Apr 22, 2019
Kama Utakosa Kitu Hiki Sahau Kuishi Maisha Ya Uhuru, Furaha Na Mafanikio.
Kama upo kwenye chombo cha usafiri, halafu ni usiku na tena unataka kusafiri mbali na kwa haraka zaidi, kitu cha kwanza unachotakiwa kuhakikisha chombo hicho inacho ni mwanga wa uhakika. Pasipo mwanga wa uhakika safari yako itakuwa ni ya shida kidogo, unaweza ukaenda lakini si kwa kasi na mwendo ule unaoutaka wewe.
Hata kwenye maisha yako
ukitaka kufika mbali kimafanikio kitu kimojawapo unachotakiwa kuwa nacho ni
kujifunza kuwa na msamaha. Unapokuwa na msamaha, inakusaidia kuondoa uchungu,
hasira, visasi vyote unakuwa umeweka pembeni na matokeo yake unakuwa huru
kufanya mambo mengine na kusonga mbele.
Kuishi maisha ya kutokuwa na
msamaha, ni sawa na kuendesha gari huku ukiwa umeshikilia breki, kwani kwa
kufanya hivyo mwendo wako hautakuwa mzuri, ni rahisi kukosa mwelekeo na hata
kupotea kabisa. Unatakiwa kukumbuka unapokuwa na msamaha hiyo inakuweka huru
sana wewe kuweza kufikia mafanikio yako.
Unapoamua kuishi maisha ya
kutokuwa na msamaha kitu kitakachofatia hapo kwako ni kwa wewe kuishi maisha ya
kisasi. Inapotokea ukaishi maisha ya kisasi mwanzo inaweza ikaonekana ni maisha
mazuri, lakini nikwambie maisha hayo yanakuwa ni mabaya sana kwako kwani
yatakuzuia wewe kuweza kuendelea mbele sana.
Unapokosa msamaha kabisa
ujue unakuwa maisha ambayo yanakuwa ya uchungu karibu wakati wote. Unatakiwa kujua
ufunguo mojawapo wa furaha ni wewe kujijengea tabia ya kuwa na msamaha. Kama
hautakuwa na msamaha sahau kabisa kwa wewe kuweza kuishi maisha ya furaha au
maisha ya uhuru.
Kwa mujibu wa wataalumu wa
saikolojia na mafanikio, inasemekana moja ya siri muhimu ya kuishi maisha marefu
na yenye faida kila siku ni kwamba kabla hujalala, jifunze kumsamehe kila mtu
ambae amekukosea. Unapowasamehe watu hao ambao wamekukosea hiyo ni njia ya wewe
kuendelea kufanikiwa kwenye mambo yako.
Ni bora ukasamehe na kusahau
kuliko ukashindwa kusamehe na kukumbuka. Elewa, kusamehe kila wakati kunaendana
na Baraka, lakini kutokusamehe kunakuumiza wewe na kunakupotezea sana milango
mikubwa ya Baraka ambayo inatakiwa itokee kwako. Kwa hiyo ipo haja ya wewe kuweza
kusamehe kwa namna yoyote ile.
Kabla hujamaliza siku yako unatakiwa ujue ni watu gani ambao
wanahitaji msamaha wako na wasamehe hata usipowaambia. Usichome daraja moto mara
baada ya kuvuka mto. Nikwambie huwezi kujua utatumia daraja hilo mara ngapi
tena kwa usafiri. Ipo faida ya kuishi maisha ya msamaha, hebu anza leo kuishi
maisha hayo uone faida zake.
Jiulize ni wapi unakwama hadi
ushindwe kutoa msamaha, je msamaha unaotaka kuutoa kwani unalipiwa? Kama msamaha
unaotaka kuutoa ni bure, hebu samehe na kisha baki huru na maisha yako. Maisha yako
hayatakuwa mabaya kisa umemeshindwa kusamehe, zaidi utajenga maisha ya
mafanikio makubwa kwako.
Fanyia
kazi haya na chukua hatua kuhakikisha ndoto zako zinatimia.
Tunakutakia kila la kheri na
endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku kujifunza maisha na
mafanikio.
Pia
rafiki, kama unapenda kujifunza zaidi kuhusu mafanikio, karibu kwenye kundi la WHATS APP LA MAFANIKIO, kujiunga tuma
neno THE UNIVERSITY OF WINNER’S
kwenda 0713 048 035, hapo utapata
utaratibu mzima wa kujiunga.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO
YAIMARIKE,
Ni
wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na
mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 713 048 035,
Email; dirayamafanikio@gmail.com
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.