Nov 22, 2022
WAZO LA KUJIAJIRI: Biashara Ya Vikombe Vya Chai Vyenye kubadili Rangi Vikiwekwa Chai Au Maji Ya Moto.
Naam,
wala usishangae najua tumezoea kunywa chai kwa kutumia vikombe hivi vya kawaida
ambavyo havina kitu cha kushangaza pindi utuamiapo. Sasa katika wazo letu la
kujiajiri tunakuleta wazo jipya ambalo kwa baadhi ya watu huenda likawa ni geni
kabisa. Wazo hili si jingine bali ni vikombe vya udongo ambavyo hubadili
mwonekano hasa pale vinapowekwa maji ya moto au chai.
Vikombe
hivi ni vizuri sana ndugu yangu kwa sababu ya uimara wake lakini najua pindi
utakapoamua kuifanya biashara ya vikombe hivi utawashangaza wengi sana na
kiukweli utapata wateja wengi sana. Chukua sekunde chache wawaze mamantile
waliopo mtaani kwako, usiishie hapo endelea kuwaza mahotel ambayo upo nayo
karibu.
Endelea
kuwaza wale watoto ambao hawapendi kunywa chai, vipi ukimpa mtoto huyo chai
kwenye kikombe ambacho kitaonesha sura yake pamoja na jina lake bila shaka
mtoto huyo hata kusumbua tena kwenye suala la kunywa chai na uji pia, kwa
sababu mtoto huyo atashangaa majabu ya kikombe hicho pia hivyo atakunywa tu.
Endelea
kuwaza kwa sauti ya chini, Vipi mumeo anaamka asubuhi kabla ya kwenda kazini
anakuta umemuwekea maziwa kwenye kikombe kimeandikwa “ I love you Benson” na
hilo ndilo jina la mumeo na akimaliza kunywa chai hiyo hayo maandishi yanatopea
hadi kesho tena kikombe hicho kikiwekewa chai, bila shaka mumeo huyo
atafarijika na michepuko haitakuwa
nafasi tena na utafurahia ndoa yako.
Kwa
mifano hiyo michache utaona ni kwa namna gani vikombe hivo jinsi vitakavyokupa
hela nyingi kwa sababu kwa hapa nchini kwetu havipo kwa wingi, hivyo bado ni
fursa ambayo ni mbichi kabisa. Hivyo ni nafasi yako mwafaka wa kukamatia fursa
hii na kuanza kuifanyia kazi ili uanze pia kujitengenezea pesa.
Kumbuka;
Vikombe hivi hubadilisha rangi, picha,
maneno kila vinapowekwa chai au maji ya
moto hivyo ni fursa sana kama utaifikiria
kwa jicho la tatu.
-------------------------------------------------------------------------------------------------
MUHIMU: Kama utakuwa upo tayari na unahitaji kufanya biashara hii
wasiliana na uongozi wa DIRA YA MAFANIKIO kwa nambari 0757 909 942 au bofya
namba hii tuwasiliane kupigia whatsapp wa.me/+255757909942 hii au email yetu ya dirayamafanikio@gmail.com
------------------------------------------------------------------------------------------------
Makala hii imeandikwa; Benson Chonya
------------------------------------------------------------------------------------------------
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.