Jan 16, 2015
Huyu Ndiye Kinyozi Anayemiliki Magari 75, Soma Hapa Kujua Zaidi.
Unaweza ukaona ni kitu kama cha kushangaza au haiwezekani lakini
huu ndio ukweli, binadamu anapoamua kujikubali na kuthamini kile anachokifanya anauwezo
mkubwa sana wa kufika mbali kimafanikio kuliko anavyofikiri. Ukweli huu unakuja
kujidhihirisha wazi, kwa kijana Ramesh Babu ambaye anavuna utajiri wa kutosha
kutokana na kunyoa tu. Mfanyabiashara Leonard Willoughby aliwahi kusema; ‘siku utakayoanza kuishi kwa kuifuata mipango
yako unayopanga, kila kitu katika maisha yako kitabadilika kabisa.’
Inawezekana watu wengi wanaufahamu msemo huo, lakini Ramesh Babu anajitapa
kuyatendea kazi maneno hayo.
Babu ambaye ni kinyozi bilionea pekee nchini India, anasema
aliuchukua ushauri wa Willoughby na kuamua kuutendea kazi tangu siku ya kwanza
alipousikia na kwamba maisha yake yalianza kubadilika.
Kwa mujibu wa Jarida la ‘Your story’ la nchini India, Babu
amefanikiwa kuvuka vizingiti kadhaa vya umaskini hadi kufikia kuwa mmoja wa
watu maarufu nchini humo akiwa na uwezo wa kununua gari aina yoyote anayoitaka. Asema kuwa mwaka 1994 alinunua gari lake la kwanza aina ya
Maruti, lakini aliendelea na kuhifadhi fedha kidogo kidogo alizokuwa anazipata
hadi mwaka 2004, alipoanzisha kampuni ya kokodisha magari, ikiwa na magari saba
wakati huo.
Hadi kufikia mwaka jana, kinyozi huyo amenunua magari 75 kati ya
hayo matano ni ya kifahari yakiwemo, Mercedes, BMW, Audi, mabasi kumi na lile
analolipenda liitwalo Rollsw Royce. Pamoja na utajiri huo
mkubwa alionao Babu, bado anaendelea na kazi yake ya kinyozi. Akisimulia maisha
yake ya awali, anasema kuwa alizaliwa katika familia masikini, baba yake
alikuwa kinyozi na kwamba alifariki mwaka 1979 wakati Babu akiwa na miaka saba. “Baba yangu alituachia biashara ya saluni Mtaa wa Brigade ambalo
mjomba wangu alichukua akaanza kuiongoza. Anawa anatupa kiasi kidogo cha fedha.
Tulikuwa tunakula chakula kimoja kwa siku ili tuweze kuishi tu,” anasimulia.
Anasema alipokuwa shule ya msingi, alilazimika kufanya kazi ili
kuweza kujikimu kimaisha kwa kupata kiasi kidogo cha fedha. “Nilikuwa nikibeba magazeti na chupa za maziwa na kitu kingine
chochote ambacho kingeweza kupunguza ugumu wa maisha ya mama yangu. Hii ndiyo
sababu ya kuhitimu masomo yangu,” anasema. Baadaye alifanikiwa uendelea
na masomo yake, jambo lililomfanya mama yake aanzishe ugomvi na mjomba
aliyekuwa akisimamia duka baada ya kugoma kutoa fedha za matumizi. “Ndipo nilipomwambia mama nitachukua saluni na kukiendesha
mwenyewe. Hakupenda uamuzi huo kwa kuwa alifikiri nitaacha masomo, lakini
nilianza kazi hiyo.
“Asubuhi nilikuwa saluni, jioni nilikwenda masomoni kisha usiku
nilikuwa saluni tena na kufanya kazi hadi saa 7 usiku. Hivyo ndivyo nilivyoanza
kuitwa kinyozi,” anasema.
Milango ya baraka inafunguka
Mwishoni mwa mwaka 1993, Babu alinunua gari la mtumba aina ya
Maruti Van. Kwa kuwa mjomba wangu alikuwa ameshanunua gari moja alinishawishi
na mimi kununua.ilibidi babu yangu aweke nyumba yake dhamana nini nimchukue
mkopo. “Binti katika nyumba ambayo mama yangu alikuwa
akifanya kazi, aliniuliza kwa nini sikodishi gari badala yake naliegesha tu
nyumbani. Alinifundisha namna ya kusimamia biashara hiyo, kwangu alikuwa kama
dada yangu,” anasimulia. Kuanzia mwaka 1994 ndipo Babu alipojiingiza
rasmi kwenye biashara ya kukodisha magari. Magari ya kwanza niliyapata katika
Kampuni ya Intel, alikokuwa anafanya kazi Nandini Akka.
“Taratibu nilianza kuongeza magari kwenye yadi yangu. Kufikia
mwaka 2004 nilikuwa na magari sita tu, biashara ilikuwa haifanyi vizuri
kutokana na ushindani mkali uliokuwapo. “Kwa sababu kila mtu
alikuwa na magari madogo ya kawaida, nilitaka ninunue magari ya kifahari
kupunguza ushindani,” anasema. Babu anasema siku aliponunua gari lake la
kwanza la kifahari mwaka 2004, kila mtu alimwambia kuwa amefanya kosa kubwa.
Niliogopa lakini sikuwa na namna zaidi ya kuendelea na mpango wangu.
“Nilijiambiwa mwenyewe kuwa ningeuza magari kama hali ingekuwa
mbaya. Bahati nzuri kwangu biashara ililipa sana. Nilikuwa mtu wa kwanza katika
Bangalore yote kuagiza magari ya kifahari mapya,” anasema.
Babu anasema kama unataka kufanya biashara lazima uwe tayari
kukabiliana ana hatari yoyote itakayojitokeza, wakati akinunua Rolls Royce
mwaka 2011 rafiki zake walimwonya kuwa anacheza ‘kamali’ na biashara yake. “Niliwaambia nilishajitosa mwaka 2004, kwa nini nisijaribu tena
miaka kumi baadaye? Ilinigharimu fedha nyingi, lakini kama ilivyokuwa mwanzo
biashara ililipa sana” anasema.
Changamoto
Changamoto kubwa kwake ni gharama za kulipa kodi ya ushuru wa
barabara, kiasi kwamba sijui jambo hilo nilifanyaje. Babu asema mwanzoni wakati anaanza kufanya biashara ya magari
alikuwa akilipa kodi kila baada ya miezi minne, lakini sasa atalazimika
kubadili utaratibu huo kwa kuwa kodi zimekuwa kubwa mno kiasi kwamba zinaweza
‘kumvurugia’ mpango wake wa kununua magari ya Limousines na mengine ya kifahari
mwaka 2015. Babu anawaambia watu wanaotaka kuwa kama yeye:
“Fanya kazi kwa bidii, kuwa mcheshi, mambo mengine yanayobaki ni bahati tu.”
Kuhusu ndoa yake
Babu ameoa na ana watoto watatu, wote wakiwa ni wanafunzi.
Watoto wawili wa kwanza ni wasichana, mtoto wa mwisho ni mvulana. “Nitawafundisha watoto wangu kufanya kazi zangu zote mbili
(kunyoa na kukodisha magari),” anasema Babu. Babu anasifika kwa
kutokuwa mwanachama wa klabu yoyote kwa kile anachosema kuwa hana nafasi ya
kujihusisha na mambo hayo.
Kinyozi huyo hupenda kuitumia Jumapili yote katika saluni yake,
jambo linalomaanisha kuwa hana kitu anachokiita ‘mapumziko’.
Amewahi kusafiri kwenda Ujerumani kama mtalii na Singapore kwa
ajili ya kwenda kujifunza kunyoa nywele za wanawake.
Nini cha kujifunza hapa.
1. Thamini kile unachokifanya, acha kukidharau kina uwezo wa kukupa mafanikio makubwa sana unayotaka.
2. Fanya kazi kwa bidii sana utafanikiwa.
3. Jifunze kutokana na kazi unayoifanya kisha, ongeza ufanisi
Nakutakia kila la kheri katika safari yako ya mafanikio, endelea kutembelea DIRA YA MAFANIKIO kila siku.
Nini cha kujifunza hapa.
1. Thamini kile unachokifanya, acha kukidharau kina uwezo wa kukupa mafanikio makubwa sana unayotaka.
2. Fanya kazi kwa bidii sana utafanikiwa.
3. Jifunze kutokana na kazi unayoifanya kisha, ongeza ufanisi
Nakutakia kila la kheri katika safari yako ya mafanikio, endelea kutembelea DIRA YA MAFANIKIO kila siku.
Makala hii imeandikwa na Goodluck Eliona wa Gazeti la
Mwananchi.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.