Nov 17, 2022
Hivi Ndivyo Njia Ya Mafanikio Ilivyo...
Njia ya mafanikio ni ndefu. Hakuna njia ya mafanikio iliyo fupi. Njia ya mafanikio ni ndefu kwa sababu, katika urefu huo huo, ndimo kuna kujifunza kwingi.
Ikiwa unatafuta njia ya mkato, basi wewe unatafuta kuwa na msongo wa mawazo na kijichanganya zaidi. Njia za mkato hazina kujifunza zaidi utaumia tu wewe.
Mafanikio ni sawa na mbio za muda mrefu. Mafanikio sio mbio za muda mfupi, hivyo inakubidi ukubali kujifunza kwa namna yeyote ile. Ili ujifunze lazima ufuate njia ndefu.
Kuna hadithi moja, inayoeleza kwa ufasaha juu ya hili kuwa ni muhimu kufuata njia ndefu iliyoko kwenye mpango wa Mungu ili kufanikiwa na kujifunza mengi zaidi.
Kulikuwa na ndege mmoja ambayo alikuwa mzuri sana. Ndege huyo kila ilipokuwa ikifika jioni alikuwa anatua kwenye mti na kuanza kuimba nyimbo nzuri sana za kuvutia.
Siku moja wakati anaimba, mara alitokea mtu akiwa ameshikilia boksi, yule ndege akauliza, vipi mbona umebeba boksi kama zito hivi humo ndani lina nini? yule mtu akamwambia lina minyoo.
Yule ndege akafikiria akamwambia basi, naomba mmoja. Yule mtu akamwambia nipe na wewe nyoa moja na mimi nakupa mnyoo mmoja. Basi ndege akakubali akawa anatoa nyoa, anapewa mnyoo, mwisho wa siku ndege akajikuta hana manyoa karibu yote.
Ule uzuri aliokuwa nao ukawa umetoweka. Akawa hawezi kuruka tena. Kitu kikubwa kilichomwathiri ni kutaka kutafuta njia ya mkato ya kutafuta chakula wakati njia nzuri alikuwa nayo.
Hivyo, ndivyo athari za kutafuta njia za mkato zinavyojitokeza. Ni vyema na ni bora ukafata njia ndefu ikawa na manufaa kuliko njia fupi yenye majanga makubwa.
Kila la kheri katika kufikia mafanikio makubwa.
Endelea kujifunza kupitia MafanikioApp na dirayamafanikio.blogspot.com kwa ajili ya kujifunza.
Kama unapenda kujiunga na kundi la mafanikio ili uweze kujifunza zaidi mambo mengi ya mafanikio. Tuma neno THE UNIVERSITY OF WINNER'S kwenda 0687449428 na utapewa utaratibu wa kuunganishwa.
Hakimiliki©2022 Imani Ngwangwalu. Haki zote zimehifadhiwa. Makala hizi hutolewa kwa ajili ya kuboresha maisha yako. Rukhsa 'kushare' na usibadili kitu chochote bila ruhusa ya mwandishi.
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.