Oct 6, 2021
Njia mbili ziletazo mafanikio maishani.
Katika kufikia mafanikio yoyote yale, huwa zipo njia za kuweza kufikia mafanikio hayo. Hakuna mafanikio ambayo yanapatikana nje ya njia husika za mafanikio.
Na kwa kawaida, zipo njia mbili bora za kuufikia mafanikio. Hizi ni njia halali ambazo zinatumiwa na watu wote wenye mafanikio ya kweli na halali duniani.
Njia ya kwanza; Njia ya kawaida.
Hii ni njia ambayo mtu anafikia mafanikio makubwa kutokana na malengo anayoyafatilia kila siku. Hapa lazima uwe na malengo ya kuyafatilia kila siku.
Katika njia hii unakuwa na malengo yako, lakini wakati huo huo unakuwa unaenda nayo mdogo mdogo hadi kuweza kufanikiwa kwa kiasi kikubwa.
Hii ni njia bora, inayoaminika, kwa sababu kuna kujifunza mengi ndani yake, ingawa inataka muda na uvumilivu, lakini mwisho wa siku utafika.
Njia ya pili; Njia isiyo ya kawaida.
Hii ni njia isiyo ya kawaida kwa sababu ndani yake kuna kuwa na hali hatarishi nyingi. Kwa mfano, kuna kuweka mtaji mkubwa ndani yake au kuchukua hatua kubwa kabisa.
Katika kutekeleza njia hii iko hivi, unakuwa unafata njia ile ya kawaida kama kawaida, isipokuwa katika njia hii kuna vitu ambavyo vinaongezeka.
Katika njia hii lazima utenge kiasi fulani cha pesa, ili kuingiza katika 'dili' ambazo zinajitokeza kati kati lakini wakati huo ukiendelea na njia ya kwanza.
Kufata njia ya pili hatumaanishi njia ya kwanza umeiacha, hapana unakuwa nayo, isipokuwa hii unaitumia kama ziada kutengenezea pesa ndefu.
Hizi ndio njia kubwa mbili, ambazo zinatumiwa na watu wengi
wenye mafanikio kuweza kufanikiwa. Ni muhimu kutumia njia zote mbili ili
kujihakikishia mafanikio.
Kila la kheri katika kufikia mafanikio yako.
Kama unapenda kujiunga na kundi la mafanikio ili uweze kujifunza zaidi mambo mengi ya kimafanikio. Tuma neno THE UNIVERSITY OF WINNER'S kwenda 0687449428 na utapewa utaratibu wa kuunganishwa.
Hakimiliki©2021 Imani Ngwangwalu. Haki Zote Zimehifadhiwa. Makala hizi hutolewa kwa ajili ya kuboresha maisha yako. Ruksa 'kushare' na usibadili kitu chochote bila ya ruhusa ya mwandishi.
Oct 5, 2021
Zingatia Jambo Hili Sana, Litakusaidia Kufanikiwa.
Inapotokea kuna kitu hukijui, kuwa mtu wa shukrani, kwa sababu umepata fursa nzuri ya kujifunza juu ya kitu hicho.
Inapotokea unapitia magumu katika maisha yako, shukuru pia, kwani magumu hayo yanakufanya uwe bora na imara.
Ikiwa pia unapitia changamoto sana, huo sio wakati wa kukimbia, bali ni wakati wako wa kujiboresha kimaisha.
Unapokuwa umechoka kwa sababu ya kazi, basi pia huo ni muda wa kushukuru, kwa sababu kuna mabadiliko umefanya.
Kama umefanya makosa, pia shukuru, kwa sababu hiyo inakukumbusha ni kipi ambacho hutakiwi tena kukifanya.
Ni rahisi sana kuwa na shukrani na mambo mazuri, lakini pia jifunze kuwa na shukrani hata kwenye changamoto.
Watu wengi si wepesi sana wa kushukuru pale wanapokutana na magumu. Ni watu ambao wanakuwa hawaoni zuri lolote.
Kipo kitu chanya au kizuri unaweza kukiona pia kwenye changamoto. Usilalamike, jifunze kupitia changamoto yako.
Yapo mafanikio na baraka ambazo zimejificha kwenye changamoto. Unatakiwa uyaone mafanikio hayo.
Changamoto unazopitia zina uwezo wa kukufanya, ujifunze, ukue na kuwa jasiri wa kufikia mafanikio yako.
Zingatia, mafanikio yako utaendelea kuyapata kama utakuwa mtu wa shukrani katika kila eneo la maisha yako.
Kuwa na shukrani ni msingi mkubwa sana wa mafanikio yako. Anza
leo kuwa mtu wa shukrani, utafanikiwa.
Kila la kheri katika kufikia mafanikio yako.
Kama unapenda kujiunga na kundi la mafanikio ili uweze kujifunza zaidi mambo mengi ya kimafanikio. Tuma neno THE UNIVERSITY OF WINNER'S kwenda 0687449428 na utapewa utaratibu wa kuunganishwa.
Hakimiliki©2021 Imani Ngwangwalu. Haki Zote Zimehifadhiwa. Makala hizi hutolewa kwa ajili ya kuboresha maisha yako. Ruksa 'kushare' na usibadili kitu chochote bila ya ruhusa ya mwandishi.
Oct 4, 2021
Mawazo Kumi (10) Yatakayokupa Nguvu Kubwa Yakufikia Mafanikio Yako.
Mafanikio siku zote yanaanza na mawazo. Kama hakuna wazo sahihi ieleweke pia hakuna mafanikio sahihi ambayo yataweza kuchipua kwa nje, sana sana utakuwa ni mtu wa kushindwa kila wakati. Kupitia makala haya utajifunza mawazo muhimu yatakusaidia kuweza kufikia mafanikio yako. Karibu na twende tujifunze;-Oct 3, 2021
Weka Umakini Wako Wote Kwenye Vitu Hivi Na Utafanikiwa.
Kila wakati zingatia kile kinacholeta mabadiliko sana kwenye maisha na unatakiwa kuachana na kile ambacho hakileti mabadiliko kwenye maisha yako. Kama unaendelea kufanya vitu ambavyo havileti matokeo chanya kwako huko ni kujipoteza.Oct 2, 2021
Jinsi Ya Kupika Tambi Za Mayai.
Oct 1, 2021
Hiki Ndicho Kitu Kinachokuzuia Kufanya Mabadiliko Kwenye Maisha Yako.
Wakati ulipokuwa shule ulisoma sana na kuhakikisha unafaulu ili kukwepa maumivu ya kufeli. Pia kuna wakati umeweka juhudi nyingi sana ili kukwepa maumivu ya aina fulani na kutafuta mahala sahihi kwako.
Tunaambiwa kitu chenye nguvu ya kubadili tabia yako na mafanikio ni maumivu. Waulize wote ambao wamefanikiwa na ambao wanafikiri chanya kuhusu mafanikio, watakwambia maumivu yamewasaidia sana kubadilika na kuweza kufika hapo walipo mpaka leo.