Mar 11, 2019
Tabia Muhimu Zitakazokusaidia Kukupa Mafanikio Kwa Kiasi Kikubwa.
Moja ya sheria ya msingi na ya muhimu katika mafanikio yoyote yale ni kuwa na tabia nzuri. Tabia ni moja ya kitu ambacho ni cha msingi sana katika kukupa mafanikio yale uyatakayo. Ukiangalia wengi wanaoshindwa, chanzo kinaanzia kwenye tabia zao.
Tuchukulie
kwa mtu anayataka mafanikio, kuwa na malengo tu peke yake na kuyafanyia kazi
haitoshi, lazima mtu huyu awe na tabia zinazoendana na malengo hayo, kama kuwa
na matumizi mazuri ya pesa au utunzaji wa muda mzuri.
Unapokuwa
na tabia mbaya na huku ukitaka mafaniko, ni wazi hutaweza kufanikiwa na
utahangaika sana kufikia mafanikio hayo. Mpaka hapo unaona tabia ni kitu cha
msingi sana katika kukufanikisha wewe kwenye maisha yako.
Unaweza
ukawa na mafanikio makubwa sana, ikiwa utajenga tabia bora za kukusaidia
kufanikiwa kwa kiasi kikubwa kila wakati. Je, unataka kuzijua tabia hizi ni
zipi za kukusaidia wewe kuweza kufanikiwa kwa kiasi kikubwa?
1. Tabia
ya kutafuta msaada.
Hakuna
mtu ambaye anaweza kufanikiwa akiwa peke yake. Kila mtu anahitaji msaada kwa
mtu mwingine hata kama msaada huo ni kidogo sana lakini msaada huo unahitajika
ili kuweza kujenga mafanikio ya kudumu.
Unapokuwa
unawasiliana na wengine na wakajua changamoto zako, ni rahisi sana kwa wao
kuweza kukusaidia wewe na kupiga hatua mbele za kimafanikio. Usijaribu kuishi
kipeke yako yako, tafuta msaada kwa wengine na utafanikiwa pia.
2.
Tabia ya kuchukua hatua.
Unayo
nafasi kubwa sana ya kufikia mafanikio yoyote yale unayoyataka kwenye maisha,
lakini kama huchukui hatua nikwambie tu, utakufa kwa msongo wa mawazo. Najua una
mawazo mazuri lakini hayawezi kufanya kazi mpaka uchukue hatua.
Huhitaji
kuwa na hamasa ili uchukue hatua, wewe chukua hatua kwa hali yoyote uliyonayo. Acha
kuendelea kufikiria sana juu ya ndoto zako, chukua hatua. Soma vitu vya
kukusaidia na kisha amua kuchukua hatua na ukijenga tabia hii itakusaidia sana.
3.
Tabia ya kutokuishi kimazoea.
Maisha
ya watu wengi yanakuwa mabaya kwa sababu ya kuishi sana kimazoea. Kuishi kimazoea
ni sumu kubwa sana ya wewe kuweza kufikia mafanikio makubwa. Unatakiwa ujue namna
ya kuishi nje ya mazoea yako ili uweze kufanikiwa zaidi.
Kila
wakati tafuta namna ambayo itakusaidia wewe kuweza kuishi nje ya mazoea yako. Ikiwa
lakini kila wakati unaishi kwenye mazea hayo hayo itakuwa ni ngumu sana kwako
kuweza kusonga mbele na kupigia hatua hasa za kimafanikio.
4. Tabia
ya kusema hapana.
Hii ni
moja ya tabia nzuri sana kwako wewe kuindeleza ili kufikia mafamikio. Unatakiwa
kujifunza kusema hapana kwa mambo mengi sana. Unatakiwa ujue kusema hapana kwa
wanaokupotezea muda wako au kwa yale mambo usiyoyahitaji.
Ikiwa
wewe utakuwa ni mtu wa kukubali kila kitu, kwamba kitu hiki kiwe hivi au vile
ni ngumu sana kuweza kupiga hatua sahihi za kimafanikioo husika. Jifunze kusema
hapana kwa kila kitu ambacho hakina manufaa kwako wewe.
5.
Tabia ya kuchukua majukumu yako.
Unatakiwa
ujue kila mtu ana changamoto zake za kimaisha, lakini kama unashindwa
kuwajibika na majukumu hayo na kila wakati kutaka kulaumu tu watu wengine, hilo
tu nikwambie utakuwa ni miongoni mwa watu ambao watashindwa sana.
Nikwambie
tu, kubali kuwajibika kwa kila jambo linalokuhusu wewe. Wajibika kwenye ndoto
zako, wajibika kwenye maisha yako ya kila siku. Kila wakati ujue jinsi ya
kuwajibika na hapo utaweza kupiga hatua za mafanikio sahihi kwako.
Hivi
ndivyo unavyoweza ukatumia tabia hizo vizuri na zikakusaidia wewe kuweza kufanikiwa
kwa kiasi kikubwa sana kwenye maisha yako kama unavyotaka iwe. Ni jukumu lako
wewe sasa kuchukua hatua na kuhakikisha unasonga mbele.
Fanyia kazi haya na chukua
hatua kuhakikisha ndoto zako zinatimia.
Tunakutakia kila la kheri na
endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku kujifunza maisha na
mafanikio.
Pia
rafiki, kama unapenda kujifunza zaidi kuhusu mafanikio, karibu kwenye kundi la WHATS APP LA MAFANIKIO, kujiunga tuma
neno THE UNIVERSITY OF WINNER’S
kwenda 0713 048 035, hapo utapata
utaratibu mzima wa kujiunga.
Kama
wewe ni mfugaji wa kuku na unahitaji vifaranga bora, waone DM POULTRY FARM PROJECT kwa huduma ya uhakika. Hawa ni wauzaji wa
vifaranga wa kuku aina ya KUROILER,
SASSO, KIENYEJI ASILIA na KUCHI. Kwa mahitaji ya vifaranga wasiliana nao
kwa 0767 048 035 au 0686 141097 na
wote mnakaribishwa.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO
YAIMARIKE,
Ni
wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na
mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 713 048 035,
Email; dirayamafanikio@gmail.com
Mar 10, 2019
Ikiwa Unaishi Hivi, Maisha Yako Ni Mafupi Sana.
Ni jambo ambalo watu
hulisema mara nyingi bila kujua maana
yake. Unaweza kukuta mtu akisema, ‘ndio
maana amekauka, ana roho mbaya sana’. Ukimuuliza ni kwa nini anahusisha
kukauka au afya mbaya na roho mbaya au kukosa upendo alikonako mtu, hataweza
kukupa jibu sahihi. Lakini, anajua kwamba, kukauka huwapata wenye roho mbaya. Kauli
hiyo ina ukweli mkubwa wa kutosha. Watu wengi ambao wanatengeneza nguvu nyingi
hasi, hatimaye nguvu hizo huwarudia na kuwadhuru.
Kwa sehemu kubwa,
madhara ya nguvu hizo huja kujitokeza
kwenye miili yao. Mtu ambaye anaumwa mara kwa mara, anaweza kuwa anaumwa tu kwa
sababu nyingine, lakini pia anaweza kuwa anaumwa kutokana na nguvu hasi
anazotengeneza. Nikisema nguvu hasi, nina maana ya kufikiri na matendo ambayo
yanamuumiza mwenye mawazo na matendo hayo, pia wale wanaomzunguka. Kwa mfano,
mtu asiyeweza kusamehe, mwenye visasi, mwenye kijicho, mpenda makuu, mshindani
na mengine ya aina hiyo.
Kuna watu ambao hutengeneza sana nguvu hasi
kwa kufikiri kwao na tabia zao. Kwa kawaida, nguvu hasi huwa zinadhuru hisia na
mwili wa mhusika. Kwa vipi? Hebu tutazame kushindwa kusamehe na kijicho. Mtu ambaye
hawezi kusamehe, anajiweka mahali ambapo muda wote anakuwa kwenye hasira, hisia
chungu na mikakati ya kulipa kisasi. Hii ni sawa na mtu ambaye ana kijicho, kwa
mfano. Huyu naye, muda mwingi wa maisha yake, atakuwa akiumia kwani, kila
wengine wakifanikiwa kwa chochote, atajihisi vibaya tu. kwa hiyo, hisia zake
zitakuwa zinachokozeka karibu muda wote.
Kwa kawaida, hisia zetu
zinapochokozeka, tunaiiingiza miili yetu kwenye kuzalisha kemikali au homoni
ambazo wakati huo hazihitajiwi. Kwa uzalishwaji huo wa kemikali zisizohitajika
mwilini, tunaiumiza miili yetu kwa njia mbalimbali. Kemikali hizo, hatimaye
huanza kutuumiza kwa kuteleta maradhi mvalimbali miilini mwetu. Hili ni jamba
ambalo limethibitishwa kitaalamu.
Kuna maradhi zaidi ya
kumi ambayo chanzo chake ni mihemko yetu, maradhi ambayo kitaalamu hufahamika
kama Emotionally Induced Diseases. Haya
ni pamoja na maumivu ya mwili, tumbo, kufunga choo na mengine. Ndiyo maana,
wale watu wote wanaokwenda hospitalini wakiwa wanaumwa, ambao wanaambiwa vipimo
havioneshi maradhi yoyote, ukiwachunguza, utagundua kwamba, wanakabiliwa na
hofu, mashaka, visasi na matatizo
mengine ya kihisia.
Sisemi kwamba, wote
wanaopimwa na kuonekana hawana maradhi ndivyo walivyo, hapana. Lakini wengi
kati yao ndivyo walivyo. Hata wale wanaodaiwa kuwa na mapepo pia, utakuta
baadhi ni wale wenye hisia chungu. Kwa sababu ya maumivu ya kimwili na yale ya
kiakili, unakuta watu hawa wakiwa dhaifu. Kama walivyo wagonjwa wengine, suala
la udhaifu wa kimwili hujitokeza sana kwa watu hawa, kwani pamoja na maradhi
yanayoletwa na hisia chafu, kinga ya mwili hushuka sana pale miili inapohemkwa
mara kwa mara.
Ni rahisi kwa hali
hiyo, watu wenye roho mbaya kukauka au kukosa afya imara. Ingawa siyo kweli
hata hivyo kuwa watu wote wenye afya mbovu, inatokana na roho mbaya, hapana. Lakini,
kwa wale walio na roho mbaya, yaani kufikiri na tabia zenye kuzalisha nguvu
hasi, ni rahisi zaidi kwao kukosa afya bora kama tulivyoona. Ndiyo maana
tunasema hivi, kama unaishi maisha haya kuwa na roho mbaya tu, maisha yako ni
mafupi kwa sababu utakuwa ni wa afya mbovu kitu ambacho ni hatari sana kwako.
Nakutakia kheri ya
mwaka mpya, endelea kutembelea DIRA YA MAFANIKIO kujifunza na kuhamasika kila
siku.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA
MAISHA YAKO YAIMARIKE,
IMANI
NGWANGWALU,
0713
048 0345/dirayamafanikio@gmail.com
Mar 9, 2019
Kama Mambo Yako Yako Hovyo, Yaweke Sawa Kwa Kufanya Hivi.
Ikiwa
kuna wakati unaona maisha yanakuchanganya hasa kutokana na changamoto
unazokutana nazo, usije ukakubali ukafanya kosa la kuchanganywa huko, badala
yake tuliza akili yako na tafuta mwelekeo sahihi wa maisha yako kwa kuweka
mambo sawa.
Ikiwa
unaona pia unaweka juhudi nyingi sana na juhudi hizo hazikupi matunda sahihi,
hapa tena usikatishwe tamaa, endelea kuweka juhudi, lakini tafuta kuelewa kwa
nini juhudi zako hazikufanikishi na anza kutafuta njia nyingine itakayokupa
matokeo makubwa kwako na kuweka mambo sawa.
Upo
wakati katika maisha yako ambapo kuna mtu au watu watakurudisha nyuma hata bila ya wewe
kutegemea. Inapotokea wakati kama huu, sio swala la kutupa lawana na
kusikitika, bali ni kuuvaa ujasiri na ushujaa na kutafuta mwelekeo upya kwa
kuweka mambo yako sawa.
Kuna
wakati katika maisha yako unajiona upo
njia panda, huelewi hata ufanye nini, inapofika wakati huu , jifunze kuweka
nguvu za uzingativu katika kitu kimoja na kutafuta mwelekeo sahihi
utakaokusaidia kuweka mambo yako sawa na yakae katika mkao wa mafanikio.
Zipo
nguvu nyingi na kubwa sana katika maisha yako, ambapo nguvu hizo zinauwezo wa
kubali hali yoyote ambayo unayo na unaona ni
mbaya na nguvu hizo hadi kukupa mafanikio halisi kama vile unavyotaka
iwe.
Ndio
maana, badala ya kulalamika na kutoa kila aina ya visingizio, jitahidi sana
kuweka mambo yako sawa, kila unapoweka juhudi ya kuweka mambo yako sawa, utajifunza
na kugundua kwamba kumbe unaweza ukatawala maisha yako kwa jinsi unavyotaka.
Je,
katika maisha yako kuna kipi ambacho unakiona ndio tena basi kimeharibika na
hakiwezi kukusaidia hata kufanikiwa. Kama kipo kitu cha namna hiyo, anza
kikiweka sawa na kutafuta njia ya itakayofanya kitu hicho kikupe matunda
uyatakayo.
Fanyia kazi haya na chukua
hatua kuhakikisha ndoto zako zinatumia.
Tunakutakia kila la kheri na
endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku kujifunza maisha na
mafanikio.
Pia rafiki,
kama unapenda kujifunza zaidi kuhusu mafanikio, fursa za mafanikio
zinapopatikana, ajira pamoja na uwekezaji, karibu kwenye kundi la WHATS APP LA MAFANIKIO, kujiunga tuma
neno THE UNIVERSITY OF WINNER’S
kwenda 0713 048 035, hapo utapata
utaratibu mzima wa kujiunga.
Pia
kama wewe ni mfugaji wa kuku na unahitaji vifaranga bora, waone DM POULTRY FARM PROJECT kwa huduma ya
uhakika. Hawa ni wauzaji wa vifaranga wa kuku aina ya KUROILER, SASSO, PURE KIENYEJI na KUCHI. Kwa mahitaji ya vifaranga
wasiliana nao kwa 0767 048 035 au 0686
141097 na wote mnakaribishwa.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO
YAIMARIKE,
Ni
wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na
mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713
048 035,
Email; dirayamafanikio@gmail.com
Mar 8, 2019
Kama Utaruhusu Kelele Hizi…Utashindwa Kufanikiwa.
Usisikilize kila kitu |
Zipo
kelele nyingi sana katika dunia hii ya habari. Utasikia hiki mara utasikia kile,
ilimradi kukicha tu zipo habari na taarifa nyingi ambazo zinatolewa ambazo
lengo lake wewe uzisikie na pengine kuzifanyia kazi.
Usipokuwa
makini utajikuta kila kitu unataka kufatilia. Sasa njia ya kuweza kujiokoa na
kelele hizo na kuweza kufanikisha malengo yako ni kwa wewe kuweka nguvu zako za
uzingativu kwa kile unachokifanya.
Angalia
kipi unakifanya, kisha kifatilie kitu hicho kila siku. Kelele za huku mara kule
acha kuzifatilia zitakupoteza. Kumbuka, mikwenzi mingi ilimpoteza mbwa
mawindoni, usiwe miongoni mwa watu watakao potea kwa sababu ya kelele.
Simamia
na fatilia mipango yako kwa kuweka nguvu za uzingativu kwa kile ukifanyacho na
utafanikiwa. Kuendelea kusikiliza kelele au kila linalosemwa utakuwa ni sawa na
mtu ambaye ameamua kujipoteza yeye mwenyewe.
Katika
dunia ya sasa, ni rahisi sana kusikia fursa hii au ile, lakini kwa ukweli
uliowazi wewe kama wewe huwezi kufanya kila kitu. Kama ni fursa ni lazima
utafanya chache na si kila fursa itakuwa yako.
Hivyo
unatakiwa kuwa makini na taarifa unazozipokea. Unatakiwa kuwa mtulivu na usiwe
mtu ambaye unaendeshwa na mihemiko isiyo ya maana. Kelele za dunia zisikuyumbishe
hata kidogo, fuata malengo yako.
Ikitokea
umekubali kuyumbishwa na dunia au na kelele za dunia, basi utaishi kama bendera
fuata upepo maana hutafika popote. Utagusa hiki mara kile na kila kitu utakuwa
unakianza na kukiacha kila ukisikia kuna kingine kizuri kinalipa.
Kuanzia
leo jifunze kuweka masikio yako pamba, jifunze kuweka nguvu zako za uzingativu
eneo moja, mahali ambapo utafanya kitu na kitaonekana cha thamani. Ukiziba masikio
usisikie kitu, utajenga uwezo mkubwa wa kufanikiwa.
Chukua
hatua kwa kufanyia kazi hicho ulichojifunza na endelea kutembelea
dirayamafanikio.blogspot.com kujifunza na kuhamasika zaidi kila siku.
Ni
wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na mjasiriamali,
Blog, dirayamafanikio.blogspot.com
Mawasiliano; +255 713
048 035,
Email; dirayamafanikio@gmail.com
Mar 7, 2019
Sehemu Sahihi Ya Kuanzia Mafanikio Yako Ni Hii Hapa.
Bila
kujali upo mbali kimafanikio kwa kiasi gani, lakini bado unayo nafasi ya
kuchagua kuendelea mbele kwenye safari ya mafanikio yako.
Si
kitu cha ajabu sana kwako na kwa wengine pia wanapoona wako mbali kimafanikio,
hasa kwa kuwalinganisha na wengine wanaanza kukata tamaa.
Kitu
ambacho watu hawa wanakuwa hawajui ni kwamba, mafanikio hayategemei sana au
hayajali eti upo umbali gani, bali kinachojalisha ni mwelekeo wako.
Mwelekeo
ndio kitu cha msingi sana katika safari yako ya mafanikio. Hiyo ikiwa na maana
pale ulipo kwa sasa unaelekea wapi kimafanikio.
Kama
mwelekeo wako ni sahihi, basi hakuna shaka hata kama mwendo wako ni kidogo kama
wa kinyonga lakini wakati upo utafanikiwa.
Kikubwa
ambacho hutakiwi kukipoteza kwenye maisha yako ni ule mwelekeo wa kule
unakoenda kwenye maisha yako. Ukipoteza mwelekeo ndio basi huwezi kufanikiwa.
Watu
wengi hawafanikiwi katika maisha sio kwa sababu ya kwamba wapo mbali kwa hiyo
ni ngumu kufanikiwa. Hawafanikiwi kwa sababu hawana mwelekeo.
Hata
katika mazingira ya kawaida kitu chochote kikikosa mwelekeo hakiwezi kufika
kule kinakotakiwa kufika, lazima kitapotea hapa katikati.
Kwa
mfano, ukiangalia ndenge inaporuka hewani inakuwa na mwelekeo fulani unaongozwa
na rubani. Inapotokea mwelekeo huo haupo, basi ndege haiwezi kufika.
Na
maisha yako hayana tofauti sana na hivyo. Maisha yako yanahitajji mwelekeo
kwanza na sio wapi ulipo kimaisha ndio hatma yako iamulie.
Kama
umekuwa bado unasingizia kwamba eti uko mbali kimaisha na ndio maana
hufanikiwi, huo sio ukweli ni uongo.
Wewe
sehemu ya kuanzia kwenye safari yako ya mafanikio ni kutafuta mwelekeo.
Ukiupata mwelekeo basi njia kuu ya mafanikio umeiona.
Inatakiwa
sasa kujiuliza karibu kila siku, mwelekeo wa maisha yako uko wapi. Kitu gani
utakachofanya ambacho kitakupa mwelekeo sahihi wa maisha yako.
Hutakiwi
kulaumu hata siku moja pale ulipo, unatakiwa ushukuru kwanza, kwani sehemu
ulipo hapo ndipo unatakiwa kuanza kutafuta mwelekeo wa mafanikio yako.
Hutaweza
kufanikiwa kama hautataka kuanza kutafuta
mwelekeo wako, sehemu sahihi ya kuanzia mafanikio kama nilivyosema ni kujua
mwelekeo wako pale ulipo.
Hakuna
kitu ambacho kitaweza kushindikaa kwako, kwa sababu utakuwa umeamua kutafuta
kwa dhati sehemu ya kuanza kutafuta mfanikio yako.
Amua
leo iwe siku ya kuanza kutafuta sehemu sahihi ya kuanzia mafanikio yako kwa
kutafuta mwelekeo wa wapi uende.
Usiruhusu
mtu akwambie huwezi kufika kule unakotaka kufika kimafanikio, wakati una uwezo
wa kuanza kutafuta mwelekeo wako na kusonga mbele unao.
Usiruhusu
mtu akakukatisha tamaa iwe kwa vitendo au kwa chochote kile kwamba wewe upo
mbali sana na hautaweza kufanikiwa.
Usiruhusu
tena wewe mwenyewe ndani yako ukajiambia kwamba, kwa maisha haya niliyonayo
ndio basi tena siwezi kufanikiwa.
Hautakiwi
kuruhusu chochote kile ndio kiwe kikwazo chanzo cha wewe kushindwa kuwa na mwelekeo
sahihi wa maisha yako.
Kila
wakati unatakiwa kujua ule uwezo wa kufanikiwa na kufika ngazi ya juu
kimafanikio unao, kwa sababu sehemu
sahihi ya kuanzia mafanikio yako umeshaiona.
Kama
kuna watu wao wanaendelea kukubeza, waache waendelea kukubeza na hiyo itakula
kwao, wewe endelea kuchanja mbuga kutafuta mwelekeo wako kimafanikio.
Hutakiwi
tena kujiuliza uliza au kumuuuliza mtu kwamba ni wapi mafanikio yako yanaweza kuanzia au ni sehemu gani.
Kitu
cha kukumbuka ulichojifunza hapa ni kwamba, sehemu sahihi ya kuanzia mafanikio
yako ni kwa wewe kuchukua hatua za kutafuta mwelekeo wa mafanikio yako.
Fanyia
kazi haya na chukua hatua kuhakikisha ndoto zako zinatumia.
Tunakutakia
kila la kheri na endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku
kujifunza maisha na mafanikio.
Pia
rafiki, kama unapenda kujifunza zaidi kuhusu mafanikio, fursa za mafanikio
zinapopatikana, ajira pamoja na uwekezaji, karibu kwenye kundi la WHATS APP LA MAFANIKIO, kujiunga tuma
neno THE UNIVERSITY OF WINNER’S
kwenda 0713 048 035, hapo utapata
utaratibu mzima wa kujiunga.
Pia
kama wewe ni mfugaji wa kuku na unahitaji vifaranga bora, waone DM POULTRY FARM PROJECT kwa huduma ya
uhakika. Hawa ni wauzaji wa vifaranga wa kuku aina ya KUROILER, SASSO, PURE KIENYEJI na KUCHI. Kwa mahitaji ya vifaranga
wasiliana nao kwa 0767 048 035 au 0686
141097 na wote mnakaribishwa.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO
YAIMARIKE,
Ni
wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na
mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713
048 035,
Email; dirayamafanikio@gmail.com
\
Subscribe to:
Posts
(
Atom
)