Aug 30, 2018
Tabia Za Kiutendaji Zinazowatofautisha Matajiri na Maskini.
Leo nitazungumza na wewe kuhusu tabia kuu ambazo huwatofautisha watu waliofanikiwa na wale wasiofanikiwa, hivyo naomba ukae mkao wa kula kwani chakula hiki ni adimu sana pia ni maalum sana kwako wewe msakatonge mwenzangu.
Sababu kubwa ya watu wengi waliofanikiwa na ambao
wanaishi ndani ya ndoto zao ni kwamba watu huamini sana kile ambacho
wanakifanya. Kuamini kile wanachokifanya ndicho kilichowapelekea watu hao
waendelee kuishi ndoto zao kila jua lichomazapo.
Sababu nyingine ambayo inawafanya watu wenye mafanikio
waendelee kufanikiwa ni kwamba watu hao mara baada ya kuona changamoto fulani
wao walitafuta njia ya kutafuta majibu ya changamoto husika.
Hiyo ni kwa upande waliofanikiwa, ila unapokuja upande
huu mwingine ni kwamba watu wengi wameshindwa
kuziishi ndota zao kwasababu, mosi ni kwamba watu hao huwa hawamini kile
ambacho wanakifanya.
Hivi hujawahi kukutana na mtu fulani kisha akakwambia
nafanya jambo hili kwa kujaribu tu? Bila shaka utawakuta umeshawahi kukutana na
watu wengi wenye kauli kama hizi. Ukichunguza kauli kama hizi utagundua bayana
ya kwamba ni wazi kabisa watu hawa hata kile wanachokifanya hawakiamini, kwa
mtindo huu mafanikio yapo kweli?
Pamoja na kutoamini kile wanachofanya lakini pia watu
hawa ni wazuri sana wakutafuta sababu, na sababu hizi ni zile zisizokuwa na
msingi yaani watu hawa ni wazuri sana kwa kutafuta visingizio.
Ukimuuliza hivi kwani hujafanya hivi? Mtu huyo atakuja na
majibu ya kwa sababu ya.........., majibu ya kwa sababu mara nyingi katika
safari ya mafanikio huwa si ya majibu ya msingi bali huwa ni majibu ya kujikatiza
tamaa tu.
Hivyo ndugu yangu kama ni kweli unataka mafanikio ya
kweli unatakiwa kufahamu ya kwamba kama
kweli umeamua kufanya jambo fulani wewe
fanya ila kama hauhitaji mafanikio basi endelea kutafuta sababu za kutofanya.
Mpaka kufikia nukta hiyo sina la ziada nikutakie siku
njema na mafanikio mema.
Ndimi: Afisa Mipango
Benson Chonya.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.