
Fanyia
kazi haya na chukua hatua kuhakikisha ndoto zako zinatimia.
Tunakutakia kila la kheri na
endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku kujifunza maisha na
mafanikio.
Pia
rafiki, kama unapenda kujifunza zaidi kuhusu mafanikio, karibu kwenye kundi la WHATS APP LA MAFANIKIO, kujiunga tuma
neno THE UNIVERSITY OF WINNER’S
kwenda 0687449428, hapo utapata
utaratibu mzima wa kujiunga.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.