Sep 15, 2015
Sababu Tano Kwanini Ni Muhimu Sana Kwako Kutimiza Malengo Uliyojiwekea.
Kati
ya kitu ambacho unatakiwa kukifatilia kwa ukaribu sana katika maisha yako na kukifanikisha ni malengo yako uliyojiwekea. Unapokuwa
umejiwekea malengo yanakuwa yanakupa dira, nguvu na mwelekeo wa kukusaidia
kusonga mbele na hatimaye kuwa na mafanikio ya hali ya juu.
Hakuna
mafanikio yanayoweza kutokea kama hujiwekei malengo. Mafanikio yote yawe
makubwa au madogo yanaanza na kujiwekea malengo. Bila kujiwekea malengo na
kuyatimiza maisha yako inakuwa ni kama kazi bure. Kitu cha kujiuliza hapa, ni kwanini ni muhimu
na lazima kwako kuweza kutimiza malengo yako?
Zifuatazo Ni Sababu Tano Kwanini Ni
Muhimu Sana Kwako Kutimiza Malengo Uliyojiwekea.
1. …Yanakupa ujasiri wa kutenda zaidi.
Kile
kitendo cha kujiwekea malengo na kufanikisha kinakuwa kinakupa ujasiri mkubwa
wa kutenda zaidi. Hebu hapo ulipo, jaribu kufikiri jambo ambalo umewahi
kulifanya na kulifanikisha. Kila unapolikumbuka linakuwa linakupa nguvu na
ishara ya kuwa hata mengine unaweza ukayafanya tena kwa mafanikio makubwa. Hii
ndiyo siri na faida kubwa ya kutimiza malengo yako.
2. …Yanakuwa kipimo cha mafanikio
yako.
Kutimiza
malengo uliyojiwekea ni kipimo tosha kabisa cha kule unakotaka kufika
kimafanikio. Kwa kuwa ulijiwekea malengo na umeyafanikisha inakuwa rahisi kwako
kugundua ni maeneo yapi ambayo unatakiwa kuyasimamia vizuri ili kujiandaa kwa
ajili ya safari nyingine mpya ya malengo. Hivyo, kufanikisha malengo ni kama
pima joto ya mafanikio yako kuonyesha wapi ulipo na unakwenda wapi sasa.
3. …Yanakuwa msaada kwa wengine.
Ni
jambo ambalo unalotakiwa ulijue ya kuwa tunaweka malengo si kwa ajili yetu tu,
bali pia na kwa wengine wanatuzunguka ili tuwe msaada kwao. Kufanikisha malengo
yako na kunufaika nayo wewe mwenyewe na kusahau jamii inayokuzunguka kwa
karibu, hiyo inakuwa sawa na kazi bure. Kwahiyo, ni lazima kutimiza malengo ili
kuwa msaada kwa wengine pale inapohitajika.
4. …Yanakupa changamoto.
Kile
kitendo cha kutimiza malengo uliyojiwekea ni lazima kuna changamoto ambazo
ulipitia. Kupitia changamoto hizo, naamini hazikukuacha bure kuna kitu
ulijifunza cha kukuboresha zaidi. Kwa hiyo kuna ukomavu au uzoefu ambao unakuwa
umepitia hapo, lakini ambao ukiuangalia umetokana na malengo yako uliyojiwekea
ingawa umeyafanikisha.
5. …Yanakupa furaha.
Hakuna
mtu ambaye anatimiza malengo yako, halafu ndani yake akakosa furaha. Ile hatua
ya kuwa na malengo yako, halafu ukayatimiza ni furaha kubwa sana. Kwa hiyo
utaona kuwa kwa kadri unavyoendelea kutimiza lengo hili na lile katika maisha
yako unakuwa unajijengea furaha kubwa na ya kudumu maishani mwako inaendana na
ujasiri mkubwa.
Kufanikisha
malengo yako uliyojiwekea ni jambo linalokupa manufaa mengi kwako siku hadi
siku ikiwa ni pamoja na kukujengea uzoefu ambao utakuwa unatembea nao siku zote
za maisha yako.
Kwa
leo naomba tuishie hapa rafiki, tukutane tena katika siku nyingine kwa ajili ya
kujifunza na kuboresha maisha yetu kwa pamoja.
Nakutakia kila la kheri katika harakati za kuboresha maisha yako
na endelea kutembelea DIRA YA MAFANIKIO kujifunza na kuhamasika.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Ni wako rafiki katika mafanikio,
Imani
Ngwangwalu,
Kama una maoni, ushauri au changamoto yoyote inayokuzuia kufikia
mafanikio yako wasiliana nami kwa email dirayamafanikio@gmail.com au simu 0713 048035 kwa ushauri na msaada wa haraka.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.