Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Friday, March 24, 2017

Kinachokupotezea Mafanikio Yako Sana Ni Hiki Hapa.

No comments :
Acha kujidanganya kwamba unatafuta mafanikio wakati hata unashindwa kubadili tabia ndogo ndogo za kukupeleka kwenye mafanikio yako, huo utakuwa ni uongo mkubwa.
Acha kuendelea kujidanganya kwamba kesho yako itakuwa bora wakati hata leo hii hufanyi kitu cha uhakika cha kubadilisha maisha yako. Maisha yako kiukweli hayataweza kubadilika.
Acha kuendelea kulaumu watu wengine kwa maisha yako kuendelea kuwa mabaya. Mtu wa kwanza unayetakiwa kumlaumu ni wewe mwenyewe hasa kutokana na mienendo na tabia zako.
Sio kwa sababu maisha ni magumu kwa sasa, basi unachanganyikiwa na kuona kila kitu hakifai kwako na kwa wengine. Maisha yanahitaji sana utulivu wa hali ya juu ili ufanikiwe, unatakiwa ujue hili.

Kama unaona maisha yako yamekweda hovyo, jichunguze, panga mipango yako upya kwa umakini na utulivu na hata wala usikurupuke katika hilo. Utulivu ni kitu cha msingi sana ambacho kinaweza kukupa mafanikio.
Tabia mbaya na mienendo mibovu ulionayo hiyo ndiyo inaokufanya au naweza kusema inaharibu maisha yako moja kwa moja. Angalia hilo halafu utaujua ukweli ambao ninakwambia.
Kila wakati jiulize, unaendelea kukua kimafanikio, au unarudi nyuma? Kama unarudi nyuma, kama nilivyosema kuwa makini sana na tabia na mienendo yako, hiyo ndiyo inayokukwamisha.
Kama umefika wakati kwako wa kusema uko 'serious' na mafanikio yako, basi hakuna namna nyingine ya kufanya zaidi ya kubadilisha tabia zako na kujenga tabia zitakazokuwezesha kufanikiwa.
Kumbuka pia kinachokupotezea mafanikio yako, ni tabia ambazo unazo na unazibeba kila wakati, hicho ndicho kitu kikubwa kinachokupotezea mafanikio yako ya leo na kesho.
Nikutakie siku njema na kila kheri,
Ni wako rafiki katika mafanikio,
IMANI NGWANGWALU,
0713 04 80 35,

No comments :

Post a Comment