May 23, 2015
Hivi Ndivyo Tunavyowaalika Watu Wabaya Katika Maisha Yetu.
Nikupe
siri moja? Kwamba, wataalamu hivi sasa wamegundua kwamba, asilimia 95 ya muda
wote, ambapo sisi binadamu hutendewa ubaya na wengine, ni sisi ambao tunakuwa
tumewaalika watu hao kututendea hivyo bila kujua.
Kila
kitu tunachofanya, hasa vile vitendo ambavyo havihusishi kuzungumza, ni mwaliko
kwa watu wanaotuzunguka . Kutabasamu kwa mfano ni mwaliko. Hii ni kama ilivyo kuweka
ndita, kuonesha huzuni usoni, kuonesha hasira usoni au kuwa na uso wenye
kuonesha dhati ya mambo muda wote. Hii yote ni mialiko pia.
Mtu
anasimama vipi, anatembea na kukaa vipi, na yenyewe pia ni mialiko tosha,
tofauti na tunavyofahamu sisi. Hebu siku moja ukiwa kwenye mkusanyiko wa watu,
jaribu kuwatazama watu hao mmoja mmoja na kujiuliza, kila mmoja kati yao
anawaalika watu wengine kumtendea vipi. Halafu jiulize, watu hao wanatendewa
kwa namna wanavyowaalika watu kuwatendea?Jibu kwa asililmia 95 litakuwa,
‘ndiyo’ kubwa kabisa.
Ukitaka
kumwalika mtu akutendee ubaya, fanya kwa njia yenye kuvuta ubaya huo. Kukunja
ndita kunafanya watu wengine kuogopa kuwa karibu nawe, hata kama huna nia mbaya
nao. Kutabasamu huwakaribisha watu wenye kupenda urafiki kuwa karibu nawe.
Lakini kwa kufanya kinyume na hapo, hivyo ndivyo utakavyozidi kuwaalika watu
wabaya katika maisha yako.
Kubinua
midomo kwa dharau huweza kuwaleta kwako watu ambao mtakwaruzana nao kwa sababu,
tayari wamekuhukumu hata kabla hawajakufahamu. Aliyesaidia kuwafanya wakuhukumu
ni wewe mwenyewe. Kwa hiyo, kama ni kuwaalika ni wewe mwenyewe unayefanya
hivyo. Waalike wale ambao ni wema basi, badala ya kuwaalika watakaokuumiza
kihisia.
Hebu
tazama namna watu wanaotembea wakiwa wamejiinamia na wamejipinda wanavyoishi.
Mara nyingi ukichunguza maisha yao utagundua kwamba, yana kuonewa na hofu,
kutokujiamini na mashaka. Kutembea kwao kinaaonyesha kile kinachokwenda kwenye
ma
wazo yao. Ni rahisi watu wa namna hii kuweza kuonewa tena na tena.
Kama
hutaki kuishi kwa mashaka, ni lazima uwakimbie watu wanaoweza kukufanya uingie
kwenye maisha ya mashaka. Huwezi kukimbia kama wewe mwenyewe unaishi kimashaka.
Kama unataka maisha yasiyo na ushirikina ndani, ni lazima uwakimbie watu
wanaohusudu ushirikina. Kwa kukimbia, ni wewe kutokuwa sehemu ya ushirikina
wowote.
Kwa
kuwa sasa unajua kwamba, mara nyingi kama siyo zote, sisi wenyewe ndiyo ambao
tunaowaalika watu na kutufanyia ubaya au wema, ni uchaguzi wetu. Tunatakiwa
kujiweka kwenye mazingira ambayo yatawavuta watu wema kwetu, kama tunataka
amani. Kama tunataka shari, tunaweza kujiweka kwenye njia ambayo tutawavuta
wakorofi kuwa karibu nasi zaidi.
Tunakutakia
kila la kheri katika safari yako ya mafanikio, endelea kutembelea DIRA YA MAFANIKIO kwa elimu na maarifa bora yatakayoboresha maisha yako.
DAIMA
TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE.
IMANI NGWANGWALU,
0713 048035,
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.