Aug 21, 2018
Huu Ndio Uongo Unaokuzuia Ushindwe Kuchukua Hatua.
Uwe unajua au hujui unatakiwa kujua kuna wakati upo uongo unaojijaza mwenyewe na kwa bahati mbaya sana uongo huo ndio unaokuzuia ushindwe kuchukua hatua za kuelekea kwenye mafanikio yako uliojipangia kuyafikia
Inawezekana
unajiuliza inawezekanaje na kivipi mtu ukajijaza mwenyewe uongo, ndio
inawezekana kabisa kwamba ukajidanganya mwenyewe na ukajipoteza kutokana na
mawazo ambayo unajisemea mwenyewe kila wakati.
Hapa
kupitia makala haya nataka nikuonyeshe uongo ambao unajiambia wewe mwenye na
kwa uongo huo unakuzui wewe kuweza kuchukua hatua za kufikia mafanikio yako. Je,
uongo huo ni upi unaojiambia?
1.”Siko
tayari kufanya jambo hili kwa sasa.”
Kuna
watu ambao wanajidanganya katika hili nakuona kile wanachotakiwa kukifanya kwa
sasa hawako tayari, nikiwa na maana watu hawa wanakuwa wanadai maandali mengine
zaidi bado yanahitajika ili waweze kuchukua hatua.
Matokeo
yake watu hawa huendelea kujiandaa wee na mwisho hushindwa kuchukua hatua
kabisa. Sasa huu ni uongo ambao wengi wanajidanganya, wakati unatakiwa kuchukua
hatua hata kama unajiona hauko tayari lakini wewe chukua hatua.
2. “Natafuta
wazo bora zaidi.”
Moja
ya kizuizi kinachowazuia watu wengi kushindwa angalau kuchukua hatua ya kwanza
tu kwa kile wanachokifanya ni kutokana na wao kuendelea kutafuta wazo bora
zaidi la kibiashara badala ya kulifanyia kazi lile walilonalo.
Utakuta
mtu ana mawazo mazuri tu ya kibiashara lakini unaona mtu huyo anaendelea
kutafuta wazo lingine bora na kuacha kutumia hata lile wazo walilonalo. Huo ni
uongo mwingine wa kuamini lipo wazo bora zaidi la kufanyia kazi.
3. “Nimeshachelewa
kwenye mradi huu.”
Kati
ya mojawapo ya wazo linalopoteza wengi ni kule kwa wengine kuamini mradi wanaoufanya
tayari wameshachelewa wakiwa na maana kwamba mradi huo tayari unafanywa na watu
wengi na jambo ambalo si sahihi.
Kuendelea
kuwa na mawazo haya ni kujidanganya tu, hakuna kitu ambacho umechelewa wewe kufanya
kwa sehemu yako na weka juhudi vya kutosha na kuhakikisha hadi unaweza
kufanikiwa vya kutosha.
Kwa kumaliza
makala haya, tambua huo ndio uongo ambao wengi wanajidanganya na unawafanya
washindwe kuchukua hatua za kufikia mafanikio yao.
Fanyia kazi haya na chukua
hatua kuhakikisha ndoto zako zinatimia.
Tunakutakia kila la kheri na
endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku kujifunza maisha na
mafanikio.
Pia
rafiki, kama unapenda kujifunza zaidi kuhusu mafanikio, karibu kwenye kundi la WHATS APP LA MAFANIKIO, kujiunga tuma
neno THE UNIVERSITY OF WINNER’S
kwenda 0713 048 035, hapo utapata
utaratibu mzima wa kujiunga.
Kama
wewe ni mfugaji wa kuku na unahitaji vifaranga bora, waone DM POULTRY FARM PROJECT kwa huduma ya uhakika. Hawa ni wauzaji wa
vifaranga wa kuku aina ya KUROILER,
SASSO, KIENYEJI ASILIA na KUCHI. Kwa mahitaji ya vifaranga wasiliana nao
kwa 0767 048 035 au 0686 141097 na
wote mnakaribishwa.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO
YAIMARIKE,
Ni
wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na
mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713
048 035,
Email; dirayamafanikio@gmail.com
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.