Apr 23, 2019
Kama Utapoteza Jambo Hili, Hutalipata Tena Maishani Mwako.
Katika kijiji kimoja kulikuwako na watu watatu ambao walikuwa na safari ndefu sana ya kuelekea mbali na mahali walipokuwa wanaishi, safari hii ilikuwa ni mahususi kwa ajili ya kujitafutia riziki zao za kila siku ambazo zilipatikana katika msitu fulani uliokuwa mkubwa sana.
Watu
hawa walitembea kwa umbali mrefu sana ikafika mahala wakawa wapo katikati ya pori ambapo walianza kuingia na
hofu ndani mwao, watu hawa majina yao ni, mtu wa kwanza alikuwa akifahamika
kama moto, mtu wa pili alikuwa akifahamika kama maji na mtu wa tatu alikuwa
hajulikani ni nani.
Wakiwa
katikati ya pori wakiwa wamejawa na
wasiwasi na wanakokwenda huku
wakiwa hawaelewi watafika lini na muda gani, mmoja wao akawambia wenzake “ jamani eeh hebu
tusimame tuelezane kitu kimoja, huyu
hakuwa mwingine bali alikuwa ni moto, huku tukokwenda nahisi tunaweza tukapotea.
Kama
tunaweza tukapotea inabidi tuambiane ishara mapesa kabisa kwamba je, kama
ukipotea utawezaje kujulikana sehemu uliyopo? yeye moto akasema ikitokea tumeenda mahali na tukagawana kila
mtu njia yake na ikawa haileweki mtu mwingine yupo wapi, mimi kama moto ikatokea nimepotea basi
msisumbuke kunitafuta ninyi angalieni ishara ya moshi popote utakapouona moshi
unapotokea basi hapo ndipo
nitakapokuwepo.
Wakati
huo wote moto anazungumza maji na yule mwingine ambaye hajulikani wakasema
sawa mkuu sisi tumekuelewa.
Ikafika
zamu ya maji naye kuzungumza, maji akasema “ moto mimi nakubaliana na wewe hata
mimi nahisi kabisa kuna kila dalili zote za kupotea katika msitu huu, hivyo
kama ikitokeo tumegawanyika na mimi nikapotea, mimi ili niweze kuonekana wala
usisumbuke wewe angalia ishara ya kijani, ukiona sehemu ya kijani hapo ndipo
utakaponipata.
Baada
ya moto na maji kuzungumza hayo ikafika zamu ya mtu wa tatu ambaye
hajulikani kuzungumza, yeye akasema
“jamani mimi mwenzenu sitabiriki” mimi
nikipotea sielewi mtanipataje kwa kweli maana mimi sina ishara yeyote ile
nitakayoifanya ili mnione.
Sasa mimi na wewe tujiulize huyo mtu wa
tatu alikuwa ni nani? Ambaye alisema hana ishara yeyote ile endapo
atakuwa apotea? Endele kutafakari kisha unipe jibu.
Ila
kwa kuwa umekuwa mzembe wa kuumiza kichwa basi ngoja nikupe jibu, mtu wa tatu
alikwa ni muda.
Fundisho la hadithi hii ni:
Katika
maisha yako poteza vitu vyote utavipata lakini usije ukapoteza muda wako huwezi
kuupata, tumeona kuwa moto ukipotea ishara yake huwa ni moshi, pia tumeona maji yakipotea ishara unaweza
kuona ni ukijani katika uoto lakini muda ukipotea basi andika umeumia kwasababu
muda huo hauwezi kurudi tena.
Kwahiyo
tunafundishwa poteza vingine kwenye
maisha ila usithubutu kuja hata siku moja kuja kupoteza muda wako, kwani ukipoteza muda hakuna ishara
itakayokuonesha namna ya kupata ule muda ulioupoteza.
Hivyo
fundisho kubwa hapa ni kuhakikisha unatumia muda wako vizuri ila kwa baadae
usije ukajuta kwamba ulikuwa mjinga kwa kupoteza muda wako kwa kiasi hicho.
Nikutakie
kila la kheri na tafakari njema ya hadithi hii, byee.
MAKALA HII IMEANDIKWA NA AFISA MIPANGO
BENSON CHONYA.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.