Aug 27, 2018
Huu Ndio Ukweli Unaouma Utakaofanya Maisha Yako Yawe Bora.
Ni jambo la kawaida kwa watu wengi kuwa na ndoto na malengo, lakini ipo tofauti kubwa sana kati ya watu ambao wanafanikisha malengo yao na wengine wanashindwa kufanikisha malengo yaani hawa wanakuwa wanaota tu pasipo kufikia malengo.
Kwa nini
hali hii inakuwa inatokea wengine wanakuwa na uwezo wa kufanikisha malengo yao
na wengine wanakwama kufanikisha? Hapa ndipo unatakiwa ujue ukweli mgumu,
ukweli unaouma ambao utafanya maisha yako yawe bora.
Je,
nikuulize hapo ulipo upo tayari kuupokea ukweli mchungu ambao utabadilisha
maisha yako? Kama uko tayari nyosha mkono, nikupe ukweli huu, ila mara baada ya
kupokea ukweli huo, utakusaidia sana kukubadilisha maisha yako kwa ujumla.
1. Hatua ya kwanza ni ngumu
kutekelezeka.
Inaeleweka
siku zote ili kufanikisha jambo lazima kuchukua hatua. Hata hivyo kwa bahati mbaya
sana siku zote hatua ya kwanza mara nyingi inakuwa ni ngumu sana kuweza
kutekelezeka. Kama usipoweka juhudi na kujituma sana huwezi kuchukua hata hatua
ile ya kwanza. Kuna watu wanakuwa wanakwama hata kabla hawajachukua hatua ya
kwanza. Fanya ufanyalo, tumia nguvu zote na kuhakikisha unaanza.
2. Wewe ndie sababu ya kujirudisha nyuma
sana.
Hakuna
mtu mwenye mchango mkubwa sana wa kukurudisha nyuma zaidi yako. Unajirudisha nyuma
kutokana na hofu ambazo unazo, unajirudisha nyuma kwa sababu ya kushindwa
kuchukua hatua mapema na pia unajirudisha nyuma kwa sababu ya visingizio. Unatakiwa
uyaepuke haya yote ili ufanikiwe.
3. Mambo makubwa yanataka muda na juhudi
ili kuyafanikisha.
Hakuna
jambo kubwa ambalo unaweza ukalifanikisha kwa haraka na upesi kama unavyotaka. Siku
zote mambo makubwa yanataka muda na juhudi kubwa sana ili yaweze kutimia. Kama una
haraka zako na hutaki kuweka muda katika kutimiza makubwa, utaishia kupata vitu
vidogo sana maishani mwako.
4. Sio kila mtu yupo tayari kukusaidia.
Pamoja
na kwamba unaweza ukaona unazungukwa na watu wengi wema, lakini nikwambie tu
unapopata changamoto si kila mtu yupo tayari kukusaidia kufanikiwa na kufika
juu. Wapo wengine watakudidimiza chini na hutaamini, ili usitape tabu weka
akilini hii, si kila mtu yupo tayari kukusaidia kama unavyofikiri wewe iko
hivyo.
5. Huwezi kufanikiwa bila kujitoa mhanga.
kama
unafikiri utafanikiwa tu kirahisi pasipo kuhatarisha baadhi ya mambo basi
utakuwa ni mtu ambaye unajidanganya sana. Lazima ifike muda au wakati uhatarisha
baadhi ya vitu kwa ajili ya mafanikio yako. Hatari haziwezi kutoka kabisa ila
kama unafikiri mafanikio ya namna hiyo yapo huwezi kuyapata katu maishani.
6. Huwezi kutawala kila kitu.
Ukweli
huu unakuja hasa pale unapotaka kutawala tabia na matendo ya watu. Huwezi hata
siku moja kutawala tabia na matendo ya watu. Vipo vitu unavyoweza kutawala
lakini si kutawala tabia zao na ukazimiliki kwa jinsi wewe unavyotaka iwe. Tawala
yale unayoyaweza lakini si kutawala kila kitu utashindwa na hautaweza kufanya
hivyo.
7. Huwezi kufanya kila kitu mwenyewe.
Kama
ambavyo huwezi kutawala kila kitu wewe, basi huwezi kufanya kila kitu mwenyewe.
Yapo majukumu inabidi uwaachie watu wakusaidaie, vinginevyo ukiwa wewe kama
wewe yatakushinda. Wale wanaong’ang’ania kufanya mambo yao peke yao wanashindwa
kutoka au kuweza kufanikiwa kabisa kwa sababu ni ngumu hiyo.
8. Kukosea ni lazima.
Huwezi
ukafanya jambo lolote pasipo kufanya makosa. kukosea ni lazima kutokee kila
wakati unapoelekea ndoto zako. Na kunapotokea kukosea kwa namna yoyote
usichukie, amua kujifunza kupitia kukosea huko ambako unashindwa na si kuchukia
na kuona kila kitu ndio kimeishia hapo na huwezi kufanikiwa tena.
Fanyia
kazi haya na chukua hatua kuhakikisha ndoto zako zinatimia.
Tunakutakia kila la kheri na
endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku kujifunza maisha na
mafanikio.
Pia
rafiki, kama unapenda kujifunza zaidi kuhusu mafanikio, karibu kwenye kundi la WHATS APP LA MAFANIKIO, kujiunga tuma
neno THE UNIVERSITY OF WINNER’S
kwenda 0713 048 035, hapo utapata
utaratibu mzima wa kujiunga.
Kama
wewe ni mfugaji wa kuku na unahitaji vifaranga bora, waone DM POULTRY FARM PROJECT kwa huduma ya uhakika. Hawa ni wauzaji wa
vifaranga wa kuku aina ya KUROILER,
SASSO, KIENYEJI ASILIA na KUCHI. Kwa mahitaji ya vifaranga wasiliana nao
kwa 0767 048 035 au 0686 141097 na
wote mnakaribishwa.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO
YAIMARIKE,
Ni
wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na
mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713
048 035,
Email; dirayamafanikio@gmail.com
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.