Jan 30, 2019
Ongeza Uwezo Wako Wa Kupata Pesa Kwa Kufanya Mambo Haya.
Upo uwezekano mkubwa wa wewe kuongeza uwezo
wako wa kupata pesa zaidi ya hapo ulipo ikiwa utafuata misingi sahihi ya pesa
jinsi inavyotaka. Kila kitu kina kanuni zake ikiwamo hata kanuni za kupata
pesa.
Kama bado unashangaa kwa nini wengine wana
pesa nyingi na wewe huna, hiyo yote ni kwa sababu wanazifanyia kazi kanuni za pesa
bila kujali wanazitumia kwa bahati mbaya au kwa kujua.
Huna haja ya kuendelea kukosa pesa kila
wakati. Umefika wakati wa kukubali kujifunza na kutumia kanuni za pesa ili
zikusaidie kuongeza uwezo wako wa kupata pesa na kufanikiwa maishani mwako.
Kupitia makala haya, naomba nikuachie dondoo
kadhaa zitakazoweza kukusaidia moja kwa moja kuongeza uwezo wako wa kupata pesa
na kuwa mtu wa mafanikio. Karibu tujifunze kwa pamoja;-
1. Jifunze mambo ya pesa kila siku. Jifunze
kwenye vitabu, pia jifunze kwenye semina. Huwezi kufanikiwa kipesa kama
hujachukua hatua za kujifunza jinsi pesa inavyofanya kazi.
Unalazimika kujua jinsi pesa inavyoweza
ikawekezwa na kudumu katika maisha yako. Yote haya hayawezi kuja kwenye upande
wako kama uchawi bali ni kwa wewe kuweza kujifunza.
Ongeza uwezo wako wa kupata pesa kila siku. |
2. Tafuta mshauri (Mentors) atakayekuwa
anakuongoza kwenye mambo yako ya pesa pale unapokwama au unataka kusonga mbele
zaidi. Hili linaweza kuwa jambo ni dogo kwako lakini ni muhimu kwako.
Watu karibu wote ambao wana mafanikio kila
siku wana watu ambao wanawafuata au wanawashauri kila mara katika mambo ya
pesa. Hali hiyo hupelekea kuwaweka juu kimafanikio.
3. Kama upo kwenye madeni, tafuta namna ya
kuondoka huko. Madeni ni sumu kubwa ya
mafanikio kama utakuwa nayo kwa muda mrefu. Kama una madeni mengi, upo
uwezekano wa nidhamu yako ya kipesa ikawa mbovu.
Weka mpango imara ambayo itaweza kukutoa
kwenye madeni na kuanza kuishi kwa uhuru wa kifedha. Hutaweza kufika mbali kimafanikio
ikiwa kila wakati ni mtu wa kudaiwa, hutaweza kufanya kitu chochote.
4. Jilipe wewe kwanza kila ukipata pesa
yoyote ile. Kila aina ya pesa unayoipata, tenga kiasi kidogo na ujilipe kama
mtafutaji wake. Usiache kujilipa hata kama pesa uliyopata ni kidogo.
Pesa ile ambayo utakuwa unajilipa wewe
kwanza, huna haja ya kuwa nayo na haraka kuitumia. Kama ambavyo tumekuwa
tukisema iache iwe nyingi baada ya hapo iwekeze.
5. Tafuta namna pesa zako zitakavyoweza
kukulinda pale unapokuwa umeumia au kufa na kuacha watoto wadogo. Kuwa na
ulinzi wako kama bima vile, lakini wewe bima yako inaweza ikawa pia vitega uchumi vyako mbalimbali.
Hapa unatakiwa ujifunze kuwekeza mapema
wakati bado ukijana mwenye nguvu. Kwa kadri jinsi unavyozidi kuwekeza pesa zako
zitakulinda hata pale utakopokuwa umeshazeeka au kupatwa na matatizo yoyote.
Hivyo ndivyo unavyoweza kuongeza uwezo wako
wa kupata pesa kama utazingatia mambo hayo matano kama yalivyowekwa wazi
kupitia makala haya. Naamini umejifunza kitu na chukua hatua.
Endelea kutembelea
dirayamafanikio.blogspot.com kila siku.
Kila la kheri katika kufikia mafanikio makubwa na tupo pamoja.
Ni wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa
mafanikio, mwandishi na mjasiriamali,
Blog,
dirayamafanikio.blogspot.com
Mawasiliano; +255
628 929 816, +255 713 048 035,
Email;
dirayamafanikio@gmail.com
Jan 28, 2019
Mambo Matatu Ya Kukusaidia Kukuongoza Kwenye Safari Ya Ujasiriamali Na Kukupa Mafanikio Makubwa.
Kila mtu anatamani biashara anayoifanya ifanikiwe, kila mtu anatamani akiingia kwenye ujasiriamali mambo yake yanyooke sana na yawe ya mafanikio makubwa. Hiki ndicho kitu ambacho watu wengi sana wanapenda kiwe kwenye maisha yao.
Hata
hivyo uelewe hivi, unapochagua kuingia kwenye biashara, ujue kabisa umechagua kabisa kuingia kwenye ulimwengu wa
wapambanaji haswa, yaani ulimwengu wa ujasiriamali. Hivyo, unapoingia kwenye
dunia ya ujasiriamali kuna mambo lazima
uyajue kwanza.
Pasipo
kuyajua mambo haya, nakuhahakikishia kabisa, utakwama sana na itafika mahali
utajiona wewe si kitu na si lolote. Pengine jiulize, mambo hayo ni mambo gani
ambayo yatakusaidia kukuongoza kwenye safari ya ujasiriamali na kukupa
mafanikio?
1. Tambua jinsi ya kukabiliana na hali
yoyote ile.
Unapoinguia
kwenye biashatra na huku ukaingia na mawazo ya aina moja tu kwamba mimi naenda
kupata, basi utakuwa unajiweka kwenye wakati mgumu sana. Kwa kuwa umechagua
kuingia kwenye biashara ujie kabisa kuna kupata na kukosa.
Inapotokea
umepata unashukuru Mungu, lakini inapotokea umekosa pia unashukuru Mungu kwa
matokeo hayo na kuchukua uamuzi wa kusonga mbele. Usiingie kwa akili ya kupata moja kwa moja
utapotea.
2. Tambua kuna hali hatarishi.
Zipo
hali hatarishi nyingi sana au ‘risk’ hasa pale unapochagua
kuingia kwenye ulimwengu wa biashara. Hali hizi hatarishi unatakiuwa kupambana
na kukabiliana pasipo na hofu yoyote kwani kwa kuzishinda huko ndiko unafanikiwa.
Kama
umeamua kuingia kwenye biashara au
ujasiriamali na ukawa mwoga na hali hiz hatarishi basi utakuwa unapotea. Kwa
kujua kuna hali hatarishi basi itakuwa ni njia sahihi ya namna ya wewe
kuongozwa kwentye njia ya mafanikio ya ujasiriamali wako.
3. Tambua kukabiliana na hofu.
Wale
wanaofanikiwa si kwamba ni watu ambao hawana hofu kabisa, ni watu ambao wana
hofui kama wewe ila wanaamua kukabiliana na hofu zao hivyo hivyo pasipo kujali
nini kinaendelea ndani mwao juu ya hofu hizo.
Hata
wewe unaweza kukabiliana na hofu hizo hivyo hivyo kila siku. Kuna wakati utakutana
na mambo yatakayokuwa magumu kwako
lakini unatakiwa kujifunza jinsi ya kukabaliana nayo na uatafika wakati utakuwa
mshindi kweli.
Fanyia
kazi haya na chukua hatua kuhakikisha ndoto zako zinatimia.
Tunakutakia kila la kheri na
endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku kujifunza maisha na
mafanikio.
Pia
rafiki, kama unapenda kujifunza zaidi kuhusu mafanikio, karibu kwenye kundi la WHATS APP LA MAFANIKIO, kujiunga tuma
neno THE UNIVERSITY OF WINNER’S
kwenda 0713 048 035, hapo utapata
utaratibu mzima wa kujiunga.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO
YAIMARIKE,
Ni
wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na
mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 713 048 035,
Email; dirayamafanikio@gmail.com
Jan 1, 2019
Acha Kuishia Hapa Tu, Fanya Mabadiliko Ya Kudumu Ya Maisha Yako.
Leo ni siku ambayo watu wengi wanaamini wakati wa kufanya mabadiliko mapya umewadia. Kwani nini wanaamini iko hivyo ni kwa sabbau leo ni mwaka mpya, kwa hiyo imani ile ya kubadilisha mambo leo iko juu sana.
Kama
unaamini hivyo kwamba kuna sehemu ulishindwa na huu ndio wakati wa kufanya mabadiliko
kwako, tafadhari, fanya mabadiliko hayo na acha hata kidogo kuishia kati, kama
ni mabadiliko hayo endelea kuyafanya maishani mwako kote na yasiwe ya kitambo.
Mabadiliko
ya kweli katika maisha yako hayaji tu kwa sababu leo ni mwaka mpya, bali
yanakuja kwa sababu unatakiwa kubadlili maisha yako haswaa na kila siku pasipo
kusubiri kitu chochote cha nje ikiwa pamoja na msukumo wa nje.
Leo hii
kama wewe mwenyewe umeamua kweli iwe siku yako ya mabadiliko, naomba uzaliwe upya kweli. Acha kuishia tu kusheherekea mwaka mpya na kusahau kufanya mabadiliko
ya kweli na ya kudumu katika maisha yako.
Usiwe
mtu ambae umejipa ‘ubatizo’ wa kuzaliwa upya na halafu kesho nikukute unarudia
maisha yale yale ya zamani yanayokurudisha nyuma. Weka mikakati mizito ya
kuamua kubadilisha maisha yako kweli na acha lelemama.
Kama
umeamua kufanya mabadiliko ya kweli fanya kweli, acha utoto na acha kujirudisha
nyuma kwa namna yoyote ile ambayo ni hatari kwa afya ya mafanikio yako. Jambo la
kuzingatia sana kwako ni kuhakikisha lazima unasonga mbele .
Najau
kwa miaka mingi umepitia makubwa ya kupanda na kushuka, lakini hiyo nikwambie
tu inatosha, sasa ni wakati wako wa kuleta mabadiliko ya kudumu katika maisha
yako na mabadiliko hayo unaweza ukayaanza leo.
Asikuzuie
mtu, kisikuzuie kitu, amua kufanya mabadiko ya kweli katika maisha yako na mabadiliko
hayo yasiishie tu katika siku za mwanzo za mwaka bali yawe endelevu kizazi na
kizazi hadi iwe kumbukumbu kwako kubwa na kudumu.
Ngoja
leo nikupe baraka zote za kukutakia heri ya mwaka mpya, lakini mwaka huu uwe
kweli wa mabadiko ya kudumu kwako na usiwe mwako ambao uwe wa majuto kwako tena
kama ambavyo imekuwa pengine ikitokea.
Naamini
hilo litafanikiwa kwako na Mungu atakubariki ikiwa utachukua hatua sahihi. Kama
nilivyosema, acha kuishia kusheherekea mwaka mpya tu, bali amua kufanya
mabadiliko ya kweli ya maisha yako.
Fanyia
kazi haya na chukua hatua kuhakikisha ndoto zako zinatimia.
Tunakutakia
kila la kheri na endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku
kujifunza maisha na mafanikio.
Pia
rafiki, kama unapenda kujifunza zaidi kuhusu mafanikio, karibu kwenye kundi la WHATS APP LA MAFANIKIO, kujiunga tuma
neno THE UNIVERSITY OF WINNER’S
kwenda 0713 048 035, hapo utapata
utaratibu mzima wa kujiunga.
Kama
wewe ni mfugaji wa kuku na unahitaji vifaranga bora, waone DM POULTRY FARM PROJECT kwa huduma ya uhakika. Hawa ni wauzaji wa
vifaranga wa kuku aina ya KUROILER,
SASSO, KIENYEJI ASILIA na KUCHI. Kwa mahitaji ya vifaranga wasiliana nao
kwa 0767 048 035 au 0686 141097 na
wote mnakaribishwa.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO
YAIMARIKE,
Ni
wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na
mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 713 048 035,
Email; dirayamafanikio@gmail.com
Subscribe to:
Posts
(
Atom
)