Oct 17, 2018
Hivi Ndivyo Jinsi Unavyopanga Kuwa Maskini.
Katika hali ya kawaida,
kila binadamu anaishi kwa kupanga vitu vya kufanya. Katika zoezi zima la mpango,
kuna makundi mawili ya watu. Kundi la kwanza ni watu waliopanga kutokuwa na
mpango wowote wa maisha yao na kundi la pili ni watu waliopanga
kuwa na mpango wa maisha yao.
Kundi la watu waliopanga
kutokuwa na mpango, maisha yao yanategemea zaidi imani na matumaini. Kwa
kawaida watu hawa wanaamini mambo yote yanapangwa na Mungu, na kwa hiyo, wao ni
kufanya yale tu yanayowajia vichwani mwao kila waamkapo asubuhi.
Imekuwa ni kitu cha
kawaida kusikia wengi wa kundi hili wakinena “Hata ufanyeje, Mungu kama
hajapanga unajisumbua bure! huwezi kufanikiwa”. Kauli za namna hii ni za
kukata tamaa ya maisha na pia yule anayeambiwa anakatishwa tamaa pia—anza kukaa
mbali na wenye kutoa kauli hizi ni hatari kwa mafanikio yako.
Tabia hii ya kutokupanga
aina ya matokeo unayoyataka ndiyo inayopelekea watu kuishi maisha ya kufuata
upepo kama siyo mkumbo. Pia ni tabia hii inayowafanya watu kuwa na mipango ya
muda mfupi na kupenda matokeo ya haraka.
Kwanini
tunasema ni lazima kuwa na mpango? Kwasababu
kuna vitu vikubwa viwili ambavyo vina nguvu sana katika maisha yako; navyo ni
MUDA na MABADILIKO. Muda una nguvu kwasababu, utake usitake lazima muda uende
na mabadiliko ni hivyo hivyo, lazima yaje utake usitake .
Njia pekee ya kuweza kuwa
na mamlaka juu ya muda na mabadiliko ni wewe kuwa na mpango. Binadamu wote
tumepewa uwezo wa kuweza kupanga nini cha kufanya hata kama hakijatokea.
Tofauti na wanyama
wengine, wao huweza kuishi kwa kufuata matukio au hali ya wakati huo. Wanyama
hawana kabisa mpango unaoweza kuwaongoza kwenda kwenye mwelekeo wa maisha
wanayoyataka.
Ikitokea malisho yameisha
wao uhamia sehemu nyingine na hiyo sehemu nyingine wakikuta wanyama
wanaowawinda watarudi huko ambako walihama mwanzoni.
Ajabu na kweli ni kwamba
watu wengi wanaishi kwa kufuata mabadiliko yanayojitokeza kwenye mazingira yao.
Kikubwa hapa ni wewe kubadilika na siyo kubadilishwa na mabadiliko. Ukisubili
kubadilishwa na mabadiliko maana yake mabadiliko yatakubadilisha jinsi
yanavyotaka.
Yawezekana wewe unajiona
uko sawa na mambo yako yanaenda vizuri, lakini ujue kuwa ukiwa na maisha ambayo
huna mpango ulio katika maadishi, hapo ujue kuwa lazima ufuate kile ambacho
mabadiliko yatakuletea na siyo wewe unavyotaka mabadiliko yawe. Ndiyo maana
tunaambiwa kwamba ufunguo pekee wa mtu kuweza kudhibiti MUDA na MABADILIKO ni
kuandika “mpango”.
Mpango
maana yake ni kwamba wewe mwenyewe unapanga aina ya mafanikio unayoyataka
kabla ya kuanza kuyatafuta. Mafanikio yoyote makubwa lazima upange kuyapata.
Kwahiyo, tuseme kuwa mafanikio yako yapo tayari, kinachosubiliwa sasa hivi ni
mpango kazi wako. Kama umepanga kutokuwa na mpango—tambua kuwa “Usipopanga
kupata mafanikio, basi ujue unapanga kimya kimya kuwa masikini”.
Mpango
ndio unakupa mwelekeo mzuri wa unakotakiwa kwenda. Kama wewe ndiye
unayeshika upinde na mshale basi “Mpango” ndio unasaidia kuelekeza wapi mshale
uende—wewe unachagua upande gani mshale upige. Athari za kutokuwa na mpango
ambao unatuongoza juu ya nini cha kufanya ni pale tunapojikuta tunadhibitiwa na
maisha badala ya sisi kuyadhibiti maisha.
Mpango
unakupa nguvu na uwezo wa kuuamrisha muda ukufanyie nini. Ikiwa
umepanga kutokuwa na mpango, basi ujue muda ndio utakupangia nini cha kufanya.
Inafika kipindi fulani muda wenyewe unakulazimisha kufanya vitu ambavyo hupendi
kuvifanya. Ulikuwa na nafasi ya kuamrisha muda, lakini hukuitumia, sasa ni zamu
ya muda wenyewe kukuamrisha cha kufanya.
Ukiwa huna mpango unakuwa
ni mtu wa kuishi kwa matumaini. Lakini kumbuka kuwa watu wengi wanaoishi kwa
matumaini mara nyingi ni maskini. Kwahiyo, unahitaji mpango ambao ndio
utakujengea imani ya kufanikiwa.
“Imani ni bora zaidi
kuliko matumaini” jitahidi kuwa na imani juu ya mpango wako,
huku ukizidi kuutekeleza kwa nguvu zako zote—hakika mafanikio uliyolenga kupata
lazima yatokee tu!
Habari njema ni kwamba
Mungu yupo anasubiri mpango wako ili aubariki. Mafanikio yako makubwa yapo,
lakini utayapata tu endapo utaandika leo mpango wako. Ukishindwa kupanga
unapanga kuwa maskini—habari ndio hiyo!.
Kuendelea kupata maarifa
mengi jiunge na kundi la Whats app kwa
ajili ya kujifunza zaidi. Kujiunga tuma neno THE UNIVERSITY OF WINNER’S kwenda 0713 04 80 35 ili kuunganishwa.
Oct 16, 2018
Aina Ya Watu Ambao Hawafanikiwi Katika Maisha.
Katika
maisha wapo watu ambao ninaweza sema kwa jinsi ya sifa zao au kwa jinsi ya
tabia zao walizonazo sio rahisi kufanikiwa. Hawa ni wale watu ambao tunasema ni
aina ya watu ambao hawafanikiwi katika maisha yao.
Inawezekana
ukawa huzijui sifa za watu hawa ambao hawafanikiwi katika maisha yao, lakini
kupitia makala haya utajifunza sifa hizo za watu ambao kwa kiuhalisia huwa
hawafanikiwi hata iweje, pengine wabadilike mara moja.
Najua
hapo ulipo unataka kujua kwa hamasa kubwa watu ambao hawafanikiwi katika maisha
yao huwa wana sifa zipi. Nami bila choyo yoyote, nakukaribisha bila hiana na
twende kwa pamoja kujifunza sifa za watu ambao hawafanikiwi katika maisha.
1. Watu ambao kazi yao ni kulaumu na kulalamika.
Mara
nyingi watu ambao ni walalamikaji sana, kufanikiwa kwao katika maisha huwa sio
rahisi. Hili hutokea kwa sababu, husau majukumu yao ya msingi juu ya maisha yao
na kuwapa wengine mzigo huo kwamba ndio wamesababisha maisha yawe hivyo.
Hata
wewe ukiwa mtu wa kulalamika na kulaumu, utakuwa ni miongoni mwa watu ambao
hawataweza kufanikiwa katika dunia hii, hadi pengine ubadilike. Ukifatilia,
utaelewa vyema aina hii ya watu jinsi walivyowengi na wanakwama kweli.
Wapo ambao hawabadiliki, hawafanikiwi. |
2.Watu wanaojadili matatizo badala ya
njia za kutatua matatizo.
Kama
umekuwa ni mtu wa kujadili matatizo badala ya kutafuta njia za kutoka kwenye
tatizo hilo, basi ni miongoni mwa watu ambao hawawezi kuja kufanikiwa katika
maisha yao. Ili upate unachokitaka unatakiwa kujifunza kutatua changamoto na si
kuzijadili. Kujadili changamo zako sana
ni kujikwamisha mwenyewe.
3. Watu ambao hawataki kubadilika hata
kama wanafanya makosa.
Wapo
watu ambao ni wabishi na ambao maishani mwao ni kama wamegoma kubadilika
kabisa. Hata watu hawa wakikosea bado kubadilika kwao ni kugumu sana. Hiyo
haitoshi si watu wa kujifunza hata kidogo iwe kwenye vitabu au kupitia wengine.
Pia watu hawa ni miongoni mwa watu ambao sio rahisi kuweza kufanikiwa.
4. Watu ambao ni watumwa kwa mambo yasio
ya msingi.
Kuna
watu ambao ni watumwa wa mambo yasiyo ya msingi ambayo kiuhalisia yanawarudisha
nyuma sana kwenye maisha yao. Unapokuwa mtumwa sana pengine pombe kwa sana au wanawake
ka wingi, unajitengenezea shimo la kushindwa kwako. Kwa lugha nyingine hivyo ni
vitu ambavyo vinapoteza pesa ukiviendekeza vibaya.
5. Watu wanaojilinganisha sana na
wengine.
Acha
kufanya kosa la kujilinganisha na wengine kwenye maisha yako. Unapojilinganisha
na wengine utashindwa kuwa bora pasipo kujua na mwisho wa siku utashangaa
unakwama. Itakuwa badala ya kufanya mambo yako, unakua unakazana tu uwe kama
fulani, hapo utakwama.
Hawa
ndio watu ambao wana sifa nyingi za kutokufanikiwa katika maisha yao. Kama una
sifa miongoni mwa hizo unabidi uwe makini sana ili na wewe usije ikafika mahali
ukakwama na kubaki hapo. Jenga maisha yako makubwa ya kimafanikio kwa
kujitahidi kutoka kwenye sifa hizo kama unazo.
Endelea
kujifunza kupitia diramafanikio.blogspot.com kila siku kwa ajili ya kuhamasika
na kujifunza zaidi.
Ni wako
rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na
mjasiriamali,
Blog, dirayamafanikio.blogspot.com
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713
048 035,
Email; dirayamafanikio@gmail.com
Oct 15, 2018
Hii Ndiyo Mbegu Muhimu Sana Kwa Ajili Ya Mafanikio Yako.
Kila
mtu ana uwezo mkubwa sana ndani yake wa kufikia mafanikio makubwa, lakini kwa
bahati mbaya ni wachache sana wanaojua kwamba uwezo huo wanao na waliobaki
hawaamini kabisa hata kwamba uwezo huo mkubwa wanao ndani mwao.
Kitu
ama hali hii inatokea kwa watu hawa kushindwa kuamini wana uwezo mkubwa ni kwa
sababu moja tu, watu hawa hawajaambiwa na mtu kwa msisitizo au hawajatiwa moyo
sana hadi kuweza kuamini uwezo mkubwa ulio ndani mwao.
Ni kweli
watu hawa uwezo wa kufanikiwa wanao lakini wanashindwa kufanya hivyo kwa sababu
ya kukosa mbegu muhimu ya kupewa matumaini kwamba uwezo huo wa kufanikiwa wanao
kama wanavyowaona watu wengine wakifanikiwa pia.
Kama
vile ulivyo udongo hata uwe mzuri vipi na una rutuba ya kila aina, lakini
udongo huo ukikosa mbegu au usipopanda chochote hakiwezi kuota kitu, na vivyo
hivyo hata uwe na uwezo mkubwa vipi lakini usipopanda mbegu ya kutiwa moyo ni
kazi bure.
Hamasa
na kumpa mtu moyo na kumwaminisha kwamba anaweza ni kitu ambacho kinahitajika
sana katika kila maisha ya mwanadamu. Hii ndio mbegu ya msingi sana katika
mafanikio ambayo wengi hawaijui.
Ndio
maana kama unaipa akili yako hamasa kila wakati ni rahisi sana kuweza
kufanikiwa. Wengi wanashindwa kwa sababu ya kuzipa akili zao ‘matango pori’ kwa kulisha mambo
yasiyofaa ambayo yamejaa hofu.
Unatakiwa
kuelewa unatakiwa kupewa mbegu ya hamasa, mbegu ya kutiwa moyo ili kuweza kufanikiwa na kufika juu kabisa
kimafanikio. Ukiwa na msingi mzuri wa mbegu hii utafanikiwa tu kwenye maisha
yako.
Kama
unafikiri natanaia waangalie watu ambao wamelelewa katika mazingira ya kupewa
sana moyo kwamba mafanikio yanawezekana. Utakuta ni kweli na wao wamefanikiwa
kwa sababu wanalishwa vitu kama hivyo hivyo kila siku.
Yapo
mabadiliko makubwa sana yanayotokea kwa wengine na ndani mwako hasa pale
unapoamua kujipa moyo na kuwapa moyo wengine. Hakuna kinachoshindikana
unapojipa moyo, kwa vyovyote tu utasogea hata iwe kwa kutambaa.
Kujipa
moyo na kuwapa moyo watu wengine ni mojawapo ya mbegu ya mafanikio ambayo
unatakiwa kuitumia kila wakati. Acha mizizi ya mbegu ya kutia moyo ikue na hakikisha
imekuwa vya kutosha na hapo utaona matunda ya mafanikio yako.
Endelea
kujifunza maisha na mafanikio kupitia dirayamafanikio.blogspot.com kila siku.
DAIMA
TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Ni
wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na
mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713
048 035,
Email; dirayamafanikio@gmail.com
Oct 2, 2018
Sababu Kubwa Inayokufanya Usianze Kuchukua Hatua Ni Hii…
Moja ya sababu kubwa inayopelekea watu wengi kuahirisha mambo na kushindwa kuchukua hatua ni kule kufikiri kuna vitu havijakamilika katika kulifanikisha jambo hilo. Mtu anakuwa anaahirisha kwa sababu anakuwa anaona bado hajawa tayari kufanya jambo hilo kabisa.
Uelewe
hivi, ni jambo zuri kufanya kitu chako ukiwa umekamilika kwa asilimia mia moja.
Hata hivyo hiyo isiwe sababu ya wewe kutokuanza, unaweza ukaanza kwa hali
yoyote uliyonayo hata kama unajiona hujakamilika sawa sawa.
Usiwe
na wasiwasi juu ya kuanza jambo fulani huku ukiwa umekamilika kwa asilimia mia
moja, kitu cha kwanza unachotakiwa kujua ni juu ya wewe kuanza. Fanya ufanyalo
na uhakikishe umeanza kufanya jambo lako na usisite hata kidogo kuanza.
Kwa
muda ulionao, kwa chochote kile ulichonacho, anza. Usisubiri ukamili wa jambo
lolote ule ndio uanze. Usijiweke kwenye mtego wa kuahirisha kwa sababu ya
kuanza. Kikubwa anza na kile ulichonacho na hapo ulipo na usisubiri kitu.`
Kama
ukitaka uwe kamili kila kitu ndio uanze kufanya hicho unachotaka kufanya, hebu
jiulize utajifunza nini kwenye safari ya mafanikio yako? Endelea kufanya huku
ukiwa unajifunza na utafika muda utayafikia imafanikio yako kwa kiasi kikubwa.
Watu
wengi ikiwa pamoja na wasomi mambo yao yanashindwa kukamilika au kufanyika
kikamilifu kwa sababu tu ya wao wenyewe kutaka kufanya mambo yao wakiwa kamili
kwa kila kitu, nikiwa na maana ni watu wa kutafuta ukamili sana.
Naomba
labda nikwambie hivi, hata wale watu unawaona wamefanikiwa sana, hawakuanza wakiwa
na kila kitu, walianza kidogo na vile walivyonavyo, ila kilichowafanya wakawa
hivyo ni kwa sababu ya wao wenyewe kujifunza na kukua.
Ukikubali
kuendelea kufanya huku ukijifunza na kukua, itafika muda hata kama ulianza na
kidogo sana lakini nakupa uhakika utaweza kufanikiwa na kufika mbali
kimafanikio, kwa nini, kwa sababu umeamua kufanya pasipo kujali ukamili.
Ili uweze
kuondokana na hali ya kuahirisha mambo, acha kabisa kusubiri uwe kamili kwa asilimia
zote, wewe fanya hivyo hivyo na utafika muda utaweza kufanikiwa katika hilo na
ndoto zako zitatimia na kuwa kweli.
Fanyia
kazi haya na chukua hatua kuhakikisha ndoto zako zinatimia.
Tunakutakia kila la kheri na
endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku kujifunza maisha na
mafanikio.
Pia
rafiki, kama unapenda kujifunza zaidi kuhusu mafanikio, karibu kwenye kundi la WHATS APP LA MAFANIKIO, kujiunga tuma
neno THE UNIVERSITY OF WINNER’S
kwenda 0713 048 035, hapo utapata
utaratibu mzima wa kujiunga.
Kama
wewe ni mfugaji wa kuku na unahitaji vifaranga bora, waone DM POULTRY FARM PROJECT kwa huduma ya uhakika. Hawa ni wauzaji wa
vifaranga wa kuku aina ya KUROILER,
SASSO, KIENYEJI ASILIA na KUCHI. Kwa mahitaji ya vifaranga wasiliana nao
kwa 0767 048 035 au 0686 141097 na
wote mnakaribishwa.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO
YAIMARIKE,
Ni
wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na
mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713
048 035,
Email; dirayamafanikio@gmail.com
Subscribe to:
Posts
(
Atom
)