Oct 16, 2018
Aina Ya Watu Ambao Hawafanikiwi Katika Maisha.
Katika
maisha wapo watu ambao ninaweza sema kwa jinsi ya sifa zao au kwa jinsi ya
tabia zao walizonazo sio rahisi kufanikiwa. Hawa ni wale watu ambao tunasema ni
aina ya watu ambao hawafanikiwi katika maisha yao.
Inawezekana
ukawa huzijui sifa za watu hawa ambao hawafanikiwi katika maisha yao, lakini
kupitia makala haya utajifunza sifa hizo za watu ambao kwa kiuhalisia huwa
hawafanikiwi hata iweje, pengine wabadilike mara moja.
Najua
hapo ulipo unataka kujua kwa hamasa kubwa watu ambao hawafanikiwi katika maisha
yao huwa wana sifa zipi. Nami bila choyo yoyote, nakukaribisha bila hiana na
twende kwa pamoja kujifunza sifa za watu ambao hawafanikiwi katika maisha.
1. Watu ambao kazi yao ni kulaumu na kulalamika.
Mara
nyingi watu ambao ni walalamikaji sana, kufanikiwa kwao katika maisha huwa sio
rahisi. Hili hutokea kwa sababu, husau majukumu yao ya msingi juu ya maisha yao
na kuwapa wengine mzigo huo kwamba ndio wamesababisha maisha yawe hivyo.
Hata
wewe ukiwa mtu wa kulalamika na kulaumu, utakuwa ni miongoni mwa watu ambao
hawataweza kufanikiwa katika dunia hii, hadi pengine ubadilike. Ukifatilia,
utaelewa vyema aina hii ya watu jinsi walivyowengi na wanakwama kweli.
Wapo ambao hawabadiliki, hawafanikiwi. |
2.Watu wanaojadili matatizo badala ya
njia za kutatua matatizo.
Kama
umekuwa ni mtu wa kujadili matatizo badala ya kutafuta njia za kutoka kwenye
tatizo hilo, basi ni miongoni mwa watu ambao hawawezi kuja kufanikiwa katika
maisha yao. Ili upate unachokitaka unatakiwa kujifunza kutatua changamoto na si
kuzijadili. Kujadili changamo zako sana
ni kujikwamisha mwenyewe.
3. Watu ambao hawataki kubadilika hata
kama wanafanya makosa.
Wapo
watu ambao ni wabishi na ambao maishani mwao ni kama wamegoma kubadilika
kabisa. Hata watu hawa wakikosea bado kubadilika kwao ni kugumu sana. Hiyo
haitoshi si watu wa kujifunza hata kidogo iwe kwenye vitabu au kupitia wengine.
Pia watu hawa ni miongoni mwa watu ambao sio rahisi kuweza kufanikiwa.
4. Watu ambao ni watumwa kwa mambo yasio
ya msingi.
Kuna
watu ambao ni watumwa wa mambo yasiyo ya msingi ambayo kiuhalisia yanawarudisha
nyuma sana kwenye maisha yao. Unapokuwa mtumwa sana pengine pombe kwa sana au wanawake
ka wingi, unajitengenezea shimo la kushindwa kwako. Kwa lugha nyingine hivyo ni
vitu ambavyo vinapoteza pesa ukiviendekeza vibaya.
5. Watu wanaojilinganisha sana na
wengine.
Acha
kufanya kosa la kujilinganisha na wengine kwenye maisha yako. Unapojilinganisha
na wengine utashindwa kuwa bora pasipo kujua na mwisho wa siku utashangaa
unakwama. Itakuwa badala ya kufanya mambo yako, unakua unakazana tu uwe kama
fulani, hapo utakwama.
Hawa
ndio watu ambao wana sifa nyingi za kutokufanikiwa katika maisha yao. Kama una
sifa miongoni mwa hizo unabidi uwe makini sana ili na wewe usije ikafika mahali
ukakwama na kubaki hapo. Jenga maisha yako makubwa ya kimafanikio kwa
kujitahidi kutoka kwenye sifa hizo kama unazo.
Endelea
kujifunza kupitia diramafanikio.blogspot.com kila siku kwa ajili ya kuhamasika
na kujifunza zaidi.
Ni wako
rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na
mjasiriamali,
Blog, dirayamafanikio.blogspot.com
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713
048 035,
Email; dirayamafanikio@gmail.com
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.