Apr 24, 2019
Usipoteze Muda Wako, NI Utajiri Wa Kesho Yako.
Muda ni mchache, maisha uliyonayo au maisha tuliyonayo ni mafupi, kwa hiyo kila muda na fursa unayoipata hata kama ni ndogo sana, tafadhari itumie vizuri na kwa uhakika mkubwa. Kutumia muda wako hovyo, hakuna tofauti na wewe kuamua kupoteza fursa za mafanikio yako tena kwa makusudi.
Ili kutumia muda wako
vizuri, unatakiwa kufanya kile kinachotakiwa kufanyika kwa wakati ule hata kama mwili wako uwe unataka au hutaki. Moja ya kanuni ambayo inatumika na watu ambao
hawafanyi kitu katika maisha, ni kutokuchukulia leo katika umuhimu wake. Kama leo
yako unaiona ipo ipo tu, upo kwenye wakati wa kupoteza.
Maisha ya mafanikio
yanatengemezwa na hatua ndogo ndogo sana za kila siku. Inapotokea wengine
wanasita kuchukua hatua wewe unatakiwa kuchukua hatua na si kupoteza muda na
kusema nitafanya siku nyingine. Muda ulionao ni wa dhahabu, ukipotea umepotea,
kama ukijua thamani ya muda wako hutaweza kuupoteza tena.
Moja ya siri ya kufikia
mafanikio yako ni kutumia kwa usahihi kila fursa ambayo unaipata. Muda unakwenda
na kupaa, unatakiwa kuwa rubani kuendesha muda wako kwa usahihi. Jiulize, usipotumia leo fursa za mafanikio unazozipata
unataka kutumia fursa hizo lini au wakati gani, naamini unanipata vyema.
Mwanamafanikio William Ward
moja katui ya maandiko anasema, “unatakiwa ujifunze kujiendeleza kwa kusoma
wakati wengine wamelala, unatakiwa kuwekeza wakati wengine hawaoni fursa,
unatakiwa kujiandaa kwa kila kitu wakati wengine wanacheza”. Acha kupoteza muda
wa maisha yako kwa chochote, utumie vizuri.
Elewa hakuna muda bora kama
huu ulionao kwa sasa. Kama utakuwa ni mtu kupoteza muda wako na kusubiri, hicho
unachosubiri upo uwezekano hutaweza kukifanya tena au utakifanya kwa tabu. Wengi
wanaoahirisha mambo ukumbuke huja kuyafanya tena mara nyingi huwa ni ngumu sana
kwao kuweza kutokea.
Apr 23, 2019
Kama Utapoteza Jambo Hili, Hutalipata Tena Maishani Mwako.
Katika kijiji kimoja kulikuwako na watu watatu ambao walikuwa na safari ndefu sana ya kuelekea mbali na mahali walipokuwa wanaishi, safari hii ilikuwa ni mahususi kwa ajili ya kujitafutia riziki zao za kila siku ambazo zilipatikana katika msitu fulani uliokuwa mkubwa sana.
Watu
hawa walitembea kwa umbali mrefu sana ikafika mahala wakawa wapo katikati ya pori ambapo walianza kuingia na
hofu ndani mwao, watu hawa majina yao ni, mtu wa kwanza alikuwa akifahamika
kama moto, mtu wa pili alikuwa akifahamika kama maji na mtu wa tatu alikuwa
hajulikani ni nani.
Wakiwa
katikati ya pori wakiwa wamejawa na
wasiwasi na wanakokwenda huku
wakiwa hawaelewi watafika lini na muda gani, mmoja wao akawambia wenzake “ jamani eeh hebu
tusimame tuelezane kitu kimoja, huyu
hakuwa mwingine bali alikuwa ni moto, huku tukokwenda nahisi tunaweza tukapotea.
Kama
tunaweza tukapotea inabidi tuambiane ishara mapesa kabisa kwamba je, kama
ukipotea utawezaje kujulikana sehemu uliyopo? yeye moto akasema ikitokea tumeenda mahali na tukagawana kila
mtu njia yake na ikawa haileweki mtu mwingine yupo wapi, mimi kama moto ikatokea nimepotea basi
msisumbuke kunitafuta ninyi angalieni ishara ya moshi popote utakapouona moshi
unapotokea basi hapo ndipo
nitakapokuwepo.
Wakati
huo wote moto anazungumza maji na yule mwingine ambaye hajulikani wakasema
sawa mkuu sisi tumekuelewa.
Ikafika
zamu ya maji naye kuzungumza, maji akasema “ moto mimi nakubaliana na wewe hata
mimi nahisi kabisa kuna kila dalili zote za kupotea katika msitu huu, hivyo
kama ikitokeo tumegawanyika na mimi nikapotea, mimi ili niweze kuonekana wala
usisumbuke wewe angalia ishara ya kijani, ukiona sehemu ya kijani hapo ndipo
utakaponipata.
Baada
ya moto na maji kuzungumza hayo ikafika zamu ya mtu wa tatu ambaye
hajulikani kuzungumza, yeye akasema
“jamani mimi mwenzenu sitabiriki” mimi
nikipotea sielewi mtanipataje kwa kweli maana mimi sina ishara yeyote ile
nitakayoifanya ili mnione.
Sasa mimi na wewe tujiulize huyo mtu wa
tatu alikuwa ni nani? Ambaye alisema hana ishara yeyote ile endapo
atakuwa apotea? Endele kutafakari kisha unipe jibu.
Ila
kwa kuwa umekuwa mzembe wa kuumiza kichwa basi ngoja nikupe jibu, mtu wa tatu
alikwa ni muda.
Fundisho la hadithi hii ni:
Katika
maisha yako poteza vitu vyote utavipata lakini usije ukapoteza muda wako huwezi
kuupata, tumeona kuwa moto ukipotea ishara yake huwa ni moshi, pia tumeona maji yakipotea ishara unaweza
kuona ni ukijani katika uoto lakini muda ukipotea basi andika umeumia kwasababu
muda huo hauwezi kurudi tena.
Kwahiyo
tunafundishwa poteza vingine kwenye
maisha ila usithubutu kuja hata siku moja kuja kupoteza muda wako, kwani ukipoteza muda hakuna ishara
itakayokuonesha namna ya kupata ule muda ulioupoteza.
Hivyo
fundisho kubwa hapa ni kuhakikisha unatumia muda wako vizuri ila kwa baadae
usije ukajuta kwamba ulikuwa mjinga kwa kupoteza muda wako kwa kiasi hicho.
Nikutakie
kila la kheri na tafakari njema ya hadithi hii, byee.
MAKALA HII IMEANDIKWA NA AFISA MIPANGO
BENSON CHONYA.
Apr 22, 2019
Kama Utakosa Kitu Hiki Sahau Kuishi Maisha Ya Uhuru, Furaha Na Mafanikio.
Kama upo kwenye chombo cha usafiri, halafu ni usiku na tena unataka kusafiri mbali na kwa haraka zaidi, kitu cha kwanza unachotakiwa kuhakikisha chombo hicho inacho ni mwanga wa uhakika. Pasipo mwanga wa uhakika safari yako itakuwa ni ya shida kidogo, unaweza ukaenda lakini si kwa kasi na mwendo ule unaoutaka wewe.
Hata kwenye maisha yako
ukitaka kufika mbali kimafanikio kitu kimojawapo unachotakiwa kuwa nacho ni
kujifunza kuwa na msamaha. Unapokuwa na msamaha, inakusaidia kuondoa uchungu,
hasira, visasi vyote unakuwa umeweka pembeni na matokeo yake unakuwa huru
kufanya mambo mengine na kusonga mbele.
Kuishi maisha ya kutokuwa na
msamaha, ni sawa na kuendesha gari huku ukiwa umeshikilia breki, kwani kwa
kufanya hivyo mwendo wako hautakuwa mzuri, ni rahisi kukosa mwelekeo na hata
kupotea kabisa. Unatakiwa kukumbuka unapokuwa na msamaha hiyo inakuweka huru
sana wewe kuweza kufikia mafanikio yako.
Unapoamua kuishi maisha ya
kutokuwa na msamaha kitu kitakachofatia hapo kwako ni kwa wewe kuishi maisha ya
kisasi. Inapotokea ukaishi maisha ya kisasi mwanzo inaweza ikaonekana ni maisha
mazuri, lakini nikwambie maisha hayo yanakuwa ni mabaya sana kwako kwani
yatakuzuia wewe kuweza kuendelea mbele sana.
Unapokosa msamaha kabisa
ujue unakuwa maisha ambayo yanakuwa ya uchungu karibu wakati wote. Unatakiwa kujua
ufunguo mojawapo wa furaha ni wewe kujijengea tabia ya kuwa na msamaha. Kama
hautakuwa na msamaha sahau kabisa kwa wewe kuweza kuishi maisha ya furaha au
maisha ya uhuru.
Kwa mujibu wa wataalumu wa
saikolojia na mafanikio, inasemekana moja ya siri muhimu ya kuishi maisha marefu
na yenye faida kila siku ni kwamba kabla hujalala, jifunze kumsamehe kila mtu
ambae amekukosea. Unapowasamehe watu hao ambao wamekukosea hiyo ni njia ya wewe
kuendelea kufanikiwa kwenye mambo yako.
Ni bora ukasamehe na kusahau
kuliko ukashindwa kusamehe na kukumbuka. Elewa, kusamehe kila wakati kunaendana
na Baraka, lakini kutokusamehe kunakuumiza wewe na kunakupotezea sana milango
mikubwa ya Baraka ambayo inatakiwa itokee kwako. Kwa hiyo ipo haja ya wewe kuweza
kusamehe kwa namna yoyote ile.
Kabla hujamaliza siku yako unatakiwa ujue ni watu gani ambao
wanahitaji msamaha wako na wasamehe hata usipowaambia. Usichome daraja moto mara
baada ya kuvuka mto. Nikwambie huwezi kujua utatumia daraja hilo mara ngapi
tena kwa usafiri. Ipo faida ya kuishi maisha ya msamaha, hebu anza leo kuishi
maisha hayo uone faida zake.
Jiulize ni wapi unakwama hadi
ushindwe kutoa msamaha, je msamaha unaotaka kuutoa kwani unalipiwa? Kama msamaha
unaotaka kuutoa ni bure, hebu samehe na kisha baki huru na maisha yako. Maisha yako
hayatakuwa mabaya kisa umemeshindwa kusamehe, zaidi utajenga maisha ya
mafanikio makubwa kwako.
Fanyia
kazi haya na chukua hatua kuhakikisha ndoto zako zinatimia.
Tunakutakia kila la kheri na
endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku kujifunza maisha na
mafanikio.
Pia
rafiki, kama unapenda kujifunza zaidi kuhusu mafanikio, karibu kwenye kundi la WHATS APP LA MAFANIKIO, kujiunga tuma
neno THE UNIVERSITY OF WINNER’S
kwenda 0713 048 035, hapo utapata
utaratibu mzima wa kujiunga.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO
YAIMARIKE,
Ni
wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na
mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 713 048 035,
Email; dirayamafanikio@gmail.com
Subscribe to:
Posts
(
Atom
)