Aug 19, 2018
Mbinu Kumi Muhimu Za Kufanikiwa Kipesa Na Maisha Kwa Ujumla.
Maisha ni mjumuiko wa mbinu na kanuni mbalimbali ambazo ukizitumia ni rahisi kukuwezesha kufanikiwa sana. Mafanikio hayaji kwa siri moja tu, zipo siri au mbinu nyingi ambazo ukizitumia zitakupa mafanikio ya moja kwa moja.
Kwa kutumia
mbinu hizo unaweza ukafanikiwa kipesa au unaweza ukafanikiwa kwa maisha ya nje
iwe uongozi au vyovyote vile. Kupitia makala haya naomba nikwambie mbinu muhimu
ambazo ukizifanyia kazi zitakufanikisha kufanikiwa.
1. Kuwa
na maono
tu ya kile unachotaka kukifanya hiyo peke yake haitoshi unatakiwa kuongeza imani
na moyo wa kusonga mbele. Kwa maneno mengine bila maono, imani sahihi
ya mafanikio na moyo wa kuweza kusonga mbele huwezi kufika popote.
VISION + FAITH + COURAGE= SUCCESS
Yapo
maono ambayo kwako na kwa wengine yanaonekana kama ndoto yaani maono
yasiyotimia. Maono hayo ili uweze kuyafikia lazima uwe na imani na moyo wa
kusonga mbele hata kama unahofu yaani ‘courage.’
Ukiwa na vitu hivyo utafanikiwa.
2.
Kaa tayari kujiandaa na kitu chochote kinachoweza kujitokeza
kwenye maisha yako ya kiuchumi. Maisha
yanabadilika, uchumi ulionao unaweza ukawa bora sana, lakini jiulize kesho
mambo yakibadilika unafanyaje? Umejiandaa na mabadiliko hayo?
Unatakiwa
kujifunza kukaa tayari kwa nyakati na mabadiliko yoyote yale ambayo yanakuwa yanajitokeza
kwenye maisha yako. Usiyumbishwe na mabadiliko, bali jiandae na mabadiliko
yanayoweza kutokea kwako.
3.
Haijalishi utakulia katika mazingira yapi, lakini msingi mmojawapo mkubwa wa
mafanikio ambao unatakiwa kuujenga na utakusaidia sana ni ukweli/truthful na ukarimu/honest. Hii ni misingi muhimu sana ya mafanikio yako
endelevu.
Watu
wengi kwa bahati mbaya sana wanalelewa katika uongo mwingi, wanatengeneza
kipato kwa njia ya uongo, ni jambo ambalo ni hatari sana katika kujenga
mafanikio ya kudumu. Jifunze ukweli na ukarimu utakusaidia sana.
4. Kila
mtu ndani yake awe anajua au hajui lakini amebeba watu hawa, mtu
maskini, mtu tajiri, mtu mkweli, mtu mwongo, mtu shujaa na jasiri, mtu mnyonge
na dhaifu na aina nyingine ya watu. Hawa ni aina ya watu walio ndani
mwa kila mtu.
Hapa
ni uamanuzi wako wewe mwenyewe ni ubebe mtu yupi na ambaye utaamua kumtumia ili
akusaidia kufanikiwa. Mtu yeyote unaweza ukatoka naye ni swala la kuamua sifa
ama ‘character’ ipi unataka kukua
nayo kwenye maisha yako yote.
5. Kama
pesa huwezi kuziona kwenye akili yako, kama pesa huwezi kuziona kwenye kichwa
chako, basi hata mikononi mwako pesa huwezi kuziona. Pesa unalazimika kwanza kuziona
kwenye akili yako kabla hazijakufikia mikononi mwako.
Wengi
ambao wanakosa pesa si kwamba pesa hizo hawazioni mikononi mwao bali hata kwenye
akii zao hawaoni pesa hizo. Anza kuona fursa za pesa akilini mwako kwanza tuone
kama pesa utazikosa mikononi mwako tena.
6. Usisubiri
umri uende ndio uanze kutafauta hatma ya maisha yako, usisubiri miaka iende
huku ukiendelea kutafuta kazi moja na kuelekea nyingine. Hakikisha una biashara
yako iliyosimama, hakikisha una maisha yako yanayojitegemea huku ukiwa bado
kijana na mapeema, hiyo itakusaidia sana.
Hatma
ya kesho yako amua kuitegeneza leo hata kama ni kwa tabu sana,
lakini tafadhali itengeneze hatma ya kesho yako leo leo hata kama ni kwa tabu. Kesho
itafika na mambo yanaweza yakabadilika utapata shida sana kama hukuwekeza kujiandaa
mapema. Amua kuitengeneza kesho yako nzuri leo hata kama ni kwa gharama sana.
7. Kama
leo hii ikitokea huna pesa, huna kazi, huna pa kulala, huna chakula ni
kitu gani ambacho utakwenda kufanya? Utachanganyikiwa au utahaha au ni
kitu gani ambacho utafanya? Fikiria kidogo halafu ujijibu mwenyewe.
Najua
wengi watakimbilia kusema kwamba watakwenda kutafuata kazi na kufanya. Jibu lolote
utakalolitoa hiyo inayoonyesha ni jinsi ulivyokuwa ‘programudi.’ Kwa aliye ‘programudi’
tokea awali kuwa mjasiriamali atasema anaenda kufanya biashara.
8. Wazazi na walimu wanasisitiza sana mtoto asome vizuri,
apate elimu bora. Kitu ambacho wanasisitiza hapo ni ule ulinzi na hawasisitizi
uhuru. Kitu kizuri kuliko vyote hapo ni
uhuru na sio ulinzi kama wengine wanavyofikiri.
Kitu
cha kufanya ni kubadili mtazamo wako kutoka kwenye kutafuta ulinzi na kutafuta uhuru
wa kipesa. Kwa bahati mbay au nzuri kwa chochote unachokitafuta sana na
kitu hicho kitakupelekea kukosa kitu kingine, angalia ni kipi muhimu sana
kwako.
9.
Lipo kundi kubwa sana la watu ambalo linafata mipango iliyokufa, mipango hiyo
inaweza ikawa ya wazazi, ndugu au rafiki. Kwa nini nasema mipango
iliyokufa nikiwa na maana, kama unafata mipango ya mtu aliyeshindwa kifedha na
wewe utashindwa tu na hiyo inakuwa ni sawa na kufuata mpango ambao umekufa
tayari.
Kila
wakati fata mipango imara ya mtu aliyefanikiwa kifedha na wewe utafanikiwa. Ikiwa
lakini utafata mipango ya mtu aliyeshindwa kimafanikio na wewe utashindwa tu. Jiulize
sasa unafata mipango iliyokufa au unafata mipango iliyo hai? Ukifata mipango ya
mtu aliyeshindwa enelwa unafata mipango mfu, mipango iliyooza.
10. Hebu
jiulize, unawezaje kubadilisha fikra za mtu ambaye yeye tokea anakua amefundishwa kwamba
ili uwe na maisha mazuri ni lazima kwanza uwe na kazi. Kubadilisha fikra
kama hizi ni kazi kubwa na inayotaka uwe na moyo mkubwa ili fikra hizi ziweze
kubadilika, hapa ndipo tatizo la wengi lilipo kwa sababu ya hilo.
Ndio
maana hata iweje wapo watu ambao hawawezi kuwa wafanyabiashara kwa sababu, ni
watu ambao wao wanajua jinsi ya kupokea mshahara na si kitu kingine. Kwa hiyo
kama wewe unaona una damu ya ujasiriamali kazana vivyo hivyo, waache ambao
hawataki kuwa wajasiriamali utawauzia bidhaa wewe.
Fanyia
kazi haya na chukua hatua kuhakikisha ndoto zako zinatimia.
Tunakutakia kila la kheri na
endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku kujifunza maisha na
mafanikio.
Pia
rafiki, kama unapenda kujifunza zaidi kuhusu mafanikio, karibu kwenye kundi la WHATS APP LA MAFANIKIO, kujiunga tuma
neno THE UNIVERSITY OF WINNER’S
kwenda 0713 048 035, hapo utapata
utaratibu mzima wa kujiunga.
Kama
wewe ni mfugaji wa kuku na unahitaji vifaranga bora, waone DM POULTRY FARM PROJECT kwa huduma ya uhakika. Hawa ni wauzaji wa
vifaranga wa kuku aina ya KUROILER,
SASSO, KIENYEJI ASILIA na KUCHI. Kwa mahitaji ya vifaranga wasiliana nao
kwa 0767 048 035 au 0686 141097 na
wote mnakaribishwa.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO
YAIMARIKE,
Ni
wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na
mjasiriamali,
Blog; dirayamafanikio.blogspot.com,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713
048 035,
Email; dirayamafanikio@gmail.com
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.