Aug 18, 2018
Hawa Ndio Watu Ambao Hutakiwi Kuwapa Msaada Wako.
Kati
ya jambo ambalo unatakiwa kuwa nalo makini sana ni pale unapotaka kutoa msaada.
Inaweza ikawa ni ukweli unaouma, lakini iko hivi si kila mtu anahitaji msaada
wako, wapo watu ambao msaada wako hawataki ila wewe unajipendekeza tu kwao.
Si
kwambii usitoe msaada, toa msaada ila kwanza anza na kuchunguza, hutakiwi kutoa
msaada wowote hovyo hovyo kama unagawa karanga. Hebu waangalie matajiri misaada
yao wanatoa hovyo kwani? ni watu makini sana katika kutoa misaada yao.
Hata
wewe unatakiwa kuwa hivyo, pamoja na kwamba wewe unaweza ukawa ni mtu mkarimu,
lakini ukarimu wako usipitilize na kuwa matatizo kwako kwa kutoa msaada ambayo
itakuumiza wewe na kukufanya ujute, kwa nini ulitoa msaada.
Pengine
naomba nikuulize, hujawahi kuona watu wakilalamika au wakisononeka kwa sababu
ya kutoa misaada yao ambayo baade iliwageukia? Wapo watu wa namna hiyo ambayo
misaada yao iliwatokea puani na kuwa maumivu makubwa.
Kama
hujanielewa vizuri naomba nikwambie hivi, si watu wote wanahitaji msaada wako,
chagua wale ambao wanahitaji msaada wako kweli na wape. Utajuaje hilo, naomba
nikwambie watu ambao hutakiwi kuwapa msaada wako hata iweje.
1. Usitoe msaada kwa watu ambao
hawastahili kupata msaada wako.
Naamini
kabla hujatoa msaada wowote, kuna watu ambao unaona kabisa kutokana na vigezo
ulivyoweka unasema watu hawa wanastahili msaada wangu. Kama unaona watu hawa hawajatimiza
vigezo, usitoe msaada huo.
Kwa mfano,
tuchukulie umeanzisha huduma ya aina fulani iwe semina au kitu chochote na
unataka wartu walipie ndio wapate huduma hiyo. Inapotokea baadhi ya watu
wameshindwa kulipia usitoe huduma hiyo kwao hata kidogo.
Hata
inapotokea wamekujia na maombi ya uwape huduma bure kataa, maana hao
hawastahili msaada wako. Tatizo la watu wengi wanapenda sana kuwanyonya watu
wengine, na hawataki kuingia gharama yoyote ile wanataka vya bure tu.
Kwa
hiyo unapoona watu hawako tayari kufata vigezo, basi ujue watu hawa hawataki
kulipa gharama na kama watu hawako tayari kulipa gharama na msaada wako pia wanauona
si kitu na ndio maana hata gharama unazoweka hawalipi.
Usiwe
rahisi kutoa msaada, na kama umeamua kutoa msaada wa bure hakikisha kuna namna
unayofaidika kwenye msaada hupo pasipo watu hao kujua au hata kwa kujua.
Kikubwa usikubali kunyonywa na ukabakizwa mweupe kwa sababu ya msaada.
2. Usitoe msaada kwa watu ambao hawako
tayari kupokea msaada wako.
Kuna
wakati unaweza ukawa una nia nzuri tu ya kutoa msaada, kwa mfano, kuwashauri rafiki zako au ndugu zako juu ya
kufanya mradi wa aina fulani ambao ni mzuri na utawatoa kiuchumi toka sehemu
moja na kwenda nyingine.
Lakini
nikwambie hivi, watu hao ambao unakuwa umepanga kuwapa msaada huo kama hawako
tayari kuupokea na wala hawana hamasa na shauku ya kuupokea msaada huo, inakuwa
ni sawa na kazi bure na tena watakuwa adui zako wakubwa
Hapa
kitu unachotakiwa kuwa nacho makini ni kuangalia usitoe masada wowote ule kwa
kujipendekeza ili uonekane ni mwema. Dunia
na watu wake hawana shukrani, unaweza ukajuta sana kwa nini ulimsaidia sana
mtu huyu au watu wale.
Ni jambo
la kusikitisha na kupoteza muda wako sana kama unawasaidia watu ambao hawasaidiki.
Hapa ndipo umuhimu wa kuchunguza mazingira watu unawaotaka kuwasadia wanataka
msaada wako au hawaututaki hata kuusikia kwenye masikio yao.
Kikubwa
kwako hapo kaa kimya, kama kuna watu wanahitaji msaada wako kweli wa hali na
mali najua watakuja kwako lakini si kutoa msaada kwa watu ambao hawako tayari
kuupokea na wala hawana shukrani, achana na hiyo baishara mara moja.
Kwa
kuhitimisha makala hii ieleweke hivi, hao ndio watu ambao hutakiwi kuwapa
msaada, lakini hata hivyo na wewe usitoe msaada kama huna uhakika msaada huo
utaufanikisha kwa asilimia kubwa kama inavyotakiwa iwe.
Mazingira
yoyote yatakayopelekea wewe ukashindwa kufanikisha msaada utajenga uadui mkubwa
sana kati yako wewe na yule ambae ulikuwa umeamua kumpa msaada tena kwa nia
iliyo njema, kuwa makini katika hilo.
Fanyia kazi haya na chukua
hatua kuhakikisha ndoto zako zinatimia.
Tunakutakia kila la kheri na
endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku kujifunza maisha na
mafanikio.
Pia
rafiki, kama unapenda kujifunza zaidi kuhusu mafanikio, karibu kwenye kundi la WHATS APP LA MAFANIKIO, kujiunga tuma
neno THE UNIVERSITY OF WINNER’S
kwenda 0713 048 035, hapo utapata
utaratibu mzima wa kujiunga.
Kama
wewe ni mfugaji wa kuku na unahitaji vifaranga bora, waone DM POULTRY FARM PROJECT kwa huduma ya uhakika. Hawa ni wauzaji wa
vifaranga wa kuku aina ya KUROILER,
SASSO, KIENYEJI ASILIA na KUCHI. Kwa mahitaji ya vifaranga wasiliana nao
kwa 0767 048 035 au 0686 141097 na
wote mnakaribishwa.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO
YAIMARIKE,
Ni
wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na
mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713
048 035,
Email; dirayamafanikio@gmail.com.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.