May 15, 2015
Hii Ndiyo Nguvu Hatari Inayoaminiwa Na Wengi Katika Mafanikio.
Vitendo vinavyohusisha masuala ya uchawi vimeenea sana ndani ya jamii yetu, na vimekuwa ndivyo gumzo kubwa sana miongoni mwa watu katika jamii. Na siyo hapa kwetu tu, bali hata katika nchi kubwa zilizoendelea nako ni hali kama ya hapa kwetu.
Kuna baadhi ya watu ambao wanaona na kuhisi
kwamba, uchawi ni ushirikina na mazingaombwe ambayo watu hawapaswi kuyatilia
maanani. Kwa maoni ya watu hawa, uchawi ni mambo ya kidhahania tu. Hata hivyo,
kwa walio wengi, uchawi ni jambo zito sana.
Kulingana na watafiti wa
masuala ya uchawi , wao wanasema kwamba, zaidi ya nusu ya watu ulimwenguni kwa
namna moja ama nyingine wanaamini kwamba, uchawi ni kitu au nguvu halisi ambayo
inaweza kuathiri au kudhuru maisha ya binadamu.
Mamilioni ya watu duniani
wanaamini kuwa uchawi ni mbaya, hatari na unapaswa kuogopwa sana. Kwa mfano,
sehemu kubwa ya nchi za Afrika, imani katika mizungu, ulozi na nguvu nyingine
za aina hiyo imekolea sana katika maisha ya kila siku ya wakazi wa bara hili na
hata kusababisha wachawi na walozi kuwa ni watu wanaochukiwa na kuogopwa sana
katika jamii mbalimbali za kiafrika.
Lakini, labda suala la
msingi tunalopaswa kujiuliza ni kwamba, kwa nini idadi ya watu wanaoshiriki na
kukumbatia vitendo mbalimbali vya kichawi na kishirikina inazidi kuongezeka kwa
kasi kubwa kila kuchapo? Na watu hao wako tayari kulipa kiasi chochote cha
fedha ili waweze kuhudumiwa na wachawi hao.
Mara nyingi kwa hapa kwetu
sio ajabu kusikia mtu akisema kuwa, yuko tayari hata kuuza nyumba yake ya
thamani pamoja na mali nyingine, ili apate fedha za kutosha kwenda kwa waganga
kuulizia habari au kupiga ramli kwa lengo la kutaka kufahamu chanzo cha kifo au
vifo vya watu wao wa karibu.
Watu wengi hivi sasa katika
jamii yetu, kila wanapokwama kidogo katika masuala mbalimbali ya kimaisha, basi
haraka huona ni bora kukimbilia kwa mafundi ili wakatafutiwe ufumbuzi wa shida
zao.
Dhana hii ya uchawi na
ushirikina kwa ujumla inajaribu kumuonesha na kumwelezea binadamu kuwa, ni
kiumbe asiyejiamini na wakati wote huamini kwamba, kuna nguvu nyingine iliyo
nje yenye uwezo mkubwa kuliko wake. Wakati wote hudhani kwamba, ni kupitia
nguvu hiyo pekee iliyo nje yake, ndipo anapoweza kusuluhisha na kutatua
migogoro yake ya kimaisha inayomkabili.
Kwa wakazi wengi wa Afrika
na Asia, suala la uchawi au ushirikina kwa ujumla, kwao ni jambo la kawaida
sawasawa na kufanya biashara ya njugu sokoni. Kwa hiyo kwa maneno mengine, hii
ndiyo nguvu inayoaminiwa na wengi kuwapa mafanikio katika maisha yao.
Hata hivyo, baadhi ya sababu
kuu zinazowafanya watu wavutiwe zaidi na uchawi au ushirikina ni kama
ifuatavyo: wengi wao wanaona kuwa, uchawi unauwezo mkubwa wa kuwaondolea
umaskini na mateso yanayoambatana nao.
Pia wapo wanaoutumia katika
suala zima la kufanikisha mapenzi, ikiwa ni pamoja na kuwavuta na kuwadhibiti
wapenzi wao.
Wengine huamini uchawi
unaweza matatizo ya kindoa, kizazi, kibiashara na kujiongezea bahati au
kurekebisha nyota zao kwa kuondoa nuksi na mikosi. Kuna wengine ambao hutumia
uchawi na ushirikina ili kupata kazi wanayoitamani, kupandishwa cheo makazini,
kukuza na kufanikisha biashara zao, bila kusahau kutafuta utajiri. Na bado
wengine huvutiwa na uchawi na ushirikina kwa sababu ya udadisi tu.
Jamii yetu hata hivyo, ina
mifano mingi hai inayohusu suala zima la kukithiri kwa vitendo vya uchawi na
ushirikina miongoni mwa watu. Hapa nitajaribu kueleza kwa uchache tu. Kwa mfano
imani ya kudhaniwa mtu amekufa wakati yuko mahali amefichwa na mchawi, kuchukua
mazao shambani kwa mwingine, kuua biashara ya mtu ama kumfanya mtu aondoke kwao
na kutokurudi tena.
Hii ni baadhi tu kati ya
mifano mingi ya nguvu ya kichawi kama zinavyoaminika katika jamii. Zamani,
mambo ya kuamini uchawi yalikuwa yakifanyika kwa siri kubwa sana, lakini kwa
sasa yako wazi. Siku hizi hata majirani wakigombana kidogo tu kuhusu mipaka ya
maeneo yao hawaishii kutishiana kuwa
watalogana. Mwingine anaweza kusema kwamba, ‘ukileta mchezo nitakuendea kwetu
kukushughulikia tuone kama baada ya mwezi mmoja hutaanza kuokota makopo’ na
mambo mengine mengi.
Na mwisho ili mtu aweze
kuondokana na kujiepusha na hofu ya uchawi na ushirikina, anapaswa kutupa na
kuharibukila kitu kinachohusiana na uchawi, hii ni kama amejiingiza kwenye
vitendo vya kichawi.
Pia, anapaswa kujenga imani
thabiti kuelekea yale anayotaka kuyatimiza katika maisha yake. Imani hii isiyoyumba,
itamsaidia sana kudhibiti uchawi kutoka kwa wengine au kujizuia asijiingize
kwenye vitendo vya kishirikina.
Vilevile ni mtu kuamini
kwamba, kuna nguvu nyingi, lakini ili nguvu ikuumize ni lazima uikaribie kwa
kauli na vitendo vyako. Kama ukitenda na kutoa kauli muafaka, ni vigumu uchawi
kukudhuru, kinyume cha hapo ni lazima kuwe na maumivu.
Tunakutakutakia kila la
kheri katika safari ya mafanikio yako, endelea kutembelea DIRA YA MAFANIKIO
kujifunza kila siku.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA
MAISHA YAKO YAIMARIKE,
IMANI
NGWANGWALU,
0713
048035,
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.