Jan 30, 2019
Ongeza Uwezo Wako Wa Kupata Pesa Kwa Kufanya Mambo Haya.
Upo uwezekano mkubwa wa wewe kuongeza uwezo
wako wa kupata pesa zaidi ya hapo ulipo ikiwa utafuata misingi sahihi ya pesa
jinsi inavyotaka. Kila kitu kina kanuni zake ikiwamo hata kanuni za kupata
pesa.
Kama bado unashangaa kwa nini wengine wana
pesa nyingi na wewe huna, hiyo yote ni kwa sababu wanazifanyia kazi kanuni za pesa
bila kujali wanazitumia kwa bahati mbaya au kwa kujua.
Huna haja ya kuendelea kukosa pesa kila
wakati. Umefika wakati wa kukubali kujifunza na kutumia kanuni za pesa ili
zikusaidie kuongeza uwezo wako wa kupata pesa na kufanikiwa maishani mwako.
Kupitia makala haya, naomba nikuachie dondoo
kadhaa zitakazoweza kukusaidia moja kwa moja kuongeza uwezo wako wa kupata pesa
na kuwa mtu wa mafanikio. Karibu tujifunze kwa pamoja;-
1. Jifunze mambo ya pesa kila siku. Jifunze
kwenye vitabu, pia jifunze kwenye semina. Huwezi kufanikiwa kipesa kama
hujachukua hatua za kujifunza jinsi pesa inavyofanya kazi.
Unalazimika kujua jinsi pesa inavyoweza
ikawekezwa na kudumu katika maisha yako. Yote haya hayawezi kuja kwenye upande
wako kama uchawi bali ni kwa wewe kuweza kujifunza.
Ongeza uwezo wako wa kupata pesa kila siku. |
2. Tafuta mshauri (Mentors) atakayekuwa
anakuongoza kwenye mambo yako ya pesa pale unapokwama au unataka kusonga mbele
zaidi. Hili linaweza kuwa jambo ni dogo kwako lakini ni muhimu kwako.
Watu karibu wote ambao wana mafanikio kila
siku wana watu ambao wanawafuata au wanawashauri kila mara katika mambo ya
pesa. Hali hiyo hupelekea kuwaweka juu kimafanikio.
3. Kama upo kwenye madeni, tafuta namna ya
kuondoka huko. Madeni ni sumu kubwa ya
mafanikio kama utakuwa nayo kwa muda mrefu. Kama una madeni mengi, upo
uwezekano wa nidhamu yako ya kipesa ikawa mbovu.
Weka mpango imara ambayo itaweza kukutoa
kwenye madeni na kuanza kuishi kwa uhuru wa kifedha. Hutaweza kufika mbali kimafanikio
ikiwa kila wakati ni mtu wa kudaiwa, hutaweza kufanya kitu chochote.
4. Jilipe wewe kwanza kila ukipata pesa
yoyote ile. Kila aina ya pesa unayoipata, tenga kiasi kidogo na ujilipe kama
mtafutaji wake. Usiache kujilipa hata kama pesa uliyopata ni kidogo.
Pesa ile ambayo utakuwa unajilipa wewe
kwanza, huna haja ya kuwa nayo na haraka kuitumia. Kama ambavyo tumekuwa
tukisema iache iwe nyingi baada ya hapo iwekeze.
5. Tafuta namna pesa zako zitakavyoweza
kukulinda pale unapokuwa umeumia au kufa na kuacha watoto wadogo. Kuwa na
ulinzi wako kama bima vile, lakini wewe bima yako inaweza ikawa pia vitega uchumi vyako mbalimbali.
Hapa unatakiwa ujifunze kuwekeza mapema
wakati bado ukijana mwenye nguvu. Kwa kadri jinsi unavyozidi kuwekeza pesa zako
zitakulinda hata pale utakopokuwa umeshazeeka au kupatwa na matatizo yoyote.
Hivyo ndivyo unavyoweza kuongeza uwezo wako
wa kupata pesa kama utazingatia mambo hayo matano kama yalivyowekwa wazi
kupitia makala haya. Naamini umejifunza kitu na chukua hatua.
Endelea kutembelea
dirayamafanikio.blogspot.com kila siku.
Kila la kheri katika kufikia mafanikio makubwa na tupo pamoja.
Ni wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa
mafanikio, mwandishi na mjasiriamali,
Blog,
dirayamafanikio.blogspot.com
Mawasiliano; +255
628 929 816, +255 713 048 035,
Email;
dirayamafanikio@gmail.com
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.