Aug 23, 2018
Mambo Ambayo Umekuwa Ukidanganywa Sana Kuhusu Pesa Na Uwekezaji.
Kati
ya kitu ambacho kinatafutwa sana na wengi hapa duniani ni pesa. Pesa imekuwa
ikitafutwa usiku na mchana karibu na watu wote. Hali hii imekuwa iko hivyo kwa
sababu ya umuhimu wa pesa katika kutusaidia kufikia malengo yetu.
Lakini
pamoja na pesa kutafutwa hivyo, bado watu wengi wamekuwa wana hadithi nyingi za
uongo kuhusiana na pesa hata swala la uwekezaji kwa ujumla. Kila inapotajwa pesa au uwekezaji wakati
mwingine kumekuwa na uongo mwingi sana wa kupotosha.
Ni
lengo la makala haya kukuwezesha kutambua mambo ambayo umekuwa ukidanganywa juu
ya pesa na uwekezaji. Mambo hayo ni yepi? Fuatana nami katika makala haya
mwanzo hadi mwisho tuweze kujifunza kwa pamoja:-
1.
“Unahitaji pesa nyingi ili kuwekeza”.
Wengi
wetu bado tunaendelea na fikra mgando za kuamini kwamba ili uweze kuwekeza ni
lazima uwe na pesa nyingi. Kutokana na uongo huo, tumekuwa tukisubiri tupate
mitaji na pesa nyingi ili tuweze kuwekeza.
Kwa
taarifa yako huo ni uongo ambao umekuwa ukidanganywa. Kwa dunia ya sasa jinsi
ilivyo, kitu kikubwa unachohitaji ni wazo na taarifa sahihi za mafanikio ili
kuwekeza. Kama ni mtaji unahitajika sio lazima uwe mkubwa sana kama
unavyofikiri.
Kwa
hiyo kama umesimama na huwekezi kwa kisingizio cha kukosa mtaji,
unajichelewesha mwenyewe. Zinduka kwenye huo usingizi na anza kutumia kidogo
ulichonacho kufanya uwekezaji unao faa kwako. Naamini kipo kitu ulichonacho
hata kidogo cha kukusaidia, hauwezi kukosa vyote.
2.
“Uwekezaji ni hatari”
Jambo
la pili ambalo wengi wamekuwa wakidanganywa sana kuhusu pesa na uwekezaji kwa
ujumla ni kwamba, uwekezaji ni ‘risk’
kubwa sana. Nafikiri umeshawahi kusikia hadithi za namna hii sana kuwa
uwekezaji ni hatari.
Kutokana
na wengi kupokea hadithi za namna hii na kuzikubali kupelekea kutokufanya
uwekaji wowote ule. Unajua ni kwa nini? Kwa sababu wameshaambiwa uwekezaji ni
hatari na ni ‘ risk’ kubwa sana.
Huu
ni uongo ambao umekuwa ukidanganywa kwa muda mrefu. Na kwa bahati mbaya umekuwa
ukijisahau pia kwamba uwekezaji sio hatari kubwa sana kama unavyofikiri, ila
unachangamoto zake na ni njia mojawapo nzuri ya kukufikisha kwenye uhuru wa
kipesa.
3.
“Mshahara ndio kila kitu”
Acha
kuendelea kuugua na kuamini hadithi za kwamba wale wanaolipwa mshahara ndio
kila kitu. Kama hicho ndio kilio chako na unaamini tosha kabisa kwamba eti kwa
sababu wewe hukusoma na hulipwi mshahara basi maisha yako yameharibika.
Sikiliza
nikwambie rafiki, maisha ni mipango. Jiwekee taratibu zako za kutengeneza
kipato na jiamini zaidi, utafanikiwa. Kama unafanya kazi acha kuwadanganya
wengine kwamba ukiwa na mashahara ndio uhakika wa mafanikio.
Mafanikio
ya kweli hayaji kwa sababu ya mshahara unaolipwa. Mafanikio makubwa na ya
uhakika yanakuja kutokana na mipango yako imara uliyojiwekea na kuifata kila
siku.
Ukiangalia
na kufuatilia hizo ndizo hadithi ambazo una danganywa sana kuhusu pesa na
uwekezaji. Mengi yamekuwa yakisemwa sana kuhusu pesa na wekezaji kitu ambacho
sio kweli.
Endelea
kujifunza kupitia dirayamafanikio.blogspot.com kila siku.
Napenda
pia kuchukua fursa hii kukukaribisha kwenye kundi la Whats App ili tuweze kujifunza pamoja na kwa ukaribu zaidi. Kujiunga
tuma neno MAFANIKIO YANGU, kisha
ikifutia na namba yako kwenda 0713 04 80
35 ili uanganishwe.
TUNAKUTAKIA
KILA LA KHERI KATIKA SAFARI YA MAFANIKIO.
Ni
wako rafiki,
IMANI NGWANGWALU,
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.