Aug 17, 2018
Mambo Makuu Mawili (2) Yanayokufanya Uendelee Kuwa Maskini.
Habari za muda huu mpenzi msomaji wa blog ya DIRA YA MAFANIKIO bila shaka u mzima wa afya na unaendelea vyema na majukumu yako ya kila siku. Naomba nichukue walau dakika zako kadhaa kuweza kukuja mambo makuu mawili ambayo yatakufanya uendelee kuwa maskini endapo utaendea kuyang’ang’ania. Na mambo hayo ni;
1. Kutenda bila
kufikiri.
Wapo baadhi ya watu wanashindwa kufikia katika kilele cha
mafanikio yao hii ni kwa sababu watu hao hawataki kujitoa kwa moyo wote katika
kufanya vitu ambavyo wanafanya. Hata wale wanaojitoa kwa moyo vile vile huwa
wanafanya vitu hivyo pasipo kufanya uchunguzi wa kina juu ya mambo ambayo
wanayafanya.
Watu hawa ndio wale ambao utakuta wanatumia nguvu nyingi
kuliko kuishirikisha akili, na kitendo hiki ndicho watalamu wa masuala ya
mafanikio huita msuli tembo matokeo sisimizi, yaani watu hao hujikuta vitu
mbalimbali ilimladi wameafanya.
Na ukweli ni kwamba katika kundi hili kuna watu wengi
sana ambao wamejikusanya kwa pamoja katika kundi hili na hawa ndio wale
wanaongoza kwa kusema vyuma vimekaza, nami nasema ya kwamba kama na wewe upo katika kundi hili na hutaki
kubadilika ninasema utapata tabu sana.
Nisikutishe kwa maneno ya msingi bali unacahotakiwa
kufanya katika maisha yako ili uweze kufanikiwa ni kuhakikisha kwa kila jambo
unalotaka kulifanya au ambalo unalifanya ni kuhakikisha unatenda jambo kwa
kuwekeza fikra zako katika jambo hilo. Hiiitakusadia sana kujua mchakato mzima
wa jambo hilo matokeo yake kiujulma.
2. Kufikiri bila
kutenda.
Mtafiti mmoja kutoka chuo cha kikuuu cha harvard nchini
Marekani aitwaye Sabrina Deogratius yeye aliwahi kusema ya kwamba kufikiri bila
kutenda ni mawazo ya mtu mfu, hii ikiwa ni sawa na kusema nataka kufanya jambo
fulani bila kuchua hatua stahiki ya kutenda jambo hilo haya huwa yanaitwa ni
matamanio tu.
Na katika kundi hili la watu wenye matamanio limebeba
idadi kubwa sana ya watu, na watu hao ndio wale wenye utajiri sana wa meneno
ila ndio maskini wa kutupwa, wao vinywa vyao hujaa ahadi zisizotekelezeka. Watu
hao ndio wale wenye kuamini vitu ambavyo havipo, utakuta hata ukitaka
kuwashirikisha jambo fulani la kimaendeleo watakwambia jambo hilo haliwezekani
hii ni kwa sababu wao huishia kuwaza tu na si kufanya.
Hivyo ndugu yangu maisha yanakwenda kasi sana hivyo
yakupasa nawe uweze kuendana na kasi hiyo kwa kuhakikisha ya kwamba kila
unalolifikiri kama ni jambo lenye manufaa kwako na jamii ambayo inakuzunguka ni
vyema ukahakikisha unalifanya kwa kina.
Kwa nukta hiyo kwa leo sina jambo la ziada nikutakie siku
njema na mafanikio mema.
Ndimi Afisa Mipango:
Benson Chonya
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.