Sep 4, 2015
Jifunze Jinsi Ambavyo Unaweza Kuwa Mhamasishaji Mkubwa.
Zipo
ndoto nyingi sana ambazo sisi binadamu tunakuwa nazo katika maisha ya kila
siku. Wapo ambao wanapenda kuwa madaktari, marubani, walimu na hata wapo
wanaopenda kuwa wahamasishaji wa kimataifa ingawa ni wachache lakini wapo.
Unapoamua
kuwa mhamasishaji maana yake katika maisha yako umeamua kuwatia moyo wengine
kupitia maandishi yako au kile unachotaka kukizungumza moja kwa moja katika
jamii yako. Unakuwa hauna tofauti sana na wahubiri wa injili tofauti yake wewe
unakuwa unahubri injili ya mafanikio.
Tunaona
katika Dunia ya leo wapo wahamasishaji wakubwa kama vile akina Brian Triacy,
Donald Trump, Robert Kiyosaki, Dale Carnegie, Bo Sanchez na wengineo wengi
ambao wameamua kuisadia Dunia kwa sehemu kubwa kutokana na kile wanachosema
kupitia maandishi yao au vinywa vyao.
Wapo
watu wengi sana ambao hawakuwa na matumaini na mafanikio, lakini wamepata mafanikio
na kufanikiwa kusonga mbele kimaisha baada ya kuwasikiliza au kuwasoma watu hao.
Tena wakati mwingine wanafanikiwa hata watu hao ambao ni wahamasishaji wanakuwa
hawana habari.
Inawezekana
na wewe ukawa moja kati ya watu wenye ndoto kama hizi kubwa katika maisha yako
na kuwa mhamasishaji mkubwa wa mambo mbalimbali katika jamii zetu ikiwa pamoja na
mafanikio.
Ni
jambo nzuri kwa sababu unakuwa unatoa mchango moja kwa moja kwa jamii kupitia
ujuzi ulionao, hiyo inakuwa ni sawa na kutoa sadaka ambayo baadae itakurudia
kwa namna tofauti. Na ukumbuke pia unapowasamasisha wengine, inakuwa unajipa
nguvu ya wewe ya kuweza kufanikiwa zaidi.
Lakini
kama ilivyo kwa mambo mengine huwezi kuwa mhamasishaji mkubwa mpaka ujifunze
kujenga misingi imara na thabiti kunzia leo. Hicho si kitu cha kukurupuka kama
utafanya hivyo ni wazi utadondoka ikiwa hutajiandaa kusimama vizuri.
Kujiandaa
huku inaweza ikawa ni kujisomea vitabu ama kuangali yale wanayofanya. Ukumbuke
kuwa utakuwa unaongea au kuwaandikia watu wengi pengine zaidi ya elfu mbili hivi, kwa hiyo maandalizi yanahitajika tena
kwa lazima.
Ni
mambo gani ambayo unatakiwa kuyazingatia kwa sasa ili uweze kuwa mhamasishaji
mkubwa na bora zaidi?
1. Anzia pale ulipo.
Anza
kuzungumza na watu ulionao katika mazingira uliyopo. Kama kuna kitu ambacho
unapenda kuwapa cha kuwahamasisha na kikawafanya wabadili maisha yao wape kitu
hicho bila ya kuogopa wala kusita. Kama umeamua kuandika andika kwa ajili yao
au kama umeamua kuzungumza zungumza pia kwa ajili yao mpaka maisha yao
yabadilike. Hivi ndivyo unavyoweza kuanza kwa hatua za mwanzoni kuwa mhamasishji
mkubwa na mwenye mafanikio.
2. Chukua somo ambalo watu wanapenda
kulisikia.
Ni
vyema katika mada zako ambazo unataka kuzitoa, hakikisha unalenga somo ambalo
watu wanapenda kulisikia. Kama ni mafanikio, hakikisha unatoa mada ambayo
inagusa jamii yako na kutatua matatizo makubwa na kuwaweka watu hao huru. Kwa
kufanya hivyo utawavuta wengi ambao watatamani tena kusikia kwako mambo mengi
ya mafanikio. Na hivyo ndivyo ambavyo utakuwa unajenga misuri taratibu ya kuwa
mhamasishaji mkubwa.
3. Jifunze kutoa mada kwa wengine
bila gharama.
Kama
umeamua kutoa mada kwa njia ya semina mwanzoni fanya semina hizo bila gharama
yoyote ile au weka gharama za kawaida zisiwe kubwa sana. Hii itakusaidia kukupa
uzoefu na itakujengea nguvu kubwa ya kujiamini hali itakayosababisha au
kukupelekea wewe kuwa mhamasishaji mkubwa.
Kwa
kufanyia kazi mambo hayo matatu yanauwezo mkubwa kabisa wa kukufanya ukawa
mhamasishji mkubwa na mwenye mafanikio makubwa na ambaye unaingiza kipato
kikubwa.
Nakutakia ushindi katika safari yako ya mafanikio na
endelea kutembelea DIRA YA MAFANIKIO kwa
kujifunza na kuboresha maisha yako kila siku.
Ni
wako rafiki katika mafanikio,
IMANI NGWANGWALU,
0713 048 035,
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.