Jul 1, 2020
MAMBO YA KUJUA KABLA HUJAACHA KAZI.
Naamini umejifunza masomo ya kuyajua kabla hujaacha kazi, lakini pia mbali na masomo hayo hapa kuna mambo ya kuyajua kabla hujaacha kazi.
Haya ni mambo ambayo unatakiwa
ujikumbushe ili kujenga
msingi mzuri wa ujasiriamali.
Naomba twende pamoja kujifunza mambo hayo;-
Jambo #1. Kabla hujaacha kazi, unatakiwa ujue, jinsi ya kubadilisha bahati mbaya na kuwa bahati nzuri.
Kama hujui jinsi ya kubadilisha bahati mbaya, na kuwa bahati
nzuri, usijaribu kuacha
kazi utajiumiza sana. Ujasiriamali una mambo mengi sana ya changamoto.
Hivyo kwa kadri unavyokutana na changamoto ngumu kabisa,
unatakiwa ujue jinsi ya kuzibadilisha changamoto hizo na kuwa bahati nzuri.
Kama ukishindwa, basi tulia na ajira.
Jambo # 2. Kabla hujaacha kazi, unatakiwa kujua, ni shughuli zipi zinatengeneza biashara ya mafanikio.
Biashara haihusishi mauzo tu peke yake. Kama ndio umetoka
kwenye ajira na una akili ya kuwaza mauzo peke yake, utakwama. Unatakiwa ujue
biashara inahusisha mambo mengi.
Zipo shughuli nyingi zinazotengeneza mafanikio ya
biashara kama huduma kwa wateja, usafi, au mawasiliano mazuri na wateja.
Kabla hujaacha kazi, unatakiwa kuzingatia haya kwanza.
Kama utaingia kwenye ujasiriamali na umegoma
kujiendeleza, utashindwa sana, kwa sababu kwenye ujasiriamali zipo changamoto
nyingi na zinazotaka kichwa chako kiwe kizuri.
Na kwa sababu ya changamoto hizo inatakiwa muda wote uwe
bora na pia wanaokuzunguka wawe bora. Yote haya utayapata kwa wewe kuamua
kujifunza na kujinoa.
Jambo # 4. Kabla hujaacha kazi, jifunze kidogo elimu ya uhasibu.
Kwa kujifunza elimu hii, itakusaidia sana kujua mtiririko
wa pesa katika biashara, pia itakusaidia kujua bajeti ya biashara na yako
kitaalamu zaidi, tofauti na ungekuwa hujui.
Kama kwako ni ngumu kujifunza elimu hii, basi, biashara
ikikua kidogo, ajiri angalau mhasibu anayejua vizuri na uwe unamlipa. Hii
itakusaidia kujenga biashara yako kwa mafanikio.
Jambo la #5. Kabla hujaacha kazi, kumbuka kuwa safari yako ya mafanikio inaanzia ndani ya moyo na roho yako.
Hapa kabla hujaacha kazi unatakiwa ujiulize, ndani mwako
unaona mafanikio? Hii ikiwa na maana kwamba mafanikio yako lazima uyaone ndani
kwanza kabla hayajaonekana kwa nje.
Hata kwa hatua unazochukua inatakiwa zidhihirishe kile
kilicho moyoni mwako. Kama mafanikio moyoni huyaoni usijaribu kuacha kazi,
maana hata kwenye ujasiriamali hutafanikiwa pia.
Jambo #6. Kabla hujaacha kazi, unatakiwa ujue, kitu chochote unachotaka kukiuza, kina bei tatu za msingi. Bei ya chini, bei ya kati na bei ya juu.
Kama utachagua kuuza kitu hicho kwenye bei ya chini,
unatakiwa ujue pia dakika yoyote ataibuka mtu wa kushindana na wewe.
Ili uwe mshindi katika kuuza kwa bei ya chini unatakiwa uwe na njia nzuri sana
ya kuuza bidhaa yako.
Kama utachagua kuuza bidhaa zako kwa bei ya juu, pia jifunze
kutoa huduma bora. Kama
huelewi hili vizuri, nenda kwenye hotel zinazotoa huduma kwa bei ya juu uone
vizuri kile wanachokifanya ni nini kwenye biashara zao.
Jambo #7. Kabla hujaacha kazi, unatakiwa kujua na kukumbuka, mauzo=kipato.
Kama utakuwa unataka
kuacha kazi na ukajigundua kwenye
mauzo haupo vizuri.,
nikwambie tu, jifunze kuuza kwanza, halafu ndo uache kazi. Kama huwezi
kuuza, hiyo ni shida kwako kufanikiwa.
Tunaambiwa asilimia kubwa ya watu wengi huwa tunazaliwa
hatujui kuuza. Hata hivyo unaweza kujifunza kuuza ili uwe mjasiriamali mzuri,
vinginevyo utakwama. Anza kujifunza
kuuza, utafanikiwa.
Jambo # 8. Kabla hujaacha kazi, unatakiwa kujua vizuri jinsi ya kutumia pesa zako vizuri.
Ni wazi wajasiriamali walio wengi, hawajui jinsi ya
kutumia pesa zao vizuri. Wanajikuta wanatumia tu pesa hawajui zitarudi vipi.
Sasa usiingie kwenye mtego huo.
Ili uwe mjasiriamali mwenye mafanikio, unatakiwa kujua
kila shilingi ya pesa yako inakwenda wapi. Ukiona unafika sehemu unashangaa
pesa zako zimeenda wapi, bado hujajua jinsi ya kuzitumia.
Jambo #9. Kabla hujaacha kazi, anzisha biashara ya pembeni kwa ajili ya kujifunza ujasiriamali.
Hakuna ambae anaweza akaendesha baiskeli pasipo
kujifunza. Hata kwenye biashara mambo yako hivyo, unatakiwa uwe na biashara ya
mazoezi kabla hujaacha kazi na kuingia kwenye ujasiriamali.
Usije ukafanya kosa la kuacha
kazi, wakati hata hujui ABC za ujasiriamali ziko vipi. Ukiwa unafanya biashara huku umeajiriwa,
itakupa ukomavu wa wewe kufanikiwa kibiashara.
Jambo #10. Kabla hujaacha kazi, tafuta mshauri wa mafanikio/mentor.
Ni ngumu sana kwa wajasiriamali wengi, kuwa na mshauri wa
mafanikio, lakini kabla hujaamua kuacha kazi, hakikisha una mshauri huyu wa
mafanikio ambae atakuongoza katika njia sahihi.
Kama unaona kumpata
mshauri wako wa mafanikio ni ngumu, basi amua kufanya
vitabu viwe ndo mshauri wako. Kwenye vitabu unatakiwa kujifunza sana na
itakusaidia kufanikiwa.
Jambo #11. Kabla hujaacha kazi, tafuta mtandao wa wajasiriamali.
Usije ukakimbilia kwenye ulimwengu wa ujasiriamali, kama
huna mtandao wa ujasiriamali. Kitendo cha kuwa na mtandao huu, kitakusaidia
sana wewe katika safari yako ya kimafanikio.
Inakubidi utafute mtandao, ambao kwako unaona unakufaa na
kukusaidia. Kila wakati jumuika katika mikutano yao ili kupata uzoefu
utakaokujenga, kukulea na kukusaidia kufikia malengo.
Jambo #12. Kabla hujaacha kazi, tazama mtazamo wako.
Ikiwa mtazamo wako unaona tu kwamba ukiingia kwenye
ujasiriamali unapata mafanikio ya
moja kwa moja, unajidanganya. Inakubidi ujue kwamba zipo changamoto na
unatakiwa kuzifanyia kazi.
Ukijua hili, au ukaamua kuingia na mtazamo huu, wa
kutambua changamoto za ujasiriamali, utakusaidia kupambana na changamoto
zinazojitokeza.
Mwisho; kabla hujaacha kazi, unatakiwa uwe na imani sahihi
kwenye ujasiriamali na kuielewa vizuri, misingi sahihi ya ujasiriamali.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.