May 19, 2015
Hizi Ndizo Mbinu Muhimu Za Kimafanikio, Ambazo Ukizitumia Ni Lazima Uwe TAJIRI.
Habari za leo mpenzi msomaji wa mtandao huu wa DIRA YA MAFANIKIO. Tunaamini unaendelea vyema na majukumu ya kuboresha maisha yako. Pia tunapenda kuchukua nafasi hii kukushukuru wewe kwa kuendelea kuwa msomaji mzuri wa mtandao huu. Karibu sana na usichoke kujifunza kila siku hapa ilikuweza kuboresha maisha yako.
Ieleweke kuwa kwa kadri
unavyozidi kujifunza zaidi ndivyo unavyozidi kuwa bora hata kwa yale
unayoyafanya katika maisha yako. Hivyo unakuja kuona kuwa silaha pekee ambayo
hutakiwi kuiacha katika safari yako ya mafanikio ni kujifunza kila mara na kila
siku. Unapokuwa unajifunza unakuwa unapata mbinu mbalimbali ambazo
zitakuwezesha kufanikiwa.
Kwa kuzijua mbinu hizo
itakusaidia wewe kukurahisishia kufika kwa urahisi katika safari yako ya mafanikio.
Watu wengi wenye mafanikio wanajua mbinu muhimu za kimafanikio zilizowasaidia
kuwafanya kuwa matajiri, lakini mara baada ya kujifunza sana. Katika makala hii
ya leo tutajifunza juu ya mbinu muhimu za kimafanikio, ambazo ukizitumia ni
lazima ufanikiwe.
Mbinu hizi zimeweza kuleta
matokeo ama mabadiliko makubwa sana kwa wale wote ambao wamezitumia. Kama
utazitumia hata wewe katika safari yako ya mafanikio, utafanikiwa. Lakini
tambua kuwa kwa kuzielewa mbinu hizo tu, haitoshi wewe kuwa tajiri tu kwa ghafla.
Muda unahitajika ili uweze kufikia malengo yako. Je, unajua mbinu hizo ni zipi?
Hizi
Ndizo Mbinu Muhimu Za Kimafanikio, Ambazo Ukizitumia Ni Lazima Uwe TAJIRI.
1. Jitoe
mhanga juu ya maisha yako.
Hakuna ubishi juu hili, kama
kweli nia yako nikutaka mafanikio ni lazima kujitoa kikamilifu. Hautaweza
kufanikiwa kama utayachukulia maisha yako kama mchezo fulani. Kitu pakee
unachotakiwa kufanya ni kujitoa mhanga juu ya maisha yako na kukubali kulipia
kila gharama inayohitajika ili kuweza kufikia mafanikio unayoyataka.
Ni lazima ujifunze kufanya mafanikio
kuwa ni kitu cha lazima. Ukiwa na wazo hili uwe na uhakika ni lazima ufanikiwe
kwa vyovyote vile. Watu wengi wenye mafanikio ni watu wa kujitoa na kupigania
ndoto za maisha yao kila siku. Hicho ndicho kitu unachotakiwa hata wewe kukifanya ili
kutimiza malengo yako kwa uhakika. Kwa kujitoa mhanga katika maisha yako ni
mbinu muhimu kwako itakayokufanikisha ikiwa utaitumia.
2.
Jilipe kwanza wewe.
Hili ni jambo ambalo
tumekuwa tukikwambia mara kwa mara sana, juu ya umuhimu wa kujilipa wewe
kwanza. Kiasi chochote cha pesa unachokipata ni lazima utenge asilimia kumi
ambayo utajilipa wewe ukiwa kama mtafutaji wake. Haiwezekani ukamlipa kila mtu
ama ukalipia huduma muhimu kama bili ya maji, umeme, kodi na zinginezo halafu
ukajisahau wewe ambaye ni mzalishaji wake.
Kujilipa wewe kwanza, ni
mbimu muhimu sana kwako wewe ambayo ukiitumia ni lazima ikufikishe kwenye
utajiri. Unachohitaji kufanya wewe sasa kama huna tabia hii ni kuweza kuelekeza
nguvu zako kwenye kujilipa wewe kwa kila shilingi unayoipata. Kumbuka itakuwa
ni ngumu sana kwako kuweza kuwa tajiri ikiwa utakuwa unamlipa kila mtu na
kujisahau wewe. Ukijilipa kwanza, hiyo pesa itakusaidia kwenye kuwekeza zaidi,
pale itakapokuwa nyingi.
3.
Jitengenezee miradi mingi.
Haitawezekana na haitakuja kutokea
hata siku moja eti ukawa tajiri kwa sababu ya kutegemea kazi yako hiyo tu moja
unayoifanya, hiyo itakuwa ni ngumu sana kwako. Kama nia yako ni kutaka kuufikia
utajiri hakikisha unajitengenezea miradi ya kutosha, ambayo itakuwa inaingiza
pesa nyingi zitakazoweza kukusaidia kukamilisha lengo lako hilo.
Na kama ikitokea wewe
unataka kuanzisha biashara ya aina moja basi, hakikisha biashara yako hiyo
unaitengenezea matawi ambapo hapo itakuwa inakuwa zaidi. Hii ndiyo siri
mojawapo kubwa ambayo matajiri wengi wanaitumia kufikia utajiri wao. Kama
unafikiri natania angalia ama jaribu kufatilia na kuchunguza kidogo tu,
utagundua ama kuona wingi wa miradi waliyonayo.
4.
Andaa bajeti ya kukuongoza.
Hili ni jukumu muhimu sana
kwako ambalo unatakiwa kulianzisha ili kufikia kule unakotaka kufika katika
safari yako ya mafanikio. Ni lazima kama hutaki kupotea katika safari yako,
jitengenezee bajeti itakayo kuwa ikikuongoza katika matumizi ya pesa zako. Acha
kutumia tu pesa zako eti kwa sababu zipo mfukoni.
Weka utaratibu kila kitu
unachokinunua unakiandika katika kijitabu chako cha bajeti ambacho utakuwa
nacho. Kwa kufanya hivyo utajikuta hutaweza kupoteza pesa nyingi hovyo. Kwani
pesa hizo zinakuwa zinautaratibu maalum unaoeleweka. Kabla hujanunua kitu unaweza
ukajiuliza ni kweli kina umuhimu na nisiponunua itakuwaje. Ukiwa na kijitabu
kidogo ambacho kinaweka bajeti yako wazi ni lazima ufikie mafanikie makubwa.
5.
Kuwa na pesa ya dharura.
Ni ukweli uliowazi mara
nyingi katika jamii zetu tunazoishi matatizo ni kitu ambacho hakikwepeki kwa
namna yoyote ile. Ili kuweza kukabiliana na hali hiyo ni vizuri ukawa na ‘account’ maalum kwa ajili ya dharura tu.
Pesa hii itakusaidia wewe pindi tu unapopata matatizo ndipo utakapoitumia na si
vinginevyo.
Kama itatokea huna pesa hii,
kila utakapokuwa unapata tatizo kidogo kitu kitakachokuwa kikitokea ni lazima
utakuwa unakwenda moja kwa moja kwenye kuharibu mtaji wako kwa maana huna pesa
kwako ya dharura. Kwa kuishi maisha ya kuwa na pesa ya dharura ama ‘account’ ya dharura hiyo itakusaidia
sana katika safari yako ya kuelekea kwenye utajiri.
6.
Kuwa na tabia ya kutoa.
Hii pia ni mbinu muhimu ya
kimafanikio, ambayo matajiri wengi wanaitumia kufikia malengo yao. Unapopata
kiasi fulani cha pesa ni muhimu pia ukajijengea tabia ya kutoa kwa lengo la
kusaidia. Hii inakuwa ni kama sadaka ama shukrani kwako na kwa ulimwengu ambao
umekusaidia kukupa kile ulichonacho.
Mbinu hii, ina matokeo
makubwa sana chanya hasa pale inapotumika. Hata hivyo pia ni kanuni ya kiroho.
Unashauriwa pia kutoa asilimia kumi ya mapato yako kwa jamii, hii ni kama shukrani
kama nilivyosema. Hautakiwi pesa zako kutumia wewe tu, bila kuwa na msaada kwa
jamii hiyo itakuwa ni sawa na uchoyo.
Kwa kuhitimisha makala hii,
hizo ndizo mbinu muhimu za kimafanikio ambaza unaweza ukazitumia na kukupa
mafanikio makubwa na hatimaye kuufikia utajiri unaoutafuta katika maisha yako.
Tunakutakia kila la kheri
katika safari yako ya mafanikio, endelea kutembelea DIRA YA MAFANIKIO kwa
kujifunza na kuboresha maisha.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA
MAISHA YAKO YAIMARIKE,
IMANI
NGWANGWALU,
0713
048035,
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.